Waislamu tujitahidi kufuata sheria tunapokuwa kwenye nchi za wenzetu

digba sowey

JF-Expert Member
Mar 1, 2017
7,865
14,283
Viongozi wa kijamii katika mji wa Rajasthan nchini India wanasema mtu mmoja ambaye ni muislam ameuawa kwa kupigwa risasi na watu wanaoamini ng'ombe kuwa mungu wao.
Ummar Khan alikua akisafirisha ng'ombe yeye na mwenzake katika kitongoji cha Alwar wakati walipovamiwa na wahindu.
Wanasema kwamba mwili wa kijana huyo ulitupwa karibu na reli kuharibu ushahidi.
Polisi katika mji wa Rajasthan wameanzisha upelelezi juu ya tukio hilo.
Wahindu huamini kuwa ng'ombe ni mungu kwao na huwachukulia kwa namna ya upekee sana.
Zaidi ya watu kumi wameuawa tokea mwaka 2015 kwa sababu kama hizo. Chanzo :bbc news
 
Hao wahindu wamekosa uvumilivu wa kidini, tatizo ni shule ndogo. Kuna wengine waliwakuta waislamu wanasafirisha nyama ya ng'ombe wakawanywesha mkojo wa ng'ombe ndiyo chai na Mavi ya ng'ombe ndiyo mkate.1
 
Tatizo letu waislam hatuna subira
 
We jamaa sio mzima,unafkiri baada ya uhindu dini gani inafuata kwa watu wengi india?
 
Mleta mada; usisahau Khan ni Mhindi ingawaje akina Khan wengi wapo Pakistan kutokana na matunda ya ukoloni!

Walichofanya hao Wahindu ni upumbavu sawa na tunaofanya Waafrika! Wanaoamini ng'ombe ni Mungu ni wao lakini sio Waislam!!

Ni sawa sawa na kutoa tahadhali kwa Wakristo kutosema Yesu ni Mungu kwa sababu tu Waislamu wanaamini Yesu sio Mungu! HAIWEZEKANI.
 
So kwamba we ndo sio mzima kwakua hujui kuwa akina khan in wapakistani?
Wapo akina khan kibao wahindi ..ushahidi tafuta wasanii kama akina amirkhan ,salman khan nk nk

Pakistan na India wameshabihiana kwa mengi sababu hapo mwanzo walikuwa taifa moja ,sasa kutoitaja Pakistan inawia vigumu kujua moja kwa moja kama ni mpakistan wakati mada inaonyesha alikuwa ndani ya india
 
Kumbe uliniwahi! Na ndio maana nimemuuliza atuambia kama wale akina Khan waliojazana Bollywood sio Wahindi!
 
Viongozi wa kijamii katika mji wa Rajasthan nchini India wanasema mtu mmoja ambaye ni muislam ameuawa kwa kupigwa risasi na watu wanaoamini ng'ombe kuwa mungu wao.
Ummar Khan alikua akisafirisha ng'ombe yeye na mwenzake katika kitongoji cha Alwar wakati walipovamiwa na wahindu.
Wanasema kwamba mwili wa kijana huyo ulitupwa karibu na reli kuharibu ushahidi.
Polisi katika mji wa Rajasthan wameanzisha upelelezi juu ya tukio hilo.
Wahindu huamini kuwa ng'ombe ni mungu kwao na huwachukulia kwa namna ya upekee sana.
Zaidi ya watu kumi wameuawa tokea mwaka 2015 kwa sababu kama hizo. Chanzo :bbc news
Wahindu wananyanyasa sana wenzao, hasa wale wanaochukuliwa daraja la chini hawaruhusiwi kutazama wala kupita kwenye makazi ya wale wanaochukuliwa daraja la juu.
Kama wa daraja la chini akiwa na jina linafanana na wa daraja la juu inabidi abadili jina lah sivyo atauawa.
Yani ni ubaguzi kweli...
 
Back
Top Bottom