Waislam washtuka? Ujumbe wa hali mbaya ya maisha na siasa wasambazwa baada ya Swala ya Iujumaa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Waislam washtuka? Ujumbe wa hali mbaya ya maisha na siasa wasambazwa baada ya Swala ya Iujumaa

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by thatha, Aug 19, 2011.

 1. t

  thatha JF-Expert Member

  #1
  Aug 19, 2011
  Joined: Apr 29, 2011
  Messages: 15,234
  Likes Received: 179
  Trophy Points: 160
  Leo nimeshuhudia baadhi ya miskiti maarufu nchini baada ya swala ya la Ijuma waislam walikuwa wakigaiwa karatasi .waislam wengi walikuwa wakiwania karatasi hizo kwa hamu
  karatsi hizo zenye page 2 zianelezea hali ya siasa nchini na maisha ya Tanzania kwa ujumla baada ya uchaguzi mkuu 2010.

  Karatasi hiyo yenye Kichwa cha habari"ENYI WENYE AKILI: IMESHINDWA DEMKORASIA, KATIBA YAKE MPYA ITAWEZA?

  Katika karatasi hizo ,inazungumzia hali ya maisha ya mtanzania baada ya uchaguzi mkuu huku ikiwalaumu baadhi ya wanasiasa na masheikh waliokaribu na wanasiasa hao kuwa ndio chanzo.

  "Leo tumeshuhudia kwa macho yetu na ya vizazi vijavyo mfumuko mkubwa wa bei za bidhaa muhimu,ikiwemo bei ya umeme licha ya ulaghai uliopo an kupatikana kwa mgao, kupanda nauli za mabasi, migogoro ya kukosekana mahitaji ya msingi vyuo vacuum, ajabu kubwa ni kupanda kwa bei ya mafuta ya taa kwa hoja ya kuthibiti uchakuaji Bia ya kutaja msusuru wa kashfa ya fedheha kubwa za rushwa na ufisadi ukiwemo kuibuka kwa fidia ya mabilion ya fedha za Downs,maafa ya miripuko ya mabomu ya gongo la Mboto............

  Kwa upende wa Zanzibar hali ndio hiyo, bei za vyakula ziko juu, hususan chakula maarufu kama mchele................
  (hizb ut-Taharir Afrika ya mashariki 19,08,2011)

  NIMESHINDWA KUIWEKA SCANNED DOCUMENT KTOKANA NA PRIVILLAGE YANGU NDANI YA JF
   
 2. Chimunguru

  Chimunguru JF-Expert Member

  #2
  Aug 19, 2011
  Joined: May 3, 2009
  Messages: 9,843
  Likes Received: 270
  Trophy Points: 180
  Iweke yote basi mkuu tuisome na kuidadavua
   
 3. Gama

  Gama JF-Expert Member

  #3
  Aug 19, 2011
  Joined: Jan 9, 2010
  Messages: 9,223
  Likes Received: 1,411
  Trophy Points: 280
  Tueleze ni msikiti upi huo na turushie nakala ya hilo andiko ili tuchangie vizuri.
   
 4. K

  KAPONGO JF-Expert Member

  #4
  Aug 19, 2011
  Joined: May 29, 2009
  Messages: 1,374
  Likes Received: 165
  Trophy Points: 160
  Taarifa hiyo imetolewa na asasi inayoitwa Hizb ut Tahrir Afrika Mashariki inahamasisha watu, kwa muhtasari wake, umuhimu wa uukatae mfumo wa kibepari kwa maelezo kuwa ndiyo kiini cha matatizo ya hali ngumu za maisha na kero nyingine. Wanasema kelele za kutaka katiba mpya ni ujanja wa wanasiasa wa kuficha kiini cha matatizo, ingawa wanasema kuna umuhimu wa kuwa na katiba mpya kutokana na mapungufu ya katiba ya zamani..na kuweka angalizo kuwa katiba hiyo mpya isitokane na matakwa ya kibinaadamu ambayo yana wingi wa kasoro, bali itokane na Muumba chini ya kivuli cha dola ya kiislamu ya 'Khilafah Rashidah' ambazo wamesema dalili za kurejea kwake zipo wazi, hususan Mashariki ya Kati.
   
 5. Gama

  Gama JF-Expert Member

  #5
  Aug 19, 2011
  Joined: Jan 9, 2010
  Messages: 9,223
  Likes Received: 1,411
  Trophy Points: 280
  Wametetea weeeeeeee, wametetea weeeeeeeee hatimae wamegundua kuwa wanatetea ndicho sicho. Nasubiri kuwaona wakituomba radhi.
  <br />
  <br />
   
 6. Njowepo

  Njowepo JF-Expert Member

  #6
  Aug 19, 2011
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 9,297
  Likes Received: 381
  Trophy Points: 180
  Wanagundua leo!!!!
   
 7. p

  propagandist Member

  #7
  Aug 19, 2011
  Joined: Aug 12, 2011
  Messages: 93
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hizbu ul tahriri taasisi hii ni ya wanafiki na ni vibaraka makao makuu yake yapo uingereza na hapa viongozi wake ni mussa kileo, hawana mashiko kwa waislam hapa nchini, wanaonekana kama vibaraka wa wazungu,
   
 8. A

  Anold JF-Expert Member

  #8
  Aug 19, 2011
  Joined: Jul 15, 2010
  Messages: 1,374
  Likes Received: 296
  Trophy Points: 180
  Wanayolalamikia yana mantiki lakini sidhani kama kuna suluhisho kutokana na sababu mbalimbali ambazo sioni kama ni vizuri kuziandika hapa. Wajifunge mkanda, wazidi kuliombea taifa ili Mungu ashushe rehema zake maisha yaende vizuri.
   
 9. MaxShimba

  MaxShimba JF-Expert Member

  #9
  Aug 19, 2011
  Joined: Apr 11, 2008
  Messages: 35,816
  Likes Received: 129
  Trophy Points: 160
  Waende Somalia kusaidia.
   
 10. p

  pat john JF-Expert Member

  #10
  Aug 19, 2011
  Joined: Mar 31, 2009
  Messages: 245
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Wanayosema ni kweli. Lakini wanaweza kuaminika katika kauli zao au wana ajenda ya siri?
   
 11. M

  Mrdash1 JF-Expert Member

  #11
  Aug 19, 2011
  Joined: Sep 21, 2010
  Messages: 1,379
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Mimi nilijua tu, wataanza kudhihakiana na baadae ngumi!!!!
   
Loading...