Waislamu Wakasirishwa na Wimbo wa Timu ya Soka ya Ujerumani | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Waislamu Wakasirishwa na Wimbo wa Timu ya Soka ya Ujerumani

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Bikra, Aug 6, 2009.

 1. Bikra

  Bikra Senior Member

  #1
  Aug 6, 2009
  Joined: May 13, 2009
  Messages: 103
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  Wimbo ulioimbwa na mashabiki wa timu ya soka ya Ujerumani ya FC Schalke 04 inayoshiriki ligi kuu nchini humo umewakasirisha waislamu baada ya mashabiki hao kumhusisha mtume Muhammad katika nyimbo yao.
  Washabiki wa FC Schalke 04 ambayo inashiriki ligi kuu ya Ujerumani, Bundesliga wamewakasirisha waislamu kwa kumuimba mtume Muhammad katika nyimbo yao ya kuishangilia timu yao.

  Ubeti wa tatu wa wimbo huo ulikuwa na maneno "Muhammad alikuwa ni mtume ambaye alikuwa hajui chochote kuhusiana na soka".

  "Lakini katika rangi zote nzuri duniani, alipenda rangi ya Bluu na Nyeupe (rangi za timu ya Schalke)".

  Klabu hiyo ilitumiwa mamia ya email toka kwa waislamu wenye hasira baada ya vyombo vya habari vya Uturuki kutoa ripoti za wimbo huo.

  Polisi wa mji wa Gelsenkirchen, inapotokea timu hiyo, walisema kuwa wameyapokea na wanayachunguza malalamiko ya waislamu kwa umakini zaidi.

  Mkuu wa baraza la waislamu wa Ujerumani, Aiman Mazyek, alisema kuwa baraza la waisalamu halina mpango wa kuupiga marufuku wimbo hao lakini linataka maelezo zaidi kujua chanzo na sababu za kutolewa kwa wimbo huo.

  Website ya shirika la habari la Ujerumani, Deutsche Welle ilisema kwamba wimbo huo unaoitwa "Bluu na nyeupe, jinsi ninavyokupenda" ulitungwa mwaka 1924 lakini haijulikani ni lini ubeti unaomzungumzia mtume uliingizwa kwenye wimbo huo.

  Klabu ya FC Schalke 04 ilisema kuwa imepokea malalamiko mengi kwa njia ya email na simu na wanayafanyia kazi malalamiko hayo baada ya waislamu kutishia kuanzisha kampeni za kususia mechi za timu hiyo iwapo wimbo huo hautafutwa au ubeti huo kuondolewa katika wimbo huo.

  FC Schalke 04 imewaomba wanazuoni wa kiislamu nchini humo waupitie tena wimbo huo kujua kama unaukashifu uislamu au la.
   
 2. M

  Mugishagwe JF-Expert Member

  #2
  Aug 7, 2009
  Joined: Apr 28, 2006
  Messages: 295
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Waislam hao ambao wanataka kususia mechi hizo wako wangapi hadi watake wasikilizwe ? Je ni kweli Muhammed aliijua soka ?
   
 3. Mateso

  Mateso JF-Expert Member

  #3
  Aug 7, 2009
  Joined: Aug 6, 2008
  Messages: 244
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Kinachowaudhi nini? Kwa uelewa wangu ni kwamba si mtume mohamed tu hakuwa na habari na mpira wa miguu ILA NI WOTE WALIOISHI KIPINDI HICHO kwa maana wakati huo mpira wa miguu haukuwepo. Vile vile hawa mashabiki wanajivunia kuvaa jezi zenye rangi alizozipenda mtume ambazo ni bluu na nyeupe. Kwa namna nyingine wanajiita wajukuu wa Mtume. Sasa wanaolalamika wanalalamikia nini? Nafikiri watu huwa wanasoma bila kutafakari au kusasambua waliyosoma. ACHENI HIZO.
   
 4. Mponjoli

  Mponjoli JF-Expert Member

  #4
  Aug 7, 2009
  Joined: Feb 29, 2008
  Messages: 668
  Likes Received: 13
  Trophy Points: 35
  Mambo mengine ndugu zangu yanapitiliza. Kama alikuwa hajui lolote kuhusu soka mbona ni kitu cha kawaida?
   
 5. PakaJimmy

  PakaJimmy JF-Expert Member

  #5
  Aug 7, 2009
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 16,236
  Likes Received: 309
  Trophy Points: 180
  Achaneni na hawa watu wa kulalamikia kila kitu!

  Ukisema ukweli wanalialia, ukidanganya maandamano! Lipi jema kwa hawa ndugu zetu?

  Kwa kweli nawahurumia sana watu wenye position za kutoa statement au mihadhara kwa hawa ndugu, maana wanahitaji kujiandaa mno, ukibadili hata nukta, au penye `b uweke `c , basi jioni yake maandamano!

  Kwa mimi binafsi nisingeweza!
   
 6. K

  Kakalende JF-Expert Member

  #6
  Aug 7, 2009
  Joined: Dec 1, 2006
  Messages: 3,259
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 135
  Maneno yenyewe hayaonyeshi kashfa yoyote lakini yakiachiwa yaendelee inaweza kuwa mwanzo wa mizaha mingine ambayo huletea kugusa imani za watu na kuamsha hisia kali za waisilamu.
   
 7. Waberoya

  Waberoya Platinum Member

  #7
  Aug 7, 2009
  Joined: Aug 3, 2008
  Messages: 11,600
  Likes Received: 3,893
  Trophy Points: 280
  Thats how they are, dunia nzima siyo Tz tu, hii inatokana na bibi yao(mama Ishmael) kulalamika na kuondoka nyumbani mwa Ibrahim! so soku zote

  1. Wanaona wanaonewa
  2. Wanatafuta haki
  3.kutaka public attention
  4.kulinda dini kupitiliza(kumbuka ilienezwa kwa upanga)
  5.inferiority complex
  6. Uvivu wa kufikiri
  7.Kufikiri kuwa ukiilinda dini unaenda peponi ukienda peponi utapata wanawali bikra 7! na kuendeleza libeneke!
  8. Kutoelezana ukweli ndani yao wenyewe na wote wanotaka kuwafungua macho wanaonekana wabaya wanazabwa vibao haijalishi rais au nani

  observe them, read them this is how they are , mbaya haijalishi kama mtu amesoma au la!
   
Loading...