Waislamu kuzindua mwongozo wa uchaguzi Alhamisi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Waislamu kuzindua mwongozo wa uchaguzi Alhamisi

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by JoJiPoJi, Aug 26, 2009.

 1. JoJiPoJi

  JoJiPoJi JF-Expert Member

  #1
  Aug 26, 2009
  Joined: Aug 8, 2009
  Messages: 2,471
  Likes Received: 1,424
  Trophy Points: 280
  Hidaya Kivatwa na Salim Said
  http://www.mwananchi.co.tz/newsrids.asp?id=14158

  SHURA ya Maimamu wa Tanzania, kesho inatarajia kuzindua rasmi mwongozo kwa Waislamu kuhusu uchaguzi mkuu wa 2010 na moto wa siasa za ukombozi.

  Uzinduzi huo unatarajiwa kufanyika katika viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam, kuanzia saa 8:00 mchana.

  Akizungumza na waandishi wa habari Kinondoni jijini Dar es Salaam jana, Katibu wa kamati kuu ya siasa ya taasisi hiyo, Sheikh Ponda Issa Ponda, alisema uzinduzi huo utahudhuriwa na zaidi ya masheikh 100 kutoka katika mikoa 22 ya Tanzania Bara.

  Alisema mwongozo huo utagusia masuala mbalimbali ya kitaifa yakiwemo ya kijamii, kisiasa na kiuchumi.

  “Mwongozo unahusisha masuala ya elimu, afya, uchumi, demokrasia, siasa na kilimo. Mambo mengi zaidi tutayaeleza katika uzinduzi ,” alisema Sheikh Ponda.

  Alisema kila mkoa utatoa masheikh watano ambao watawawakilisha Waislamu wa mikoa yao na baadaye kuwarejeshea salamu za pamoja za Waislaam kwa serikali ya CCM.

  Alisema mWongozo huo utakuwa na salamu na ujumbe maalum kwa serikali kufuatia kitendo chake cha kukaa kimya wakati Kanisa Katoliki, lilipotoa waraka ambao kimsingi unahatarisha amani, usalama na umoja wa kitaifa.

  “Ndani ya mwongozo wetu kuna ujumbe maalum kwa serikali ya CCM kwa kule kakaa kimya kwake kimya baada ya Kanisa Katoliki kutoa waraka ambao kimsingi jamii na serikali zinajua kabisa kwamba unahatarisha umoja wa kitaifa,” alisema Sheikh
  Ponda.
  Alisema huko nyuma, viongozi wa madhehebu ya Kiislamu walijaribu kutoa elimu ya uraia, lakini serikali iliwakamata na kuwawe ndani kwa madai ya uchochezi.

  "Je waraka na ilani ya Wakatoliki hazileti uchochezi,” alihoji Ponda.
  Alisema mwongozo huo utaweka mwelekeo na msimamo wa pamoja wa Waislamu kuelekea katika uchaguzi wa serikali za mitaa utakaofanyika mwezi Oktoba mwaka huu na uchaguzi mkuu wa urais, ubunge na udiwani utakaofanyika mwakani.
   
 2. MaxShimba

  MaxShimba JF-Expert Member

  #2
  Aug 26, 2009
  Joined: Apr 11, 2008
  Messages: 35,816
  Likes Received: 129
  Trophy Points: 160
  Waislam, kaazi kweli kweli, hivi uislam ni dini kweli au cult ya kiaina?
   
 3. jambo1

  jambo1 JF-Expert Member

  #3
  Aug 27, 2009
  Joined: Jul 5, 2009
  Messages: 242
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Hey....
  its good ideal..tunatarajia mwongozo utakuwa bomba na mwiba kwa CCM,kwani wao ndo wamekuwa wapingaji wakuu wa elimu ya uraia,we are waiting for that...2po pamoja.
   
 4. RealTz77

  RealTz77 JF-Expert Member

  #4
  Aug 27, 2009
  Joined: May 18, 2009
  Messages: 742
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  sasa huo mwongozo una tofauti gani na ule wa katoliki?mi siamini kabisa hawa waislamu viongozi wao kama wana akili,hope ni mambo ya kitoto na utoto unawasumbua.yani unapinga mwongozo wa mwenzio then unatoa wakwako wa aina hiyo hiyo,hii ni akili au matope?kwani wao hawavunji amani?why wa wakatoliki ndo uvunje amani?they are nuts i believe.na hakuna mtu ataeupinga kama ndo matarajio yao,waweke ufitini,uwongo,udini hawatasikia hata neno from katoliki wala govt
   
 5. Nono

  Nono JF-Expert Member

  #5
  Aug 27, 2009
  Joined: Feb 11, 2008
  Messages: 1,305
  Likes Received: 86
  Trophy Points: 145
  Kazi kweli kweli. Lini tutajifunza kuwa wabunifu? kwanini kazi yetu iwe kufungwa kamba kuvutwa kama kondoo?
  Inaonekana tunatoa waraka kwa kuwa Wakatoliki wametoa.

  Je, tumepima kwa mapana na kutafakari maudhui ya waraka wa wakatoliki?

  Je, waraka wetu ni kuwajibu wakatoliki au ni kutoa mwongozo kwa Watanzania tunapoelekea uchaguzi mkuu ujao, ili kuhakikisha kuwa tunapata serikali itakayokuwa inawajibika kwa wananchi wake na sio kwa mafisadi na wateule wachache?

  Inasikitisha kuwa kumbe waraka unaelekezwa kwa wakatoliki na sio kulenga kumkomboa mTanzania!!!!!!!!!

  Kazi kweli kweli!
   
 6. Shapu

  Shapu JF-Expert Member

  #6
  Aug 27, 2009
  Joined: Jan 17, 2008
  Messages: 1,920
  Likes Received: 241
  Trophy Points: 160


  Kweli wanadamu tumetofautiana.
   
 7. MwanaFalsafa1

  MwanaFalsafa1 JF-Expert Member

  #7
  Aug 27, 2009
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 5,566
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 135

  And this is different from waraka wa kanisa katoliki how?..........Ngoja tuone wale walio kuwa wanau lalamikia waraka ule kama wata lalamikia waraka huu nao kwa nguvu, kasi na ari ile ile.
   
 8. Barubaru

  Barubaru JF-Expert Member

  #8
  Aug 27, 2009
  Joined: Apr 6, 2009
  Messages: 7,162
  Likes Received: 30
  Trophy Points: 0
  Bado kunakuja WARAKA wa WASABATO, Waraka wa Anglican, Waraka wa Walutheri n.k.

  Nafikiri nchi inaelekea pabaya zaidi kama kila mtu atatoa waraka wake. Hoja yangu ni ile ile kwanini kila dini isianzishe chama chake cha siasa, kama wao mabingwa wa kutoa waraka?
   
 9. B

  Boney E.M. JF-Expert Member

  #9
  Aug 27, 2009
  Joined: Jan 22, 2007
  Messages: 425
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 35
  Kibabu Kingunge mwanasiasa mkongwe, asiye na dini kutokana na kujikita zaidi katika ukomunisti, ameanzisha vagi ambalo halina maana kiasi kwamba hata wale waliokuwa wamelala nao sasa wanataka wasikike kuwa walikuwa na jambo la muhimu kwa jamii.
   
 10. BinMgen

  BinMgen JF-Expert Member

  #10
  Aug 27, 2009
  Joined: Jun 18, 2008
  Messages: 1,816
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 145
  HIVI UKRISTO NI DINI KWELI..? inakuwaje unachonga sanamu halafu unaliabudu! hii akili au matope!
   
Loading...