Waislamu 6,700 wa Rohingya wameuawa Myanmar ndani ya mwezi mmoja pekee

kimsboy

JF-Expert Member
Oct 17, 2016
8,991
17,888
Shirika la Madaktari Wasio na Mipaka MSF limesema kwa akali Waislamu 6,700 wa jamii ya Rohingya waliuliwa katika kipindi cha mwezi mmoja nchini Myanmar, tangu operesheni mpya iliyoungwa mkono na serikali ianzishwe na jeshi la nchi hiyo dhidi ya jamii hiyo ya wachache.

Shirika hilo limeyasema hayo leo Alkhamisi na kuongeza kuwa, miongoni mwa Waislamu hao wa Rohingya waliouawa ni watoto wadogo 730 wenye umri chini ya miaka mitano.

Mkurugenzi wa Matibabu wa shirika hilo, Sidney Wong amesema takwimu hizo zimetokana na uchunguzi wa kina wa taasisi hiyo kwa familia zipatazo 2,434.
Amesema karibu asilimia 70 ya vifo hivyo vimetokana na majeraha ya risasi za jeshi la nchi hiyo, katika operesheni yake maalumu mkoani Rakhine, kuanzia mwishoni mwa mwezi Agosti mwaka huu.

Kwa mujibu wa uchunguzi wa Shirika la Madaktari Wasio na Mipaka, asilimia 9 ya Waislamu hao wa Rohingya waliuawa kwa kuteketezwa kwa moto hadi kufa wakiwa ndani ya majumba yao, huku asilimia 5 wakipoteza maisha kutokana na kupewa kichapo cha mbwa na wanajeshi hao makatili wa Myanmar wakisaidiwa na Mabudha wenye misimamo ya kuchupa mipaka.

Hii ni katika hali ambayo, jeshi hilo limekuwa likidai kwamba eti 'limeua watu 400 pekee' katika operesheni zake mkoani hapo.

Jinai kubwa wanazofanyiwa Waislamu hao na wanajeshi na Mabudha wa nchi hiyo wenye misimamo ya kufurutu ada katika mkoa wa Rakhine magharibi mwa Myanmar tangu tarehe 25 mwezi Agosti mwaka huu, hadi sasa zimepelekea kuuliwa maelfu ya Waislamu Warohingya, mbali na kusababisha wengine zaidi ya laki 6 na elfu 50 kuwa wakimbizi.


Parstoday.com
 
unaweza usiamini na kukubali ,lakini ndivyo maisha ya watu wasio na hatia yanavyokwenda! MUNGU tusaidie tuweze kuwa na huruma na tukithaminia bila kujali tofauti zetu.
 
Kama hamuwezi kuheshimu imani za watu wengine na kufikiria yenu ndio sahihi, daima mtaishi tu kama wakimbizi siku zote.
 
Halafu mbona nchi za kiislamu hawawapokei hao wakimbizi,mfano wakimbizi wa Syria,Iraq,Afghan wanataka kukimbilia Ulaya na Marekani na si nchi za watukufu wenzao.
 
Mabudha wakiamua sio wa mchezo mchezo kama manasara na mayahudi mnaowafanyia kila aina ya vitimbi lakini wao ni msamaha kwanza. Buddha akishasema imetosha ni kweli imetosha wala hatanii. Washaurini wawe wapole vinginevyo wakiendelea kushupaa watamalizwa. Always, kila penye vurugu duniani hawa jamaa wamo; ajabu sana.
 
Wanafki wa magharib hutowasikia wakikazia hiyo report
Si wazungu tu ambao hawana mpango hata jumuia za nchi za kiislamu hawana mpango pia.Wao ukitaka wawe na mpango basi choma moto msaafu,tangaza Jerusalem ni mji mkuu wa wayahudi,chora katuni ya
mtume and the like.Ila wakiuana wenyewe kwa wenyewe huko Yemeni,Syria,Libya,misri kwao ni poa tu.Hivi umeshasikia wameandamana juu ya hao warohingya waliouawa?
 
Mabudha wakiamua sio wa mchezo mchezo kama manasara na mayahudi mnaowafanyia kila aina ya vitimbi lakini wao ni msamaha kwanza. Buddha akishasema imetosha ni kweli imetosha wala hatanii. Washaurini wawe wapole vinginevyo wakiendelea kushupaa watamalizwa. Always, kila penye vurugu duniani hawa jamaa wamo; ajabu sana.
Unajua hats Shia walikuwa wananyanyaswa sana na wasuni,Ila sasa na wao wameghairi haaa!wamekuwa wakatili hatari mpaka wasuni wanaomba pooo.Case study ni hezbollar walichowafanyia waasi wa kisuni wa Syria,PMF...hawa ni volunteer wa kishia Kule Iraq ni wakatili vibaya kwa wasuni,Houthi kule Yemeni.Hivyo wamegundua hawatakiwi kuchekewa
 
Back
Top Bottom