Wahitimu wenye alama za kawaida wanafanya vizuri sana kwenye kazi

Niccolo Machiavelli

JF-Expert Member
Feb 7, 2017
1,881
3,636
Mimi ni HR katika benki mmoja hapa Tanzania. Kila baada ya miaka 2 huwa tuna utaratibu wa kuajiri vijana waliohitimu chuo kwa program ya “Graduate Management Trainees (GMT).

Hawa GMT recruits huwa tunachukua First Class na Upper Second na program huchukua miaka 2 ya mafunzo katika department zote hapa ofisini. Baada ya miaka 2 kuisha huwa tunawapeleka kwenye department walikofanya vizuri sana kipindi cha mafunzo.

Tuna utaratibu pia wa kuchukua graduates wengine kwenye entry levels mbali mbali hapa ofisini bila kujalisha ufaulu chuoni.

Ila kuna kitu kimoja ambacho nimekigundua katika miaka 10 ya kazi yangu. Graduates wa second class degree ndio wanaongoza kwa performance ofisini. Targets wanazitimiza kwa wakati na wanatoa mawazo ambayo yana faida kubwa kwenye kampuni.

Hawa 1st class wengi ni watu wa kawaida sana. Utamkuta ofisini anadai alipata 1st class Honours chuo lakini performance ni ya kawaida sana. Hiki ni kitu ambacho huwa kinanitatiza sana.
 
FILE610.JPG

Hao wanaitwa vipanga kazi yao kubwa katika masomo huwa ni "kumeza" na siyo kuelewa!
 
Anajifariji kwa lipi sasa

Wewe mwenye 4.8 umegundua nini hapo changanyikeni

JF ukitetea jambo fulani unawekwa kwenye hilo jambo
Mfano ukitetea single mama na wewe utaitwa single mama,ukitetea wanaume unaonekana ni wa kiume...teh!

Mie sikuwa na hiyo GPA ya 4
Lakini kwa ninavyoona mtu mwenye first class hata kama hatakuwa mzuri sana kazini basi hawezi kuwa mbovu kabisa
 
JF ukitetea jambo fulani unawekwa kwenye hilo jambo
Mfano ukitetea single mama na wewe utaitwa single mama,ukitetea wanaume unaonekana ni wa kiume...teh!

Mie sikuwa na hiyo GPA ya 4
Lakini kwa ninavyoona mtu mwenye first class hata kama hatakuwa mzuri sana kazini basi hawezi kuwa mbovu kabisa
Haya turudi kwenye mada mtoa mada kasema nini na wewe umejibu nini?
 
vipanga wengi walikua wanakariri, alafu kuna wale wenyew alama zao ni C aijalishi pepa ni ngumu au rahisi miaka yote wenyewe wanapata C C tu, hawa wa aina hii.. ni talented sama wanajua wanachokifanya lakini hawatumii effort kubwa kufanya wonders
wale waliokuwa wanaweka A A kwa mitiani yako msinikasirikie jaman😅😅
 
Ume generalize ila kuna ukweli fulani hapa kiukweli First class nyingi ni za wanafunzi very static wao Muda wa chuo hawataki kujichanganya na inshu zingine zaidi ya msuli tu yani ata kujua mazingira ya mkoa anaosoma ni shida wengi wana ushamba mwingi sana wanaamini elimu tu ndio itawatoa tena ukute first class then kasoma kayumba wanakuwa na less exposure sana ukitaka kuona Avarage student ni competent wakati unafanya recruitment ficha vyeti wapime wote uone watakao shine ni wapi yani Average students wako best sana japo hizi first class tunazihitaji pia for academics purpose ila kiupande wa performance za private company basi jua first class hawatakuletea wonders zozote, Wako very static
 
Back
Top Bottom