Wahuni wa Ghana walivyoiliza Idara ya Ulinzi ya Marekani kwa zaidi ya miaka 10

Personal experience

Sept mwaka jana ilikuwa mara yangu ya kwanza kukanyaga ardhi ya Marekani. Kuna vitu viwili-vitatu nikuwa navifanya pale Arlington City, Washington DC.
59903e10df0c4bfef39b7f1dae6b8812.jpg

Nikiwq nakatiza mitaa ya Crystal City, DC.

Nikiwa na mwezi mmoja tu tangu nimalize shahada yangu ya UDSM, sikuwa na familia (mke + watoto), sikuwa na assets kama hati ya nyumba, shamba, kiwanja na kadhalika, hivyo nilipitia vikwazo vingi sana hadi kupatiwa visa ya Marekani. Kitu kimoja kilichonisaidia ni kwamba nilikuwa nimesajili kampuni ya biashara, operations zilikua zimeanza miaka miwili iliyopita, na account ya biashara ilikuwa ina digits zisizo na shaka, biashara ilikuwa tayari ina assets za kutosha za kuprove kuwa lazima nitarudi nchini. Hivyo nikafanikiwa kuwa granted visa ya Marekani daraja B-1/B-2.
5a952c55030548909120070648ffb476.jpg


Kimsingi ili kupata visa ya US inabidi uthibitishe beyond reasonable doubts kuwa ukisafiri kwenda US utarudi nchini kwako ndani ya muda uliopanga na si kuzamia.

Process nzima ya kupata visa haikuwa lelemama, ulikuwa ni mchakamchaka ambao kiukweli unanyima usingizi.

Tuendelee...

Kwanza kabisa niseme tu wazi, mimi ni 1st generation katika familia/ukoo wetu kwenda US, hivyo sikuwa na guidance yoyote, sikufahamiana na mtu yoyote ambae angeweza kuniongoza, sikuweza kufetch experience yoyote, hivyo ilinilazimu nikomae kivyangu.

Process ya kupata Visa ilianza kwa kujaza online form inayoitwa DS 160 iliyopo kwenye web ya embassy ya Marekani. Ile form ni ndefu sana, ina maswali mengi mno, mengi yalikuwa ni very technical na ya kiintelijensia sana. Niliumiza kichwa sana kuhakikisha naijaza kwa umakini. Nilitumia karibu siku 5 hadi kuisubmit - hata kabla sijaisubmit niliirudia mara 10_10.

Baada ya kusubmit hatua iliyofuata ilikuwa kwenda Citi bank ipo pale Posta, nikalipa $160. Baada ya kulipa nikapata codes fulani ambazo nilizitumia kuomba interview slot. Nakumbuka siku ya interview niliomba iwe Jumatano saa 2 asubuhi.

Hapo tayari nimeshapata tetesi jinsi ambavyo Waafrika wananyimwa visa ya Marekani, nikaGoogle kwamba Marekani wanaingiza $56 mil kila mwaka kutoka Afrika kwa visa vinazokataliwa. Nilikuwa na hofu kubwa sana, hasa nikizingatia nilikua kipindi ambacho sitaki kupoteza hata 'Jero'.

Siku ya interview nikajiandaa vizuri sana, tayari nimekunywa nondo za kutosha kutoka Google, nikabeba makabrasha na documents zangu zote, nikavaa kiheshima haswaa (vijana wa kileo wanasema 'mapigo ya kifaza'), nikafika pale embassy hata kabla ya muda (kuzuga kuonesha kuwa sina mambo ya kiafrika ya kuchelewa).

Pale nilipigwa search ya kufa mtu, nikaacha vitu vyote security nikaingia sehemu ya kusubiri interview. Ni eneo la wazi ambapo watu wote waliopangiwa kufanya interview siku hiyo wanakaa.

Tuliokuwa na interview siku hiyo tulikuwa kama watu 30, kulikuwa na msanii mmoja maarufu (sitamtaja jina), pia alikuwepo mtoto mmoja maarufu wa Raisi Nyerere na pia alikuwepo jamaa mmoja wa TISS ambae yeye alitumwa na waziri fulani (huyu jamaa hakupitia process zozote, aliweka documents zake pale pa'kufanyiwa interview, akapewa maelekezo kisha akasepa).

Kabla interview hazijaanza tuliweka kaplatform uchwara tukawa tunadiscuss mambo kadha wa kadha hasa uchaguzi wa US. Yani mimi ndio nilijiona kilaza, kuna jamaa anajua vitu vyote inside-out vinavyoihusu US na blah blah kibao. Alikuwa anamwaga nondo kuhusu Marekani, miji yake, utamaduni wa Wamarekani, Siasa za marekani, akaanza kutoa 'tips' za maswali ya interview ya kupata visa (nilikuja kugundua kuwa huyu jamaa ni member humu JF - japo sikuweza kung'amua identity yake). Hakika Huyu jamaa alinipa hofu sana, nilihisi kwa nilivyo 'shallow' lazima nitanyimwa Visa - nikajipange vizuri zaidi.

Pia kuna mama mwingine tulikuwa nae akawa anasema alivyojaribu kuomba visa na kunyimwa kila mara, ile ilikuwa mara yake ya 5 anaitwa kwenye interview. (Kumbuka: ukiwa rejected kwenye interview, inabidi urudi uanze application upya na utalazimila kulipa $160 upya), kwa mantiki hiyo, mama yule tayari alitumia $640 kuapply visa). Swala la huyu mama liliniongezea hofu, sikutaka tena story za kijiwe cha mule ndani. Nikajitenga pembeni nikachukua vitabu fulani vya utalii vilikuwa pale nikawa nasoma soma.

Sasa muda wa interview ukaanza, mtu mmoja mmoja anapita kwa ndani kidogo, kuna kidirisha (kama bank kwa teller), then anaanza kuhojiwa na wafanyakazi wa pale embassy. Mtu anayekubaliwa visa basi analazimika kuacha passport yake pale na kupangiwa tarehe ya kuja kuchukua visa yake. Asiyekubaliwa anapewa vitu vyake vyote aondoke navyo.

Katika watu 30, mimi nilikuwa wa 23. Watu wengi walionitangulia walikuwa wananyimwa visa, wengine hadi wanalia pale dirishani. Kiukweli kwenda US ni kama 'dream come true' kwa sisi ambao tulitokea 'the other side of poor neighbourhoods'.

Yule jamaa wa JF aliyekuwa anajua vitu vyote vya States akafika pale dirishani akiwa na mbwembwe nyingi, anapiga kingereza kidogo kisicho na kigugumizi tofauti na mimi. Sikuweza kusikia mahojiano yao, lakini Kitu kilichonistua yule jamaa alirudi na passport yake mkononi, kuashiria kua amenyimwa visa. Pale matumaini ya kupata visa yakaniishia kabisa, moyo ukafadhaika sana. Yule mtoto wa Nyerere aliacha passport yake pale, lakini pia yule msanii alinyimwa.

Zamu yangu ikafika. Moyo ulikuwa unatokota na uwoga 'si wa nchi hii'. Nilivyofika pale dirisha la interview yule jamaa akagundua nina hofu ya hali ya juu sana.

Mahojiano yakaanza. (Hapo ninatetemeka kwa hofu na woga).

Consular: Morning!

Mimi: Yes! Morning

Consular: Akatabasamu kidogo, kisha akauliza - Your sir please!

Mimi: Nikiwa sijitambui nikajibu - Yes sir please .

Jamaa akasmile tena, akaniuliza kwa kiswahili cha kuunga unga. Aiseee!! Hapo nilifunguka si mchezo.

Tulivyoendelea na conversation ndivyo nilivyozidi 'kugain momentum' hadi nikawa kwenye hali yangu ya kawaida.

Statement ya mwisho ikawa "Congratulation sir, you've been granted the US visa, leave your passport with me, and you'll collect it tomorrow together with your visa". Aisee! Feeling ile ilikuwa ya kipekee sana sana. keshowe nilivyokuja kuchukua visa tulikuwa watu wanne tu kati ya wale 30 tuliofanyiwa interview.

Lakini still baada ya kupata visa yangu nilijiuliza sana kwanini US inatubania kupata visa zao?
Kwanini processes ni nyingi mno? kwanini gharama ni kubwa mno?
Je hakuna alternative ya kuingia US bila usumbufu wote huo?

After all sikujali sana kwa sababu tayari nilishapata visa yangu, na vile isingenisaidia kitu kuhoji masharti kila nchi inayojiwekea katika kukaribisha wageni.

Lakini kitu kilichonishangaza zaidi ni wakati nilipofika DIA - Dulles International Airport.

Nikiwa kwenye foleni wakati wa passport control nikamuona black mmoja kasimamishwa muda mrefu sana pale dirishani kwa 'immigration official', lakini white walikua wanapita fasta sana (hata hawakuchukua zaidi ya dakika 1).
28c653aa4fe986c38c81601906f5b192.jpg


Zamu yangu ikafika. Nilipofika tu pale dirishani jamaa kwanza aliniangalia usoni kwa sekunde kadhaa na mimi nikamkazia jicho, 'mubashara' (live) kabisa bila kupepesa kope. Akaniomba passport, nikampa. Akaipitia page baada ya page - kisha akaniuliza "What took you to all these countries?". Kwasababu nilijua nipo 'clean' na nina makaratasi yote muhimu, nikamjibu kwa dharau "I cleared it out when I was in those countries, now I'm in the US - ask me about US". Jamaa akaScan kwanza passport yangu, then akaendelea kunihoji maswali yake ya kiintelijensia. Mimi wala sikutaka kuongea sana, hasa ukizingatia ngeli imekaa kushoto , nilichokifanya ni kumjibu kila swali kwa maelezo machache na kumpa makaratasi. Nilikaa pale kwa dakika 16 - to be exact.
db5af0c14ce4e8184eb51154c0d3b389.jpg


Nilivyoruhusiwa nilijiuliza sana, kwanini hawa jamaa wako 'so arrogant' na nchi yao na wanadharau sana. Nilitamani na sisi waAfrika tuwe na kauwezo ka kuwashikisha adabu na kuwakomoa hawa jamaa.
e7cf991d82e1af7b880d7c5f7df50267.jpg
Muonekano wa nje kutoka kwenye dirisha la hotel room nilipofikia

Watoto wa Accra wakanipa sababu ya kuwadharau Marekani na vyombo vya ulinzi na usalama.

Jumanne Nov 8 2016 dunia yote ikielekeza macho kufuatilia uchaguzi mkuu wa Marekani. kuna jambo kubwa sana lilitokea Accra ambalo lilikosa 'Air time' mubashara kutokana na media zote kuelekeza nguvu kwenye uchaguzi mkuu wa uraisi. Tukio hili la kustaajabisha, lililosukwa kwa akili kubwa sana na wahuni wa Ghana, na lilinipa sababu ya kuwaona Wamarekani ni 'watupu'.

Kwa zaidi ya muongo mmoja bendera ya marekani ilikuwa inapeperushwa nje ya jengo kuu-kuu la rangi ya pink katikati ya mji mkuu wa Ghana, Accra.

Mgeni yeyote aliyeingia ndani ya jengo hilo alikutana na picha kubwa ya Rais Barack Obama ikining'inia ukutani. Mapokezi-mezani kulikuwa na kitabu cha wageni chenye seal halali ya idara ya ulinzi ya Marekani. Kila mgeni alikabidhiwa coupon yenye maelekezo, na mwisho kulikuwa na maandishi "Welcome to the US embassy in Ghana".
be13a8e86278a975d03e5fc65338b524.jpg


kijana machachari na mipango ya kibabe

Mwaka 2004 kijana wa umri wa miaka 23 aitwae Yaw Kwabedo anahitimu shahada ya sheria ya chuo kikuu cha Ghana - idara ya sheria. Alihitimu akiwa mmoja wa wanafunzi wenye ufaulu wa juu zaidi darasani kwake.

Kama ilivyo kwa vijana wengi wa Afrika Magharibi, Yaw alikua na ndoto na matamanio ya kwenda na kufanya kazi Marekani kama mshauri wa masuala ya kisheria katika makampuni makubwa.

Aliandaa makabrasha yake yote muhimu, kisha akaanza mchakato wa kupata visa ya Marekani. Aliomba visa mara 4 lakini alinyimwa, alipoteza kiasi kikubwa cha pesa lakini bado aliziishi ndoto zake. Ilimbidi auze baadhi ya mali za nyumbani kwao ikiwemo simu pamoja na runinga, kisha akaomba visa kwa mara ya 5. Lakini bado hakufikia vigezo, akanyimwa tena. Aliumia mno.

Kwabedo aliamini fika kuwa Ubalozi wa Marekani umemdharau na kumdhalilisha. Hivyo, 'piga - uwa - galagaza' atafanya kila awezalo kulipiza kisasi ambacho aliamini lazima angeidhalilisha marekani katika uso wa dunia. Aliapa gharama zake zote alizotumia kuomba visa na kunyimwa zingerudi, pamoja na fidia juu. Aliapa kuwawezesha waghana wote watimize ndoto zao za kuishi Marekani.

Kisasi kinasukwa kwa ustadi wa hali ya juu sana

Feb 2005, Yaw akiwa anatimiza miaka 24 alimwita rafiki yake wa karibu ambaye alihitimu mafunzo ya uhandisi wa kompyuta, kisha akamshirikisha wazo lake ambalo lililenga kuidhalilisha Ubalozi wa Marekani, Idara ya ulinzi na usalama pamoja na vyombo vya kiintelijensia vya Marekani. Huyu rafiki alisita sana akihofia uwezo na nguvu waliyonayo Maafisa wa ulinzi wa Marekani. Lakini Yaw alifanikiwa kumshawishi, na wakaendelea na mipango.

Yaw alihitaji funding, hivyo aliwaingilia watu wenye uhasama na Marekani na kuwashirikisha mpango wake, aliwaendea Waturuki, akawafafanulia vizuri ramani nzima ya mpango aliousuka. Dili likakubali. Hawa Waturuki pia wakaleta jamaa zao Waholanzi wakaunganisha nguvu na resources.

Yaw akaingia Ghana akakodi jengo kubwa lilolopo barabarani kabisa. Akajenga mlingoti kisha akaning'iniza bendera ya Marekani. Material aliyotumia inafikirisha sana - ukiwa mbali ni bendera ya Marekani iliyopungua namba ya nyota _ kati ya zile nyota 50, na kadri unavyozidi kuisogelea rangi inafifia hadi mwisho ukiifikia inakuwa bendera ya Ghana.
63f4fe1bb6c1084c1b2c60bafa92055c.jpg
Jengo lililopeperushwa bendera ya marekani kwa miaka 10.

Yaw akawaomba waturuki wale watafute 1st grade fingerprint scanner. Yule mhandisi akapewa jukumu ya kutambua software systems zinazotumiwa na Ubalozi wa Marekani. Kisha Wakazinunua kutoka kampuni kubwa ya Marekani ya mitandao. Hivyo waliweza kung'amua processes zote zinazotumiwa na wafanyakazi wa Ubalozini (consular).

Nje ya jengo lile Yaw akafunga satellite 2 za usalama, na pia nje kidogo ya lile jengo akafungua duka dogo la kuuza nguo na viatu.

Wakakodi apartment za hali ya juu na kununua magari kadhaa ya kusafirisha abiria.

vyombo vya ulinzi, usalama na uhamiaji vilivyodhalilishwa

Mwaka 2006 mpango mzima unaanza kutekelezwa rasmi. Yaw na team yake wakaanza kuingia mavyuoni, mitaani, vijiweni, vijijini, mjini pamoja na nje ya balozi halisi ya Marekani na kuzungumza na Waghana waliotoswa visa ya kuingia Marekani.
9a5c856d8a3e90ab6e5f2de453d1776b.jpg
Ubaalozi halisi ya Marekani nchini Ghana.

Wote waliokubali mpango wa kina Yaw wakawasafirishwa hadi Accra karibu na ofisi yao, wakawapa hifadhi katika apartment walizokodi pamoja na chakula.

Kisha kila asubuhi walifatwa kutoka wanapoishi na kupelekwa ofisini, huko michakato ya kutengeneza visa bandia ilifanyika kwa ustadi wa juu sana.

Waliweza kufoji vyeti vyote kwa kiwango cha daraja la kwanza, kuanzia taarifa za kibenki, hati za umiliki wa mali, hati za kuzaliwa, vyeti vya daktari, barua za mialiko, barua feki za kupata kazi na admissions za chuo n.k.

Kwa umakini uliotukuka, visa ya kwanza ilitengenezwa, kisha mteja akalipiwa gharama zote za kuingia Marekani na team ya Yaw. Huyu alitolewa kama chambo kuthibitisha uhalisia wa visa hiyo. Baada ya masaa 26 ya safari, Yaw alikenua meno yote 32, pamoja na timu yake wakapiga mvinyo wa pamoja baada ya yule jamaa waliyemtoa chambo kupokelewa na kukaribishwa Marekani kwa visa yao waliyoipika jikoni.
4a2bf975d43d550cf898d454d7c2f251.jpg
Sampuli tu ya visa ya Marekani.

Lengo la muda mrefu la Yaw lilionekana kutimia. Mamia kwa maelfu ya Waghana wakawa wanachongewa visa za kuingia US. Huduma yao ikashamiri hadi nchi za jirani kama Cote d'Voire, Togo na Nigeria. Baada ya muda kidogo nchi za mbali kama Kenya, S.A, India, Palestine, Cameroon n.k. nazo zikaanza kupatiwa huduma.

Wakaanza kujitangaza chinichini kupitia vipeperushi, billboards na magazeti ya udaku. Yaw na timu yake wakaanza kupiga pesa ndefu sana, wateja walimiminika si kawaida. Ilifika kipindi gharama zikapanda hadi kufikia $6000, watu bado walimwagika - walipiga pesa sana. Hakika idara ya Ulinzi (department of Defence) ilidhalilishwa kupita maelezo, tena na kijana wa kawaida kabisa, mbaya zaidi - hawakudhalilishwa kwa masaa kadhaa ama siku kadhaa, bali ndani ya miaka 10 na miezi kadhaa.

Marekani anaamka usingizini - Operation Spartan Vanguard.

Nov 15, 2015 idara ya uhamiaji inashtuka baada ya kugundua kua kuna idadi kubwa sana ya wananchi wa baadhi ya nchi wanapata vibali vya kuingia Marekani, ilhali nchi hizo awali hazikuwa na idadi kubwa ya wananchi wake wanaoingia Marekani.

Upelelezi unaanza... Idara ya ulinzi inatoa tamko la kusitisha kutoa visa kwa baadhi ya nchi kwa muda wa mwezi mmoja. Mshangao mkubwa unaibuka; balozi hazitoi visa, lakini kuna watu bado wanaingia Marekani kwa visa mpya kabisa zinazoonesha wamezitoa ubalozini.

Msako 'wa kufa mtu' unapigwa, wasafiri wote wenye visa mpya kutoka nchi ambazo Marekani ilisitisha kutoa visa zao wanaanza kupelelezwa (interrogated). Pole pole wakaanza kukusanya taarifa, hadi wakafika conclusion kuwa kuna wahuni Ghana ndio wamesababisha fedheha hiyo kwa nchi kubwa yenye ulinzi wa hali ya juu zaidi.

Uvamizi katika ubalozi bandia wa Marekani - Vyombo vya usalama vya Marekani vilitambua fika kua Yaw na timu yake hadi kuweza kufanikisha zoezi la kuidhalilisha Marekani, walijipanga sana. Hivyo, hata wao walibidi 'wajikoki' haswa wasijekudhalilika tena. Zoezi zima la uvamizi halikuwa la 'kispoti spoti'.

Uvamizi huo ulipewa jina la 'Operation Spartan Vanguard'. Kiufupi, operation 'spartans' zote huanzishwa na Marekani kwenye mashambulizi ambayo vikosi vya usalama vimeshindwa kabisa kupata taarifa za awali juu ya eneo wanalopanga kushambulia, hivyo wanajipanga vizuri sana na kwa tahadhari ya juu kwakuwa wameshindwa kumsoma vizuri adui yao. Mara nyingi operatins hizi hazinaga mwisho mzuri. Mfano ni :- Operation Spartan Shield, Operation Spartan Strike, Operation Spartan Fury, Operation Spartan Jordan n.k.
7b3f588f260dfb297934a87df7487750.jpg
Wanajeshi katika 1 ya operation spartan.

Kikosi cha maangamizi kilishiba haswa, hawakufahamu kuwa adui zao ni watu 'walaini'. Kikosi kiliundwa na askari wa Ubalozi wa Marekani, maafisa wa polisi wa Ghana wenye mafunzo ya kijeshi ya Marekani, Taasisi ya upelelezi ya Ghana (Ghana detective bureau), kikosi cha kimataifa maalumu kwa kupamba na uhalifu, askari wa Ubalozi wa Canada, Askari wa uhamiaji wa Marekani pamoja na INTERPOL.

Tena na tena kwa mara nyingine Marekani anadhalilishwa, dunia nzima inamkodolea macho. Kina Yaw wanaisambaratisha Marekani kiulaini kabisa.

Yaw pamoja na timu yake wakiwa ndani ya ofisi yao, tayari walielewa mchezo mzima uliokuwa unaendelea, hawakuwa na papara, hawakuhutaji kujaza risasi kwenye magazine zao. Waliweza kutazama movie nzima wakivamiwa 'mubashara' (live) kupitia satellite mbili walizotegesha nje ya jengo lao.

■ Satellite ya kwanza ilionesha eneo la kuingia ndani ya ofisi yao. Hivyo adui asingeweza kuwafikia bila wao kumshtukia.

■ Satellite ya pili ilionesha usalama la eneo lao la siri la maficho.

Walivyoona wanavamiwa walimuita mmoja wa kijana wa kazi kisha wakampa kichupa, na kumuagiza akifungue kisha akitupe kwenye 'dustbin' ambayo ilikua mlango wa kuingilia. Kichupa hiko kilikuwa ni 'lachrymation spray' - hii ni chemikali kali sana yenye kusababisha muwasho mkali mno sehemu za wazi za mwili (macho, masikio, pua, skin pores, na yale mashimo mengine ya ndani ya c.hupi).
a526cf6eb3d020905776b02a24ebce60.jpg
askari wa Spartan vanguard wakihenyeshwa.

Baada ya hapo Yaw na team yake wakatoroka kupitia 'built in tunnels' - mifereji ya ndani, ambayo ilipita chini kwa chini na kutokea kwenye lile duka la nguo na viatu nje ya ofisi yao. - Baada ya hapo lazima waingie bar kupongezana .

Kikosi kazi kile cha Wamarekani kiliambulia muwasho 'wa upupu' na kuwakamata baadhi ya wafanyakazi ambao wala hawakuelewa shughuli haramu ziliyokuwa zikiendelea mule ndani.

Upelelezi bado unaendelea, hadi leo kiongozi mkuu wa shambulizi la Spartan vanguard hajaeleza kupatikana kwa wahalifu wakuu na dau nono tayari limetangazwa kwa atakayefanikiwa kukamatwa kina Yaw.

Katika uvamizi huo vitu kadhaa vilipatikana vikiwemo passport 190 (kutoka nchi 10 tofauti), printer 5 za kisasa, HD camera, mihuri bandia 75, laptop 8, smartphones pamoja na documents zinginge nyingi.
d38d5d54bf34e204c7e58851e2882e83.jpg
baadhi ya vitu vilivyopakipatikana
6bbb9b66110e3f4c1b0f583de4d5267a.jpg


Kinachowaliza zaidi taasisi za usalama za Marekani

Wizara ya ulinzi, kitengo cha uhamiaji na maafisa wa usalama wa Marekani wameshindwa kabisa kung'amua mafumbo yafuatayo;-

○Wahuni wa Ghana wenye teknolojia ya kawaida kabisa wamewezaje kukamilisha zoezi 'sensitive' kama hilo kwa zaidi ya muongo mzima?!

○Wameshindwa kung'amua ni visa ya daraja gani ilikuwa inatengenezwa na wahuni hao?!

○Wameshindwa kabisa kung'amua utofauti kati ya visa halali na visa bandia.

○Wameshindwa kung'amua idadi kamili ya watu walipewa visa hizo, wangapi walirudi nchini kwao na wangapi bado wanaishi Marekani.

○Wameshindwa kung'amua jinsi gani wataweza kuwatambua na kuwakamata waliokabidhiwa visa bandia na kuingia Marekani.

○Watawezaje kumzuia Yaw na team yake kuendelea kuchapisha visa hizo bandia. Vipi kama wakiunganisha nguvu na maadui wao wakubwa?!

○Wameshindwa kabisa kupata 'identity' kamili ya Yaw na team yake. (Kwa kifupi jina la Yaw ni la kufikirika tu - uchunguzi unaendelea).

○Je ni kivipi wataweza kujisafisha na fedheha hiyo katika dunia paba ya kiintelijensia - watawezaje kuficha udhaifu wao??

My take

Wakati dunia nzima ikiiheshimu na kuisujudia marekani katika swala la ulinzi na usalama, bado naamini kuna vitu vingi vinahitaji kuwa 'fixed'. Nakubali Jeshi lao ni pana sana, lina maaskari wengi na wenye uwezo na fitness nzuri, wamewekeza pesa ndefu, wana miundombinu, vifaa, mbinu na teknolojia za hali ya juu, lakini akitokea mtu mmoja tu mwenye nia thabiti, anaweza 'kuwachambua kama karanga', kuwageuza kama chapati na kiwadhalilisha kwa kadri atakavyo machoni mwa kila mtu, tena mchana kweupeee.

-Meanwhile nafuatilia mubashara uzi wa mkuu The bold jinsi Usama bin Laden alivyowashikisha ukuta Wamarekani.

Baadhi ya taarifa nimepakua kutoka Source mbali mbali za internet zikiwemo:-
BBC News How did fake US embassy operate in Ghana for a decade? - BBC News
US Department of staste Regional Security Office Ghana Shuts Down "Fake Embassy"
BBC focus on Africa BBC World Service - Focus on Africa, 04/12/2016 GMT
The Washington post Mobsters ran a fake U.S. Embassy in Ghana for 10 years, flying the flag and issuing visas for $6,000
Pamoja na source zingine nyingi.

~Ontario

ONTARIO;

Nikupongeze kwa namna ya pekee kabisa kwa namna ulivyoweza kuleta habari hii kwa umahiri mkubwa sana. Nachelea kusema kuwa kama wewe si mwandishi wa habari au Profesa wa masomo ya lugha, basi you must be extra-ordinarily gifted and intelligent.

Pamoja na hayo kuna mambo kadhaa naomba nijaribu kuchangia. tafadhali naomba nianze kwa kukuliuza maswali kadhaa.

Hilo jengo lililokuwa linapeperusha bendera ya Marekani, hiyo bendera ilikuwa inaonekana ya Marekani ukiwa bado uko mbali au ilikuwa inageuka kuwa ya Marekani baada ya kuwa umeikaribia? Na hiki kitu unadhani kilikuwa kinasaidia chochote kwenye plan yao akina Yaw? Na kwa namna yoyote ile, kwa nini Marekani hawakuweza kuchukua hatua wakati walikuwa wanaona kuna jengo wasilolielewa linapeperusha bendera yao?

Nachelea kusema kuwa hii habari inaweza kuwa ni scam kwa sababu kadhaa kama nitakavyozianisha hapa chini

MOSI:Ni pardox na ni impossible kwamba Marekani inaweza ikashindwa kumkamata mtuhumiwa ambaye tayari imeshamu-identify ambaye ni individual na si taasisi, tena kutoka Ghana.

PILI:Waliokuwa wanapewa VISA GENUINE za Marekani naamini mpaka leo wapo kwenye Database YA VISA zitolewazo na Balozi zote za Marekani duniani kote, na kwa idadi yao na majina yao, wakati wale waliokuwa wanapewa VISA FEKI na akina YAW, hawakuwepo na hawapo kwenye database hiyo

TATU: Kutokana sababu namba mbili hapo juu, wenye VISA FEKI hawakuwa na uwezo wa kupita kwenye sehemu zote za PASSPORT CONTROL kwa sababu kwa sabau PASSPORT CONTROL hawaangalii tu kwamba una VISA GEBUINE, wanaangalia pia kama jina lako lipo kwenye database yao ya watu waliowapatia VISA. Hii inamaanisha kuwa wakishaona VISA yako ni GENUINE lakini jina lako linamiss kwenye database yao, wanakuweka pembeni kwanza ili waangalie kwanza kuna kitu gani kimetokea, na hapo lazima wakukamate tu!

NNE: Swala la kwamba Marekani walishindwa kung'amua ni wangapi waliingia kwa VISA FEKI siyo sahihi kwa sababu hili lingekuwa swlaa la kujumlisha na kutoa tu. Walioingia na VISA GENUINE hata leo ukiiuliza Marekani inakupa idai yao kamili, hivyo wanaoongezeka kutoka hapo ndiyo wangeweza kuwa na VISA FEKI.

TANO: Haiwezekani mtu akafanya hujuma kwa Nchi yenye Teknolojia ya juu kama Marekani kwa muda wote huo wa miaka 10, ingekuwa kwa muda wa mwezi mmoja hapo ningeweza kuwa convinced. Kwa miaka 10 au hata mwaka mmoja tu ni IMPOSSIBLE! Hata kwa Nchi nyingine ndogo za kwetu hapa Afrika pia haiwezekani. Ingekuwa labda mwezi mmoja hapo ningeweza kufikiria kidogo

SITA: Waliokuwa wanafanya forgery ya VISA FEKI, walikuwa na lengo la kutokujulikana, kwa nini tena waamua kuweka Bendera ya US kwenye jengo lao wakati walikuwa wanajua kuwa ni forgery?

SABA:Umesema kuwa VISA ilifikia hadi dola 6,000 kitu kinachoonekana kuwa hata wateja wa VISA hizo walikuwa wanajua kuwa ni VISA hizo ni feki. Kama wateja walikuwa wanajua kuwa VISA ni feki na kwamba walikuwa wananunua kwa magendo, kulikuwa na haja gani ya wauza VISA kuweka bendera ya Marekani kwenye jengo lao?

NANE: Kulikuwa na mantiki gani ya kuweka Bendera ya US kwenye jengo feki la ubalozi wa Marekani wakati Ubalozi halisi wa Marekani ulikuwepo na ulikuwa unajulikana uko wapi?

TISA: Kwenye hujuma hizi, umetaja kuwa raia wa UTURUKI na UHOLANZI nao pia walihuiska . Sina uhakika sana kuhusu UTURUKI lakini UHOLANZI ni mshirika mzuri wa Marekani na EU, kwa hiyo haiwezekani raia wa Uholanzi kuhusika kwenye hujuma dhidi ya taifa la Marekani (Negen: U zei dat burgers van TURUKI en HOLIDAY ook in dit programma waren opgenomen. Ik ben niet zo zeker van DRAAI maar VAKANTIE is een goede bondgenoot van de Verenigde Staten en de EU, dus Nederlandse burgers kunnen niet deelnemen aan sabotage tegen de VS)

KUMI: Hapakuwa na haja ya kuweka picha ya Rais Obama ndaNi ya ofisi ambayo ilikuwa inatengeneza VISA FEKI, na ambamo wateja wake walikuwa wanaingia wakiwa wanjua kuwa wanaenda kununua VISA FEKI!

KUMI NA MOJA: Ukiangalia INITIAL INVESTMENT iliyotumika kattika maandalizi ya kutengeneza VISA FEKI na motive iliyosababisha mtu amue kutengeneza visa hizo, vinakosa uhusiano!

Na kama kweli habari hii ni ya kweli, basi marekani ilishawakamata wahusika ila wakaamua kuwatumia katika maswala mengine
 
Maswali yako kamwe autapata jibu kwasababu mtoa mada alishajiondoa jf
ONTARIO;

Nikupongeze kwa namna ya pekee kabisa kwa namna ulivyoweza kuleta habari hii kwa umahiri mkubwa sana. Nachelea kusema kuwa kama wewe si mwandishi wa habari au Profesa wa masomo ya lugha, basi you must be extra-ordinarily gifted and intelligent.

Pamoja na hayo kuna mambo kadhaa naomba nijaribu kuchangia. tafadhali naomba nianze kwa kukuliuza maswali kadhaa.

Hilo jengo lililokuwa linapeperusha bendera ya Marekani, hiyo bendera ilikuwa inaonekana ya Marekani ukiwa bado uko mbali au ilikuwa inageuka kuwa ya Marekani baada ya kuwa umeikaribia? Na hiki kitu unadhani kilikuwa kinasaidia chochote kwenye plan yao akina Yaw? Na kwa namna yoyote ile, kwa nini Marekani hawakuweza kuchukua hatua wakati walikuwa wanaona kuna jengo wasilolielewa linapeperusha bendera yao?

Nachelea kusema kuwa hii habari inaweza kuwa ni scam kwa sababu kadhaa kama nitakavyozianisha hapa chini

MOSI:Ni pardox na ni impossible kwamba Marekani inaweza ikashindwa kumkamata mtuhumiwa ambaye tayari imeshamu-identify ambaye ni individual na si taasisi, tena kutoka Ghana.

PILI:Waliokuwa wanapewa VISA GENUINE za Marekani naamini mpaka leo wapo kwenye Database YA VISA zitolewazo na Balozi zote za Marekani duniani kote, na kwa idadi yao na majina yao, wakati wale waliokuwa wanapewa VISA FEKI na akina YAW, hawakuwepo na hawapo kwenye database hiyo

TATU: Kutokana sababu namba mbili hapo juu, wenye VISA FEKI hawakuwa na uwezo wa kupita kwenye sehemu zote za PASSPORT CONTROL kwa sababu kwa sabau PASSPORT CONTROL hawaangalii tu kwamba una VISA GEBUINE, wanaangalia pia kama jina lako lipo kwenye database yao ya watu waliowapatia VISA. Hii inamaanisha kuwa wakishaona VISA yako ni GENUINE lakini jina lako linamiss kwenye database yao, wanakuweka pembeni kwanza ili waangalie kwanza kuna kitu gani kimetokea, na hapo lazima wakukamate tu!

NNE: Swala la kwamba Marekani walishindwa kung'amua ni wangapi waliingia kwa VISA FEKI siyo sahihi kwa sababu hili lingekuwa swlaa la kujumlisha na kutoa tu. Walioingia na VISA GENUINE hata leo ukiiuliza Marekani inakupa idai yao kamili, hivyo wanaoongezeka kutoka hapo ndiyo wangeweza kuwa na VISA FEKI.

TANO: Haiwezekani mtu akafanya hujuma kwa Nchi yenye Teknolojia ya juu kama Marekani kwa muda wote huo wa miaka 10, ingekuwa kwa muda wa mwezi mmoja hapo ningeweza kuwa convinced. Kwa miaka 10 au hata mwaka mmoja tu ni IMPOSSIBLE! Hata kwa Nchi nyingine ndogo za kwetu hapa Afrika pia haiwezekani. Ingekuwa labda mwezi mmoja hapo ningeweza kufikiria kidogo

SITA: Waliokuwa wanafanya forgery ya VISA FEKI, walikuwa na lengo la kutokujulikana, kwa nini tena waamua kuweka Bendera ya US kwenye jengo lao wakati walikuwa wanajua kuwa ni forgery?

SABA:Umesema kuwa VISA ilifikia hadi dola 6,000 kitu kinachoonekana kuwa hata wateja wa VISA hizo walikuwa wanajua kuwa ni VISA hizo ni feki. Kama wateja walikuwa wanajua kuwa VISA ni feki na kwamba walikuwa wananunua kwa magendo, kulikuwa na haja gani ya wauza VISA kuweka bendera ya Marekani kwenye jengo lao?

NANE: Kulikuwa na mantiki gani ya kuweka Bendera ya US kwenye jengo feki la ubalozi wa Marekani wakati Ubalozi halisi wa Marekani ulikuwepo na ulikuwa unajulikana uko wapi?

TISA: Kwenye hujuma hizi, umetaja kuwa raia wa UTURUKI na UHOLANZI nao pia walihuiska . Sina uhakika sana kuhusu UTURUKI lakini UHOLANZI ni mshirika mzuri wa Marekani na EU, kwa hiyo haiwezekani raia wa Uholanzi kuhusika kwenye hujuma dhidi ya taifa la Marekani (Negen: U zei dat burgers van TURUKI en HOLIDAY ook in dit programma waren opgenomen. Ik ben niet zo zeker van DRAAI maar VAKANTIE is een goede bondgenoot van de Verenigde Staten en de EU, dus Nederlandse burgers kunnen niet deelnemen aan sabotage tegen de VS)


Na kama kweli habari hii ni ya kweli, basi marekani ilishawakamata wahusika ila wakaamua kuwatumia katika maswala mengine

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom