Sinoni
JF-Expert Member
- May 16, 2011
- 6,187
- 10,664
Shirika la habari la AFP limemnukuu Kamishna Mkuu wa Haki za binadamu wa Umoja wa Mataifa akisema katika ripoti yake ya jana (Jumatatu) kuhusu kuvunjwa haki za Waislamu wa kabila la Rohingya huko Myanmar hususan kunyimwa haki ya kuwa raia, kufanyishwa kazi kwa kulazimishwa na kutenzwa nguvu pamoja na kukandamizwa kijinsia kuwa ni mambo ambayo yanaweza kuhessabiwa ni jinai na uvunjaji wa haki za binadamu dhidi ya Waislamu hao.
Kwa mujibu wa ripoti hiyo, kuna uwezekano vitendo vya jinai wanavyofanyiwa Waislamu hao na uwezekano wa kutokea mashambulizi mengine makubwa dhidi yao, vikahesabiwa kuwa ni uhalifu wa kitaasisi na ni jinai dhidi ya binadamu.
Serikali ya mabudha huko Myanmar inawanyima Waislamu haki yao ya kuwa raia na wanadai eti Waislamu hao ni wahajiri wanaoishi nchini humo kinyume cha sheria wakati Waislamu wanasema kuwa wamekuwa wakiishi nchini Myanmar kwa karne nyingi na hawajui nchi kuwa nchi yao isipokuwa Myanmar.
Ikumbukwe kuwa zaidi ya Waislamu laki moja wa kabila ya Rohingya walilazimika kukimbia makazi yao katika jimbo la Rakhine la magharibi mwa Myanmar baada ya mabudha wenye misimamo mikali kufanya mauaji ya kutisha dhidi ya Waislamu hao mwaka 2012.