Waimbaji wa makundi ya dini kushiriki kampeni | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Waimbaji wa makundi ya dini kushiriki kampeni

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by Anfaal, Aug 24, 2010.

 1. Anfaal

  Anfaal JF-Expert Member

  #1
  Aug 24, 2010
  Joined: Jan 19, 2010
  Messages: 1,157
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Hivi karibuni kwenye hutuba ya kuvunja Bunge Rais Kikwete aliwatahadharisha wananchi juu ya kuwatumia dini wakati wa kampeni. Lakini cha kustaabisha makundi ya dini yamekuwa yakiripotiwa kushiriki kikamilifu katika kampeni hizo.

  Hoja ni kwamba, hivi Chama fulani cha upinzani, kikitumia hivi vikundi vya dini kwenye kampeni tafsiri yake itakuwa ipi? Ni kwanini basi CCM yenye kujinadi kutenganisha siasa na dini isionyeshe hilo kwenye kampeni? Kwanini watu wanajifanya hawalioni hili?

  Na hawa jamaa walivyostrategic vikundi hivi vya dini hutumiwa katika baadhi ya maeneo ya nchi, ni kwanini wasitumie mikoa yoote mpaka Zenji? Tuanzie hapo...
   
 2. Rufiji

  Rufiji JF-Expert Member

  #2
  Aug 24, 2010
  Joined: Jun 18, 2006
  Messages: 1,710
  Likes Received: 161
  Trophy Points: 160
  Mzee unatania, yaani vikundi vya kwaya vinashiriki katika kampeni ? Hapana, hii ni chini ya mkanda. NEC wako wapi ? Tusipokuwa makini hawa walafi wa madaraka watatugawa. Kusema ukweli hili jambo limeniudhi mpaka ngozi yangu imesisimka.
   
 3. Nyambala

  Nyambala JF-Expert Member

  #3
  Aug 24, 2010
  Joined: Oct 10, 2007
  Messages: 4,470
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  Kumbe huwa kuna wakati macho yako yanaona eeh? Mimi nilifikiri na wewe ni wale binded CCM followers, otherwise good point bro!!!!!
   
 4. Abdulhalim

  Abdulhalim JF-Expert Member

  #4
  Aug 24, 2010
  Joined: Jul 20, 2007
  Messages: 16,472
  Likes Received: 126
  Trophy Points: 160
  Mimi wala hainibabaishi, watz wacha Mungu wale wanaofuata dini kwa vitendo hawazidi asilimia 1. Wangine tunatumia dini kama kisingizio tunapoguswa kwene maslahi yetu. nukta.
   
 5. Safari_ni_Safari

  Safari_ni_Safari JF-Expert Member

  #5
  Aug 24, 2010
  Joined: Oct 5, 2007
  Messages: 22,481
  Likes Received: 5,862
  Trophy Points: 280
  Bila bongoflava,Komba,Taarab na hizi kwaya CCM kamwe haitopata wasikilizaji.............watu wanajaa kusikiliza burudani.........na wengi wanaletwa kwa mabasi hawaji wenyewe....
   
 6. Nguruvi3

  Nguruvi3 Platinum Member

  #6
  Aug 24, 2010
  Joined: Jun 21, 2010
  Messages: 12,224
  Likes Received: 7,346
  Trophy Points: 280
  Niogezee tu, kuna gazeti moja limeonyesha viongozi wa dini wakiwa wamejipanga mwanza kumpokea mwenyekiti wa CCM na mgombea urais JK. Wamepewa kipaumbele mstari wa mbele na viongozi wa CCM. Viongozi wa dini wana haki ya kushiriki shughuli za kijamii kama raia wengine, lakini kwanini wasiachwe kujichanganya na wananchi wengine hadi inafikia wanapewa kipaumbele!!!!!!!!!!.
  Tumeambiwa tusichanganye dini na siasa, sijui ni haki kuchanganya siasa na dini. Tume ya uchaguzi haya hamyaoni hadi mtakaposikia watu wameanza kuvurugana?
  Hivi Dr Slaa akikusanya kwaya za kanisani na kaswida za misikitini na kuanza kuzunguka nazo katika helikopta atakuwa na tofauti gani na JK aliyelakiwa na Maaskofu na mashehe pale Mwanza.
  NEC Mnajua hatari za mambo haya au mumekaa kimya kwavile aliyewapa ugali ndiye anayepalilia wa kwake? mnaipeleka wapi nchi!
   
 7. Mwanamayu

  Mwanamayu JF-Expert Member

  #7
  Aug 24, 2010
  Joined: May 7, 2010
  Messages: 7,947
  Likes Received: 2,093
  Trophy Points: 280
  Tatizo kubwa ni kwamba Rais aliye madarakani sasa hivi ni mgombea wa CCM, hivyo si raisi kutenganisha mambo haya. Nionavyo mimi hao viongozi wa dini walifika hapo kumlaki kama Rais na si mgombea wa urais!
   
 8. Mwanamayu

  Mwanamayu JF-Expert Member

  #8
  Aug 24, 2010
  Joined: May 7, 2010
  Messages: 7,947
  Likes Received: 2,093
  Trophy Points: 280
  Hivi vikundi vya kwaya za dini kama wanaimba nyimbo za dini basi ni tatizo lakini kama wametunga nyimbo za kisiasa za CCM sioni shida. Shida kama wataanza kuimba nyimbo za dini na kumwiingiza JK, hapo ni issue kubwa tu! Mfano, "Yesu tunakushukuru kwa kutuletea Rais kijana na handsome, Dr. JK, kuwa kiongozi wetu bora, Mungu twa kushukuru, Mungu twakuomba umpe afya njema, na kwa maombezi ya Bikira Maria mama wa Mungu..." La! Kama ni wimbo aina hii basi Advocate Tendwa, Jaji Lewis na wengine lazima waindoe CCM kwenye kinyang'aniro hiki mara moja!!!!!!!!!
   
 9. DOUGLAS SALLU

  DOUGLAS SALLU JF-Expert Member

  #9
  Aug 24, 2010
  Joined: Nov 13, 2009
  Messages: 11,659
  Likes Received: 4,755
  Trophy Points: 280
  CCM hata wangevunja sheria vipi hakuna wa kuwagusa, NEC ni maliyao, Msajili wa vyama ni kada wao, majeshi yote ya ulinzi na usalama yanapokea amri toka Lumumba. Ila kwa upande wa hao waimbaji wa nyimbo za Injili kwenda kuikampenia CCM ni kuanguka kiroho, kwani Injili ni habari njema iletayo wokovu, sasa wao kujiunga na mafisadi hiyo tena si habari njema, kwani hata hizo hela wanazolipwa hela chafu.
   
 10. Lekanjobe Kubinika

  Lekanjobe Kubinika JF-Expert Member

  #10
  Aug 24, 2010
  Joined: Dec 6, 2006
  Messages: 3,067
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  Kweli!
   
 11. H

  Hashvene Member

  #11
  Aug 24, 2010
  Joined: Aug 22, 2010
  Messages: 6
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hiyo ni misuse ya kipaji ambacho wamepewa na Mungu ili kumtumikia sasa kama wao wanaitumikia CCM kwa nyimbo na mapambio,hiyo sio njia ya kushiriki katika siasa.Labda kuna mungu kawafunulia katika maono wamfanyie hiyo kazi...,lakini sidhani kwani kuna maono mengi waliofunuliwa na hawakutenda labda kuna kitu kidogo kutoka kwa "mungu" wakishiriki kuimba ktk kampeni
   
 12. Muadilifu

  Muadilifu Senior Member

  #12
  Aug 24, 2010
  Joined: Sep 26, 2007
  Messages: 150
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Kama kuna sehemu iliniudhi sana, basi ni kuona viongozi wa dini wamejipanga mstari mbele kabisa kumlaki mgombea urais kwa tikiti ya CCM. Sina hakika kama waliingizwa mkenge au walikuwa wanajua wanachokifanya. Hawa ni viongozi ambao waumini wao ni wanachama wa vyama mbali mbali tofauti tofauti. Sasa hawa waumini wachukue uamuzi gani kama tayari viongozi wao wameamua kuegemea upande mmoja. Labda niambiwe kuwa watajipanga hivyo hivyo kuwapokea kina Mutamwega, Prof Lipumba, Dr. Slaa na wagombea wengine wote.

   
 13. kaburunye

  kaburunye JF-Expert Member

  #13
  Aug 24, 2010
  Joined: May 12, 2010
  Messages: 675
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Ni kikundi gani hicho cha kwaya kimetumika kwenye kampeni?? Itabidi niongee na Rozi Mhando awe anaambatana na Dr Slaa kutoa burudani wakati wa kampeni kama hii maneno inaruhusiwa. Malaria Sugu a.k.a Jeykey uko wapi kutoa comments zako katika hili??? Kama ingetokea kwa CHADEMA ungehukumu haraka kuwa CHADEMA ina udini.
   
 14. N

  Nanu JF-Expert Member

  #14
  Aug 24, 2010
  Joined: May 29, 2009
  Messages: 1,224
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Ni kweli FLORA Mbasha na kundi lake walishiriki kampeni za Mwanza. Angalia kwenye blog ya michuzi.
  Hata hawa vijana wa Bongo Flavour badala ya kuwa kioo cha jamii nao wanaambatana na Kikwete kwenye kampeni. Ilitakiwa katika miziki yao walenge jamii nzima na siyo mgombea au chama fulani. Nao sasa wamekuwa TOT (wanamilikiwa na CCM?) Je Sheria za kampeni zinafuatwa kwa hili?
   
 15. Safari_ni_Safari

  Safari_ni_Safari JF-Expert Member

  #15
  Aug 24, 2010
  Joined: Oct 5, 2007
  Messages: 22,481
  Likes Received: 5,862
  Trophy Points: 280
  MALARIA SUGU yuko lupango na akiwa huku alizirai saa 9.32 siku ya jumamosi
   
 16. Anyisile Obheli

  Anyisile Obheli JF-Expert Member

  #16
  Aug 24, 2010
  Joined: Dec 13, 2009
  Messages: 3,304
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 135
  uko sahihi mkuu,laiti Mungu angetupa japo jicho la roho kidogo hata hao waliotumika na ccm kukampeni si wana dini
  bali watafuta vya ufalme wa dunia tu, hawana lolote, nyimbo hizo siyo mahali pake huu ni uhuni wazi wazi
   
 17. m

  mramba Member

  #17
  Aug 24, 2010
  Joined: Jul 23, 2009
  Messages: 30
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hivi karibuni kwenye hutuba ya kuvunja Bunge Rais Kikwete aliwatahadharisha wananchi juu ya kuwatumia dini wakati wa kampeni. Lakini cha kustaabisha makundi ya dini yamekuwa yakiripotiwa kushiriki kikamilifu katika kampeni hizo. Hoja ni kwamba, hivi Chama fulani cha upinzani, kikitumia hivi vikundi vya dini kwenye kampeni tafsiri yake itakuwa ipi? Ni kwanini basi CCM yenye kujinadi kutenganisha siasa na dini isionyeshe hilo kwenye kampeni? Kwanini watu wanajifanya hawalioni hili? Na hawa jamaa walivyostrategic vikundi hivi vya dini hutumiwa katika baadhi ya maeneo ya nchi, ni kwanini wasitumie mikoa yoote mpaka Zenji? Tuanzie hapo...

  mjomba ck hizi sio zile za kale watu walipokuwa wanamwimbia Mungu kwa ajili ya utukufu wake....
  ck hizi wapo kimaslahi zaidi kwani Gospel zimeonekana zinalipa kuliko miziki mingine. Hivyo hao hawana wito wa kumtumikia Mungu
   
 18. Takalani Sesame

  Takalani Sesame JF-Expert Member

  #18
  Aug 24, 2010
  Joined: Jun 24, 2008
  Messages: 588
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Hao ndio CCM, wazee wa double standard..kujisaidia ajisaidie kuku akijisaidia bata kahara. Hapo hujagusa matumizi ya rasilimali za serikali kwa ajili ya chama. Hapo hujagusa utekaji nyara wa ziara za kiserikali kuguezwa kuwa za chama! Safari ni ndefu lakini tutafika tu!
   
 19. Livanga

  Livanga JF-Expert Member

  #19
  Aug 24, 2010
  Joined: Apr 15, 2010
  Messages: 458
  Likes Received: 29
  Trophy Points: 45
  Dada mbasha mimi nikiwa kama mmoja kati ya fan wako nimesikitishwa sana na kitendo cha wewe kukubali kuchanganya siasa na dini wakati hata yesu mwenyewe hakupenda vitu ivyo vichanganywe. nakumbuka alisema vya kaisari mpe kaisari na mungu mpe mungu.

  how can submerge urself like that sisiter, u have disapointed alot of ur fans and beginning to wonder what will happen next. are u goint to be Pastor Chrispher Mtikila. manake hatima ya kuchanganya mambo haya mawili siku zote inaishiaga kubaya.

  CHONDECHONDE

  MUNGU IBARIKI TANZANIA
   
 20. Mpambalyoto

  Mpambalyoto JF-Expert Member

  #20
  Aug 24, 2010
  Joined: Mar 26, 2010
  Messages: 752
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  1. Njaa si imani, ni siasa
  2. Angeimbia vyama vingine ni udini
   
Loading...