Waislamu watakiwa kusomesha | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Waislamu watakiwa kusomesha

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by TUKUTUKU, Feb 9, 2011.

 1. TUKUTUKU

  TUKUTUKU JF-Expert Member

  #1
  Feb 9, 2011
  Joined: Sep 14, 2010
  Messages: 11,852
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 145
  Waislamu watakiwa kuzingatia elimu za aina zote,ili ziweze kuwasaidia kwenye maisha yao.Akizungumza kwenye sherehe ya kukaribisha mfungo sita,muasissi wa kikundi cha Firqata’salaam,Ismail Salim,alisema waislamu wanatakiwa kuamka,wasitegemee elimu ya dini peke yake bali wapeleke watoto wao shuleni kuanzia msingi hadi chuo kikuu.Aliendelea kuwaasa waislamu kujenga shule binafsi nyingi,ili watoto wa kiislamu waweze kupata elimu bora na kutoa nafasi kwa watu wengi kusoma.Katika mfungo huu waislamu wanakumbushwa kufanya mema ya kumpendeza mungu kwa sababu wengi wamejisahau.(Chanzo cha habari:Mwananchi 9/02/2010,uk 8)
  My take
  Kwa kweli huu ni wakati muafaka kwa sisi waislamu kusimama kidete kuhusiana na suala la elimu,.badala ya kuendelea kuwalaumu wakristu au serikali yetu.Tuache majungu na tufanye kazi kwa juhudi, balada ya kukaa misikitini kupiga majungu muda ambao si wa sala.Kwa kufanya hivyo tutaendelea kudidimia na kuwaona wakristu kama maadui zetu.
   
 2. IGWE

  IGWE JF-Expert Member

  #2
  Feb 9, 2011
  Joined: Feb 3, 2011
  Messages: 7,752
  Likes Received: 1,326
  Trophy Points: 280
  na hapo ndipo penye hekima kiongozi wangu
   
 3. TUKUTUKU

  TUKUTUKU JF-Expert Member

  #3
  Feb 9, 2011
  Joined: Sep 14, 2010
  Messages: 11,852
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 145
  Siku zote majungu hayajengi,bali ubomoa jamii iliyoshikamana na inayoishi kwa kushiriana kwa kusaidiana,kuoleana,kuzikana na kwenye matatizo mbalimbali yanayojitokeza kwenye jamii!!
   
 4. H

  Hardwood JF-Expert Member

  #4
  Feb 9, 2011
  Joined: Sep 21, 2010
  Messages: 851
  Likes Received: 479
  Trophy Points: 80
  Mkuu wewe umekuwa mkweli mno!!!! Very good!!!! That is the fact waende shule na wajipange upya kimkakati na wala wasiendekeze uzandiki usio na mashiko.
   
 5. Kimbweka

  Kimbweka JF-Expert Member

  #5
  Feb 9, 2011
  Joined: Jul 16, 2009
  Messages: 8,608
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 145
  Elimu dunia ni muhimu pia waliyoianzisha hawakuwa wajinga waliona mbali mno
   
Loading...