Wahitimu wengi wa Vyuo Vikuu vya Kitanzania hawawezi kufanya mjadala kama huu wa watoto wa shule

Mambo hubadilika kila nyakati....saiv kuna internet ambayo imepunguza kwa kiasi kikubwa mambo ya mijadala ya face to face lakin pia internet imesababisha vijana wa sasa tuache kujieleza Sana tunavohitaji kitu fulan mfano; mtu unaweza kuhtaji kitabu flan badala ya kwenda library au kwa teacher saiv unaweza kudownload, lakn pia hata kukaa na watu mtaani(wazee, masela n.k ) kumepungua sababu ya internet. Hii inasababisha kijana akose public speaking skills na kukosa uwezo wa kujieleza mbele ya kadamnasi....turudi nyuma kwa hao vijana wa zaman, hakuna simu hakuna internet ,ukitaka kitu chochote ni lazma ufanye physical contact na mhusika, hii iliwajengea public speaking skills na uwezo mzuri wa kujieleza mbele za watu.
Hivyo Basi, vijana wa sasa hiv tujitahidi kucontact na watu face to face tupate walau confidence ya kueleweka mbele ya umati wa watu.practice make perfect.
 
Shule bora huwa zinatilia sana mkazo uwezo wa kudebate, sana. Bahati mbaya shule zetu zinazalisha waoga na wafyata mkia. Wasioweza kuhoji, wanaosubiria labda mambo yatakuwa mazuri yenyewe.
 
Siasa imevamiwa na watu wasio na uwezo kichwani..siasa imegeuzwa kuwa ajira badala ya tanuru la kuibua hoja zilizoshiba...
 
Usisahau kitu kinaitwa personality, kuna watu kulingana na walivyoumbwa, kuongea huwa ni tatizo hata kama wana hoja.

Jamii ya wasomi nchi yoyote ni mchanganyiko wa wazungungumzaji wazuri, waadishi wazuri au wenye sifa zote mbili.

Kwa maoni yangu ni vizuri tukawapima wasomi wetu kwa kuzingatia ujuzi wa walichosomea maana kuna fani nyingine hazimhitaji mtu kuwa mzungumzaji mzuri ili kuleta matokeo.
Haya hebu tuijdali hii hoja yako vizuri:

Mosi, wengi walisoma kwenye mfumo huo unaosema wewe wa kulipiwa kila kitu lakini bado wana matatizo makubwa. AU wewe huwaoni wasomi wetu wengi wenye umri kuanzia miaka 45 na kuendelea waliosoma kipindi cha Mzee Nyerere na Mzee Mwinyi ?

Pili, wengine wanasoma kuanzia shule hadi chuo-kikuu kwa pesa za wazazi wao lakini tatizo bado kubwa. Wanatafutiwa na ajira kabisa, lakini tatizo bado ni kubwa. AU mwenzangu huwaoni jinsi walivyo huko maofisini ?
 
Hao wa 1957 walikuwa wanalipiwa hadi nauli za kwenda na kurudi likizo. Shuleni na vyuoni maisha yalikuwa matamu.. na ukimaliza chuo unapangiwa kazi sio kuomba.

Siku hizi wanafunzi wa chuo inabidi wafanye vibiashara vidogo vidogo ili kwenda sawa na gharama za chuo. Siku ya kumaliza unapewa invoice ya HESLB huku ajira hakuna. Mnaosifia zamani wote ni wa kupuuzwa.
Tena walikuwa wanataka wapikiwe mayai kutoka ulaya,ya bongo hawakuyataka,
Alisimulia Mzee samwel sita alipokuwa mwanafunzi pale UDSM,kulinganisha 1957 na leo,huwatendei haki vijana wetu,
Mi Mzee wangu,siku anamaliza shule,Gari ya Serikali ipo nje inamsubili aende akaanze kazi,hata matokeo hayajatoka,leo hii una masters na kazi huna.
Mama yangu kasoma middle skuli,kipindi hicho,Waalimu wazungu,leo hii anaongea kimombo hata Profesa wa chuo kikuu hafikii hiyo fluence,may be Mkapa tu.
Unasoma kwa tabu,ukikosa mkopo,mpaka wazazi wajipige pige
 
Wewe kama mwalimu wa chuo ulichukua hatua gani kutatua hii changamoto? Hatua ulizochukua zilifanikiwa kiasi gani?
Tatizo kama hili halitatuliwi na mtu mmoja ndugu RRONDO, ni kubwa na lina mizizi mirefu. Kama mtoto hataandaliwa vizuri chini (Elementary, Primary & Secondary levels) usitegemee kama atafanya makubwa chuo kikuu. Atafaulu na kupata madaraja ya juu lakini uwezo wa kukabiliana na mazingira yake utakuwa hafifu sana...
 
Usisahau kitu kinaitwa personality, kuna watu kulingana na walivyoumbwa, kuongea huwa ni tatizo hata kama wana hoja.

Jamii ya wasomi nchi yoyote ni mchanganyiko wa wazungungumzaji wazuri, waadishi wazuri au wenye sifa zote mbili.

Kwa maoni yangu ni vizuri tukawapima wasomi wetu kwa kuzingatia ujuzi wa walichosomea maana kuna fani nyingine hazimhitaji mtu kuwa mzungumzaji mzuri ili kuleta matokeo.
Nakubaliana na wewe, uwezo wa kuzungumza na kuandika hutofautiana. Lakini hii haimaanishi kwamba mtu aliyesoma ashindwe kabisa kuwasilisha mawazo yake kwa kupitia hoja. Lakini pia mtu asipokuwa mzungumzaji mzuri basi hata utendaji wake huzungumza, kitu ambacho Tanzania ya leo kinapotea sana. Kinachoshanganza, hata ukizungumza na mtu (One to One) unakuta anapata shida....
 
Unazungumzia hawa wanaomaliza TEKU na St. John?
Wahitimu wengi wa vyuo vikuu vya kitanzania hawawezi kufanya mijadala mizuri. Kama wakifanya basi itakuwa ni mijadala ya kisiasa ambayo ni ya ndani ya nchi, lakini ukiwachukua leo hii ukawaweka vijana wa UDSM (Top Brass ya nchi) wafanye mjadala na vijana wa Pretoria, Zimbabwe, Abuja au Accra ni wachache sana watakaofanya vizuri. Hili nimeliona kwa macho yangu na kulithibitisha.........
 
Nimeangalia kwa makini sana huu mjadala na kama mtu niliyewahi kufundisha chuo nimeshangazwa sana na uwezo wa hawa wanafunzi wa Kiafrika. Kipindi wanafanya huu mjadala walikuwa ni wenye umri mdogo sana, lakini uwezo wao wa kujenga na kujibu hoja, kuzungumza lugha ngeni kwa ufasaha, ujasiri, pamoja na uwezo wa kumheshimu mzungumzaji mwingine umenishangaza.

Nafahamu fika kwamba hizo hoja zao walizijadili vizuri kabla ya mjadala, lakini kilichonifurahisha ni uwezo wao wa kuvaa vizuri uhusika na kuzijenga hoja ipasavyo. Nasikitika kusema kwamba wahitimu wetu wengi wa vyuo vikuu wanashindwa kujenga hoja kwa namna hii na kuzungumza lugha kwa ufasaha: Iwe ni Kiingereza au Kiswahili.

Kuna sehemu kubwa sana, sisi kama taifa tunakwama: Nasikika zaidi kusema kwamba hawa ndugu wa mwaka 1957, waliweza kufanya mjadala mzuri unaoeleweka kuliko wabunge wengi wa Tanzania wa mwaka 2021. Kibaya na kinachosikitisha ni kwamba wanasiasa wetu wamekuwa ni watu wanaoogopa mno mijadala, tena hadi wengine ni PhD....

Tuna kazi ya ziada kama taifa....

Wanafunzi wa UDSM wao wanaona sifa kuongea broken English ila kudebate hawawezi kabisa maana uelewa wao ni mdogo mno. Utakuta mtu kajuwa Kiingerza miaka 6 iliyopita akiwa chuoni, leo hii hajuwi Kiswahili. Kwa kweli wanachekesha mno.
 
Wanafunzi wa UDSM wao wanaona sifa kuongea broken English ila kudebate hawawezi kabisa maana uelewa wao ni mdogo mno. Utakuta mtu kajuwa Kiingerza miaka 6 iliyopita akiwa chuoni, leo hii hajuwi Kiswahili. Kwa kweli wanachekesha mno.
Kimtazamo wangu hapa kuna mawili: Kuna vijana wengi wanajitahidi sana, wanakuwa na uelewa mzuri wa vitu lakini utaalamu (Skills) wa kujieleza hawakujengewa tokea wanasoma shuleni. Siyo rahisi kuwa na mzungumzaji mzuri kama hukujengewa msingi mzuri. Hoja hii ameitoa Mkaruka hapo juu.

Kuna Debates, Morning Speeches, Poetry, Play and Drama na mambo mengnei sana ambayo yanapuuzwa leo lakini yanamsaidia sana mtoto katika kumjengea ujasiri (Confidence) na kumfundisha taaluma ya uzungumzaji mzuri. Mimi wakati nasoma tumefanya Play and Drama, Debates, tumeandika Poetry na kufanya mengineyo ambayo kiukweli yalinisaidia sana,....

Lakini pili, mjadala unaweza ukakushinda kama una uelewa mdogo. Kuna watoto unaweza kutana nao, wanaongea kiingereza hicho hadi utakimbia lakini uelewa wao wa mambo uko finyu hivyo humzuia kujenga hoja ipasavyo au mara nyingine ujasiri. Japo huyu yuko kwenye nafasi nzuri endapo atafanya jitihada.

Mwisho kabisa naamini ili wasomi tuweze kufanya vizuri mijadala yenye tija kitaifa, tunahitaji tufahamu vizuri jinsi ya kuwasilisha hoja, lakini pia tuwe na uelewa mpana wa mambo ambayo tunataka kuyajadili.....
 
Wapo watu wanajua kujenga hoja hata kwa sasa, tatizo ni kwamba 'hakuna wanunuzi wa hoja'.

Maana yangu ni kwamba, asilimia kubwa ya watanzania wa sasa hawapo tayari hata kusikiliza hoja, wengi wao amasa zao zipo kwenyr habari za kutekenya na mlipuko

Kwa mazingira kama hayo usitegemee kupata ile taste ya hoja za kisomi. Hapa enyewe jamii forum unaweza kutoa hoja lakini ukaishia kutukanwa pasipo sababu
 
6 Reactions
Reply
Back
Top Bottom