Wahubiri kwenye daladala za Tegeta - Kariakoo wamekuwa kero

Utakua na jini/pepo sio bure hayo huogopa sana kusikiliza injili yasije yakaungua moto.

Nakushauri mpokee Yesu kristo upate kuokolewa na hukumu ile ya mwisho..sadaka usiache kutoa.

#MaendeleoHayanaChama
Majin na mapepo wanayo hao wahuni wanaojificha kwenye kuhubir, kwanza majin yangekuwa yanaogopa izo injili zenu za kipuuzi mbona yangeisha tangu zamani?
 
Kumekuwa na tabia ya wahubiri kwenye route kupanda kupiga injili mwisho kuomba sadaka, mbona wa Mbagala Gongo la Mboto haya mambo hayapo?
hii mambo nilikutana nayo mandela road kipande cha buguruni-tazara mama mtumzima kapanda kaanza kushusha mistari ya mawaidha. kufika foleni ya daraja la mfugale akaanza kutaka sadaka nikaona watu wanaanza kujisachi na kuchomo mwenye buku twende jero twende. mimi kwa kweli nilisita. kufika kituo cha tazara akashula.
 
Kumekuwa na tabia ya wahubiri kwenye route kupanda kupiga injili mwisho kuomba sadaka, mbona wa Mbagala Gongo la Mboto haya mambo hayapo?
Kuna 'Mhubiri Kero' Mmoja nilipoona tu kapanda Dala Dala pale Mwenge nikajua anataka kuanza kutupigia Mikelele yake na alipoanza tu kwa Makusudi nikatafuta Ugomvi nae wa Maneno kwa kumwambia anaturushia Mate na hatuna uhakika kama kapiga Mswaki na akapaniki kisha kwa Hasira akasusa na Kushukia ITV na Injili yake ya Kero nayo ikaishia ITV.

Nakumbuka kwa hiki Kitendo nililipiwa hadi na Nauli huku Abiria wengine wakiniomba niwe napanda nao Dala Dala zao za Tegeta - Kivukoni na Tegeta - Gerezani ili niwe Nawakomesha hawa Watu ( Wahubiri Kero ) kwani Wanakereka nao mno ila hawana jinsi.

Kuna Dereva Mmoja wa Basi za Gongo la Mboto - Msasani ( Masaki ) alipoona tu 'Mhubiri Kero' kapanda kwa Makusudi akapaki Gari pembeni na kusema kuwa limeharibika hivyo Abiria tushuke na anayetaka kuwahi apande Basi lingine na kweli Abiria tukashuka na Yule 'Mhubiri Kero' nae akashuka na Biblia yake kurudi nyuma na wala alikuwa haubiri tena na Kondakta alipomuona tu anavuka Barabara ya upande wa Pili Dereva akatuita Abiria kuwa tupande kwani Kero imeshaondoka na tukaendelea na Safari yetu vizuri tu.
 
Back
Top Bottom