Majs
JF-Expert Member
- Dec 21, 2012
- 232
- 497
Waislamu wanaoishi katika eneo la kaskazini mwa dunia, hasa nchi za Scandnavia, wanakabiliwa na changamoto ya kufunga muda mrefu ambao mara nyingi huwa ni zaidi ya saa 20.
Katika nchi ya Finland ambayo idadi ya Waislamu inafikia takriban laki 1 kati ya wakazi milioni 5 (yaani asilimia 2 tu ya wakazi wa nchi hiyo), mwaka huu muda wao wa kufunga ni zaidi ya saa 22. Kwa mfano, Waislamu wa mji mkuu, Helsinki, wanakaa na swaumu kwa muda wa saa 22 na dakika 13, na huo ndio muda mchache zaidi kutokana na ukweli kwamba mji huo uko upande wa kusini mwa nchi hiyo.
Ama miji ya upande wa kaskazini, muda wa kukaa na swaumu ni zaidi ya huo. Kwa mfano, mji wa Oulu ambao ndio mji mkubwa zaidi kaskazini mwa nchi hiyo, Waislamu hukaa na swaumu kwa muda wa saa 23 kasoro dakika 7. Yaani muda wao wa kula ni saa moja na dakika 7 tu. Katika miji mingine ya kaskazini muda wa kula ni chini zaidi ya huo.
Finland ina jamii mbalimbali za Waislamu kama vile Wairaq, Wasomali, Waturuki, Wathailand na wengineo. Japokuwa Uislamu ulifika nchini humo katika karne ya 18 na 19 kupitia kwa Waislamu wa jamii ya Watatar, idadi ya Waislamu iliongezeka mwanzoni mwa miaka ya 1990 kufuatia ongezeko la wahamiaji waliokuwa wakitafuta makazi mapya huko.
Baraza la kwanza la Kiislamu nchini humo liliasisiwa rasmi mwaka 1925, na hivyo kuifanya Finland kuwa nchi ya kwanza ya Ulaya ya Magharibi kulitambua rasmi baraza la Kiislamu.
Waislamu wengi wa Finland hupendelea kufuata fat'wa zinazowapa fursa ya kufunga kulingana na nyakati za nchi ya Kiislamu iliyo karibu zaidi pindi ambapo muda wa funga unazidi saa 18, ili kukabiliana na muda mrefu wa kukaa na funga katika nchi hiyo.
Imeandaliwa na:
MKWALE