YEHODAYA
JF-Expert Member
- Aug 9, 2015
- 36,902
- 51,992
Kesi ya Yesu kuuawa ilivunja sheria zote.
Kwa mfano ukisoma Biblia utashangaa Yesu alikamatwa usiku akisali kanisani kwake porini kwenye milima ya mizeituni akiomba na wanafunzi wake ambao kwa sababu ya usingizi walikuwa wakilalala hawasali.Walimshika ndani ya kanisa lake porini ambako akitekeleza ibada yake na wanafunzi wake akitumia uhuru nwake wa kuabudu.Usiku haukuwa muda wa kazi.Kwa hiyo kisheria haikuwa sahihi kwao.Pia haikuwa sahihi kumshika akiwa ibadani kwenye chaka ambalo ndio lilikuwa hekalu lake la kuabudia
Pili aliburuzwa kwenye mahakama zao usiku.Katika historia ya sheria hakuna popote mahakama iliwahi fanya vikao vyao usiku mida isiyo ya kazi na majaji wakaendesha kesi
Tatu Kazi ya askari ni kumlinda mtuhumiwa anapopelekwa kwenye mashtaka lakini Yesu alipokuwa akipelekwa mahakamani watu walikuwa wakimzonga ,kumpiga na kumtemea mate mbele ya macho ya askari wa kirumi bila askari hao kuchukua hatua zozote
Nne alipokuwa mahakamani Askari walifanya kitendo cha kihuni alipokuwa akihojiwa na Jaji Alipokuwa akijibizana na jaji askari alimzaba kibao Yesu NDANI YA mahakama kazi ambayo si yake.Huyo askari alivunja sheria ya mahakama mbele ya jaji na jaji hakumchukulia hatua wala jeshi lake halikumchukulia hatua.
Tano,hukumu aliyotoa jaji mrumi Ponsio PILATO ilikuwa ya kihuni na haikubaliki kisheria.Alipohukumu aliuliza umati uliokuwepo mahakamani nimfanyie nini Yesu huyu? Umati ukajibu asulubiwe ,asulubiwe na akakubali na kumhukumu.Kisheria Jaji anatakiwa aangalie sheria zinasemaje kwenye vitabu vyake sio aulize waliohudhuria kusikiliza kesi mahakamani.Katika majaji wajinga waliowahi tokea duniani Ponsio pilato ndio jaji mjinga nambari wani
Sita,aliposulubiwa na kufa Askari maruhuni wa Kirumi WALIGAWANA mavazi yake.Mavazi ni mali ya mtu.Akifa mirathi huwa inatangazwa ili wapatikane warithi kisheria wachukue hizo mali.Lakini za Yesu baada ya kukata roho tu askari wa kirumi waligawiana mirathi pale pale bila kibali cha kisheria.
Nini cha kufanya??? Wakristo waiburuze serikali ya Italia (Waitaliano) iwalipe fidia kwa kumwua mtu wao na wadai mali zile walizogawana (MaVAZI YAKE YA BEI MBAYA) bila kibali cha mahakama wazirudishe na riba juu.
Pia waidai serikali ya Italia ambayo ndio iliyoteua ponsio Pilato ilipe fidia wakristo na waiombe ifukue maiti ya Ponsio Pilato ihukumiwe upya na jopo la majaji
Yesu alihukumiwa kufa na jaji mrumi Ponsio Pilato NA akauawa na askari wa Kirumi kwa hiyo warumi wana kesi ya kujibu kuhusiana na kifo cha Yesu