masopakyindi
Platinum Member
- Jul 5, 2011
- 18,173
- 13,776
Waingereza tunaweza kwa sasa kusema ndo waswahili wa Ulaya!
Ule msimamo wa " chako chako, chako changu" umedhihirika kwa hawa wenzetu waliotutawala enzi za ukoloni.
Siyo siri, hii kura ya kubaki ama kuondoka Jumuiya ya Ulaya, EU, imewaumbua vibaya.
Mtu mbinafsi hujifikiria yeye kwanza, na watu wa visiwani wana ugonjwa huu.
Kura ya kujitoa EU kama maamuzi ya waingereza imeibua hasira ya nia ya kuitenga Uingereza na biashara karibu zote, ikiwemo nia ya kuhamisha makao makuu ya kibiashara toka London kwenda Paris au Berlin.
Pamoja na kura hiyo ni wafanya biashara duniani kukosa imani na hela ya Uingereza, hivyo kuanguka thamani vibaya.
Wenzetu wa visiwa vilivyo karibu wajitathmini na msimamo wao unaolingana na msimamo wa Uingereza.
Kama alivosema Mwalimu , dhambi ya kujitenga Zanzibar itawaadhibu wazanzibari zaidi kuliko Tanganyika, funzo tumeliona live.