Wahusika Daraja La Kigamboni Mnasubiri Hili Jiwe/Tofali Liangukie Gari??!!

RRONDO

JF-Expert Member
Jan 3, 2010
51,719
107,771
Hivi kuna watu wanakagua hili daraja au wamekaa ofisini na kwenye vile vibanda kukusanya hela? Wiki mbili zilizopita nilipita hapo darajani nikaona nguzo imegongwa na hii kingo ya flyover. Ile nguzo sasa hivi imeondolewa, ila hili tofali bado lipo pale pale na limekaa vibaya sana kuegamia chini ambako kuna magari yanapita.

Inahitaji nini kuliondoa na kulirudisha hapo lilipochomoka? Au mnasubiri liangukie gari au mtu mwingine agonge hapo ashuke nalo chini?!!

upload_2017-11-7_9-46-58.jpeg
 
Huyo Jamaa aliyegonga hapo inaonekana alikimbia, sasa kuanza mchakato wa kujenga bila kunyoosha maelezo ya traffic inakuwa ngumu. Ndo maana unaona hawa Jamaa wamenyuti.

Inavyoonekana ni gari ndogo na ni nyeusi... Tafadhali wenye gereji toeni ushirikiano.
 
Gari ndogo isingeweza kukimbia. Maanake imegonga nguzo ya taa kwanza ikalazwa chini ndio akapiga na hio kingo, gari ndogo kung'oa hio kingo hawezi kukimbia.
 
KWELI MADEREVA TZ WASHAMBA TAYARI MMESHAGONGA NGUZO ZA DARAJA, IPO SIKU DEREVA ATATUMBUKIA BAHARINI, NA FLYOVER ITAKUWAJE ?
 
3 Reactions
Reply
Back
Top Bottom