Wahubiri tumieni X-mas hii kuwaonya Polisi na Mwigulu

“It used to be that a man could keep out of trouble if he behaved himself. Now he will only keep out of trouble if he behaves himself, the police behave themselves, and court behaves itself.”
Agona Apell,
 
Kazi ya majeshi ni kulinda mipaka , usalama wa raia na mali zao baaasi , LAKINI SI KUISAIDIA CCM KUKANYAGA KATIBA .

Na hili nataka kila mbumbumbu aelewe , maana siku ya siku huwezi kujitetea kwamba ulitii amri ya mtu , mfano hai ni Saddam Husein na kundi lake .
Saadam si alitengenezewa zengwe kuwa ana silaha za sumu?je zilipatikana?acha kutoa mifano dhaifu
 
Ni furaha gani unaipata kwa wananchi wasio na hatia kuteswa ?

Halafu huyu unayemsifia kuzima upinzani mbona anatumia majeshi yote , yeye kama anao uwezo na anaamini anakubalika kama anavyodanganywa ( Tuzo ya Forbes ) , kwanini tusikutane naye jukwaani ?
Ni weak ktk kujenga hoja, hawezi kushawishi hata anapo fanya jambo sahihi yeye ni kutumia ubabe na nguvu tu
 
Ni kweli mkuu nakuunga mkono pia wasisahau kumkumbusha mwenyekiti wetu wa ufipa yy ndie aliyekuwa anashinda na Ben Masaa yote iweje akae kimya na bila hata kutuambia Ben yuko wapi Mara ya mwisho ilikuwaje yupo tu atueleze bring back our Ben
Mbona amesema kupitia Mwanasheria wa Chama juu ya namba iliyowasiliana kwa mara ya mwisho na Ben na ameitoa kwa Polisi, unachotaka cha zaidi ni nini hasa, na kwa nini hutaki Polisi ambacho ndicho chombo halali cha kuchunguza masuala kama haya kisifanye shughuli yake?
Kikatiba hakuna mtu au kikundi kinachoruhusiwa kuanzisha jeshi la aina yoyote Tanzania, sasa unataka Mhe. Mbowe awe na Polisi wake wa kufanya uchunguzi badala ya Polisi waliopo kikatiba? Soma Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya Mwaka 1977, Ibara ya 147 (1) hadi (4) Vingenevyo unatakiwa kuufyata!!!
 
Nani anaeteseka?
Rais ndio amiri jeshi,na majeshi yote yapo kwa ajili yake,hii ni duniani kote.Hata Rais wa chadema akipata madaraka atalitumia jeshi hilo hilo,hawezi kulivunja.
Fanya kazi dada,mambo ya kuongea uongo majukwaani yanapoteza muda,wakati wa uchaguzi kila mtu atapimwa kwa kazi yake
Acha ujuha, uwe unasoma kwanza na kuelewa hoja za wenzako kwanza kabla hujakurupuka. Hakuna aliyekataa kwamba Rais ndiye Amiri Jeshi Mkuu, suala hapa ni kuyatumia majeshi haya kwa misingi isiyokusudiwa na Katiba. Rais akiwa pia ni mwanasiasa anapaswa kujibu hoja za kisiasa jukwaani na si kutumia ubabe wa majeshi. Majeshi ayaache yalinde raia na mali zao pamoja na mipaka ya nchi.
 
Ni wapi umeona au kusikia Rais ameamrisha majeshi yafanye undava?
 
Mbona amesema kupitia Mwanasheria wa Chama juu ya namba iliyowasiliana kwa mara ya mwisho na Ben na ameitoa kwa Polisi, unachotaka cha zaidi ni nini hasa, na kwa nini hutaki Polisi ambacho ndicho chombo halali cha kuchunguza masuala kama haya kisifanye shughuli yake?
Kikatiba hakuna mtu au kikundi kinachoruhusiwa kuanzisha jeshi la aina yoyote Tanzania, sasa unataka Mhe. Mbowe awe na Polisi wake wa kufanya uchunguzi badala ya Polisi waliopo kikatiba? Soma Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya Mwaka 1977, Ibara ya 147 (1) hadi (4) Vingenevyo unatakiwa kuufyata!!!
Nashukuru kama mmeanza kugundua umuhimu wa Polisi nyie c mlikuwa mnajinadi MNA intelejensia Kali ya kugundua hili la Ben mmefeli wapi? Au baada ya kufeli mmeamua kuwaachia Polisi mlichoshindwa nyie mnaojua kila kitu,na hiyo ibara ktk katiba ulitoitaja na wale mafundi welding mlionao ni wa kazi gani?
 
Kwani polisi na Mwigulu wameajiriwa na wahubiri?Hamjui nchi inavyoendeshwa kila kada imewakataa, chadema mnatapa tapa.
Magufuli amekamata kila jamii,juzi mmemuona akiongea na Pengo,jana kawasili Singida kwa maadhimisho ya sikukuu.Nani atakemea serikali?
Magufuli ameanza kuujua mchezo wa siasa vizuri,angalau kwa mwaka huu mmoja amefanikiwa kuzima kelele za upinzani

Kwani Rais alichaguliwa ili kuzima kelele za wapinzani?
 
UNAPASWA WAKATI UNAANDIKA NI VYEMA UKAJUA KITU GANI UNAANDIKA KATIKA BIBLIA HAKUNA KITU KINACHOITWA X-MASS BALI KUNA CHRISTMAS
Hakuna x-mass wala christmass kwenye biblia,iwe ya kiprotestanti yenye vitabu 66 au ile ya kikatoliki yenye vitabu 72!
 
"polisi hutumwa na wakubwa wao kutekeleza wanayofanya.msiwalaumu"
Mwigulu Nchemba
 
Nashukuru kama mmeanza kugundua umuhimu wa Polisi nyie c mlikuwa mnajinadi MNA intelejensia Kali ya kugundua hili la Ben mmefeli wapi? Au baada ya kufeli mmeamua kuwaachia Polisi mlichoshindwa nyie mnaojua kila kitu,na hiyo ibara ktk katiba ulitoitaja na wale mafundi welding mlionao ni wa kazi gani?
Ndugu yangu 'relis', hapa tunaongelea uhai wa mtu. Ben ametoweka, hatujui lililompata. Tuna Serikali yenye vyombo vya ulinzi na usalama wa raia. Ben ni raia wa Tanzania. Serikali na vyombo vyake vya ulinzi na usalama vilipaswa kumlinda asitoweke. Sasa kwa kuwa ametoweka, ni jukumu lao kufanya uchunguzi wa kina na haraka ili sisi raia wa nchi tujue nini kimempata mwenzetu. Ikiwa na Mwenyekiti anahusika basi kila jiwe ligeuzwe juu chini ili ukweli ujulikane. Hapa tusifanye utani na suala linalohusu maisha ya binadamu mwenzetu.
Waweza kuandika chochote, ila usisahau kuwa maandishi yako yanadhihirisha ukubwa au udogo wa ubongo wako!!!!
 
Ni wapi umeona au kusikia Rais ameamrisha majeshi yafanye undava?
Yeye ndiye Amiri Jeshi Mkuu; unapoona jeshi hasa la Polisi likikamata watu hovyo hovyo na hasa wale wenye mrengo wa Upinzani, kwa akili ya kwaida tu ujue kuna baraka zake. Ndiyo maana wengine wakahoji juu ya rais mwenye PhD kutokuwa na uwezo wa kujenga hoja za kisiasa badala yake anajiegemeza zaidi kwa vyombo vya dola. Tabia hiyo inahafifisha demokrasia katika nchi yetu. Na sasa tumeanza kuchekwa hata na majirani zetu
 
Hakika katika watu walioongoza kwa kuchukiwa na kulaaniwa mwaka huu ni polisi. Hata dhana ya serikali kuonekana kama ya kidukiteta unasababishwa na polisi

Polisi wametishia rais,polisi wameshukiwa kuua,polisi wanetuhumiwa kutesa wakosiaji na watu wengine kwa mujibu wa Tundu Lissu,polisi wamekamata wakosoaji wa serikali kwa hoja za ajabu kabisa. Polisi wamemkamata Mkuu wetu Max Mello kwa hoja zisizo na mashiko kabisa.

Wamemdhalilisha na kumbughudhi Polisi wamewakamata waandishi wa habari,wabunge wa Ukawa katika hali ya kukandamiza demokrasia

Katika yote haya waziri mwenye dhamana amekuwa kimya huku akiwaonya raia wasiwaseme vibaya raia. Hapa tumembana JF kuhusu kupotea kwa Ben Saanane hakuna mkakati mahususi alioutoa zaidi ya kusema Ben ni family friend wake

Kabla hali haijawa mbaya,ni wakati wenu sasa wachungaji,makasisi na wahubiri kumkemea na kumuonya Mwigulu na polisi kwa maana waumini wenu tumechoshwa nao
Wachungaji hawatumikii matakwa ya UKAWA. Wala hawaongozwi na hisia za Tundu Lissu. Wamefundishwa kutii mamlaka zilizopo kwani zimetokana na Mungu. Christmas njema.
 
Yeye ndiye Amiri Jeshi Mkuu; unapoona jeshi hasa la Polisi likikamata watu hovyo hovyo na hasa wale wenye mrengo wa Upinzani, kwa akili ya kwaida tu ujue kuna baraka zake. Ndiyo maana wengine wakahoji juu ya rais mwenye PhD kutokuwa na uwezo wa kujenga hoja za kisiasa badala yake anajiegemeza zaidi kwa vyombo vya dola. Tabia hiyo inahafifisha demokrasia katika nchi yetu. Na sasa tumeanza kuchekwa hata na majirani zetu
Unataka azuie polisi kufanya kazi yao?
 
Back
Top Bottom