Waisrael 170 wakwama Zanzibar bada ya ndege yao kupatwa na matatizo

Mlaleo

JF-Expert Member
Oct 11, 2011
13,212
9,511
170 Israelis stranded in Zanzibar
Arkia discovers technical issues with plane, passengers sleep on airport benches while waiting for flight home. Arkia: We'll provide hotels.
upload_2017-10-30_0-57-53.jpeg


Zaidi ya Waisrael 170 Wamekwama Mjini Unguja baada ya kutokea hitirafu katika Ndege ya Shirika la ''Arkia'' kwa zaidi ya Masaa 60 au Siku nne sasa.

Abiria walikuwa wasafiri kuelekea Israel tokea Jumatano iliyopita, kwa Ndege ya Shirika hilo la Israel Ndege namba AIZ628. Kuchelewa huko kulitokana na matatizo ya kiufundi yaliyogunduliwa katika ndege hiyo.

Abiria wote 170 hadi sasa wanasubiria usafiri hapo Airport, Wamelala kwenye Mabenchi ya uwanja wa Ndege.

Meirav Alon, ambae Dada ''Efrat'' yake amekwama aliiambia kituo cha habari cha Channel 2 kuwa nadhani wanajisikia hawana msaada wowote kule na mzimu wa ndoto mbaya hauelekei kuisha. Kuna Ndege tatu zimeenda Israel ambapo wangetufaulisha tokea hili Tatizo litokee ''lakini Shirika hili limeamua kutusumbua abiria kwa makusudi kabisa'' alisema.

Shirika la Ndege lilitoa taarifa kuwa Kwa kuwa safari ya kuelekea Israel imesitishwa kwa sababu za kiufundi na tunahitajika kubadilisha spea mpya ya ndege yetu, Mtaalam kutoka Israel alisafiri haraka kuelekea eneo la tukio huko Zanzibar, na aliweza kurekebisha tatizo na Ndege ingeweza kusafiri kesho yake Asubuhi, Lakini kabla ya kuruka tena wakagundua Tatizo lingine na kusema hawataweza kuruka angani hadi vifaa vingine vije vitumwe kutoka Israel.

Shirika hilo la Ndege baada ya kuona mambo mazito likasema litatuma ndege maarum mchana huo wa Ijumaa kuwachukua abiria wake wote, Kwa kuwa Sabato ilikaribia Abiria hawakuweza kusafiri na walitegemea kusafiri Jumamosi Jioni Sabato itakapokuwa imeisha kurejea Israel.

Shirika hilo la Ndege liliomba kumradhi kwa mioyo iliyoumia kwa Abiria wote na kuwaahidi kuwalipia hotel bora kabisa huko zenji na walisema wanajali zaidi Usalama wa Abiria wao na kuwa tatizo halikuwa kubwa sana ila kutokana na hali halisi kama spea n.k ndio ilisababisha uchelewaji kuwa mkubwa.

''Wafanyakazi wa Arkia wamekuwa sharp kuwafahamisha kila maendeleo ya ndege kwa abiria wake''

hiyo si wangeomba Bombadier yetu ipige long trip nayo ionje anga zenye baridi na joto kali...


170 Israelis have been stranded for over 60 hours in Zanzibar, due to a technical issue in the Arkia plane which was to bring them to Israel.

The passengers were scheduled to fly to Israel on Wednesday, on Arkia Israeli Airlines' Flight AIZ628. However, the flight was delayed due to several technical failures discovered in the plane.

All 170 passengers are currently waiting at the airport, sleeping on the airport's benches.

Meirav Alon, whose sister Efrat is stranded in Zanzibar, told Channel 2 that there is a feeling of helplessness, and that the nightmare will not end.

"The company could have switched planes. There have been three flights from Israel to Zanzibar since these issues were discovered," she said. "Instead, the company prefers to abuse its passengers."

Arkia responded, "Prior to the plane's scheduled return to Israel, we discovered an issue which required a replacement part. Expert Israeli mechanics were immediately flown to the scene, and solved the problem so that the plane would be able to leave for Israel early the next morning. Prior to takeoff, however, we discovered another failure which required us to send a technical part from Israel."

"Arkia has decided to send a special plane this afternoon to bring the passengers home. We will bring them to Israel at approximately midnight. Those passengers who observe Shabbat (Sabbath) will return to Israel immediately after Shabbat ends on Saturday night.

"Arkia apologizes for the heartache, but we wil not compromise on flight safety. We will ensure each passenger is hosted comfortably in a hotel. These issues are not complicated, but the sequence of events caused additional delays.

"Arkia staff are working constantly to ensure the passengers are informed of every development."

Source
 
hiyo si wangeomba Bombadier yetu ipige long trip nayo ionje anga zenye baridi na joto kali...
Aisee abiria wangeomba warudishiwe nauli kidogo coz hiyo Bombadier ni sawa na daladala za mwenge, usifananishe pangaboi na vitu kama hivo mkuu!!
 
Aisee abiria wangeomba warudishiwe nauli kidogo coz hiyo Bombadier ni sawa na daladala za mwenge, usifananishe pangaboi na vitu kama hivo mkuu!!
Bombadier ipo sawa japo haieleweki tu Mwanza wanaijua vizuri japo kaskazini ilikwama ikashindwa kupiga reverse..

Ingetokea Nchini Tanganyika haswa MZIZIMA CITY am sure mzee wa kiki angepiga kiki hadi Netanyau angepata taarifa zake na angemuomba ndege zilizochoka choka awaletee wananchi wa mkoa wake kwani wanashida ya usafiri
 
Bombadier ipo sawa japo haieleweki tu Mwanza wanaijua vizuri japo kaskazini ilikwama ikashindwa kupiga reverse
Sasa route ya dar to kaskazini ilikwama itaweza mikikimikiki ya zenji to israel?
Itachemsha njiani boss
 
jamani...wawalinde hao wateul wa Mungu Wasje dhuriwa na magaidi
 
Waisrael siwaamini hata dakika moja, nawachukuliaga kama wote ni majasus, huenda kuna mission hapo hakuna chakuharibika kwa ndege.
 
Bombadier ipo sawa japo haieleweki tu Mwanza wanaijua vizuri japo kaskazini ilikwama ikashindwa kupiga reverse..

Ingetokea Nchini Tanganyika haswa MZIZIMA CITY am sure mzee wa kiki angepiga kiki hadi Netanyau angepata taarifa zake na angemuomba ndege zilizochoka choka awaletee wananchi wa mkoa wake kwani wanashida ya usafiri
 
1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom