Waisrael wasitisha maandamano baada ya onyo kali la Hamas

kimsboy

JF-Expert Member
Oct 17, 2016
8,985
17,850
Wazayuni wasitisha maandamano baada ya onyo la muqawama wa Palestina

Waziri wa vita wa utawala wa Kizayuni, Benny Gantz ameyataka magenge ya Kizayuni yasifanye tena maandamano kuelekea Msikiti wa al Aqsa huko Baytul Muqaddas baada ya wanamapambano wa Palestina kuonya kwamba wataupiga tena kwa makombora mji wa Tel Aviv kama Wazayuni watafanya maandamano hayo.

Huku hayo yakiripotiwa, Wizara ya Mambo ya Nje ya Palestina imetahadharisha kuhusu hatari ya kuendelea unyanyasaji na ukatili unaofanywa na utawala wa Kizayuni dhidi ya watu wasio na hatia na kuongeza kuwa, waziri mkuu wa Israel, Benjamin Netanyahu anavuruga kila kitu ili abakie madarakani.

Televisheni ya Rusia al Yaum imeripoti habari hiyo na kuongeza kuwa, jana Jumapili, Wizara ya Mambo ya Nje ya Palestina ilitahadharisha kuwa, waziri mkuu wa Israel, Benjami Netanyahu anapigana kufa na kupona kuhakikisha anabakia madarakani, hivyo sasa hivi anazidi kuharibu hali katika mji wa Baytul Muqaddas ili kujipapanua na migogoro inayomkabili.

Yahya Sinwar Kiongozi wa Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina (Hamas)

Wizara ya Mambo ya Nje ya Palestina imeongeza kuwa, Netanyahu anajidanganya anapodhani kwamba kadiri anavyoharibu hali ya usalama huko Quds ndipo atakapoweza kubakia madarakani kwani kama Wazayuni watavuruga hali ya usalama huko Baytul Muqaddas na katika Msikiti wa al Aqsa, basi Wapalestina nao watatoa majibu makali katika maeneo mengine ya ardhi zinazokaliwa kwa mabavu ambazo zimepachikwa jina bandia la Israel.

Kabla ya hapo pia, Yahya Sinwar Kiongozi wa Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina (Hamas) katika Ukanda wa Ghaza alikuwa ametoaonyo kali kwa Wazayuni baada ya kubainika wanapanga kufanya shambulio jingine dhidi ya Msikiti wa al Aqsa na kusema kuwa, iwapo Wazayuni watauhujumu tena msikiti wa al Aqsa basi harakati za muqawama zitauharibu mji wa Tel Aviv.

4by26918ce98ff1vvoj_800C450.jpeg
 
ACHA UVIVU WA KUFIKIRIA WEWE ISRAEL HAIJWAHI WAOGOPA WAVAA MAKOBASI HATA KIDOGO
 
Back
Top Bottom