Waislamu hawana uadui dhidi ya Wakristo, wachanga zaidi ya Sh1 milioni ujenzi wa kanisa

R.B

JF-Expert Member
May 10, 2012
6,296
2,575
[h=1][/h]

Geita. Waumini wa madhehebu ya Kiislamu mkoani Geita, wametangaza kuwa hawana uhasama na waumini wa madhehebu ya Kikristo na kuthibitisha hilo, juzi walichangia harambee ya ujenzi wa Kanisa la African Inland Church, Dayosisi ya Kalangalala.

Waumini hao wa Kiislamu walichanga zaidi ya Sh1 milioni. Akizungumza katika harambee hiyo iliyoongozwa na Waziri Mkuu aliyejiuzulu, Edward Lowasa, Katibu wa Bakwata wa Mkoa wa Mwanza, Sheikhe Salumu Bara, alisema Waislamu na Wakristo ni kitu kimoja.

Alisema ile imani iliyokuwa imejengeka katika jamii kuwa Waislamu na Wakristo ni maadui ni ya uwongo.

“Nisema Ukristu na Uislamu ni kitu kimoja, tumeamua kuishi kwa amani na upendo na sisi kama viongozi wa Bakwata Mwanza tumeanzisha umoja unaowashiriki watu 20 kutoka pande zote,” alisema Sheikhe Bara.

Kwa mujibu wa kiongozi huyo wa Kiislamu, umoja huo unalenga katika kueneza amani na kufuta udini ndani ya Mikoa ya Mwanza na Geita.

Alisema katika kuthibitisha kuwa Waislamu hawana chuki na Wakristo, wameamua kuchangia ujenzi wa kanisa hilo litakalotoa huduma za Mwenyezi Mungu.

“Hii inaonyesha kuwa Waislamu ni watu wa amani na si kama wanavyosema watu wengine,” alisema.

Katika hatua nyingine, viongozi hao wa Bakwata walitoa shukrani za dhati kwa Lowasa kwa kukemea udini na yeye binafsi kutokuwa na upendeleo wa kidini.
 
Hiyo ni hatua nzuri kama kweli yanafanyika kwa niya njema na dhati kutoka moyoni kwa pande zote. Inapaswa kuunga mkono moyo huo na kuondoa tofauti zisizojenga.
 
What is behind the tent?, tutafakar. sijajua uongozi mzima wa kiisilam uko vipi?, Je, uko kimatabaka au kila sehemu/mkoa wanajitegemea kimaamuzi?. Mie ninavyoona hili lingekuwa tamko la nchi/dunia nzima, nasio Geita na Mwanza tu. USIFUNGE NIRA...
 
Naombeni tafsiri ya udini?
Uislam hautufundishi kuwa watu wasio waislam ni maadui.
Ila neno udini huwa linatafsiriwa vibaya.
Pale ambapo waislam wanapohitaji madai yao,
kwa mfano mahakama ya kadhi, oic, waislam kupumzika siku ya ijumaa ili wafanye ibada zao kama wenzao, necta na kama hivi sasa issue ya mabint wa kiislam kwenda jeshini hapo ndo utasikia kuna udini.
Udini hautaisha kwa syle hiyo ila ni kutatua kero za kidini pekee.
Bakwata kulipa kanisa pesa ni kawaida kwani hicho ni kigango tu cha kanisa.
Hatutashangaa tukisikia kuwa jumapili moja mashekhe wa bakwata wamekwenda kanisani kufanya ibada.
 
lowasa angekuwa hayupo kwenye huu uzi wengi sana wangeweka like hapa. neno na huo mchango wa bakwata vimekuja wakati mwafaka sana. tunahitaji umoja wa kitaifa leo kuliko kipindi chochote kingine nyuma.

majuzi nimewaambia ndugu zangu wa zanzibar anayetaka kujenga msikiti kwetu mbeya anipm humu nitasaidia kupata kiwanja cha msikiti kwetu. uislamu na ukristo wote wana mzizi mmoja na uhalisia wa malengo yao ni amani miongoni mwa binadamu.

Asante kwa hii taarifa nzuri mtoa mada.

[h=1][/h]

Geita. Waumini wa madhehebu ya Kiislamu mkoani Geita, wametangaza kuwa hawana uhasama na waumini wa madhehebu ya Kikristo na kuthibitisha hilo, juzi walichangia harambee ya ujenzi wa Kanisa la African Inland Church, Dayosisi ya Kalangalala.

Waumini hao wa Kiislamu walichanga zaidi ya Sh1 milioni. Akizungumza katika harambee hiyo iliyoongozwa na Waziri Mkuu aliyejiuzulu, Edward Lowasa, Katibu wa Bakwata wa Mkoa wa Mwanza, Sheikhe Salumu Bara, alisema Waislamu na Wakristo ni kitu kimoja.

Alisema ile imani iliyokuwa imejengeka katika jamii kuwa Waislamu na Wakristo ni maadui ni ya uwongo.

“Nisema Ukristu na Uislamu ni kitu kimoja, tumeamua kuishi kwa amani na upendo na sisi kama viongozi wa Bakwata Mwanza tumeanzisha umoja unaowashiriki watu 20 kutoka pande zote,” alisema Sheikhe Bara.

Kwa mujibu wa kiongozi huyo wa Kiislamu, umoja huo unalenga katika kueneza amani na kufuta udini ndani ya Mikoa ya Mwanza na Geita.

Alisema katika kuthibitisha kuwa Waislamu hawana chuki na Wakristo, wameamua kuchangia ujenzi wa kanisa hilo litakalotoa huduma za Mwenyezi Mungu.

“Hii inaonyesha kuwa Waislamu ni watu wa amani na si kama wanavyosema watu wengine,” alisema.

Katika hatua nyingine, viongozi hao wa Bakwata walitoa shukrani za dhati kwa Lowasa kwa kukemea udini na yeye binafsi kutokuwa na upendeleo wa kidini.
 
Nadhani hali kama hii ikiendelea WANASIASA HAWATAKUWA NA MTAJI KUPITIA MADHEHEBU YA DINI!!! Hongereni Maislamu, jambo jingine acheni mihadhara ya kukashifu dini nyingine.
 
Geita. Waumini wa madhehebu ya Kiislamu mkoani Geita, wametangaza kuwa hawana uhasama na waumini wa madhehebu ya Kikristo na kuthibitisha hilo, juzi walichangia harambee ya ujenzi wa Kanisa la African Inland Church, Dayosisi ya Kalangalala.

Waumini hao wa Kiislamu walichanga zaidi ya Sh1 milioni. Akizungumza katika harambee hiyo iliyoongozwa na Waziri Mkuu aliyejiuzulu, Edward Lowasa, Katibu wa Bakwata wa Mkoa wa Mwanza, Sheikhe Salumu Bara, alisema Waislamu na Wakristo ni kitu kimoja.

Alisema ile imani iliyokuwa imejengeka katika jamii kuwa Waislamu na Wakristo ni maadui ni ya uwongo.

"Nisema Ukristu na Uislamu ni kitu kimoja, tumeamua kuishi kwa amani na upendo na sisi kama viongozi wa Bakwata Mwanza tumeanzisha umoja unaowashiriki watu 20 kutoka pande zote," alisema Sheikhe Bara.

Kwa mujibu wa kiongozi huyo wa Kiislamu, umoja huo unalenga katika kueneza amani na kufuta udini ndani ya Mikoa ya Mwanza na Geita.

Alisema katika kuthibitisha kuwa Waislamu hawana chuki na Wakristo, wameamua kuchangia ujenzi wa kanisa hilo litakalotoa huduma za Mwenyezi Mungu.

"Hii inaonyesha kuwa Waislamu ni watu wa amani na si kama wanavyosema watu wengine," alisema.

Katika hatua nyingine, viongozi hao wa Bakwata walitoa shukrani za dhati kwa Lowasa kwa kukemea udini na yeye binafsi kutokuwa na upendeleo wa kidini.

vipi bomu Arusha!!!!!!!!!!!!!
 
Yes You can....
Tujifunze na kujielimisha namna ya kumezea mambo madogo madogo, Na baadaye kuvumilana ...hakika tutapendana na kuishi pamoja bila kujali yanayosukwa na WANASIASA !!
Tuendelee kufunguka, tuondoe kinyongo.
 
Minilizani waislam ( Muuminiin) kumbe bakwatwa (tawi la CCM ) hapo kilicho fanyika ni siasa za kumsafisha Lowasa tu hamna chengine. Kwanza waislam wa Tz hatui tambui Bakwata AKA mashee ubwabwa, hao ni mtaji wa CCM.
 
suala la mchango ni la kawaida sana,mtu yoyote,wa dini yoyote,wa kabila lolote anaweza akatoa mchango wa kitu chochote..!
"anaweza maana yake sio lazima"
 
tatizo kubwa lililopo nikwamba waislamu wenyewe wametawaliwa na mgogoro mkubwa kati ya bakwata na waislamu halisi. Sasa hapo hao bakwata ndo kwanzaa wanazidi kuimarisha mgogoro wa dini yao!

Waislamu halisi wanasema BAKWATA = SERIKALI + CCM + UKRISTO sasa mimi kama ningepewa nafasi ya kushauri katika migogoro ya dini inayoikumba tanzania ningekua na haya yafuatayo

1. Serikali + CCM wajiepushe na mafungamano na bakwata wala kanisa kwakua serikali haina dini na katiba yetu yenye viraka tele nayo haina pingamizi lolote katika imani ya kuabudu. wakifanya hivyo waislamu watajijua wenyewe katika kutafuta uongozi ambao wote watakubaliana nao kuliko ilivyo leo ambapo waislamu halisi wanapinga bakwata kwakua ipo na serikali.

2. Serikali itambue madhehebu yote ya dini nchini kama dini halali alimradi zisivunje sheria za nchi. mfano ni TAG, ROMAN, SABATO, APOSTOLIC, EFATHA, EAGT, nk. bila kusahau waislamu wote na tofauti zao za kiimani kuliko ilivyo leo ambapo waislamu wasioamini kwa upande wa bakwata bado wanalazimika kuwafuata ili wafanikiwe katika harakaiti za imani zao! Serikali kama kweli inaambatana na bakwata kama wanavyosema waislamu wapinga bakwata basi wajitazame tena kwani hilo ni kosa kubwa na linaweza kwagharimu!

3. Kwa Wale wanaojiita waislamu halisi ambao hawakubaliani na bakwata wasipambane naserikali wala dini nyingine ikiwemo bakwata badala yake waendeleze ibada zao kama dhehebu jingine! haina sababu kama tunawajenga watu kiimani alafu bado tunasababisha machafuko miongoni mwa jamii zetu, mapambano si kitu chema na kamwe hakimpendezi mungu wa dhehebu lolote!

4. Serikali iache kujifanya kua haijui kinachoendelea na kujifanya inashangaaa sana mbona mambo yanasemwa kila cku hapa nchini? hakuna mchawi hebu na yenyewe iongelee wanayosema watanzania na kama wanaweza kujitakasa basi wafanye hivyo! kweli watanzania hatuelewi serikali inapeleleza nini siku zote!
 
Back
Top Bottom