Waislamu watakiwa kutokushiriki ktk maandamano ya amani

Status
Not open for further replies.
Habari za propaganda za kisiasa hizo!!! Mwaka 1995 tulikuwa na CUF kuwa chama cha kidini, mwaka 2010 tumekuwa na Chadema kuwa chama cha kidini. Tumeshuhudia mambo mengi sana ikiwa na akina Mahita kuwatuhumu waislam wenzao kuwa magaidi.

Jamani lazima tujue kuwa tuko kwenye mapambano ili kila chama kishike dola na hili ni kwa CDM, CCM,UDP au TLP. Maandamano ya Chadema kwa wenye akili finyu wanaona hayajawasaidia ila wamepata kujitangaza zaidi na kuungwa mkono kwa wingi. Walipo anza operation Sangara wenzao wa CUF na CCM waliendelea kuwadharau hivyo hivyo lakini uchaguzi wa mwaka jana umeonesha matunda ya Operation sangara kwa kuongeza idadi ya ubunge wa kuchaguliwa kama mara 10. Hivi sasa hofu ya CCM, CHEYO na MREMA ni kuwa 2015 majimbo yao wanaweza kuchukuliwa zqaidi na CDM hivyo njia rahisi ni kusema maandamano yanavunja amani na hayasaidiii kitu!!!

CCM inatumia njia nyingi ikiwemo hiyo ya radio Imam. Waislam wenye akili wanajua wanachokifanya na tutawaona wakiandamana pamoja na CDM. Waislamu wengi ni waelewa.
 
Mimi nimefika Tanga na Mikoa mingine aliyotaja huyo mweshimiwa, Kwa resorce ya Bandari, Mashamba ya Mikonge n.k, Tanga bado mko nyuma, hizi nyumba unazosema zimejengwa ni za Tangu enzi ya uhuru.

Uliona watu wakicheza bao? na hizo nyumba walitoka watu Mwanza na Moshi wakawajengea?
 
wewe sio muislam. Kama unataka radio iman ifungiwe,basi useme na slaa akamatwe.Kumbuka maneno yake aliyosema ktk mkutano Arusha.'tanzania haitatawalika tena,wangapi wanasema tz ya kikwete isitawalike' maneno hayo unayaonaje sio ya mtu mhaini.Maneno haya yanajenga au yanabomoa? Kuwa mkweli acha mapenzi na chuki

Alisema Tanzania haitatawalika baaada ya tukio gani kama unakumbuka! Wewe na Wasira ni sawa tu maana naye nilisikia akisema wakati fulani hujo Msoma. Kabla ya ku-quote mtu jiulize amesema hivyo kwa nini? Kama unakumbuka vizuri (japo sina ukika kama alisema hivyo) matamshi yalitokea baada ya mvurugiko wa maadamano ya Chadema Arusha na Polisi walio ua watu bila sababu. Hata angelikuwa wewe ungesema hivyo. Iweje polisi waue na kuvamia mikutano ya amani badala ya kuilinda mikutano hiyo. Any way. pointi yangu hapo ni hii. Nimesikia wengi waki-quote 'nchi haitatawalika' kwa haraka haraka sentensi hii inaweza kuonekama mbaya na zaidi inopotumiwa pasipo kufikiri lini ilisemwa na kwa nini. Wito wangu, kila atakayesema hivyo afafanue pia mazingira ya kwanini Mh huyo alilazimika kusema hivyo.
 
Kwa hali hii tutazidi kuwa gizani tena giza totoro tukiendelea kuwasikiliza viongozi kama hao baadhi wa kislamu kwani inaonesha wazi ndio wanaounga kutokuendelea kwa maendeleo ya kijamii na kiuchumi inaonekana wazi wameunga mkono ubadilifu wa fedha za umma na uongozi mbovu wa serikali.
Fika watakuwa hawajui fedha wanazoiba mafisadi ni za kina nani ndio maana hawana uchungu nazo na kuanzisha movement kuzidai zirudishwe.
 
Maandamano yangekuwa mapinduzi yasingeruhusiwa. Hiyo lugha ya mapinduzi imeanzishwa na CCM kama walivyoanzisha UDINI. Mie nafikiri tuwaache hao waislamu uchwara na hao mnaowaita viongozi kina Mrema sijui Cheyo waongee pumba zao. Acheni Chadema wafanye kazi za chama chao.
 
kwa sifa hiyo tu tayari wewe si muislamu anayejitambua, kwani huujui uislamu. kama wewe muislamu taja sifa kumi za munafiki

Mr. Mark heshima juu!
Naomba nikuulize je maandamano si haki ya kikatiba? Je chama cha siasa hakina haki ya kufanya maandamano?
Nashangazwa sana na nyie ndugu zetu waislam kusema maandamano ni njia ya kuleta fujo, je wewe si muelewa hata ujifunze kwa mifano ya maandamano ya kanda ya ziwa? Kule hakukutokea vurugu yoyote, hivyo waweza gundua hayana madhara yoyote, kumbuka lengo kuu la chama chochote cha siasa ni kushika dola na sivinginevyo sasa na hii inatutia imani kuwa Chadema ni chama makini kwa kuwa kina sera mathubuti ambazo zinaakisi kuleta maendeleo kwa haraka, kama utakumbuka kwenye miaka ya 61 au 62 tulilingana kabisa maendeleo na nchi kama Singapore au Thailand lakini na japo tuna kila aina ya rasilimali (watu, ardhi, kasoro uongozi bora) wametuacha sana leo kimaendeleo, je huoni serikali iliyopo imeshindwa? Hivyo Chadema kuwajuza raia ni jambo la msingi?
Hebu niambie ni chama gani kilichowafumbua macho waTZ kwa mambo maovu yanayotendeka serikalini kama sio Chadema? Dr Slaa kuwa Mkristo hii si tatizo kwani ni dini yake binafsi wala Ukristo haupo kwenye katiba ya Chadema, sasa kama utadhani Chadema ni Udini basi utakuwa Unamakengeza ya kufikiri!
Wakati JK anagombea urais 2005 wengi tulimuunga mkono si kwa sababu ni mwislam la hasha wengi tulimuona ni tumaini, kumbe si lolote, je mtu akisuasua si vema kuwakumbusha wananchi juu ya yale anayoyashindwa?
Waislam mmekwa wepesi sana kuonyesha na hata kutumiwa na viongozi wenu wa kidini kwa tafsiri mbaya ya mawazo ya viongozi wenu hao wa kinidi!
Nashangaa sana eti Chadema wataleta vurugu???? Hii ni crap ya karne!
 
Hakika kaka Majimshindo umekumbusha point muhimu sana, Mtu yeyote ambaye akili yake imetekwa na kichwa cha slaa kuikubali moja kwa moja anahitaji Dua. CDM inaonekana ni genge la wasioipenda nchi yao, wenye uchu na madaraka, wanamlazimisha padre slaa afanye hata vile mafundisho ya imani yake yasivyotaka. watanzania walio wengi wanakushangaeni sana kwa mnayojifanyisha na hivyo ndio mnakiua chama. kuamini hivyo mtaona uchaguzi ujao mtakavyo anguka. Kwani wananchi hawana shida na maandamano yenu wala nyinyi hata mkikabidhiwa nchi msidhani mnaweza kuyamaliza matatizo ya watanzania. Kama nyinyi wazalendo toeni suport katika kila sehemu mnayoona serikali haijafanya ipasavyo siyo kulalamika na kuandamana.

Hapo nilipoweka red, ndugu kila chama kina sera zake, CCM na serikali yake wanasera zinazoshabihiana na ufisadi na CDM wanasera zao za kuwaletea wananchi wa Tz maendeleo, CCM hawazikubali sera za CDM. Miaka 5 itaisha zile ahadi za JK zenye dhamani inayokaribia trillion 90 hazitatimizwa.
 
Elimu ya uraia haitolewi kwa maandamano. Maandamano ni chachu ya kuanzisha uvunjifu wa amani haswa hayo maandamno yanapoashiria kufanya mapinduzi.

Mapinduzi ya nini? Nani aliwaambia kuwa ukali wa maisha unapunguzwa kwa maandamano?

Nasema, naunga mkono kiongozi yoyote anaepinga maandamano na waliosema wanapinga hayo maandamano si viongozi wa waIslaam pekee. Jee Cheyo ni muIslaam? Jee, Mrema ni muIslaam? Mbona wote hao hawataki haya maandamano na hujawataja? Au wewe ndie unaanzisha fitina za kidini?

Majimshindo kweli wewe mzalendo! yaani pamoja na EPA,GREEN DEEP,TICS,RICHMOND,DOWANS,KAGODA,TRL NK BADO TU HUTAKI WANANCHI WACHUKUE MSIMAMO NA KUINESHA SERIKALI HAWAKUBALIANO NA HAYO MADUDU DU, AMAKWELI UMEKUWA MZALENDO WA AINA YAKE! AU LA YAWEZEKANA NI MTU MWENYE UWEZO MDOGO SANA WA AKILI AU UNAFAIDIKA NA MADUDU HAYA, NINA UHAKIKA UWEZO WAKO WA KUCHAMBUA MAMBO NI MDOGO SANA NA SIDHANI HATA KAMA UMESOMA HATA SHULE NA KAMA UMESOMA BASI AJABU SANA NA NINA ALIYEKULOGA?
 
wanaosema hivyo wanatumia mgongo wa dini...achana nao,kwani kwa kiasi kikubwa waslam ndiyo wanumia kulinganisha na wakristo,anagalia mikoa ya Rukwa,Mtwara,Kigoma,Lindi Zanzibar,Tanga ambako kuna idadi kubwa ya waslam.wengi wao hawapendi kujishughulisha kutwa kushinda kucheza bao..na maongezi ya vijiweni.Wakristo kupitia makanisa bado wanajumuia ndogo ndogo za kusaidiana na kukupeshana.

HILO WANALO!!1

Mkuu najua wewe ni Chadema tena damu! Tanzania yote maisha magumu tena kuna watu wamechoka mno na haya maisha, hiyo mikoa yako unaona kuna waislam wengi masikini kazi yao kucheza bao na kukaa vijiweni ni mtazamo wako tu, nenda vijijini kaone wananchi walivyochoka, kwa mujibu wa World Bank na IMF pato la mtanzania kwa mwaka dola 750, wewe kama Mkiristu unaona hiki kipato ni sawa? swala la kupinga maandamano ya Chadema wamepinga wengi tu, sasa wewe Muislam mmoja hakipinga wanapondwa Waislam wote hili sio sawa.
 
Waislamu nchini wameonywa kutokushiriki katika maandamano ya CHADEMA kwani yanahatarisha amani ya nchi.

Source: Radio Imani

My take:

Wana JF ktk nchi yetu huwa siwaelewi waislamu (baadhi) kwa sababu CHADEMA wanachofanya ni kutoa elimu ya uraia na pia kupeleka ujumbe kwa serikali juu ya hali ngumu ya maisha ila ndugu zetu waislamu wapo kinyume ina maana wao wana maisha mazuri ama wanatumiwa na CCM?

Nawasilisha hoja.

Huo ni uchochezi wa CHADEMA katika kutaka kuwalazimisha waislamu wawaunge mkono.

Hivi hata kwa akili kidogo tu. JE RADIO au MTANGAZAJI anaweza kuwazuia waislamu wasishiriki na wewe ukachukua kama kichwa cha habari.

Ni lazima tuwe wakweli kwani hapa lazima ujuwe kuwa unagusa IMANI za watu. Waislam wana jumuia zao ambazo zinazowaongoza kama ilivto kwa wakristo. TEC,NK kwa waislam kuna Bakwata n.k

Sasa hilo ni tamko la Bakwata au jumuia gani ya waislam
 
Waislamu nchini wameonywa kutokushiriki katika maandamano ya CHADEMA kwani yanahatarisha amani ya nchi.

Source: Radio Imani

My take:

Wana JF ktk nchi yetu huwa siwaelewi waislamu (baadhi) kwa sababu CHADEMA wanachofanya ni kutoa elimu ya uraia na pia kupeleka ujumbe kwa serikali juu ya hali ngumu ya maisha ila ndugu zetu waislamu wapo kinyume ina maana wao wana maisha mazuri ama wanatumiwa na CCM?

Nawasilisha hoja.
Kumbe nilishindwa kujua. Kumbe Wakristo wote mmesha wapa sumu kupitia kanisani ndio maana mnaleta chokochoko zenu sasa mnataka support za waislam ili muwe kamili.

Basi na waislamu wanakushangaa kwa kutaka kuleta machafuko nchini. Sisi tunataka amani kwani amani haiuzwi na Serikali ipo pamoja nasi katika kuhakikisha Amani inakuepo na kudumu hapa nchini.

sasa nimeelewa lile tamko la kanisa kule Arusha la kumkataa Meya aliyechaguliwa kihalali na kwa kufuta sheria na kanuni zote za nchi. Poleni sana mmeula wa chuya
 
Subiri Mkwere ambaye wao wanamwona mwenzao aondoke madarakani halafu atawale infidel uone kila siku watakavyokuwa wanalala barabarani kwa maandamano hata kama hali itakuwa nzuri! Hawa watu kuwaelewa lazima uwachungulie katika 3D!

Mkuu hapa napata tabu kidogo na haya maneno yako, kwa hiyo waislam wanachama wa Chadema na Wabunge waislam wa Chadema unawaweka kwenye wakati mgumu. kwa maneno yako haya ya ubinafsi unataka tuamini Chadema ni chama cha Wakiristu.
 
jamani hayo ni maoni ya muislamu katika redio na sio msimamo wa waislamu, kila mtu anahaki ya kuongea anachokiamini ilimradi tu asivunje sheria za nchi. ila kwa wale waislamu wenzangu tukumbuke mafunzo ya Mtume S.A.W alisema `` ukiona ovu likemee``
kama mtu ataacha hayo mafundisho na kutoa maoni kwa kuhongwa hela kidogo ya kula leo ili atoe matamako yakichovu na kusahau kuwa ndugu zake wanalala na njaa na kufa kwa kukosa matatibabu, hakika na yeye ataangamia vilevile.
 
Dini zitabaki kuwa dini na siasa ni siasa tu!Anayechanganya hivi vitu viwili viende pamoja haitendei haki akili yake.Cheyo sio muislam,haungi mkono mabadiliko!Ana sababu ya kimaslahi kama ilivyo kwa Mrema.Hiko kiredio gani sijui,kinatumika kuwaaminisha waislamu kuwa chadema ni ya kikristo wasiiunge mkono!Still ndani ya cdm kuna wabunge waislam!Cdm inashambuliwa na wote wanaohofu maslahi yao binafsi kuporomoka!Kuna mafisadi wengi tu ndani ya CCM wakristo.Viongozi wa ccm wamebuni propaganda ya udini kudhoofisha cdm.Imani za watu zisitumike kwa manufaa ya wachache.Na mtu anayekubali imani yake kutumika na mwingine kwa malengo ya kufanikisha na/au kuhalalisha unyang'anyi wa mali ya uma basi yeye ni mpumbavu.Watu wa dini zote tusikubali kutumika kwa manufaa ya wachache,tupaze sauti kama uma kwa pamoja kudai haki na usawa ndani ya nchi yetu.CDM hawawakilishi matatizo ya wakristo wala waislam bali ni watanzania wote wanyonge wasiofaidi rasilimali za nchi yao,waliopuuzwa,wanaouawa bila hatia,wanaoishi maisha magumu.Na ccm hii ya maslahi haifanyi haya maovu yote tunayoyajua ili kufaidi matunda na waislam wala wakristo bali ni kwa ajili yao wenyewe binafsi na familia zao!Tuwakatae kwa pamoja jamani bila kujali imani zetu,wasitupe kichwa kipumbavu kwa kutuona ni wenzao kumbe wanatumia ujinga wetu.TUSIKUBALI
 
Mrema na Cheyo ni CCM B, Hujui hawana vision

Kama Mrema na Cheyo ni CCM B, kwa nini aliyetowa mada ataje waIslaam peke yao? Anatafuta nini kwa waIslaam? WaIslaam wengine, si wote, kwani ni lazima waandamane? Au mnafikiri kuwa Chadema inaungwa mkono na wa Tanzania wote? Kama ni hivyo mmekosea, wengi sana hatuungi mkono maandamano yanayoashiria uvunjifu wa amani.
 
Dini zitabaki kuwa dini na siasa ni siasa tu!Anayechanganya hivi vitu viwili viende pamoja haitendei haki akili yake.Cheyo sio muislam,haungi mkono mabadiliko!Ana sababu ya kimaslahi kama ilivyo kwa Mrema.Hiko kiredio gani sijui,kinatumika kuwaaminisha waislamu kuwa chadema ni ya kikristo wasiiunge mkono!Still ndani ya cdm kuna wabunge waislam!Cdm inashambuliwa na wote wanaohofu maslahi yao binafsi kuporomoka!Kuna mafisadi wengi tu ndani ya CCM wakristo.Viongozi wa ccm wamebuni propaganda ya udini kudhoofisha cdm.Imani za watu zisitumike kwa manufaa ya wachache.Na mtu anayekubali imani yake kutumika na mwingine kwa malengo ya kufanikisha na/au kuhalalisha unyang'anyi wa mali ya uma basi yeye ni mpumbavu.Watu wa dini zote tusikubali kutumika kwa manufaa ya wachache,tupaze sauti kama uma kwa pamoja kudai haki na usawa ndani ya nchi yetu.CDM hawawakilishi matatizo ya wakristo wala waislam bali ni watanzania wote wanyonge wasiofaidi rasilimali za nchi yao,waliopuuzwa,wanaouawa bila hatia,wanaoishi maisha magumu.Na ccm hii ya maslahi haifanyi haya maovu yote tunayoyajua ili kufaidi matunda na waislam wala wakristo bali ni kwa ajili yao wenyewe binafsi na familia zao!Tuwakatae kwa pamoja jamani bila kujali imani zetu,wasitupe kichwa kipumbavu kwa kutuona ni wenzao kumbe wanatumia ujinga wetu.TUSIKUBALI

Sasa unataka kulazimisha hicho "kiredio" kiunge mkono maandamano yasiyo na mpango? Lengo la maandamano ni nini? Kama ni kubadili uongozi, Tanzania tunapiga kura na huwa hatuandamani.

Masuala ya udini yanahusu nini kama wewe si mdini?
 
kwa sifa hiyo tu tayari wewe si muislamu anayejitambua, kwani huujui uislamu. kama wewe muislamu taja sifa kumi za munafiki

Nashindwa kuelewa mnafundishwa na kukaririshwa nini huko madrasa(chuoni)kwenu,kwani neno upendo,uvumilivu na ustahimilivu...kwenu ni msamiati mgumu sana hata uelimikeje,..hiyo redio iman ipo kwa ajili ya propaganda mbaya kwa ajili ya maslahi yao na kikundi fulan,...mwenzio muislam safi anayejua maana ya dini yenu maake nasikia ni islam-aman unam-crash tu kwasababu haja-proveke kama jadi yenu ilivyo...aaaaaaaaaaah!..puuuuuuuuuuuuuuf
 
Waislamu nchini wameonywa kutokushiriki katika maandamano ya CHADEMA kwani yanahatarisha amani ya nchi.

Source: Radio Imani

My take:

Wana JF ktk nchi yetu huwa siwaelewi waislamu (baadhi) kwa sababu CHADEMA wanachofanya ni kutoa elimu ya uraia na pia kupeleka ujumbe kwa serikali juu ya hali ngumu ya maisha ila ndugu zetu waislamu wapo kinyume ina maana wao wana maisha mazuri ama wanatumiwa na CCM?

Nawasilisha hoja.

Akili za Sheheyaha na poorof sio prof Maji marefu utazielewa tuu
 
jamani hayo ni maoni ya muislamu katika redio na sio msimamo wa waislamu, kila mtu anahaki ya kuongea anachokiamini ilimradi tu asivunje sheria za nchi. ila kwa wale waislamu wenzangu tukumbuke mafunzo ya Mtume S.A.W alisema `` ukiona ovu likemee``
kama mtu ataacha hayo mafundisho na kutoa maoni kwa kuhongwa hela kidogo ya kula leo ili atoe matamako yakichovu na kusahau kuwa ndugu zake wanalala na njaa na kufa kwa kukosa matatibabu, hakika na yeye ataangamia vilevile.

Kawa elimishe watu wawapigie kura ili mchukuwe madaraka ki halali, huwezi ki maandamano halafu ukaitawala nchi ikawa na maendeleo.

Tanzania ni juzi juzi tumetoka kupiga kura, kuna nini zaidi? Wengi wetu tunamkubali Kikwete na uongozi wake mzuri na wa busara.

Sasa nyinyi Chadema mkaoneshe mifano kwenye majimbo mliyopigiwa kura na miji mliopata umeya, tukiona mfano mzuri, tutawaunga mkono kwa kuwapigia kura, tukiona mmemaliza miaka mitano na hamana cha maana mlichofanya kwenye majimbo yenu, basi mjuwe hatuwapi kurta zetu.

Maandamano ya mapinduzi hatuyataki, madhara yake ni makubwa kuliko faida zake!
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom