Hakikwanza
JF-Expert Member
- Dec 11, 2010
- 4,034
- 1,003
Wana Jf, kila mara huwa nakumbusha kuwa hoja hujibiwa kwa hoja. Inapojibiwa kwa hisia(emotion) basi hupoteza muelekeo.
Voingozi wa dini ni wanadamu kama walivyo wanadamu wengine, tena wapo viongozi waliooza kiimadili kuliko waamuni wao. Inategemea kiongozi huyo yupo wapi na anawaumini wenye uelewa kiasi gani.
Hoja hapa ni kumwambia sheikh kuwa kama hao ni wahuni je Tunisia, Algeria, Morocco, Egypt, Bahrain, Jordan na hata Saudia ambako king amefanya mabadiliko kuepeuka Jasmine revolution, je nako wanakula vidonge.? Ukisoma hoja za sheikh, haraka utatambua kuwa uwezo wake wa kufikiri na kupata habari ni finyu sana. Kama ilivyo CCM kule vijijini inapowaambia watu tumeleta maendeleo na watu wakapiga makofi ndivyo ilivyo katika jamii zetu zenye uelewa finyu! hatuwezi kukataa ukweli huu.
Ninachosisitiza hapa ni kuwa suala hilo lisifanywe au lisiunganishwe na imani za dini. Hao mamilion ya watu mideast wangemsikia sheikh wa dodoma pengine wangezimia wote. Lakini hata hapa JF na Tanzania kwa ujumla na pengine ndani ya msikiti huo wa sheikh kuna maelfu ya waislam waliochukizwa na kushangazwa na kauli ya sheikh. Hatutawatendea haki kama kauli ya mtu mmoja itafungamanishwa na imani za mamilioni ya watu. Kauli hii ni yake na sidhani kuwa ni ya waislam. Kama alivyowahi kusema Askofu kilaini, JK ni chaguo la mungu, ile imebaki kuwa kauli yake na si kauli ya Wakristo. Tujaribu kuchambua hoja zaidi kuliko kuweka mbele hisia zetu au kutowatendea haki wasiojihusisha na kauli za baadhi ya watu.
wewe uko sahihi maelezo yako ni safi na muafaka,tusitumia uelewa wa mtu mmoja mpumbavu hata kama ni kiongozi wa dini au asasi kujudge waumini wote kwani hawa viongozi wetu huwa wanateleza,huyo shekhe ni mawazo yake ya kijinga tu hivyo ni kumpuuza yeye tu na sio waislamu wote.