Waishi na fisi kwa miaka 44 sasa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Waishi na fisi kwa miaka 44 sasa

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by MziziMkavu, Mar 3, 2012.

 1. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #1
  Mar 3, 2012
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,620
  Likes Received: 4,611
  Trophy Points: 280
  [​IMG]
  Wakazi wa Kijiji cha Chela, Wilaya ya Kahama mkoani Shinyanga Mussa Serikali (kushoto), Doi Lukondya (katikati) na Matandalwa Lukondya wakiwa wamewashikilia fisi nyumbani wanaowafuga kwa ajili shughuli za burudani kama walivyokutwa hivi karibuni.​
  Na Shija Felician, Kahama
  FAMILIA moja katika Kijiji cha Chela, Wilaya ya Kahama mkoani Shinyanga imesimulia jinsi inavyoishi na fisi kwa miaka 44 sasa.Kijiji cha Chela ndiko alikozaliwa Waziri wa Maliasili na Utalii ambaye pia ni Mbunge wa Msalala (CCM), Ezekiel Maige na fisi hao walionekana hadharani wakati Waziri Mkuu, Mizengo Pinda alipofika katika kijiji hicho akiwa katika ziara mkoani Shinyanga wiki iliyopita.

  Familia inayofuga fisi hao ni ile inayounda kikundi cha burudani ya ngoma za jadi ambacho ni maarufu katika Kanda ya Ziwa kikijulikana kwa jina la Bununguli na kwamba fisi hao ni moja ya nyenzo za kufanikisha kazi yao.
  Mmoja wa wanafamilia wanaomiliki ngoma hiyo, Lukondya Mabiti Jinoja anasema aina ya fisi wanaofuga wanajulikana kama nhawa kwa lugha ya Kisukuma na kwamba fisi wa aina hiyo wana maumbo makubwa kuliko wale waitwao mbitimululu wenye maumbile madogo yasiyovutia.

  Alisema ingawa fisi hao wameanza kuwatumia na kuonekana hadharani siku za karibuni, familia yake imeanza kuishi na wanyama hao tangu mwaka 1968.“Ni miaka mingi inafikia 44 au 45 na katika muda wote huo tumejifunza mbinu mbalimbali za namna ya kuwakamata na tumefanikiwa kuishi nao kwa muda wote bila kupata madhara yoyote,” anasimulia Jinola.
  Jinoja ambaye ni Mwenyekiti wa Bununguli, alisema wakati wa maonyesho ya burudani za ngoma, fisi hao hutumika kunogesha na kuvutia umati wa watazamaji wa ngoma hizo.

  Wanawakamataje?
  Jinola anasema mara nyingi ukamataji wa fisi hao hufanywa kwa kutumia mbinu za kijadi ambazo hata hivyo, hakutaka kuziweka wazi.

  “Hawa mafisi hukaa kwenye mapango, kwa hiyo sisi huenda tukiwa kundi kubwa kuwavizia taratibu na tukiwakaribia huwa tunawavamia, tukiwakamata tu huwa tunawahifadhi kwenye masanduku yetu makubwa na kuwafungia, kisha huyabeba hadi nyumbani tunakowafuga,” alisema Jinola.

  Alisema fisi hufugwa kama ilivyo wanyama wengine ambao ni mbwa au paka na kwamba baada ya kuishi nao kwa siku kadhaa, huzoeana nao na baadaye huwa wapole wasiokuwa na madhara kwa binadamu.Hata hivyo, Jinoja alisema changamoto kubwa waliyonayo ni uwezo wa kuwalisha kwani fisi mmoja ana uwezo wa kula kati ya kilo mbili hadi nne za nyama kwa siku moja kulingana na ukubwa wake.

  “Natumia wastani wa kilo 16 za nyama kila wiki kuwalisha fisi wangu wanne, ni kazi kubwa kweli lakini tunajitahidi kadri tunavyoweza,” alisema.Hata hivyo, alisema baada ya familia hiyo kufanikisha mpango wa kuishi na fisi hao sasa wameweka mikakati wa kufuga chui siku zijazo.

  Ili kufahamu kwa undani jinsi wanavyowakamata fisi hao na kutumiwa kwenye shughuli za ngoma, soma gazeti hili toleo la Jumamosi ijayo.

  chanzo. Waishi na fisi kwa miaka 44 sasa

  HII FAMILIA WATAKUWA HAWA NI WACHAWI TU KUISHI NA FISI EHHH KASHEHSE KWELI.
   
 2. Inkoskaz

  Inkoskaz JF-Expert Member

  #2
  Mar 3, 2012
  Joined: Nov 6, 2010
  Messages: 6,317
  Likes Received: 438
  Trophy Points: 180
  fisi si nyara za serikali au?
   
 3. BornTown

  BornTown JF-Expert Member

  #3
  Mar 3, 2012
  Joined: May 7, 2008
  Messages: 1,716
  Likes Received: 105
  Trophy Points: 160
  hivi inamaana miaka yote hiyo hata majirani hawajui kuwa kuna fisi???
   
 4. Dr.Chichi

  Dr.Chichi JF-Expert Member

  #4
  Mar 3, 2012
  Joined: Apr 30, 2008
  Messages: 2,336
  Likes Received: 52
  Trophy Points: 145
  mhhh fisi si ndio usafiri wa wachawi??
   
 5. Angel Msoffe

  Angel Msoffe JF-Expert Member

  #5
  Mar 3, 2012
  Joined: Jun 21, 2011
  Messages: 6,797
  Likes Received: 74
  Trophy Points: 145
  Fisi ndio bodaboda za wachawi.
   
 6. Ndahani

  Ndahani JF-Expert Member

  #6
  Mar 3, 2012
  Joined: Jun 3, 2008
  Messages: 14,316
  Likes Received: 1,784
  Trophy Points: 280
  Wasukuma nao bwana...wanafuga vitu ambavyo havifugiki...fisi, nyoka, labda na mamba ingawa hakuna mito mikubwa kwao. Ina maana hawa jamaa wanafuga ng'ombe na mbuzi za kuwalishia fisi? Maana fisi hawali majani wala ugali. wanawalisha nini? Albino? Au vikongwe wanaowaua?
   
 7. TIQO

  TIQO JF-Expert Member

  #7
  Mar 3, 2012
  Joined: Jan 8, 2011
  Messages: 13,832
  Likes Received: 45
  Trophy Points: 0
  Duhh hao jamaa kwa vile ni wa magamba hakuna tatizo ila wangekuwa wa CDM au CUF siku nyingi wangekuwa wananyea debe
   
 8. Ngoromiko

  Ngoromiko JF-Expert Member

  #8
  Mar 3, 2012
  Joined: Sep 15, 2011
  Messages: 559
  Likes Received: 68
  Trophy Points: 45
  Duh! unaingiza siasa kila mahali? Huu utani umezidi sasa.
   
 9. LiverpoolFC

  LiverpoolFC JF-Expert Member

  #9
  Mar 3, 2012
  Joined: Apr 12, 2011
  Messages: 11,001
  Likes Received: 153
  Trophy Points: 160
  Ni nyaraka ya Serikali haswaaa!

  Mbaya ni serikali iliyoko madarakani ndiyo legelege,kwn yule aliyeishi na nyaraka ya serikali ni wa kumweka ndani mpaka kieleweke.

  Naaalaabuk!! Nyaraka ya serikali anakaanayo miaka 44?
  sweka lupango hii familia!
   
Loading...