Waislamu Waamua kumwaga Ugali baada ya CCM kumwaga Mboga

MZIMU

JF-Expert Member
Apr 29, 2011
4,057
1,371
Muakilishi wa Taasisi na Jumuia za Kiislamu amewataka Waislamu wote Nchini kupiga kura ya HAPANA katika kura ya Maoni ya kuidhinisha katiba Iliopendekezwa na CCM. Kiongozi huyo, ameyasema hayo jana Jangwani katika Mkutano wa Hadhara wa UKAWA wa kuwekeana Sahihi za makubaliano ya Ushirikiano wao wa Kisiasa.

Kiongozi huyo alikwenda mbali zaidi kwa kuwakumbusha Waislamu Madhila mbali mbali ambayo wamekua wakiyapata kupitia serekali ya CCM. Aliwakumbusha Waislamu Juu ya Maauwaji ya Mwembe chai na serekali kukataa kuunda Tume huru kubaiini ukweli wa tukio lile.

Vile vile alihusianisha Kifo cha Sheikh Kassim Bin Jumaa, aliekua akitoa Mawaidha katika Msikiti wa Mtoro Pale Kariakoo na Mateso aliopewa Mahabusu katika vurugu za Mabucha ya Nguruwe ikiwa yeye hakuwepo Dar-es-salaam kabisa.

Vile vile aliwakumbusha waislamu vitendo vya Kulawitiwa Masheikh akiwemo Sheikh Mselem ambaya ni Mfasiri wa Qur-an Mahiri wakiwa Mahabusu za Polisi nchini. Amesema ushahidi wa hilo ulitolewa hadharani mbele ya hakimu wakionyesha nguo zao zilizo chafuka damu na Usaha.

Kama hilo halitoshi, aliwatonoshe kidonda waislamu Kwa kuwakumbusha tukio la kupigwa risasi Mtetezi wa haki wa zao, Sheiki Ponda Issa Ponda, na mtu anaedaiwa kuwa ni askari wa jeshi la Polisi na kukakamatwa nguvu nguvu akiwa hosipitali ya Muhimbili na kusomewa Mashitaka huku akiwa na Jeraha bichi. Wakamsweka Rumande hivyo hivyo na sasa amelemaa Mkono Uliopigwa risasi.

Tukio hilo alilifananisha na Tukio la kupigwa Risasi Muandishi wa Habari Daudi Mwangosi kama Muendelezo wa Kile kinachojulikana kama NTARAHAMWE politics.
Mheshimiwa Tundu Lissu alimalizia Msumari wa Mwisho kwenye Jeneza hilo la CCM kwa kuwajulisha Watanzania na Watanganyika kua, haki zote zilizo ainishwa katika katiba hiyo, zikiwemo haki za 50/50, haki za Wazee, Haki za Makundi Mbalimbali ni Usaniii Mtupu kwani kuna kipengele katika katiba hiyo(Sehemu ya NNE, Ibara ya 20 (2)) kinasema kua haki zote hizo hazitatambulika Mahakamani.

Someni vizuri hiyo sehemu hiyo na ibara hiyo ambayo inazungumzia Utekelezaji wa Malengo ya Kitaifa. Hicho kipengele kimefichwa vizuri sana.

Nilikuwepo Jangwani!.

attachment.php
 
Do they care? As long as polisi wanaendelea kuwa wapambe wao, wataendeleza tu UKABURU wao kwa kutumia mbwa, polisi, risasi na mabomu kuendeleza ubabe wao
 
Kwani UKAWA ni kikundi cha kidini? Huyu mwakilishi wa dini alikuwa anataka nini kwa wanasiasa au UKAWA ndiyo walimwita.
 
UKAWA si chama cha siasa. Ni Umoja wa kutetea Katiba ya Wananchi. Katiba ya wananchi inayotetewa na ukawa si katiba ya wanasiasa ni katiba ya wataanzania wakiwemo wanasiasa, wasomi, wajinga, wagonjwa, wanataaluma, wanadini, wasio na dini, watoto, wazee, viongozi na waongozwa. Watanzania wote wakiwemo watu wa dini zote na wasio na dini.

Vyama vya siasa vina katiba zake na siyo hii inayozungumziwa hapa. Umeelewa?

Kwani ukawa ni kikundi cha kidini? Huyu mwakilishi wa dini alikuwa anataka nini kwa wanasiasa au ukawa ndiyo walimwita.
 
Halafu koma kutumia neno waislamu mbona mimi siko pamoja na ukawa.

Mhhh! Sasa Wewe kama Muislamu, nini Msimamo wako juu ya hayo Madhila yaliyowakuta na yanayo endelea kuwakuta Waislamu chini ya Serekali ya CCM bila kujali kama Msemaji jukwaa alilopata kutueleza hayo ni UKAWA au Sahani?
 
Kwahiyo wewe ndo mwislamu?

Sasa kama wewe au nyie na huyo shoga yako, Ni Waislamu, kuna ubaya gani kutetea haki za Waislamu pale unapopata Jukwaa la kusema hivyo, ikiwa ni UKAWA au Hotpot?. Muislamu hasa ambae sio Mnafiki kama nyinyi katu hawezi kurudisha nyuma Juhudi za Waislamu kutetea haki zao.
 
Ni sawa na kesi ya mbuzi upeleke kwa fisi,mnatumiwa.
 
Muungano wa UKAWA ndo kifo cha ccm wananchi tumeshapewa elimu na ss tutoa elimu kwa wenzetu kuipigia kura ya HAPANA rasimu ya ccm hatuwezi kuendelea kuvumilia upuuzi wa ccm tena .UKAWA NI TUMAINI LETU WATANZANIA WOTE.
 
Not anymore. This time tutachagua chama kitakacho tetea haki zetu. Enough with CCM. Wameshatudanganya sana. Wakizidiwa wanaweka wagombea Waislamu. Safari hiii sisi hatujali. Tunachagua UKAWA.
 
Muakilishi wa Taasisi na Jumuia za Kiislamu amewataka Waislamu wote Nchini kupiga kura ya HAPANA katika kura ya Maoni ya kuidhinisha katiba Iliopendekezwa na CCM. Kiongozi huyo, ameyasema hayo jana Jangwani katika Mkutano wa Hadhara wa UKAWA wa kuwekeana Sahihi za makubaliano ya Ushirikiano wao wa Kisiasa.

Kiongozi huyo alikwenda mbali zaidi kwa kuwakumbusha Waislamu Madhila mbali mbali ambayo wamekua wakiyapata kupitia serekali ya CCM. Aliwakumbusha Waislamu Juu ya Maauwaji ya Mwembe chai na serekali kukataa kuunda Tume huru kubaiini ukweli wa tukio lile.

Vile vile alihusianisha Kifo cha Sheikh Kassim Bin Jumaa, aliekua akitoa Mawaidha katika Msikiti wa Mtoro Pale Kariakoo na Mateso aliopewa Mahabusu katika vurugu za Mabucha ya Nguruwe ikiwa yeye hakuwepo Dar-es-salaam kabisa.

Vile vile aliwakumbusha waislamu vitendo vya Kulawitiwa Masheikh akiwemo Sheikh Mselem ambaya ni Mfasiri wa Qur-an Mahiri wakiwa Mahabusu za Polisi nchini. Amesema ushahidi wa hilo ulitolewa hadharani mbele ya hakimu wakionyesha nguo zao zilizo chafuka damu na Usaha.

Kama hilo halitoshi, aliwatonoshe kidonda waislamu Kwa kuwakumbusha tukio la kupigwa risasi Mtetezi wa haki wa zao, Sheiki Ponda Issa Ponda, na mtu anaedaiwa kuwa ni askari wa jeshi la Polisi na kukakamatwa nguvu nguvu akiwa hosipitali ya Muhimbili na kusomewa Mashitaka huku akiwa na Jeraha bichi. Wakamsweka Rumande hivyo hivyo na sasa amelemaa Mkono Uliopigwa risasi.

Tukio hilo alilifananisha na Tukio la kupigwa Risasi Muandishi wa Habari Daudi Mwangosi kama Muendelezo wa Kile kinachojulikana kama NTARAHAMWE politics.
Mheshimiwa Tundu Lissu alimalizia Msumari wa Mwisho kwenye Jeneza hilo la CCM kwa kuwajulisha Watanzania na Watanganyika kua, haki zote zilizo ainishwa katika katiba hiyo, zikiwemo haki za 50/50, haki za Wazee, Haki za Makundi Mbalimbali ni Usaniii Mtupu kwani kuna kipengele katika katiba hiyo(Sehemu ya NNE, Ibara ya 20 (2)) kinasema kua haki zote hizo hazitatambulika Mahakamani.

Someni vizuri hiyo sehemu hiyo na ibara hiyo ambayo inazungumzia Utekelezaji wa Malengo ya Kitaifa. Hicho kipengele kimefichwa vizuri sana.

Nilikuwepo Jangwani!.
Mbona hajazungumzia madhila ya Waislamu waliyopata toka kwa CHADEMA kumvulia Hijabu DC na pia kumweka Padre kuwa mgombea ili akiingia Ikulu akandamize Waislamu?
 
Muungano wa UKAWA ndo kifo cha ccm wananchi tumeshapewa elimu na ss tutoa elimu kwa wenzetu kuipigia kura ya HAPANA rasimu ya ccm hatuwezi kuendelea kuvumilia upuuzi wa ccm tena .UKAWA NI TUMAINI LETU WATANZANIA WOTE.
UKAWA ni tumaini la wana-UKAWA!
 
3 Reactions
Reply
Back
Top Bottom