Waislamu Walioandamana waliomba kibali cha maandamano? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Waislamu Walioandamana waliomba kibali cha maandamano?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Lyamungo, Sep 8, 2012.

 1. Lyamungo

  Lyamungo Member

  #1
  Sep 8, 2012
  Joined: Aug 17, 2011
  Messages: 91
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Jana waislamu waliandamana kudai kuachiwa kwa wenzao walioshikiliwa kwa kukataa kuhesabiwa waachiwe, swali langu ni kuwa waliomba kibali? sensa ilikuwa imeisha?
   
 2. S

  Shansila Senior Member

  #2
  Sep 8, 2012
  Joined: Jan 28, 2012
  Messages: 189
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Ingawa haisemwi bayana lkn waliozuiwa kuandamana ni cdm tu...wengine ruksa.
   
 3. byembalilwa

  byembalilwa JF-Expert Member

  #3
  Sep 8, 2012
  Joined: Aug 7, 2012
  Messages: 1,538
  Likes Received: 353
  Trophy Points: 180
  tatizo maandamano ya cdm yanaandamana na KAFARA..
   
 4. RICH OIL SHEIKH

  RICH OIL SHEIKH JF-Expert Member

  #4
  Sep 8, 2012
  Joined: Jan 2, 2012
  Messages: 882
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Yale yalikuwa maandamano ya kimya kimya no kibali, no taarifa kwa vyombo vya habari: maana taarifa zingeenea kabla ya maandamano wahuni wa c*m wangevamia na kusababisha maafa. MISSION ACCOMPLISHED
   
 5. f

  filonos JF-Expert Member

  #5
  Sep 8, 2012
  Joined: Oct 13, 2011
  Messages: 651
  Likes Received: 70
  Trophy Points: 45
  mbona nyinyi CDM hamna shukrani inamaana tangu chama chenu kianzishwe hamjwai kuandama na mkaachiwa bila vikwazo?? au nyie mnataka lazima iwe wakati huu 2 hata hao WAISLAM walisha wai andamana wakati si muafaka nao pia walipigwa na kuuwawa na wengine ni VILEMA mpaka leo
   
 6. The Son of Man

  The Son of Man JF-Expert Member

  #6
  Sep 8, 2012
  Joined: Feb 9, 2010
  Messages: 12,124
  Likes Received: 1,709
  Trophy Points: 280
  Haya mambo ya tz ni very complicated na yenye kuleta hasira!!!!!!!
   
 7. RICH OIL SHEIKH

  RICH OIL SHEIKH JF-Expert Member

  #7
  Sep 8, 2012
  Joined: Jan 2, 2012
  Messages: 882
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Mkuu mi si mshabiki wa vyama (siko cdm/ccm/cuf); nadhani hujaelewa post yangu
   
 8. Echolima

  Echolima JF-Expert Member

  #8
  Sep 8, 2012
  Joined: Oct 28, 2007
  Messages: 3,169
  Likes Received: 531
  Trophy Points: 280
  Inaonekana hujaenda shule akili yako ina Mgando nenda hata Elimu ya watu wazima(Mgumbaru) ukatoe ujinga ili akili ya kufikiri KAFARA zikutoke.Ina maana mpaka sasa karne ya 21 bado unasumbuka na Makafara ndio maana Hatuendelei.
   
 9. BEDO NYALUTOGO

  BEDO NYALUTOGO JF-Expert Member

  #9
  Sep 8, 2012
  Joined: Aug 16, 2012
  Messages: 1,324
  Likes Received: 90
  Trophy Points: 145
  napita 2 wajomba shwar!!! am tired enough!!........
   
 10. Zak Malang

  Zak Malang JF-Expert Member

  #10
  Sep 8, 2012
  Joined: Dec 30, 2008
  Messages: 5,410
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  My take:

  Makala hii ilitoka Alhamisi, siku moja kabla ya tukio la maandamano ya Waisilamu jijini Dar. Mwandishi kaandika la kweli kabisa, ingawa inavyoaminika, msamiati ‘common sense' haumo katika shughuli za polisi wetu hapa TZ.


  Siku ya Ijumaa nilibahatiwa kuwapo karibu na maandamano hayo katika eneo la Jangwani nikiwa ndani ya daladala. Polisi walifanya jambo la busara sana kutoyaingilia ingawa walikuwa wamejitayarisha kwa kila kitu.

  Wangeingilia tu kujaribu kuwatawanya waandamanaji, maafa makubwa yangeweza kutokea hasa kutokana na mori kubwa waliokuwa nao waandamanaji. Magari yangevunjwa viyoo, ajali zingetokea na hata watu kuumia na kupoteza maisha.

  Ni kweli, polisi wakitumia busara huokoa maisha. Soma makala:
  [FONT=&amp]______________________________
  Mara nyingine polisi watumie busara kuokoa maisha
  [/FONT]


  NA HILAL K. SUED


  Jaji mstaafu Thomas Mihayo aliwahi kuizungumzia hali hili katika jamii, hali ambayo kwa bahati mbaya imekuwa ikiachwa tu kuendelea kwa kasi bila hatua madhubuti kuchukuliwa.

  Wakati akichangia mada kwenye mkutano wa Chama cha Majaji Wastaafu (Tanzania Retired Judges Association – TARJA mwishoni mwa mwaka jana, Judge Mihayo alisema jamii inashuhudia utamaduni mpya na wa hatari sana ambao polepole umekuwa ukijisimika nchini.

  Alisema "ni utamaduni wa jeuri na wa kutoheshimu utawala wa sheria, haki za binadamu na utawala bora. Utamaduni wa kuwazawadia wanaoendekeza maovu haya. Utamaduni wa kutojali athari zake." Na kibaya zaidi, aliongeza kusema, "ni utamaduni wa kuwazawadia au kuwasifia watu ambao huvunja sheria na kuwaachia hivi hivi."

  Aliongeza: "Na kama vile maovu hayo yote hayatoshi, ni utamaduni wa kukwepa au kukataa waziwazi kuwajibika pale ambapo viongozi na/au asasi wanazoziongaza wanakuwa vichwa ngumu katika utendaji wao, hawafuati sheria na hata kutenda jinai au kufanya uzembe wa kuweza kwao kutiwa hatiani – hasa pale matokeo ya vitendo vyao husababisha vifo vya watu na uharibifu wa mali – mfano matukio ya MV Bukoba, Mabomu ya Mbagala na Gongo la Mboto, maafa ya Meli ya Zanzibar iliyozama na kadhalika."

  Na mapema wiki hii baada ya tukio la kifo cha mwandishi wa Channel Ten Daudi Mwangosi, Jaji Mihayo amesikika tena, safari hii katika mahojiano ya kipindi cha Channel Ten cha ‘Jenerali on Monday."

  Alisema katika miaka ya 70 polisi walikuwa wanawajibishwa vilivyo kwa matendo yao, hasa wanaposababisha vifo vya raia wakiwa mikononi mwao, bila sababu za msingi. Alisema maafisa wa polisi wa vyeo vya juu na wale wa Idara ya Usalama walikamatwa na kushitakiwa mahakamani kwa makosa ya utesaji wa raia na hata kwasababishia vifo katika mikoa ya kanda ya Ziwa (Shinyanga na Mwanza). Alisema leo hii haiwezekani kwa serikali iliyopo kuchukuwa hatua kama hizo.

  Kwa kuongezea, mwendesha kipindi, Jeneral Ulimwengu alisema enzi hizo hizo Inspekta Jenerali wa Polisi (IGP) Hamza Azizi, akiwa anaendesha gari lake usiku alimgonga mtu mmoja ambaye alikufa hapo hapo. Hakujali kitu na hata hakuripoti polisi usiku ule hadi siku ya pili yake, bila shaka baada ya kushauriwa na maafisa wenzake ndipo alipokwenda kutoa ripoti polisi.

  Rais Julius Nyerere alimvua madaraka kwa kosa la kutowajibika ipasavyo. Leo hii, Jenrali Ulimwengu alisema, kitu kama hiki hakiwezi kamwe kutokea. Badala yake ni kinyume chake.

  Alisema "miezi michache tu baada ya polisi kuuwa kwa risasi makumi ya wafuasi wa CUF wasiokuwa na silaha ambao walikuwa wakiandamana huko Pemba, rais Benjamin Mkapa aliwapandisha vyeo maafisa wa polisi, wakiwemo wale waliohusika katika tukio lile."

  Hivyo tusitegemee afisa yeyote wa polisi kuwajibishwa katika tukio la kifo cha Daudi Mwangosi. Kama alivyotamka Jaji Mihayo kuhusu utamaduni uliozoeleka, huenda baadhi yao wakazawadiwa kwa kupandishwa vyeo. Hakuna haja ya kusema kwamba jamiii inachukizwa sana na tabia hii. Huenda wanaonufaika, kwa namna fulani, au tuseme kwa matarajio fulani, ni wanasiasa walio madarakani.

  Lakini hapo hapo kuna hoja moja inayotolewa, na hii naiweka kama swali: "Jee, iwapo wale polisi, idadi yao kama saba hivi, waliomzunguka marehemu Mwangosi katika dakika zake za mwisho za uhai ambao walionyeshwa kwenye picha kadha magazetini – wangekuwa ni waandishi wa habari, na anayeuwawa angekuwa ni polisi, ingekuwaje? Wakati huu hao ‘waandishi' saba wangekuwa lupango, iwapo wangekuwa hai.

  Na kwa upande mwingine, inanishangaza kidogo kwamba hadi naandika makala hii, hakuna mtu yoyote amepelekwa mahakamani kuhusiana na kifo cha Mwangosi. Hii ni kinyume cha utaratibu uliozoeleka siku hizi wa mamlaka za serikali kuziba midomo ya vyombo vya habari visiendelee kulizungumzia suala ambalo linaiweka serikali pabaya. Tumeona hili likifanyika katika sakata la Dr Steven Ulimboka. Lakini huenda hatua kama hiyo iko mbioni.

  Hata hivyo ule uundwaji wa tume itakayochunguza mazingira ya kifo hicho unaiondolea serikali joto (heat) linaloizingira na kuweza kupumua angalau kwa muda kuhusu tukio hilo ambalo pia tunaweza kuliita ni kashfa nyingine iliyoikumba mamlaka ya serikali.

  Ni vigumu kwa polisi kukwepa hili – kwamba Mwangosi alikufa akiwa mikononi mwa maafisa na askari wa polisi. Kuna umuhimu wa kuwapo hatua za kimakusudi za kulisafisha jeshi la polisi kwa maana yakulipa muelekeo uliokuwa umepotea.

  Wengi wanasema tatizo kubwa ni kwamba jeshi hili limeingiliwa sana na wanasiasa, au pengine lenyewe ndiyo ‘limekubali' kujisalimisha kwa wanasiasa. Na ninaposema wanasiasa nina maana ya wale walio madarakani. Na hii bila shaka ni kutokana matarajio ya utawala na watawala ya ‘kulindwa' – hasa katika mazingira haya ya mfumo huu wa ushindani mkubwa wa siasa za vyama vingi.

  Kwa mfano kwa kiasi kikubwa hali hii hujitokeza wakati wa kampeni za uchaguzi – ambapo ni rahisi kubaini jeshi la polisi linaegemea upande gani.

  Nitaoa mfano uliotokea. Katika uchaguzi wa mwaka 2000, Chama cha Wananch – CUF kilifanya mkutano wake mkubwa wa kufunga kampeni katika viwanja vya Jangwani, mkutano ambao kusema lile la ukweli kabisa haujafikiwa na mkutano wa chama chochote kingine kwa umati mkubwa wa wahudhuriaji.

  Polisi, kama kawaida, walikataza maandamano yoyote ya kwenda mkutanoni au kutoka mkutanoni na walisistiza kwamba watu wasiondoke kwa makundi – yaani kila mtu aondoke peke yake.

  Akili ya kuzaliwa (common sense) itaonyesha waziwazi kwamba amri hii ya polisi – ya kuondoka mkutanon mmoja mmoja – haiwezekani hasa ikizingatiwa kwamba giza lilikuwa laanza kukaribia wakati mkutano ulipomalizika na kila mtu alitaka kurejea nyumbani kwake kwa haraka. Isingewezekana umati ule uondoke kwa namna polisi walivyotaka na hivyo makundi makundi yalikuwa lazima.

  Ghafla polisi wa kuzuia fujo (FFU) walianza kurusha mabomu ya machozi ili kutawanya watu wakati wakiondoka mkutanoni na hivyo kuzuka tafrani kubwa. Bahati nzuri hakuna aliyepoteza maisha ingawa kuna wengi waliumia, hasa wazee na wanawake.

  Hakukuwa na sababu za msingi kwa polisi kufanya vile isipokwa katika kuonyesha tu CUF ilikuwa ni chama cha vurugu. Hali hii sasa imehamia kwa Chadema. Chama chochote cha siasa kinachojitokeza kuwa tishio kwa CCM, baso mikakati hufanywa kukionyesha ni chama cha vurugu. Tuliona kwa NCCR-Mageuzi katika miaka ya 90, baadaye CUF na sasa Chadema.

  Vifo vya raia wasiohusika au kujeruhiwa kwa watu visingekuwa vinatokea iwapo polisi wangekuwa wanatumia busara kidogo. Tuwe wakweli hapa – tukio la kifo cha Mwangosi, hivi ilikuwa lazima kwa polisi kutumia nguvu yote ile? Narudia – tuwe wakweli, tusijikite tu katika ile hoja inayopigiwa debe sana – kwamba amri ya polisi ni lazima itiiwe -- liwalo na liwe.

  Hivi ni kweli msimamo wa aina hii hauna mbadala hata kama kuna watu wanaoweza kupoteza maisha? Kwani polisi siyo kazi yao kulinda usalama wa raia na mali zao kila inapowezekana na siyo kusababisha vifo vya raia hata pale vinavyoweza kuepushwa? Au jeshi la polisi hujisikia linadharauliwa vibaya sana pale amri yake yoyote ile inapokiukwa?

  Mimi nadhani polisi hufundishwa kwamba mara nyingine ni vyema kuweka pembeni amri na badala yake kutumia busara, kulingana na mazingira ya hali kadri inavyojitokeza. Naamini pia mara nyingine polisi hutakiwa kulegeza amri zao na kurudi nyuma kuokoa maisha yao na ya watu wengine kuliko kukazania kufanya lile walilolitolea amri.

  Juzi juzi nilisoma habari moja kuhusu kikundi cha wanahabari wa Chama cha Waandishi wa Habari za Mazingira (JET) wakiongozana na polisi wenye silaha waliokwenda sehemu moja mkoani Kilimanjaro kukagua uharibifu wa mazingira na vyanzo vya maji unaofanywa na wakazi wa sehemu hiyo.

  Walipofika eneo hilo wakazi waliutilia shaka ujio wao na walifikiri walikuwa na lengo la kutaka kuwapora ardhi yao. Walianza kukizingira kikundi hicho, wengi wao wakibeba silaha za jadi na wengine za moto.

  Pamoja na polisi kuamrisha warudi nyuma na pia kufyatua risasi hewani, wenyeji hao walizidi kusonga mbele. Ndipo polisi walipotoa amri kwa waandishi kupanda gari lao na kukimbia kwa haraka.

  Laiti polisi wangekazania kupambana nao, bila shaka kuna maafa yangetokea, hivyo ilikuwa ni maamuzi ya busara sana kwa polisi kulikimbia eneo hilo.

  Source: Rai
   
 11. Ufipa-Kinondoni

  Ufipa-Kinondoni JF-Expert Member

  #11
  Sep 8, 2012
  Joined: Jan 3, 2012
  Messages: 4,488
  Likes Received: 2,147
  Trophy Points: 280
  Polisi wote ni anti-CDM. Hivyo, hawakuona sababu ya kupinga kitu kisichowapinga CCM. Usitalajie kuona mtelemko katika mikutano ya CDM.

  CDM inawatisha polisi, waislamu, Jk na serikali yao.

  Kumbuka kuwa, shetani hawezi kumfukuza shetani mwenzake na waarabu wa pemba huju..........................vilemba.
   
 12. B

  B.Panther Member

  #12
  Sep 8, 2012
  Joined: Jun 5, 2012
  Messages: 52
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  kooooooooooooooooooooooooooti
   
 13. MZIMU

  MZIMU JF-Expert Member

  #13
  Sep 8, 2012
  Joined: Apr 29, 2011
  Messages: 4,080
  Likes Received: 30
  Trophy Points: 145
  Maandamano ya kweli sikuzote hayaombewi kibali. Na ndio maana maandamano haya yalifanikiwa kwani kama mtu yoyote angeyaingilia tungamaliza kesi zetu zote jana.
   
 14. AdvocateFi

  AdvocateFi JF-Expert Member

  #14
  Sep 8, 2012
  Joined: Jan 15, 2012
  Messages: 10,705
  Likes Received: 592
  Trophy Points: 280
  Kafara za CDM je zinazidi zile ambazo zinatolewagwa na wakina shehk ponda kwenye majini wanayoyafuga? Je zinazidi zile ambazo mausatdh mnazotoaga kwenye mabasi yenu kama ya Abood, shabby, ?

  THINK BIG.
   
Loading...