Waingereza waishawishi Tz uingia katika biashara za kimataifa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Waingereza waishawishi Tz uingia katika biashara za kimataifa

Discussion in 'Biashara, Uchumi na Ujasiriamali' started by MziziMkavu, Mar 21, 2010.

 1. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #1
  Mar 21, 2010
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,620
  Likes Received: 4,616
  Trophy Points: 280
  JOPO la wafanyabiashara 17, kutoka Uingereza lipo nchini kushawishi ushirikiano na wafanyabiashara wazawa kwa lengo la kuiingiza Tanzania kwenye mtandao wa biashara za kimataifa.

  Mkakati huo, pia utajadili mpango wa kuitaka serikali kutia saini mkataba wa kuondoa ushuru kwenye bidhaa zitakazoingia nchini kwa kipindi kisichopungua mwaka mmoja.

  Kundi hilo, linoangozwa na naibu ofisa mkuu wa Chama cha Wenye Biashara na Viwanda nchini Uingreza (LCCI), Peter Bishop.
  Bishop aliwaambia waandishi wa habari jijini Dar es salaam jana kuwa lengo ni kuiwezesha Tanzania kuingia katika mtandao wa biashara kubwa duniani.

  “Tukifanikiwa hili, Tanzania itaingia kwenye mtandao wa biashara kubwa duniani. Biashara za Tanzania zitatangazwa kimataifa,” alisema Bishop.

  Alisema Tanzania ikiingia kwenye mtandao huo, vituo vikubwa vya kutangaza shughuli za biashara duniani kama vile televisheni ya Cable News Networking (CNN) na Shirika la Utangazaji la Uingereza (BBC), vitatangaza biashara za nchi hii.

  Alisema kwa sasa jopo hilo linatafuta mahusiano ya kibiashara na wafanyabiashara wazawa, lakini hatua nyingine muhimu ni Tanzania kunufaika na mpango huo.
  http://www.mwananchi.co.tz/newsrids.asp?id=18619
   
Loading...