Waislamu wamtuhumu Mufti Abubakari Zuberi kujimilikisha shule kumi za BAKWATA

jembejembe

JF-Expert Member
Jun 9, 2016
572
1,000
Kampuni ya Zaim Education Development Limited,ni kampuni iliyoanzishwa na Mwalimu Ally A. Ally--ambaye ndio Mkurugenzi wa Elimu Bakwata Makao Makuu na ndugu yake Mufti Abubakar Zuberi .Kampuni ambayo imepewa kuendesha shule kumi za Bakwata,ikiwemo shule ya Bondeni Secondary Arusha,kazi ambayo kimsingi ndio kazi ya Kurugenzi ya Elimu Bakwata Makao Makuu(kazi ya Mwalimu Ally).

Jambo hilo limeleta vurugu kubwa kwa waislamu kiasi cha baadhi yao kuamua kuamua kuwahamisha watoto wao wabaosima katika shule zinazoendeshwa na taasisi ya dini ya Bakwata wakidai kuwa kiwango cha elimu kimeshuka na usimamizi Wa shule hiyo umepungua

Kampuni ya Zaim ilianzishwa kinyemela na mufti zubari kwa kazi ya kuingia mkataba wa uendeshaji wa shule/vyuo vya Bakwata tu,isiyo na uzoefu wa uendeshaji wa shule au chuo chochote nchini.

Ni aibu kwa mkurugenzi wa Elimu Mwalimu Ally A. Ally baada ya kushindwa kuendesha shule na vyuo vya Bakwata kuamua kubinafsisha uendeshaji kwa kampuni yake binafsi iliyoundwa kwa kumtumia Bwana Abubakar Juma,kwa vile tu Mwalimu Ally yupo karibu na Mufti Abubakar Zubeir na undugu wake na Mufti Abubakar Zubeir.

Mwalimu Ally A. Ally ndio pia mkurugenzi wa Alharamain Islamic Seminary na Chuo cha Ualimu Alharamain,taasisi ambazo zimekuwa zinakopa fedha benki kwa kutumia dhamana mbalimbali za Bakwata,hata kupelekea madeni makubwa yasiyolipika toka Benki.

Mwalimu Ally A. Ally anatumia vibaya undugu wake na ukaribu wake na Mufti Abubakar kujitajirisha na kuwatesa walimu maskini ambao hawalipwi jasho lao halali,tena na taasisi kubwa ya dini Bakwata.
 

feitty

JF-Expert Member
Jul 10, 2015
2,045
2,000
Baadhi ya waislamu sijui wanamatatizo gani.
Badala ya kuweka juhudi kuziimarisha hizo shule ziwe na ufaulu mzuri wanazidi kuharibu na kuweka maslahi mbele.
Sijui wanasahau kuwa zinavyozidi kufanya vibaya hakuna mtu yuko tayari kupeleka mwanae sehemu yenye elimu mbovu bora kumpeleka kwenye shule za kanisa.
Hapo wazazi wakihamisha watoto watalalamika badala ya kufanya juhudi kuboresha wao wanaharibu.
Mfano mzuri hiyo Bondeni kuna kipindi ilikuwa hooiii naona sasa hivi wameirekebisha angalau ila wanakoelekea itarudi mulemule.
 

king suleman

JF-Expert Member
Jun 28, 2014
1,681
2,000
Alie Andika Uzi Ameandika Ki Shabiki Sana Yan Hakuna Hata Conclusion Ya Mtazamo Chanya Hata Kama Wewe C Dini Hyo
 

Mzee wa Masauti

JF-Expert Member
Jul 26, 2014
2,201
2,000
Baadhi ya waislamu sijui wanamatatizo gani.
Badala ya kuweka juhudi kuziimarisha hizo shule ziwe na ufaulu mzuri wanazidi kuharibu na kuweka maslahi mbele.
Sijui wanasahau kuwa zinavyozidi kufanya vibaya hakuna mtu yuko tayari kupeleka mwanae sehemu yenye elimu mbovu bora kumpeleka kwenye shule za kanisa.
Hapo wazazi wakihamisha watoto watalalamika badala ya kufanya juhudi kuboresha wao wanaharibu.
Mfano mzuri hiyo Bondeni kuna kipindi ilikuwa hooiii naona sasa hivi wameirekebisha angalau ila wanakoelekea itarudi mulemule.


Ukitaka kujua tabia ya mtu angalia marafiki zake. Huwezi kuwa na urafiki na viongozi wa CCM halafu usiwe mwizi. Utaiba tu!

Bakwata hawatuwakalishi waislam tena. Ni wanachama wa CCM chini ya mwamvuli wa bakwata.
 

The Bourne

JF-Expert Member
Aug 24, 2017
1,077
2,000
Muft Zuberi amewekwa tu pale hana kauli, ulishawi kuona chazi za Roma au Anglican zikisimamiwa na sirikali
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom