Waislamu Walazimishwa Kula Nguruwe Ili Ziwape Nguvu | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Waislamu Walazimishwa Kula Nguruwe Ili Ziwape Nguvu

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by MziziMkavu, May 14, 2010.

 1. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #1
  May 14, 2010
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,620
  Likes Received: 4,609
  Trophy Points: 280
  [​IMG]

  Wanawake watatu wa kiislamu toka nchini Indonesia walilazimishwa na bosi wao katika kiwanda cha nguo nchini Taiwan wale nyama ya nguruwe ili ziwape nguvu na stamina ya kufanya kazi. Wanawake watatu wa kiislamu ambao ni raia wa Indonesia, walilazimishwa na bosi wao katika kiwanda cha nguo mjini Taipei wale nyama ya nguruwe au la mishahara yao itapunguzwa.

  Kwa muda wa miezi saba wanawake hao walilazimishwa na bosi wao kula vyakula vyenye nyama ya nguruwe vilivyokuwa vikigaiwa kwa wafanyakazi wa kiwanda hicho kwakuwa bosi wa kiwanda hicho alikuwa akiamini kuwa nyama ya nguruwe ingewapa nguvu na stamina ya kufanya kazi wanawake hao.

  Bosi wa kiwanda cha nguo cha Shin Hua Hang Fashion Co, Chang Wen-lin amefikishwa mahakamani kwa kuwalazimisha wanawake hao wale nyama ya nguruwe katika kipindi cha ajira yao kuanzia mwezi septemba 2008 hadi April 2009.

  Katika jalada la kesi aliyofunguliwa mahakamani, Cheng aliamini kuwa nyama ya
  nguruwe ingewapa stamina ya kufanya kazi wanawake hao na alitishia kuwakata mishahara yao iwapo wasingekubali kula nyama hiyo.

  Waendesha mashtaka wanataka Chang Wen-Lin ahukumiwe kwenda jela miezi minane.

  Wanawake hao walipelekea malalamiko yao kwa taasisi ya kutetea wafanyakazi mjini Taipei ambapo walisema kuwa walifanyishwa kazi nyingi kuliko kawaida katika kipindi cha miezi minane bila ya kulipwa chochote.

  Taasisi hiyo ndiyo ililifikisha suala hilo mahakamani kwa niaba ya wanawake hao ambao kutokana na hofu za masuala ya uhamiaji walikuwa wakihofia kurudishwa kwao iwapo wangemchukulia hatua bosi wao.

  Wanawake hao hivi sasa wametafutiwa kazi kwenye kampuni nyingine mjini Taipei.

  Kuna vibarua takribani 350,000 nchini Taiwan ambapo wengi wao wanatoka Indonesia, Philippines na Vietnam.

  Katika ripoti ya mwaka 2009 ya haki za binadamu duniani, tatizo kubwa lililotajwa kuikabili Taiwan lilikuwa ni unyanyasaji wa wafanyakazi makazini.

  Ripoti hiyo ilisema kuwa wafanyakazi wengi huogopa kuripoti matatizo yanayowakabili kwa kuhofia kupoteza ajira zao.

  http://www.nifahamishe.com/NewsDetails.aspx?NewsID=4477782&&Cat=2
   
 2. s

  sijafulia Member

  #2
  May 14, 2010
  Joined: Mar 26, 2010
  Messages: 86
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Aiseeeeee mzzizi mkavu uko no co
  no comments kweliiiiiiiiiiiii
   
 3. B

  Bull JF-Expert Member

  #3
  May 14, 2010
  Joined: Nov 4, 2008
  Messages: 984
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hivi inaleta stamina au inaleta HOMA YA NGURUWE
   
 4. Abdulhalim

  Abdulhalim JF-Expert Member

  #4
  May 14, 2010
  Joined: Jul 20, 2007
  Messages: 16,472
  Likes Received: 125
  Trophy Points: 160
  Hata Waarabu wananyanyasa migrant workers vilevile.
   
 5. B

  Bull JF-Expert Member

  #5
  May 14, 2010
  Joined: Nov 4, 2008
  Messages: 984
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0

  Sasa una justify nini hapo?
   
 6. drphone

  drphone JF-Expert Member

  #6
  May 15, 2010
  Joined: Sep 29, 2009
  Messages: 3,563
  Likes Received: 29
  Trophy Points: 145
  yani huyo boss poa sana kitimoto ni kama viagra ati
   
 7. Abdulhalim

  Abdulhalim JF-Expert Member

  #7
  May 15, 2010
  Joined: Jul 20, 2007
  Messages: 16,472
  Likes Received: 125
  Trophy Points: 160
  Wapi nimejustify?
   
 8. m

  marymar Member

  #8
  May 15, 2010
  Joined: Apr 22, 2010
  Messages: 18
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  It means before walikuwa hawana nguvu ya kufanya kazi? na aliwaajiri vp? that iz not fare
   
 9. P

  Percival JF-Expert Member

  #9
  May 15, 2010
  Joined: Mar 23, 2010
  Messages: 2,565
  Likes Received: 617
  Trophy Points: 280
  Arab mistreat migrant worker and that justify Taiwanese to mistreat Indonesian. What a logic ? they are both bad - just concentrate on issue and stop beating around the bush and divert the topic. Start another one if you have.
   
 10. Abdulhalim

  Abdulhalim JF-Expert Member

  #10
  May 15, 2010
  Joined: Jul 20, 2007
  Messages: 16,472
  Likes Received: 125
  Trophy Points: 160
  Usidandie gari kwa mbee wala usikurupukie posts ambazo huzielewi dugu zaidi ya kuonekana kituko.
   
Loading...