Wahoji Jaji Nyalali, Samatta kukosa nishani za Ikulu | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wahoji Jaji Nyalali, Samatta kukosa nishani za Ikulu

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Rutashubanyuma, Dec 14, 2011.

 1. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #1
  Dec 14, 2011
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 157,528
  Likes Received: 415,716
  Trophy Points: 280
  [TABLE="class: contentpaneopen"]
  [TR]
  [TD="class: contentheading, width: 100%"]Wahoji Jaji Nyalali, Samatta kukosa nishani za Ikulu
  [/TD]
  [TD="class: buttonheading, width: 100%, align: right"] Send to a friend [/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
  [TABLE="class: contentpaneopen"]
  [TR]
  [TD="class: createdate"] Tuesday, 13 December 2011 20:24 [/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD]

  Leon Bahati
  NISHANI zilizotolewa na Rais Jakaya Kikwete kwenye kilele cha Miaka 50 ya Uhuru, zinazidi kuibua utata baada ya baadhi ya wanasheria, wanasiasa kuhoji sababu za majajji wakongwe; marehemu Francis Nyalali, Robert Kisanga na Barnabas Samatta, kutopata.

  Nishani hizo zilizokuwa katika mafungu matatu, tayari zimelalamikiwa kutokana na baadhi ya watu waliowahi kushika nafasi za juu kiongozi ikiwamo Waziri Mkuu na Spika wa Bunge, kutopewa. Watu hao walihoji kitendo cha Serikali kuwanyima nishani hizo waliowahi kuwa mawaziri wakuu; Edward Lowassa na John Malecela pamoja na Spika wa Bunge la Tisa, Samuel Sitta.

  Jana mjadala huo uliingia sura mpya baada ya wanasheria nao kujikita kwa kuhoji kukosekana kwa Jaji Samatta, Nyalali na Kisanga katika orodha ya watu waliostahili kupewa nishani hizo.

  Jaji John Mkwawa aliliambia gazeti hili kuwa, "binafsi nisingependa kutoa dosari juu ya namna Rais alivyotoa nishani hizo, kwa sababu inategemea vigezo walivyozingatia." Lakini akasema, "kama ningekuwa nimeambiwa nipendekeze miongoni mwa majaji waliopaswa kupewa nishani hizo, nisingeacha kuwaorodhesha Jaji Augustino Ramadhan, Samatta na Abdalah Mustafa."

  Kuhusu Nyalali na Kisanga alisema, ingawa kwa kuzingatia kigezo cha miaka 50 ya Uhuru nao walipaswa kupata, tayari taifa liliwahi kuwatunuku nishani za heshima kulingana na kazi zao.Mwandishi wa Habari na Wakili wa Kujitegemea, Aloyce Komba alieleza kusikitishwa na kitendo cha Nyalali, Samatta, Nyalali na Kisanga.
  Kwa majibu wa Komba, majaji wengine waliopaswa pia kupata nishani hizo, ni Jaji Mkuu, Othman Chande na William Sekule.

  “Jaji Mkuu Mstaafu Nyalali (sasa ni marehemu) angestahili kutunukiwa nishani ya utumishi uliotukuka kutokana na kuongoza vyema Mahakama moja ya mihimili mitatu ya dola kwa miaka 23 akiwa chini ya marais wa awamu tatu; Mwalimu Julius Nyerere, Ali Hassan Mwinyi na Benjamin Mkapa,” alisema Komba. Alimuelezea Nyalali kuwa alikuwa mwadilifu, mchapa kazi na mweledi wa sheria, aliyesimamia vyema utawala wa sheria na jukumu la utoaji haki kwa majaji, mahakimu na mawakili.

  Kuhusu Jaji Kisanga, Mwanasheria huyo alisema ni Jaji mstaafu wa Mahakama ya Rufaa na Mwenyekiti wa Kwanza wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora.

  “Alistahili tuzo kwa utumishi uliotukuka na mchango wake katika masuala ya utetezi wa haki za binadamu nchini,” alisema.

  Vilevile, anamuelezea Kisanga kuwa ni Jaji aliyeongoza tume iliyoratibu maoni ya “White Paper” kuhusu muundo wa Serikali ya Muungano na masuala ya Katiba na ikapendekeza kuwapo kwa Serikali Tatu. “Haishangazi alipotunukiwa shahada ya heshima ya udaktari na Chuo Kikuu kimoja cha huko Uingereza alichowahi kusoma,” alisema Komba.

  Kuhusu Jaji Samatta, Komba alisema kuwa ndiye aliyewawezesha wahadhiri wawili wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Profesa Issa Shivji na Profesa Hamudi Majamba kutunga kitabu kuhusu maisha yake kinachoitwa ‘Utawala wa Sheria dhidi ya Watawala wa Sheria.’

  Alisema aliwahi kuwa Mkurugenzi wa Mashtaka ya Jinai (DPP) na Jaji katika Mahakama Kuu ya Zimbabwe, Jaji Kiongozi wa Mahakama Kuu ya Tanzania na Jaji Mkuu wa Tanzania aliyesimamia kwa karibu uboreshaji na usafi wa majengo ya Mahakama na kukemea kwa nguvu zote vitendo vya rushwa.

  Kwa sasa Jaji Samatta ni Mkuu wa Chuo Kikuu cha Mzumbe ambaye anaendelea na maisha maadilifu na yenye msimamo kuhusu mchakato wa kupata katiba mpya! Kuhusu majaji Jaji William Sekule na Jaji Mkuu Othman Chande, Komba alisema wameiletea sifa Tanzania katika medani ya kimataifa katika Mahakama za Umoja wa Mataifa.

  “Jaji Sekule aliyewahi kuwa DPP wa Tanzania ndiye jaji pekee aliyeendelea kudumu katika Mahakama ya ICTR Arusha tangu ianzishwe,” alisema. Alimuelezea Othman kuwa ndiye aliyewahi kuwa mwendesha mashtaka ICTR na baadae akapelekwa Mashariki ya mbali. “Amekuwa mtaalam mshauri wa haki za binadamu wa huko Sudan. Hivi karibuni jina lake lilikuwa moja ya manne ya kumrithi (Moreno) Ocampo kule (Mahakama ya Kimataifa ya Jinai) ICC.

  Kafulila ahoji Mtei kukosa

  Naye mbunge wa Kigoma Kusini, David Kafulila, alisema kwa Jaji Nyalali na Samatta kukosa nishani ni dosari kubwa, kwani wana mchango mkubwa sana katika ujenzi wa taifa.

  Kafulila alisema kwamba kuna watu kama Edwin Mtei kwa historia ya kuwa gavana wa kwanza aliyeanzisha Benki Kuu (BoT) ambayo mpaka leo ndio nguzo kubwa ya uchumi wa taifa kukosa nishani ni aibu kwa taifa.

  “ Pamoja na kutofautiana na Mwalimu Nyerere kisera na pamoja na uamuzi wake wa kwenda upinzani na kuanzisha Chadema ambacho leo ni chama kikuu cha upinzani nchini ingetosha kumuona kama raia mwenye sifa ya kupata nishani,” alisema mwisho  [/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]

   
 2. Nyani Ngabu

  Nyani Ngabu Platinum Member

  #2
  Dec 14, 2011
  Joined: May 15, 2006
  Messages: 73,651
  Likes Received: 35,408
  Trophy Points: 280
  Hivi kwani hizo nishani hazitatolewa tena huko siku za usoni? Manake watu wanalialia mno sasa nashindwa kuelewa kama Ijumaa iliyopita ndo ilikuwa mwanzo na mwisho wa kuzitoa.

  Halafu hivi zinaambatana na pesa? Ipo siku na Mwanakijiji naye atadai ya kwake...nyie subirini tu.
   
 3. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #3
  Dec 14, 2011
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 157,528
  Likes Received: 415,716
  Trophy Points: 280
  tatizo letu ni kuabudu vyeo na wala siyo mchango wa mhusika kwenye jamii....sehemu kubwa ya hivyo vyeo vimetoka katika sura ya kupendeleana.................nepotism......................na tunapoendelea kushabikia vcyeo vyao yamaanisha tunahalaisha upendeleo tajwa..............................

  kwa maoni yangu Jaji Lugakingira na Jaji Mwalusanya ndiyo nguzo za mfano wa utoaji wa haki kwa taifa hili wengine wanawafuata...................kwa hiyo kama ingelikuwepo haki kwenye hizi nishani basi hawa wawili wangelituzwa...........
   
 4. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #4
  Dec 14, 2011
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 157,528
  Likes Received: 415,716
  Trophy Points: 280
  kilio kipo kwa sababu vigezo vyake havipo wazi..............nishani kwa kawaida huandamana na pesa.............
   
 5. Nyani Ngabu

  Nyani Ngabu Platinum Member

  #5
  Dec 14, 2011
  Joined: May 15, 2006
  Messages: 73,651
  Likes Received: 35,408
  Trophy Points: 280
  Hapo hapo.....lol
   
 6. Fidel80

  Fidel80 JF-Expert Member

  #6
  Dec 14, 2011
  Joined: May 3, 2008
  Messages: 21,976
  Likes Received: 104
  Trophy Points: 145
  Komredi hizo zinaambatana na bahasha yenye mshiko ndani ndo maana watu wanahoji waliostahili wamekosa ambao hawakustahili ndo wamepata kigezo kinaweza kuwa ni fitina.
   
 7. Yo Yo

  Yo Yo JF-Expert Member

  #7
  Dec 14, 2011
  Joined: May 31, 2008
  Messages: 11,247
  Likes Received: 73
  Trophy Points: 0
  Mnashangaa nini? inawaingia akilini Anne Makinda kapata nishani ilihali Sapi Mkwawa katoswa?......
   
 8. Pukudu

  Pukudu JF-Expert Member

  #8
  Dec 14, 2011
  Joined: Jan 7, 2011
  Messages: 2,970
  Likes Received: 735
  Trophy Points: 280
  Hivi kuna Sheria yeyote inayoguide jinsi ya utoajiwa hizo na Nishani Na tuzo au bado hekima za Mwenyekiti zinaamua. Hizo in tuzo za kitaifa sio za Mtu binafsi agawe yeye apendavyo ni vizuri Sasa hili liangaliwe ikibidi itungiwe Sheria na vigezo viwe included

   
 9. Mwita Maranya

  Mwita Maranya JF-Expert Member

  #9
  Dec 14, 2011
  Joined: Jul 1, 2008
  Messages: 10,569
  Likes Received: 104
  Trophy Points: 145
  Hata mimi kwa maoni yangu, upande wa mhimili wa mahakama ningependa kusikia marehemu jaji Kahwa Lugakingira anapata nishani kwani alilitumikia taifa hili kwa uadilifu mkubwa sana. Na katika kesi alizowahi kuzisikiliza na kuzitolea maamuzi, aliitendea haki jamii ya watanzania bila upoendeleo.
  Wasiwasi hapa ni kwamba kwa kuwa vigezo na masharti havikuwekwa wazi na ikulu, vinginevyo tungepata kujua sababu za hawa watu kukosa nishani.
   
 10. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #10
  Dec 14, 2011
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,448
  Likes Received: 81,669
  Trophy Points: 280

  Kama kigezo kilikuwa ni uadilifu kama mtendaji (kama inavyodaiwa) basi Mkapa asingestahili kupata maana katika miaka 10 yote aliyokuwa madarakani hakuwa na uadilifu hata chembe.
   
 11. Nyani Ngabu

  Nyani Ngabu Platinum Member

  #11
  Dec 14, 2011
  Joined: May 15, 2006
  Messages: 73,651
  Likes Received: 35,408
  Trophy Points: 280
  Bubu, uadilifu ni subjective.
   
 12. k

  kuzou JF-Expert Member

  #12
  Dec 14, 2011
  Joined: Oct 20, 2011
  Messages: 200
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  nchi hii ina watu wengi huwezi kutoa nishani kwa kigezo kwamba mbona fulani kapata,je wale 17 walioanzisha tanu.ukitaja mtiririko hamuwezi maliza huu mjadala.ina maana walifanya kazi ili wapewe nishani
   
 13. Nyani Ngabu

  Nyani Ngabu Platinum Member

  #13
  Dec 14, 2011
  Joined: May 15, 2006
  Messages: 73,651
  Likes Received: 35,408
  Trophy Points: 280
  Kwa vile wote wanaostahili kupewa nishani hawakupata basi nadhani labda watakuja kuzipata hapo baadaye katika siku za usoni kwani wote wasingeweza kupewa kwa siku moja.
   
 14. Mupirocin

  Mupirocin JF-Expert Member

  #14
  Dec 14, 2011
  Joined: Jan 28, 2011
  Messages: 1,596
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 145
  Inategemea Rais itakavyompendeza hakuna vigezo. Ndo ilimpendeza kumpa Makinda kuliko Sitta
   
 15. P

  Phillemon Mikael JF Gold Member

  #15
  Dec 14, 2011
  Joined: Nov 5, 2006
  Messages: 8,850
  Likes Received: 2,425
  Trophy Points: 280

  nyani hata Kama zikitolewa tena karibuni haitaleta maana Kama za miaka 50 ya Uhuru,ni wazi rais na ikulu Yake kwenye hili wameburunda........ningekuwa mshauri wake ningemshauri atoe nishani kwa watanganyika /watanzania 50 waliotukuka kuliko wote kwenye maeneo yafuatayo.

  Viongozi wa kisiasa wastaafu wa juu - rais na mawaziri wakuu
  Viongozi wakuu wa mhimili wa mahakama waliotukuka.
  Viongozi wakuu wa mhimili wa bunge waliotukuka
  Wakuu wa vyombo vya ulinzi na usalama waliotukuka
  Wakuu wa taasisi za umma na binafsi waliotukuka...ie banks ,hitadhi za jamii etc
  Wanamichezo waliotukuka
  Wasomi waliotukuka
  Watanzania wa kawaida waliotukuka au kujitolea .

  Sasa naombeni tuanze kuwatambua watanganyika au watanzania waliotukuka Angalau watano Hadi kumi kwenye kila eneo nililotaja hapo juu.

  Kilichotokea ni kuwaenzi baadhi tu ya waliofanya vyema kwenye mhimili wa executive na legislative ....wingine wote wakiwamo mashujaaa wetu wameachwa.......hili limeacha kidonda.....,tusitegemee rais akumbuke kila kitu ....kwenye hili washauri wa rais hawakwepi lawama pamoja nae!
   
 16. Daudi Mchambuzi

  Daudi Mchambuzi JF-Expert Member

  #16
  Dec 14, 2011
  Joined: Nov 25, 2010
  Messages: 31,778
  Likes Received: 36,776
  Trophy Points: 280
  Rugakingira J
   
 17. Daudi Mchambuzi

  Daudi Mchambuzi JF-Expert Member

  #17
  Dec 14, 2011
  Joined: Nov 25, 2010
  Messages: 31,778
  Likes Received: 36,776
  Trophy Points: 280
  Kwenye sikukuu ya miaka 100 ya uhuru???
   
 18. Mwasi

  Mwasi JF-Expert Member

  #18
  Dec 14, 2011
  Joined: Feb 12, 2010
  Messages: 249
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 33
  Malalamiko yamezidi pongezi kwa waliopata, Ikulu wanatakiwa kutolea maelezo hii kitu.
   
 19. MachoMakavu

  MachoMakavu JF-Expert Member

  #19
  Dec 14, 2011
  Joined: Feb 6, 2008
  Messages: 370
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Hadi kufikia 2015 tutakua tumeona mengi
   
 20. prakatatumba

  prakatatumba JF-Expert Member

  #20
  Dec 14, 2011
  Joined: Oct 17, 2011
  Messages: 1,337
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 135
  Hata prakatatumba nashangaa kwanini hajapewa,Makinda amepewa kwa sababu ya uanauke,dah!alioteshwa wa kuwapa nishani
   
Loading...