Waingereza: Wazenji somo la kujifunza!

Ona sasa hivi kwa kutofautiana tu kisiasa wanakatiana mikarafuu huko Pemba!
Na yale ya kukatiana migomba,mibuni na kuchomeana nyumba kule Kagera , kukatana mapanga kule Tanga na Mwanza tena kwenye nyumba ya ibada, hilo nalo tuliiteje?Usiwe mvivu wa kutafakari
 
Karume ndo nani
Alielifuta na kuliua Azimio la Arusha, aliemfukuza Waziri wa Fedha Jamal mpaka akapata mshtuko wa moyo, aliesema Muungano ni sawa na koti, ukaliona linakubana utalivua...... aliezuia watanganyka kufanya kazi Zanzibar hata zile taasisi za muungano, ikiwemo jeshi isipokwa EAC..... Huyo ndio Karume wa Zanzibar
 
Muungano huu wa ajabu uliosalia Duniani ni wakati wake wa kupiga Kura ya maoni ili Tanganyika wajivue zigo kisha Zanzibar wafunge ndoa za Oman kisha wanyemeleaji akina Somalia waje huko wapate Tabu wataikumbuka Tanganyika jinsi ilivyotaabika kuwalisha miaka yote.
Msitujaribu.. kila siku kura ya maoni.... iko wapi? au hamtaki na nyie kufunga ndoa na Mjarumani? wacha hisia za udini!
 
Na yale ya kukatiana migomba,mibuni na kuchomeana nyumba kule Kagera , kukatana mapanga kule Tanga na Mwanza tena kwenye nyumba ya ibada, hilo nalo tuliiteje?Usiwe mvivu wa kutafakari
Huo ni utetezi wa unyasi, hilo unalijua sana na halihitaji mjadala!
 
Wakitoka tu kwenye muungano, hata kama hatuwapendi, jamaa wanachinjana kesho yake na 1964 itakuwa cha mtoto.

Kwa jinsi hao jamaa walivyo na mihemuko ya kitoto Al kaeda na Isis watakaribishwa huko kwa mikono miwili.

Ona sasa hivi kwa kutofautiana tu kisiasa wanakatiana mikarafuu huko Pemba!​
Hata kama mtu humpendi kiasi gani usifike hatua ya kumchukia, binaadam vitendo vyetu vina fanana, hakuna aliye kamilika. Kama kweli unatamani kuhubri mtazamo wako na ueleweke ninge kuomba weka list ya vitendo vya kikatili na kudhulumiana kati ya Tanganyika na Zanzibar ili tuone mtazamo wako una usahhi gani, ingawa kwamba binaadam tuna tabia za chuki na kutopendana lakini kwenye haki tutende haki hata kama itakuwa inauma au kufurahisha.

We are being targeted while they are sitting safe and sound in their palaces.
 
Back
Top Bottom