Miss Zomboko
JF-Expert Member
- May 18, 2014
- 4,498
- 9,279
Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam imewafutia mashtaka na kuwaachia huru, washtakiwa watano waliokuwa wanakabiliwa na kesi ya uhujumu uchumi kwa kujiunganishia isivyo halali bomba la mafuta, mali ya Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA).
Uamuzi huo umetolewa leo, Septemba 23, 2019 na Hakimu Mkazi Mkuu wa Mahakama hiyo, Thomas Simba, baada ya Mkurugenzi wa Mashtaka nchini Tanzania (DPP) kuieleza Mahakama hiyo kuwa hana nia ya kuendelea na kesi hiyo.
Walioachiwa huru na mahakama hiyo ni Audai Ismail (43)mkazi wa Kibaha, Chibony Emmanuel, Roman Abdon, Amina Shaban na Zubery Ally.