Wahitimu wa vyuo tusio na ajira tunakusudia kuitisha maombi ya kitaifa kuiombea serikali iwe sikivu na elevu zaidi

Samiaagain2025

JF-Expert Member
Dec 2, 2020
2,925
3,053
Tatizo la ajira za umma huanza taratibu na baadaye kuwa kubwa na sugu kabisa.

Lakini hata hivyo, zipo njia sahihi za kufanywa na jamii ikiongozwa na serikali ili kukabiliana kikamilifu na tatizo hili.

Tangu awamu ya 5 ya Utawala wa serikali,na hata awamu hii ya 6,tunaona suala la ajira kwa wasomi limekuwa ni porojo tu huku wao wakijilipa mishahara mikubwa kuliko hata uwezo wa nchi kiuchumi. Wakati mwingine tunajiuliza:
*Hivi mshahara wa mbunge(na baadhi ya viongozi) ukipunguzwa hata kwa milioni 1 Tshs kuna tatizo?
*Kwa nini kusiwe na sera ya kuwawezesha wasomi wasio na ajira(hasa vijana) ambayo itakuwa ni suluhisho la muda mfupi na la muda mrefu?
*Hivi wabunge ambao ni wawakilishi wa wananchi hawalioni hili?
*Eti Kuna waziri anahusika na ajira?
*Eti tujiajiri, mbona wao na watoto wao hawajiajiri kivile?

Ila sisi tumekusudia kuitisha maombi kitaifa ili basi serikali yetu tuiombee iwe sikivu na elevu zaidi. Hii njia ni nzuri kuliko zote na itatoa majibu muda mfupi baadaye.

Mungu ibariki Tanzania.
 
Wakiufuta,Mungu atawaandikia mioyoni mwao. Nasikia wanapanga kufungua ma veta mengine na kununua ma ndege.
Loo! Aliyeshiba hamkumbuki mwenye njaa.
 
Wasomi wanashindwa kutengeneza ajira kwa wasomi wenzao. Inauma sana.
 
Neno msomi linaanza kutumika vibaya hivi mtu akiwa na digrii Moja ni msomi?
 
Tatizo la ajira za umma huanza taratibu na baadaye kuwa kubwa na sugu kabisa.

Lakini hata hivyo, zipo njia sahihi za kufanywa na jamii ikiongozwa na serikali ili kukabiliana kikamilifu na tatizo hili...
Nafasi ya Ajira ikitokea wanaanza kuwaengua Kwa kigezo cha Umri au intake tuliomaliza. Wanasema waombe waliomaliza 2019 na 2020. 2015 -2018 tupa kule walishazeekea Mtaani. Ni maumivu Bora tusingesoma. Tujitahidi msemo maarufu hatuna mitaji labda tuwe madalali Sokoni au Vyumba na Mashamba.
 
Back
Top Bottom