Wahujumu miundombinu sawa na wabakaji wafungwe miaka 30

kmbwembwe

JF-Expert Member
Aug 16, 2012
7,238
2,000
Miundombinu ya usafiri,umeme, maji, na mawasiliano inajengwa kwa gharama kubwa na mara nyingi ni mikopo ya muda mrefu inayowatia kwenye deni hadi vizazi vijavyo. Bila miundombinu bora na ya kisasa ni ndoto taifa kupata maendeleo. Jambo lakusikitisha katika nchi yetu siku hizi watu wengi wamewehuka kwa ubinafsi na tamaa ya mali kiasi cha kuhujumu miundombinu ya barabara, reli, umeme na maji. Pia tusisahau kuna miundombinu ya gesi na mafuta inakuja. Kutokana na kujaliwa nchi kubwa miundombinu hiyo inapita sehemu kubwa zisizokaliwa na watu kwa hivyo ni rahisi kuihujumu. Watu waovu au wajinga wanahujumu miundombinu kupata vyuma vya kuuza au kwa matumizi yao binafsi. Rushwa iliyokithiri inaruhusu kila uovu na ujinga katika nchi yetu. Bado tu watu kuwauza baba zao na mama zao kupata fedha. Wanunuzi wa vyuma toka miundombinu wanafahamika lakini hatua madhubuti haichukuliwi. Walinunua hadi mabomu kwa uroho wao yakawalipukia wakaacha ila vyuma vya barabara na reli hawaachi kwa kua hawajalipukiwa na dola. Hakika wahujumu hawa ni wabakaji wa maendeleo ya taifa inastahili wafungwe jela miaka 30 sawa na wabakaji, sio uongozi wa taifa kuwachekea.
 

mutahappy

JF-Expert Member
Dec 30, 2012
529
195
Mkuu kwa wabakaji binafsi miaka 30 haiwahusu wala hata hawahojiwi.
Wanaohujumu miundo mbinu wanastahik adhabu kali sana but not under ccm Government..
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom