Waislamu Waamua kumwaga Ugali baada ya CCM kumwaga Mboga

unaposema waislamu as if ni wote-kumbe ni kikundi cha watu wachache wenye hayo mawazo-rais na makamu wake wenyewe waislam-unategemea hawa wakae upande gani?achen kulalama fanye ni mambo ya msingi-wameshindwa ISS na wengne mtaweza nyie?
 
Ningekuwa kiongozi wa UKAWA, nisingeruhusu hii propaganda. Huwezi kujenga taifa ukianza na kulibomoa vipande vipande kwa misingi ya dini kwani ndiyo mwelekeo wa ukabila na mwishowe mgawanayo waukanda kama inavyotangazawa na CCM.
 
t
Muakilishi wa Taasisi na Jumuia za Kiislamu amewataka Waislamu wote Nchini kupiga kura ya HAPANA katika kura ya Maoni ya kuidhinisha katiba Iliopendekezwa na CCM. Kiongozi huyo, ameyasema hayo jana Jangwani katika Mkutano wa Hadhara wa UKAWA wa kuwekeana Sahihi za makubaliano ya Ushirikiano wao wa Kisiasa.

Kiongozi huyo alikwenda mbali zaidi kwa kuwakumbusha Waislamu Madhila mbali mbali ambayo wamekua wakiyapata kupitia serekali ya CCM. Aliwakumbusha Waislamu Juu ya Maauwaji ya Mwembe chai na serekali kukataa kuunda Tume huru kubaiini ukweli wa tukio lile.

Vile vile alihusianisha Kifo cha Sheikh Kassim Bin Jumaa, aliekua akitoa Mawaidha katika Msikiti wa Mtoro Pale Kariakoo na Mateso aliopewa Mahabusu katika vurugu za Mabucha ya Nguruwe ikiwa yeye hakuwepo Dar-es-salaam kabisa.

Vile vile aliwakumbusha waislamu vitendo vya Kulawitiwa Masheikh akiwemo Sheikh Mselem ambaya ni Mfasiri wa Qur-an Mahiri wakiwa Mahabusu za Polisi nchini. Amesema ushahidi wa hilo ulitolewa hadharani mbele ya hakimu wakionyesha nguo zao zilizo chafuka damu na Usaha.

Kama hilo halitoshi, aliwatonoshe kidonda waislamu Kwa kuwakumbusha tukio la kupigwa risasi Mtetezi wa haki wa zao, Sheiki Ponda Issa Ponda, na mtu anaedaiwa kuwa ni askari wa jeshi la Polisi na kukakamatwa nguvu nguvu akiwa hosipitali ya Muhimbili na kusomewa Mashitaka huku akiwa na Jeraha bichi. Wakamsweka Rumande hivyo hivyo na sasa amelemaa Mkono Uliopigwa risasi.

Tukio hilo alilifananisha na Tukio la kupigwa Risasi Muandishi wa Habari Daudi Mwangosi kama Muendelezo wa Kile kinachojulikana kama NTARAHAMWE politics.
Mheshimiwa Tundu Lissu alimalizia Msumari wa Mwisho kwenye Jeneza hilo la CCM kwa kuwajulisha Watanzania na Watanganyika kua, haki zote zilizo ainishwa katika katiba hiyo, zikiwemo haki za 50/50, haki za Wazee, Haki za Makundi Mbalimbali ni Usaniii Mtupu kwani kuna kipengele katika katiba hiyo(Sehemu ya NNE, Ibara ya 20 (2)) kinasema kua haki zote hizo hazitatambulika Mahakamani.

Someni vizuri hiyo sehemu hiyo na ibara hiyo ambayo inazungumzia Utekelezaji wa Malengo ya Kitaifa. Hicho kipengele kimefichwa vizuri sana.

Nilikuwepo Jangwani!.

attachment.php
tupatie mrejesho mkuu
 
Back
Top Bottom