Waislamu wajizatiti kwa Uchaguzi Mkuu

Josh Michael

JF-Expert Member
Jun 12, 2009
2,523
77
Mufti aunda kamati kuwahamasisha nchi nzima

na Lucy Ngowi



VIJANA wa Kiislamu nchini wamehamasishwa kuchukua fomu za kugombea nafasi mbalimbali za uongozi nchini katika kipindi hiki cha kuelekea uchaguzi mkuu.
Wito huo umetolewa jana na Mwenyekiti wa Kamati ya Umoja wa Vijana wa Kiislamu Tanzania, Alhaji Sulle Seif, alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari katika Ofisi za Baraza la Waislamu Tanzania (BAKWATA), Dar es Salaam.
Alhaji Seif alisema lengo la kamati hiyo iliyoundwa na Mufti wa Tanzania, Sheikh Mkuu Issa bin Shaaban Simba, mwezi uliopita, ni kuhamasisha vijana wa Kiislamu ili waweze kuchukua fomu na kujiandikisha, pamoja na kujitokeza kugombea nafasi mbalimbali za kuomba uongozi katika uchaguzi mkuu ujao.
“Tunawahamasisha wasilale ili wawe viongozi. Kila Mtanzania ana haki ya kuchagua na kuchaguliwa. Kuanzia sasa vijana wa Kiislamu wasilale. Ombeni nafasi hizo ili mtumikie taifa kwa maendeleo ya taifa,” alisema Alhaji Seif.
Alisema hawatampigia debe kiongozi wa chama chochote cha siasa ila yule atakayeleta maendeleo ya taifa kwa uwiano wa kulinda maslahi ya taifa.
“Watu wanaweza kufikiri kuwa timu hii imeundwa kwa ajili ya kusaidia chama fulani. Si kweli, na hatuna lengo la kupigia debe chama fulani.
“Sisi tunafanya kazi na mtu yeyote kwa masharti ya Uislamu. Mtu atuhukumu kisiasa ikiwa tutafanya kazi kisiasa. Atuhukumu Kiislamu ikiwa tutafanya kazi Kiislamu,” alisema.
Alisema lengo la kamati hiyo ni pamoja na kutembelea mikoa yote ya Tanzania na kuunda kamati za mikoa, wilaya, kata na misikiti. Alisema jukumu la pili ni kuunda rasimu ya muongozo ya umoja wa vijana nchini, pamoja na kuitisha mkutano mkuu wa umoja huo kitaifa. Kamati hiyo iliundwa na Mufti Simba ikiwa na wajumbe wanane kama mkakati wa kuwahamasisha vijana wa Kiislamu kushiriki na kutumia vema haki yao ya kiraia bila kudhulumu au kubagua imani za watu wengine.


h.sep3.gif


juu
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom