Waislamu Waamua kumwaga Ugali baada ya CCM kumwaga Mboga

Muakilishi wa Taasisi na Jumuia za Kiislamu amewataka Waislamu wote Nchini kupiga kura ya HAPANA katika kura ya Maoni ya kuidhinisha katiba Iliopendekezwa na CCM. Kiongozi huyo, ameyasema hayo jana Jangwani katika Mkutano wa Hadhara wa UKAWA wa kuwekeana Sahihi za makubaliano ya Ushirikiano wao wa Kisiasa.

Kiongozi huyo alikwenda mbali zaidi kwa kuwakumbusha Waislamu Madhila mbali mbali ambayo wamekua wakiyapata kupitia serekali ya CCM. Aliwakumbusha Waislamu Juu ya Maauwaji ya Mwembe chai na serekali kukataa kuunda Tume huru kubaiini ukweli wa tukio lile.

Vile vile alihusianisha Kifo cha Sheikh Kassim Bin Jumaa, aliekua akitoa Mawaidha katika Msikiti wa Mtoro Pale Kariakoo na Mateso aliopewa Mahabusu katika vurugu za Mabucha ya Nguruwe ikiwa yeye hakuwepo Dar-es-salaam kabisa.

Vile vile aliwakumbusha waislamu vitendo vya Kulawitiwa Masheikh akiwemo Sheikh Mselem ambaya ni Mfasiri wa Qur-an Mahiri wakiwa Mahabusu za Polisi nchini. Amesema ushahidi wa hilo ulitolewa hadharani mbele ya hakimu wakionyesha nguo zao zilizo chafuka damu na Usaha.

Kama hilo halitoshi, aliwatonoshe kidonda waislamu Kwa kuwakumbusha tukio la kupigwa risasi Mtetezi wa haki wa zao, Sheiki Ponda Issa Ponda, na mtu anaedaiwa kuwa ni askari wa jeshi la Polisi na kukakamatwa nguvu nguvu akiwa hosipitali ya Muhimbili na kusomewa Mashitaka huku akiwa na Jeraha bichi. Wakamsweka Rumande hivyo hivyo na sasa amelemaa Mkono Uliopigwa risasi.

Tukio hilo alilifananisha na Tukio la kupigwa Risasi Muandishi wa Habari Daudi Mwangosi kama Muendelezo wa Kile kinachojulikana kama NTARAHAMWE politics.
Mheshimiwa Tundu Lissu alimalizia Msumari wa Mwisho kwenye Jeneza hilo la CCM kwa kuwajulisha Watanzania na Watanganyika kua, haki zote zilizo ainishwa katika katiba hiyo, zikiwemo haki za 50/50, haki za Wazee, Haki za Makundi Mbalimbali ni Usaniii Mtupu kwani kuna kipengele katika katiba hiyo(Sehemu ya NNE, Ibara ya 20 (2)) kinasema kua haki zote hizo hazitatambulika Mahakamani.

Someni vizuri hiyo sehemu hiyo na ibara hiyo ambayo inazungumzia Utekelezaji wa Malengo ya Kitaifa. Hicho kipengele kimefichwa vizuri sana.

Nilikuwepo Jangwani!.

attachment.php

Hizo ni propaganda tu wala asiwasemee waislam. Alikaa nao wapi. Anakumbusha machungu ili aonekane na yeye kwenye mgao anafaa. Wote UKAWA ni wasaka tonge.
 
Kwani UKAWA ni kikundi cha kidini? Huyu mwakilishi wa dini alikuwa anataka nini kwa wanasiasa au UKAWA ndiyo walimwita.

lakini watu wa UKAWA wana dini zao, na wengine pia tunaheshimu dini, haijalishi ni ya aina gani.
kwa hiyo dini ina nguvu katika hili
 
Kwa hiyo hoja yako ni ipi mkuu?

Hiyo ni sura ya nne, ambayo inaongelea Malengo ya kitaifa na haki mbalimbali zilizo gawiwa kama njugu, lakini mwisho wa siku zikapigwa pini na ibara hiyo.
 
.....ibara ya 20 (2)
(2) Masharti ya Sura hii hayatatiliwa nguvu ya kisheria na Mahakama
yoyote. Mahakama yoyote nchini haitakuwa na uwezo wa kuamua juu ya
suala kama kutenda au kukosa kutenda jambo kwa mtu au mahakama yoyote
au kama sheria au hukumu yoyote inaambatana na masharti ya Sura hii.
Mkuu,
Kasome vizuri kifungu hicho kwenye Rasimu ya MWISHO ya Katiba inayopendekezwa utajigundua umepotosha! Hata hivyo nitakusamehe bure kwa kuwa Rasimu zimekuwa nyingi inaweza kuleta confusion! Namshangaa hadi kinara wa UKAWA Tundu Lissu naye amenukuu vibaya kama ulivyofanya wewe! Huyu naye tunamsamehe bure maana alikimbia mjadala Bungeni hajui kilichoendelea!
 
we ------ acha uchochezi wa kidin waislam gani unaozungumzia mbona mm ni muislam lakin nshaona ukawa ni wapuuzi mi naitambua chadema siitambui ukawa bwana acheni ushoga waislam wengine tunaikubali katiba
 
Yap, tulipinge lakini tusilifanye mtaji wa kisiasa!
Hilo ni sawa kabisa hili suala ni vyema lifanyiwe mtaji ili tupate faida hapa.Chama cha CCM pamoja na hii serikali ya sasa iliyo madarakani ,kwepo kwake madarakani kumechangiwa zaidi na waumini wa dini ya kiislam na sasa kutokana na hizo taarifa za kidhalimu zilizofanywa na hii serikali chini ya chama cha ccm mimi binafsi nafikiria huu ndio muda muafaka wa kubadili views za waislam kuhusu hichi chama.Lazima waislam wote nchini wamjue adui yao ni yupi ili wengi wao waamue kujikita kwa vyama vingine vya upinzani kama vile cdm ambacho ndicho kiko tayari kuchukua uongozi nchini hivi karibuni.
Waislam huu ndio wakati wao wa kulipiza kisasi kwa kwenda kinyume na ccm ,hata ndani ya kitabu chao cha dini wameruhusiwa kulipiza kisasi na kuna sura nzima iliteremshwa kuhusu kulipiza kisasi.Hebu fikirieni sheikh mzima alawitiwe,sijui hiyo jeuri waliitoa wapi mpaka kufikia kufanya hivyo.Ile misemo yote aliyoitunga marehemu mzee Kambarage Nyerere yenye lengo la kukijenga chama chake sasa tungeanza kuirudisha na kuitumia kukivunja chama tawala.Kwa mfano,"Amka wakati ni huu"hii tunaweza kuitumia ktk kuhamasisha watu ili kuziamsha hisia na mioyo yao dhidi ya chama tawala.Najuwa kuna baadhi ya watu hawawezi kufurahia hii thread yangu lakini ukweli ni kwamba hichi chama umefikia wakati wa kupigwa vita na waislam,hakiwezi kucheza na waislam namna hii na tukaendelea kukipatia votes zetu.Enough is enough.M/Mpamba.
 
wenye roho mbaya wanajaribu kuipaka matope CCM, hii ni sawa na kuizuia mvua isinyeshe utaishia tu kupigwa radi. Mkisoma habari humu mjaribu kuzifanyia utafiti kwanza kabla ya kuchangia mada. hii ni tahadhari tu usije ukakimbiza kuku umevaa taulo
 
wenye roho mbaya wanajaribu kuipaka matope CCM, hii ni sawa na kuizuia mvua isinyeshe utaishia tu kupigwa radi. Mkisoma habari humu mjaribu kuzifanyia utafiti kwanza kabla ya kuchangia mada. hii ni tahadhari tu usije ukakimbiza kuku umevaa taulo
ccm ni sawa mgonjwa yupo ICU muda wowote anaweza kufa.
 
They can go to Saudia and practice Sharia/Kadhi et all, but not in Tanzania.
 
Back
Top Bottom