Wahujumu uchumi,Malima na silaha ya SMG na matamshi ya Nassari polisi wanatenda haki? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wahujumu uchumi,Malima na silaha ya SMG na matamshi ya Nassari polisi wanatenda haki?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Salary Slip, May 10, 2012.

 1. S

  Salary Slip JF-Expert Member

  #1
  May 10, 2012
  Joined: Apr 3, 2012
  Messages: 24,948
  Likes Received: 37,461
  Trophy Points: 280
  Watanzania wenzangu hembu tutafakari utendaji huu wa polisi.Hivi karibuni mh.Nassari na wanasisa wenzake wameripotiwa kuhojiwa na polisi juu ya matamshi waliyoyatoa kwenye mkutano wa hadhari mjini Arusha.Binafsi sipingi hatua hiyo kwani ni wajibu wa polisi.

  Hata hivyo,najiuliza maswali mengi, kwa mfano, mh.Malima alipokutwa na silaha ya kivita aina ya SMG alihojiwa na file lake lilipelekwa kwa DPP?Wakwapuaji wa fedha za EPA kama Meremeta,kagoda na Deep green finance nao walihojiwa na polisi?Na kama waliohojiwa jambo hili linaloathiri umma wa watanzania liliwekwa wazi kama hili la Nasari na wenzake na kama jibu ni hapana ni kwa manufaa ya nani?

  Wanasiasa wa upinzani hasa viongozi wa CHADEMA wamekuwa wakikamatwa na kuhojiwa na polisi mara kwa mara tena kwa uharaka wa ajabu,lakini watuhumiwa wa ufisadi na mkosa mengine inakuwa nongwa kuwakamata na inachukua muda mrefu na pengine ni baada ya kelele nyingi kupigwa.Tujiulize ktk hii ripoti ya CAG nani amekamatwa na kuhojiwa na file lake kupelekwa kwa DPP mpaka leo hii.Je waliotajwa na CAG wana makosa ambayo hawastahili kuitwa na kuhojiwa mapema kama mh.Nassari na wenzake au makosa yao yana utaratibu tofauti?

  Ni maswali ambayo mimi binafsi naona yanahitaji kutolewa ufafanuzi vinginevyo imani ya watanzania kwa jeshi la polisi itazidi kushuka na huenda ikaathiri zana nzima ya polisi jamii.
   
 2. M

  Mujwahuzia Senior Member

  #2
  May 10, 2012
  Joined: Nov 17, 2011
  Messages: 137
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Moja ya kazi ya polisi ni kutekeleza amri ya mkuu wake wa kazi ndio kwa maana muda wote ni Salutiiiiiiiii?????????? hivyo nafikiria hao Mapolisi hata wanavyotetewa juu ya matatizo wao wanaona hawastahili wao suluhu yao ni kupiga virungu kufukuza waandamanaji wanaodai haki dhuluma wanayofnyiwa wtz polisi hilo hawalioni naomba tuwaache peke yao usfikiri wao hawana shida nidhamu ya woga imewatawala wanashindwa hata kujadili shida zao.
   
 3. Ciril

  Ciril JF-Expert Member

  #3
  May 10, 2012
  Joined: Jan 10, 2011
  Messages: 5,536
  Likes Received: 1,468
  Trophy Points: 280
  Hili swali nilijiuliza tangu nilipozisikia taarifa za polisi magazetini kuwa wanamwitaji Nassari ktk kituo cha polisi kwa mahojiano kosa:maneno ya uchochezi.Zipo taarifa mbali mbali nilizowahi kuzisikia na kuziona katika television juu ya jeshi la police kupambana na uhalifu Wa aina mbali mbali.Katika uhalifu Wa silaha police huwa ni wakali sana waweza kusikia taarifa kuwa"tumepambana na kuwaua majambazi kadhaa na walikutwa na silaha kinyume cha Sheria.Police tumewahi kusikia ama kushuhudia ktk tv police wakitenda kinyume na utaratibu mfano ni kwa wale wafanya biashara Wa mahenge waliopigwa risasi na polisi/mauaji ya raia Arusha/mauaji ya raia Nyamongo huko tarime na maeneo mengine mengi.Police wanakiuka taratibu zao za kazi lakini hakuna hata mmoja anaechukuliwa hatua zozote Kali za kisheria.
  Haujapita muda mrefu tangu tukio la naibu waziri Wa nishati na madini(Adam Malima)aibiwe thamani zake pamoja na fedha ktk hotel na ndipo lilipogundulika tukio hili la yeye kumiliki silaha ya kivita kinyume cha Sheria.Katika mahojiano Yake na kituo cha tellevision cha ITV aliulizwa ni kwa nini anamiliki silaha zote hizo(pmj na pistol)na akadai kwa kinywa chake kuwa"Maisha Yangu ni zaidi ya hizi silaha".Baada ya siku moja jeshi la polisi walitoa taarifa kuwa naibu waziri Wa nishati na madini(Adam malima)hamiliki hiyo silaha anayodaiwa kuwa nayo.Nnasema hapa polisi walitumika kumsafisha na maagizo hayo ni lazima yalitoka upande Wa pili(mhimili mwingine).Hivi nchi hii ikiendeshwa kwa namna hii ya kulindana je wanyonge tutashika wapi?Sitetei uvunjwaji Wa sheria Kama alivyofanya mbunge Wa Arumeru mashariki(kwa mujibu Wa taarifa za jeshi la polisi)Ila tunataka sheria zifuatwe kwa watu wote na pasiwe na kulindana kokote ktk Jambo lolote.
   
 4. ZE DONE

  ZE DONE Member

  #4
  May 10, 2012
  Joined: Mar 3, 2012
  Messages: 82
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 15
  Hivi ndugu zangu kitu gani mnacho sumbua akili zenu, CCM imesha shindwa inatafuta kila aina ya upenyo na kutuchokonoa ili tuingie kwenye machafuko na yenyewe ndo ipate nafasi ya kuendelea kukaa hii ni rasharasha makubwa yanakuja mengi zaidi ya haya. ushauri wangu:-
  1. Kwanza napenda kuwapongeza viongozi wa juu wa chadema kwa kuto kuhamaki na kuwapa nafasi wanayoitaka hawa majambazi
  2. Pili viongozi wetu wawe makini na kauli wanazo zitoa maana hawa jamaa wanatamani sana tujikwae maana wananchi wote wapo nasi
  3. Binafsi sijajua ile kauli ya nasari ililenga kitu gani ila nasubiri atuambie maana pale viongozi wetu wanapokosea ni jukumu letu kuwakosoa ili tusijenge chama kama cha kifalme kama ccm
  4. na mwisho tusiwajali sana hawa sijui mafisadi au majambazi tujali wananchi kwanza wanataka nini na wanapendekeza nini.
   
 5. m

  mandemba Senior Member

  #5
  May 10, 2012
  Joined: Apr 7, 2012
  Messages: 103
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Hao ndio polisi wetu ujashangaa kova alivyompigia saluti marehemu kanumba...
   
 6. s

  stefanos Member

  #6
  May 10, 2012
  Joined: Feb 6, 2008
  Messages: 30
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  Nashindwa kuuelewa unafiki wa watendaji ndani ya serikali. Hivi karibuni tumesikia matamko mfululizo toka kwa Mheshimiwa Jussa wa Zanzibar akizungumza bila kumung'unya maneno juu ya Zanzibar kujitenga na Muungano hasa kwenye masuala ya mipaka ya baharini na swala la mafuta, sikuona wala kusikia anatafutwa na Polisi kulikoni Nassari asakamwe kiasi hicho??? Tuache unafiki hasa wale wanaoshadadia kutaka Nasasari ashitakiwe.
   
 7. DASA

  DASA JF-Expert Member

  #7
  May 10, 2012
  Joined: Jan 6, 2011
  Messages: 1,031
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 135
  Wakati ufuke sasa Polisi iwe ni ya watanzania sio ya CCM!!.
   
 8. Ulukolokwitanga

  Ulukolokwitanga JF-Expert Member

  #8
  May 10, 2012
  Joined: Sep 18, 2010
  Messages: 8,418
  Likes Received: 3,905
  Trophy Points: 280
  Polisi wanalipa fadhila kwa CCM kwa vile ccm imewaachia wapokee rushwa wapendavyo, wawabambikizie wananchi na viongozi wa CDM kesi, wavute bangi na kuingia nazo disko, waingie na silaha disko na upuuzi mwingine mwingi tu bila kuchukuliwa hatua. Pia kumbuka Said Mwema alipewa uongozi wa jeshi kiswahiba na JK kwa hiyo hana sifa wala uwezo wa kuongoza. Kwa sasa tuvumilie tu juu ya haya yote lakini 2015 tusifanye makosa ya kuiacha CCM madarakani. We Malima endelea kutesa tu na SMG yako lakini kumbukumbu zipo na hata ipite miaka 10 utashtakiwa tu
   
Loading...