Waislam Tanga waomba watoto wa kike wasikae dawati moja na wakiume

Status
Not open for further replies.
Hili kwenye shule za serikali halikubaliki kabisa na mbaya zaidi ni kudumaza kiwango cha uelewa kwa watoto wetu.

Mwalimu anapofundisha darasani katika mazingira ya kuwashirikisha wanafunzi kwa njia ya maswali nk, wanafunzi wamekuwa wakifaidika, kupata changamoto na kujifunza toka kwa wenzao na hii inawafanya kuongeza bidii na kulielewa somo husika kwa haraka na ufasaha zaidi.

Jamani zaidi ya yote haya mambo ya imani za dini kwenye shule za serikali ambako kuna watoto wa dini zote na wasio na dini pia hakika hii ni kuvunja katiba ya nchi, hivyo hili kama wanaliona lina umhimu sana kiimani na mtazamo wao kielimu ni bora likafanywa na kutekelezwa katika shule ambazo ni imani husika na kwa kufanya hivyo wazazi wenye mtizamo huo watapeleka watoto wao huko ili wapate elimu na malezi hayo.

Binafsi siamini kuwa kwa wanafunzi kutumia darasa moja na pengine dawati moja basi ndio kigezo cha uvunjifu wa maadili na kutofuata misingi ya imani ya dini husika la hasha, kumbe basi wazazi, walezi, viongozi wa kiroho na jamii kwa ujumla wake tujikite kuwalea watoto wetu katika maadili mema na daima tusichoke kukaa nao na kuwahusia juu ya nini wanatakiwa kufanya ili kufikia malengo yao mazuri waliyojiwekea na pale sisi wazazi ambapo tungetaka wao wafike.

Naamini kwa kufanya hivyo tutakuwa kwa kiwango kikubwa tumechangia kuijenga jamii yenye maadili mazuri yenye kumhofia Mungu na tutasadia kuijenga Tanzania yetu na kuiepusha na na hizi itikadi za udini zinazoshamiri kwa sasa kama uyoga.
 
Jamani haya nayo mapya tena. Watoto wa kike wasikae dawati moja na wa kiume ili kuleta nidhamu na usikivu. Hii imekaaje jamani. Hatua itakayofuata ni kutenga darasa la watoto wa kiume na wa kike. Tunakwenda wapi jamani. Hapana huko siko kabisa.

Source ni Nipashe radio one.

Ubaya uko wapi, watoto wa shule wanaobalehe wakikaa pamoja kuna kijimhemko ndio, na kama hawana nidhamu ndo wataanza kushikana-shikana, hapo kuna usikivu tena?

Au kwa vile waliosema ni waislamu?
 
kutengana kutawasaidia kufaulu?
Kwa nini wasiombe madawati
walimu waliobobea
Nyumba za walimu
vitabu na maabara?
 
Ubaya uko wapi, watoto wa shule wanaobalehe wakikaa pamoja kuna kijimhemko ndio, na kama hawana nidhamu ndo wataanza kushikana-shikana, hapo kuna usikivu tena?

Au kwa vile waliosema ni waislamu?

Mkuu.
Hili halihitaji ubishi kuwa haliwezekani kwenye mfumo wa nchi yetu na nakuomba uondoe inferiority complex za kusema "kwa kuwa wamesema waislamu".

Naomba niweka wazi tena! Kwa islamic perspective hili liko sahihi sana hasa kwa shule za kiislamu ambazo utaratibu uko wazi kuwa wanafunzi wanatengwa kutokana na madili ya dini yanavyo taka. Hili hawawezi kusema lifanyike Kirinjiko, Alkheri au Ubungo islamic maana ndio utaratibu na mila na desturi za shule hizo.

Kwa shule za serikali haitawezekana kamwe. Kwa sababu zifuatazo.

1. Lina mtazamo wa kidini na serikali haina dini.

2. Sasa hivi nchi inapita katika kipindi kigumu cha mihemko na hisia za udini na mabishano ya nani achinje na nani asichinje. Wenye macho mang'avu wataliona hili kuwa linaenda kutengeneza tatizo.

3. Lita chipua ubaguzi baina ya wanafunzi wa dini nyingine na waislamu. Kumbuka sasa hivi kuna baadhi ya mashule imebidi kuhamisha walimu na wanafunzi ili kutuliza hali ya sintofahamu. Hili halita kubalika.

4.Tayari kuna barua ya afisa wa elimu kueleka kupinga shughuli au mambo yenye kuleta udini mashuleni, kwa sasa hata graduation za dini maeneo ya shule itakuwa ni marufuku. Hili halitakubalika pia maana lina mtazamo wa kiimani.

5. Wazazi ndio wanataka wanafunzi wa kike watengwe, walimu wanao fundisha ndio wanajua kwa nini wanafunzi wachanganywe.

6.Huwezi kumtenga mwanafunzi darasani wakati mazingira ya nje yanamkutanisha na yale unayo mtenga nayo darasani (hasa day schools), mtoto anaenda shule na hiace amebanana na mvuliana, akirudi nyumbani hivyohivyo, nyumba za kupanga wanakaa na wavulina vibarazani, wakienda sokoni hivyohivyo...

Hili litakuwa gumu sana kwa mazingira halisi ya kitanzania.

Wazazi wa Tanga watambue kuwa watoto wao kukaa na wavulana sio kilicho changia kufeli, wanatakiwa kwenda mbele zaidi kung'amua matatizo ya watoto wao na kuya fanyia kazi, sio hilo wanalo litaka.
 
Wanawake na wanaume wote ni watu. Ni vema kuwaweka karibu tangu watoto ili wajifunze kushirikiana bila madhara. Hii concept ya kuwatenganisha inatokana na wenye imani kwamba wanawake ni kifaa kwa mwanaume. Serikali izibe masikio kwa watu kama hao.
 
hivi unataka kujua wadau tunasemaje ktk hili au unataka nn maana naona tyr umejijibu sasa cjui hii post umeweka ya nn? acha unafiki jali yanayokuhusu ww.
 
Hivi wakiristo tumekuaje?
Kwani muislam akitoa rai yake lazima ajibiwe vibaya?
KWENYE MAWODI HOSPITALINI wanavyo lala wanawake mbali na wanaume ni sababu za waisilam?
Inawezekana mungu tunayemuabudu siyo YESU KIRISTO !kama kwetu sisi waisilam ni wagonjwa na sisi matabibu , mbona tunawachukia wagonjwa?
Kwa andiko lipi?
Tusome yohana 20:16-17 ili tuwe na uhakika wa mungu.ukisoma bible mambo ya kupiga mtu mawe hayapo?

Wanafikiri MUNGU alivyosema watenganishwe kila mahali ni mjinga ila wao ndio wenye akili.

Ndio maana wao wanajidanganya kuwa hawawezi kuzaa ama kuoa ( watawa ) na matokeo yake kumbe na wao wanahisia za kujamiana kama binadamu wa kawaida na matokeo yake wanakuwa ni chakula cha mapadri...

Ulize sababu muambiwee sio kukurupuka tu !
 
Kwa hili likiangaliwa kwenye islamic perspective liko sahihi kabisa, na linawezekana tu kwenye mashule yanayo ongozwa na taasisi za kidini Mfano Alkheri, Kirinjiko, Ubungo Islamic, Ununio nk.
Lakini unapo liongelea kwa kulijumuisha lifanyike kwenye shule za serikali haitawezekana kwa sababu kwanza lina element za kufuata itikadi ya dini, itatafsirika kuwa ni wazo la wazazi wa kiislamu kwa kuwa Tanga asilimia kubwa ya wazazi wenye watoto mashuleni ni waislamu.

Kwa sasa hata utaratibu wakufanya mahafali ya kidini kwenye maeneo ya shule za serikali mkoani Tanga ni marufuku, hili ni kutokana na vurugu zilizo kuwa na hisia za udini kwenye baadhi ya mashule mkoani hapa.

Hata hivyo, kwenye hili la kuwatenga watoto wa kike wataalamu wengi wa elimu watalipinga kutokana na aina ya mfumo mpya wa ufundishaji wa sasa ambayo unatumia mbinu shirikishi, mbinu shirikishi huwezesha kuundwa kwa vikundi (groups) kwa ajili ya mijadala ya kidarasa na hata kuwasilisha, kwenye hiyo mbinu huwezi kuwatenga wanafunzi wa ke na me maana utahitaji uone ushirikiano wao kwenye kulielewa somo.

Hili litakuwa na changamoto zake ambazo bila shaka zitaangaliwa kwenye mtazamo wa kidini.

Naona ukada wa CHADEMA unazidi kukuingia na hata kusahau dini yako....!

Umeambiwa watenganishwe kwenye madawati na sio vyumba vya masomo/darasa MBONA HAMSOMI MADA MKAIELEWAAAA ??
 
kweli Mtoi umejibu vyema kabisa bila kupendelea upande wowote na kama wewe ni muislam basi wewe ni Bold Spirit.Watanzania na waafrika kwa ujumla tunahitaji kutumia busara ya hali ya juu kuhusu dini hizi kubwa ambazo zimetokea ughaibuni. Ni suala lisilopingika kuwa dini hizi tulivyoletewa zilikuja pamoja na tamaduni husika .zingine zikiwa zimeandikwa kwenye vitabu hivyo vitakatifu ambavyo havina mwanya wa amendment na mengine yakiwa hayajaandikwa ila tunaiga jinsi hao mabwana waliotuletea dini hizo wanavyoishi. Kwenye suala hili la wanafunzi wa kike na wakiume kutokukaa pamoja ni wazi kuwa ni utamaduni wa kiarabu na kwa Muumini wa kiislamu mwenye imani kali au ambaye amesoma elimu ya dini tuu na hajasoma elimu ya kawaida anachukia sana mabinti wao sio tuu kukaa dawati moja na watoto wa kiume bali wanataka hata watenhanishwe kama ilivyo msikitini.Kwangu nadhani huu ni utamaduni tuu ambao sisi kama watanzania si lazima kuufuata sana kwani hata uko uharabuni ulipotokea sasahivi unapata changamoto kubwa sana kwa wanawake wapenda mabadiliko ambao baada ya kusoma wameona utamaduni huo gandamizi kwa haki za wanawake hauna nafasi kwa karne ya sasa na wanapigana usiku na mchana kujikomboa kutokana na mfumo dume uliowachukulia wanawake kama sio viumbe wa kawaida na wakichangamana na wanaume tuu basi kinachofuata ni hisia za kingono.Kwa Tanzania kuna faida kubwa sana kwa wanafunzi kusoma wakiwa wamechanganyikana za kijamii pamoja na kitaaluma.Ni vizuri wasomi kama wewe Mtoi na wapenda mabadiliko kuwaelimisha wazee waliobobea kwenye elimu ya dini tuu na wasiopenda mabadiliko kuachana na hizo mila potofu

inawezekana tu mbona kenya kadhi mkuu analipwa na srikali na mambo yanaenda ? acheni udini hii ilikuwa rai tu
 
Kwa hili likiangaliwa kwenye islamic perspective liko sahihi kabisa, na linawezekana tu kwenye mashule yanayo ongozwa na taasisi za kidini Mfano Alkheri, Kirinjiko, Ubungo Islamic, Ununio nk. Lakini unapo liongelea kwa kulijumuisha lifanyike kwenye shule za serikali haitawezekana kwa sababu kwanza lina element za kufuata itikadi ya dini, itatafsirika kuwa ni wazo la wazazi wa kiislamu kwa kuwa Tanga asilimia kubwa ya wazazi wenye watoto mashuleni ni waislamu.Kwa sasa hata utaratibu wakufanya mahafali ya kidini kwenye maeneo ya shule za serikali mkoani Tanga ni marufuku, hili ni kutokana na vurugu zilizo kuwa na hisia za udini kwenye baadhi ya mashule mkoani hapa.Hata hivyo, kwenye hili la kuwatenga watoto wa kike wataalamu wengi wa elimu watalipinga kutokana na aina ya mfumo mpya wa ufundishaji wa sasa ambayo unatumia mbinu shirikishi, mbinu shirikishi huwezesha kuundwa kwa vikundi (groups) kwa ajili ya mijadala ya kidarasa na hata kuwasilisha, kwenye hiyo mbinu huwezi kuwatenga wanafunzi wa ke na me maana utahitaji uone ushirikiano wao kwenye kulielewa somo.Hili litakuwa na changamoto zake ambazo bila shaka zitaangaliwa kwenye mtazamo wa kidini.
bro huwa nakukubali sana your among of the jf great thinkers
 
Naona ukada wa CHADEMA unazidi kukuingia na hata kusahau dini yako....!

Umeambiwa watenganishwe kwenye madawati na sio vyumba vya masomo/darasa MBONA HAMSOMI MADA MKAIELEWAAAA ??

Mkuu.
Wala huna haja ya kuniangalia kwa kujenga picha ya itikadi ya chama, hatuongelei sera wala itikadi za vyama hapa! Tunaongelea mustakabali wa wadogo zetu huko mashuleni, na elewa kuwa tunapo ongelea mustakabali huo hatuongelei kwa kuangalia imani za dini zao.

Sina haja ya kukuambia mengi lakini najua na nina uhakika na ninacho kiandika hapa.

Unacho kisema hakiwezekani kwenye shule za serikali labda kwenye shule zetu za kidini.

Hapa tunajidiliane tu kwa kupeana elimu lakini tukae tukijua hata hiyo tume iliyoundwa na Pinda ikija na wazo kama hili itaonekana ya hovyo tu na itapingwa na wadau wengi wa elimu.
 
Naona afadhali waache mfumo uliopo kwani kuwatenga kama swala ni ngono bado watakua hawajamaliza tatizo kwani hao wakijitenga kama wana nia ya kungonoka watageukia upande wa pili ambao ni mbaya zaidi aheri wabaki walivyo badala ya kuwarahisishia kuwa wasagaji au mashoga kama swala ni ngono.
 
Kwa mawazo yangu, serikali iruhusu na kuwezesha wanafunzi wa shule za msingi zote kutumia viti na meza badala ya madawati. Ili kuwawezesha kukaa mmoja mmoja kama wafanyavyo sekondari na vyuoni kwa sababu hata kiafya mnapobanana dawati moja mnaweza kuambukizana magonjwa kama vile upele n.k. Zoezi hili liendane na kuongeza vyumba vya madarasa. Naomba kuwasilisha.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom