SoC01 Wahitimu wa Vyuo na Maisha ya utafutaji Mtaani

Stories of Change - 2021 Competition

Theb

JF-Expert Member
Jan 25, 2019
3,929
7,268
Habari zenu wana Jamii Forums, hususani jukwaa hili la "Stories of Change". Ni tumaini langu wote ni wazima.

Andiko hili litaangazia maisha ya vijana wahitimu wa vyuo waliotegemea kuajiriwa na hali imekua tofauti na matarajio yao. Mwanzo, nitaelezea maisha ya mtaani, changamoto zinazo wakabili na vipi watatue hizo changamoto, Pili, nitaelezea fursa zisizohitaji mitaji na zenye kuhitaji mitaji. Tatu, nitaelezea mchango wa serikali na sekta binafsi katika kuwasaidia vijana kupata ajira na kujiajiri. Mwisho, nitamalizia kwa kutoa ushauri wangu katika kuwawezesha vijana wahitimu kujikwamua.

Maisha ya mtaani katika jamii zetu karibia kote yana mfanano kwa asilimia kubwa. Kuanzia ngazi ya familia za wahitimu walio wengi zinafanana kiuchumi, kitamaduni na hata kimalengo. Familia nyingi katika jamii zetu Tanzania tunasoma ili tuajiriwe na sio kujiajiri kwa waliowengi, hali iliyopo kwa sasa imeenda kinyume na malengo na matarijio ya vijana waliokuwa wanasoma na wanaoendelea kusoma mashuleni mpaka vyuoni.

CHANGAMOTO ZINAZO WAKABILI VIJANA WAHITIMU KATIKA UTAFUTAJI.

1. Kushindwa kujiamini na kushindwa kuikubali hali halisi iliyopo. Wengi wameshindwa kujiamini na kufikiria nje ya kitu walichosomea na kuanza kitu kipya ina wawia ngumu.

2. Mazingira yanayo wazunguka wahitimu, jamii ina wapa wakati mgumu kwa kuwahukumu kuwa wamesoma bure, elimu yao haina faida. Hili sio sawa.

3. Ukosefu wa muunganiko baina ya wahitimu na waliotangulia kwenye utafutaji, hapa unakuta wahitimu hawana muunganiko na waliotangulia kwenye utafutaji mitaani.

4. Ukosefu wa mitaji, hususani kwenye biashara au fursa zinazohitaji mitaji.

5. Kukosa uelewa katika utafutaji wenyewe. Kutozijua fursa au kutozitambua biashara na majira yake. Maana kila biashara ina majira yake.

6. Kuchagua kazi. Baadhi ya wahitimu hii changamoto kubwa kwao. Hawako tayari kubeba hata mizigo wanaona aibu au wanaona haiba yao hawastahili kubeba mizigo.

7. Mfumo na mitaala ya elimu nchini haikidhi dhumuni la kujiajiri kwa sababu imejikita katika nadharia zaidi na sio hali halisi katika kujiajiri.

JINSI YA KUPAMBANA NA HIZO CHANGAMOTO:-

1. Wazazi wasaidie watoto wao kuchagua fani zitakazo wawezesha kujiajiri pindi watakapo hitimu vyuoni.

2. Kujikubali, kujitambua na kujichanganya na watafutaji wengine mitaani bila kuwaza au kujutia muda uliopoteza shuleni na vyuoni.

3. Kukubali hali halisi hususani kuwa tayari kwa kazi yoyote bila kuchagua kazi. Mfano baadhi ya wahitimu ni ngumu kufanya kazi kama kuuza mkaa au kununua chupa za plastiki zilizotumika kwa kuhofia taaluma yake au watu watamuonaje.

4. Kuzitambua fursa na kuwa tayari kupambana nazo maana utafutaji mtaani ni ushindani.

5. Kufanya uchunguzi wa biashara unayotaka kwenda kuanzisha, hapa itahitaji kutafiti kwa kile unachotaka kufanya mtaani.

6. Kupunguza matumizi yale yasiyo muhimu. Kuwa na matumizi sahihi ya fedha. Mfano waache unywaji wa pombe, kubet, uvutaji wa sigara au ulevi wowote na anasa zingine zinazo hitaji pesa.

7. Kufanya uchaguzi sahihi wa kile unachoweza kukifanya mtaani na sio kufuata mkumbo. Fanya unachokipenda na unachokiweza

8. Usisahau kutunza kile unachokipata hata kama kidogo. (Bandu bandu humaliza gogo)

FURSA ZINAZOWEZA KUSAIDIA WAHITIMU KATIKA UTAFUTAJI MTAANI

1. Fursa zisizo hitaji mitaji na zisizo hitaji mitaji mikubwa sana. (Hizi kwa ajili ya kuanza kujipatia mitaji kidogo kidogo)

(i) Vibarua viwandani
Kwa wale wahitimu waliopo mijini kuna viwanda, vipo vibarua vya kutwa na wale wanaolipwa kwa wiki viwandani. Kuna kubeba mizigo viwandani kupakia na kupakua mizigo inayoingia na inayotoka na kazi zingine kulingana na kiwanda husika.

(ii) Fursa kwenye standi za mabasi ya abiria
Pia kwenye standi za mabasi kuna baadhi ya fursa zisizohitaji mitaji au zinazohitaji mitaji midogo. Mfano kubeba mizigo ya abiria kuwa wakala wa kukata tiketi na kuunza bidhaa ndogo ndogo kama karanga maji, juisi na matunda.

(iii) Kununua plastiki na kwenda kuziuza
Hapa kuna hii fursa ya kununua plastiki na kwenda kuuza mfano kilo moja unanunua kuanzia 300 hadi 400 na kuuza iliyosagwa ni kuanzia 800 hadi 1200 isiyo sagwa ni 800 bei ya kuuza. Hii ni fursa japo inadharauliwa.

(iv) Kuwa dalali wa mazao shambani au magari ya kusafirisha mizigo au dalali wa nyumba na viwanja
Haihitaji mtaji kwenye kuanza uaminifu wako na kujua chimbo za unachofanya ndio mtaji wako.

(v) Kuanzisha twisheni (tuition) mtaani kwenu
Hii pia saa zingine haihitaji mtaji itahitaji tu utayari wako na uwepo wa wanafunzi wanaosoma na kuitangaza. Japo maeneo mengine hii haina nafasi maana muitiko unakua mdogo hasa vijijini.

(vi) Kubeba mizigo kwenye masoko kupakua na kupakia mazao na bidhaa mbalimbali
Tunaweza kuidharau lakini ni fursa ukibeba mizigo 25 yenye kulipwa 1000 kila mzigo kwa siku una shilingi 25000. Haitaki mtu mwenye aibu na usharobaro.

(v). Kipaji kiwe cha uandishi, uimbaji, ususi, uchoraji, na michezo
Kipaji pia ni fursa kubwa tena isiyo hitaji mtaji ila inahitaji utayari wako kujituma na ubunifu zaidi na uvumilivu uliomithilika.

(vi). Kuwa saidia fundi ujenzi, fundi wa kuchomelea dirisha na mageti, fundi randa nk,

Kusaidia fundi atakulipa kidogo itategemea na kazi iliyopo hapo unajifunza ufundi, kujiandaa kuwa fundi ili ujitegemee. Mfano saidia fundi ujenzi hulipwa sio chini ya 10,000/= kwa siku.

(vii). Kuuza mahindi ya kuchoma na ya kuchemsha.
Hii hususani sehemu zenye mikusanyiko, stand za mabasi, barabarani na kwenye vyombo vya usafiri hususani mabasi.


2. Fursa zinazohitaji mitaji mikubwa au ya kiasi. Nitataja baadhi na ambazo ni rahisi kuzitambua kama ifuatavyo:-

(i). Kununua mazao mashambani na kuleta mjini kwenye masoko
Hapa kuna mahindi, viazi aina zote, mchele mboga mboga kutoka mashambani kuleta mijini. Kikubwa kufanya tathmini vizuri.

(ii). Umachinga wa kuuza vitu mtaani kando ya barabara au kutembeza au kutengeneza banda lako sehemu inayoonekana kwa wateja

(iii). Kilimo, uvuvi na ufugaji

Kilimo kinahitaji uwe na shamba, mbegu, pembejeo za kilimo mbolea na dawa za kupulizia kuua vijidudu hatarishi kwa mazao nacho kilimo kitategemea na aina ya mazao unayolima.

Ufugaji
Mfano wa kuku lazima uwe na mtaji wa kununua kuku, pumba, uduvi na mifupa.

(iv). Udereva boda boda au bajaji
Huu nao utahitaji uwe na mtaji au upate ya mtu. Mfano bado boda hakosi kupata 25000 hadi 30000 kwa siku.

(v). Kuanzisha saloon zote za kunyoa nywele na kusuka nywele
Hapa kwa wanaume na kwa wanawake kuna kunyoa na kusuka hivyo sehemu uliyopo ikiwa na uhitaji hii ni fursa.

(vi). Huduma ya kutuma pesa kwa njia za simu.
Kuanzisha M pesa, airtel money, tigo pesa na halopesa.

(vii). Kuanzisha mgahawa, mama ntilie au ukaangaji wa chipsi na kuchoma mishkaki.

(viii). Kununua na kuuza vyuma chakavu. Hii pia ni fursa inayolipa vizuri ni jambo la kufanya uchunguzi na kuthubutu.


MCHANGO WA SERIKALI PAMOJA NA SEKTA BINAFSI KATIKA KUWASAIDIA WAHITIMU.

1. Kuwapa motisha, semina na muongozo wa namna ya kuanza ujasiriamali.

2. Kuwapatia mikopo yenye riba nafuu au isiyo na riba kabisa.(walemavu wapewe kipaumbele).
Serikali na sekta binafsi kupitia benki na taasisi zingine za kifedha watoe mikopo kwa wahitimu. Pia familia zenye uwezo ziwawezeshe vijana wao waliohitimu.

3. Mazingira wezeshi kwa watafutaji wanaoanza kutafuta mtaani. Hapa kuwaondolea kodi kandamizi. Kuboresha miundo mbinu zaidi mijini na vijijini itasaidia usafirishaji wa bidhaa.

4. Serikali itengeneze mahusiano mazuri na mataifa mengine. Itasaidi kutanua soko la nje kwenye ajira na bidhaa au mazao yatakayo zalishwa nchini.

5. Serikali na sekta binafsi zinapaswa kwa pamoja kuwaamini vijana na kuondoa kigezo cha uzoefu katika kuwapatia kazi/ajira.

6. Serikali na sekta binafsi ziwashirikishe vijana katika juhudi za kuwainua iwe mikopo au semina za kiujasiriamali.

7. Mfumo wa elimu uboreshwe hususani mitaala. Elimu itolewe kwa vitendo na ijikite katika kuwaandaa kujitegemea/kujiajiri.

8. Wazazi, jamii, serikali na mashirika binafsi kwa pamoja watambue na kudhamini karama au vipaji vya wanafunzi toka wakiwa wadogo na kuvisimamia kwa lengo la kujiajiri baadae.

9. Wahitimu wote wenye ulemavu wapatiwe kazi serikalini na mashirika binafsi moja kwa moja. Mfano ajira za mwaka 2021 ualimu na afya serikali haikuwaacha nyuma hili liendelee kila wakati.

10.Kuwe na uwazi katika masuala ya ajira. Iwe za serikali mpaka mashirika binafsi.

11. Ukabila, rushwa, umaeneo na udini viepukwe katika kuwapatia vijana ajira.

12. Waliofikia umri wa kustaafu wasiruhusiwe kuendelea kufanya kazi.

13. Uwepo mgawanyo wa kazi.
Ili mtu mmoja asifanye kazi zaidi ya kituo kimoja.

USHAURI WANGU KWA VIJANA WAHITIMU KATIKA UTAFUTAJI
Ushauri wangu kwa vijana wasaka tonge wahanga wa ajira na vijana woote watafutaji kwa ujumla napenda kutoa ushauri kama ifuatavyo:-

(i). Uvumilivu kwenye hizo fursa tunazoenda kuanzisha maana nako pia tutakutana na changamoto ila tusivunjike moyo na tusikate tamaa mapambano yaendelee.

(ii). Tuzijue hizo fursa na kutambua majira ya hizo fursa itasaidia kutambua muda gani muafaka wa kuanza tusikurupuke kuna kuanguka pia.

(iii). Kama unamtaji usianze na pesa yote ya mtaji maana hauna uhakika 100% kuwa itaenda sawa hivyo kujipanga kwa hilo ni muhimu.

(iv). Kupata ushauri kwa waliofanikiwa ni muhimu itakuongezea maarifa kwa yale usiyo yajua.

(v). Usimuamini kila mtu katika utafutaji wako wengine watakukwamisha. Mfano wanao kopa ni sumu kwako unaeanza utafutaji.

(vi). Tambua hitaji la jamii ikizungukayo. Kama jamii inataka mahindi wapelekee mahindi na sio mchele.

(vii). Ishi vizuri na watu na waheshimu watu kwa imani zao makabila yao na rangi zao. Kuwa na lugha nzuri.

(viii). Zingatia usafi kwenye ofisi yako kuwa na mpangilio mzuri pia toa huduma iliyo bora sio bora huduma.

(ix). Muhimu na la kukumbukwa kila unapopata kidogo kitunze kadri kinavyo kua kiwekeze kitaleta zaidi.

(X). Fanya shughuli halali, kuwa muaminifu, uadilifu ni muhimu na kufuata sheria za nchi yetu katika utafutaji.
 
Unapigia wapi kura.

#MaendeleoHayanaChama
Fungua andiko chini mwisho wa andiko kuna option ya ku vote gusa mara moja.


Mfano
Angalia picha chini
2021_07_25_14.23.47.jpg


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mtu anaepata tabu kupiga kura ni julishe ujishindwa kufanya haya maelekezo nayotoa hapa

Namna ya kupiga kura unafungua uzi wenyewe link hii hapa chini.

Story of Change - Wahitimu wa Vyuo na Maisha ya utafutaji Mtaani

Ukishaifungua shuka mwisho wa andiko utaona option yenye alama sawa na V mbele imeandikwa vote . Gusa tu hiyo V mara moja

Mfano angalia picha chini nimechora hicho kialama cha kupiga kura
Polish_20210726_173330991.jpg


Sent using Jamii Forums mobile app
 

Attachments

  • Polish_20210726_173330991.jpg
    Polish_20210726_173330991.jpg
    46.8 KB · Views: 35
H
Habari zenu wana Jamii Forums, hususani jukwaa hili la stories of change. Ni tumaini langu nyote ni wazima.

Andiko hili litaangazia maisha ya vijana wahitimu vyuo waliotegemea kuajiriwa na hali imekua tofauti na matarajio yao.

Naanza kwa kuelezea maisha ya mtaani na baadhi ya fursa zenye kuhitaji mitaji na zisizohitaji mitaji na changamoto zake na vipi tunaweza kuzikabili changamoto na kutuwezesha kupita katika baadhi ya hizo fursa na tuweze kujikwamua.

Maisha ya mtaani katika jamii zetu karibia kote yana mfanano kwa asilimia kubwa. Kuanzia ngazi ya familia za wahitimu walio wengi zinafanana kichumi kitamaduni na hata kimalengo. Familia nyingi za jamii zetu Tanzania tunasoma ili tuajiriwe na sio kujiajiri kwa waliowengi, hali iliyopo kwa sasa sio siri imeenda kinyume na malengo na matarijio ya vijana waliokuwa wanasoma na wanaoendelea kusoma mashuleni mpaka vyuoni.

Nitaanza na kuelezea changamoto zinazokabili vijana wahitimu wa vyuo kwa ujumla kama ifuatavyo:-

1. Kutokujiamini na kutokubaliana na ukosefu wa ajira kwa vijana wengi, nidhahiri kuwa vijana wahitimu wa vyuo ni ngumu kukubali kuwa ajira ni chache hivyo inawawia ngumu kufanya maamuzi ya kuanza kitu kipya katika fursa zilizopo mtaani.

2. Mazingira yanoyowazunguka wahitimu, jamii inawahukumu wahitimu bila kuwapa motisha au kuwashika mkono kifedha au kiushauri. Ni kawaida mtaani kusikia mtu akimwambia muhitimu umesoma una nini zaidi kunizidi..? Hizi kauli hukatisha tamaa na kuwaongezea sonona na paniki.

3. Kukosa kampani au muunganiko na watu waliotangulia kwenye mitaa, hapa unakuta wahitimu hawana muunganiko na waliotangulia kwenye mitaa kiutaftaji. Japo hio sio sana.(lack of support)

4. Kutokua na mitaji, hususani kwenye biashara au fursa zinazohitaji mitaji.

5. Kutokua na uelewa wa mitaa na utaftaji wenyewe. Yaani kutozijua fursa au kutozitambua biashara na majira yake. Maana kila biashara ina majira yake.

6. Kuchagua kazi. Hii inahusika saana baadhi ya wahitimu hii changamoto kubwa kwao. Hawako tayari kubeba hata gunia wanaona aibu au wanaona haiba yao hawastahili kubeba gunia.

Jinsi gani wanaweza kupambana na hizi changamoto:-

1. Kujikubali na kujichanganya na watafutaji wengine mitaani bila kuwaza au kujutia muda uliopoteza shuleni na vyuoni.

2. Kukubali hali halisi hususani kuwa tayari kwa kazi yoyote bila kuchagua kazi. Mfano baadhi ya wahitimu ina muwia ngumu kufanya kazi kama kuuza mkaa au kununua chupa za plastiki zilizotumika kwa kuhofia taaluma yake au watu watamuonaje.

3. Kuzitambua fursa na kuwa tayari kupambana nazo maana utaftaji mtaani ni ushindani.

4. Kuyajua mazingira ya biashara unayotaka kwenda kuanzisha, hapa itahitaji muunganiko na wanaoitambua biashara husika unayotaka kuanzisha kwenye mazingira unayopanga.

5. Kupunguza matumizi yale yasiyo muhimu, hapa matumizi yale yasiyomuhimu ambayo yanafuja pesa hainabudi kuyaacha. Mfano unywaji wa pombe, kubet, uvutaji wa sigara au ulevi wowote na anasa zingine zinazo hitaji pesa.

6. Kufanya uchaguzi sahihi wa kile unachoweza kukifanya mtaani na sio kufwata mkumbo. Je mhitimu unaweza kitu gani kama ni kilimo basi fanya kilimo kama ni ufundi fanya ufundi.

Fursa zilizopo katika jamii zetu ambazo wahitimu au mtafutaji yeyote anaweza kuzitazama na kuamua kuanza kujipatia kipato kupitia hizo fursa

Nitataja ambazo nimeziona na nazifahamu na watu wanafanya nitaanza na zisizo hitaji mitaji mikubwa au zisizo hitaji mitaji kabisa na baada ya hizo nitaangazia zenye uhitaji wa mitaji angalau mikubwa kiasi.

1. Fursa zisizo hitaji mitaji na zisizo hitaji mitaji mikubwa sana.

(i) Vibarua viwandani
Kwa wale wahitimu waliopo mijini kuliko na viwanda kuna upatikanaji wa vibarua wa kutwa na wale wanaolipwa kwa wiki kwenye viwanda. Kuna kubeba mizigo viwandani kupakia na kupakua mizigo inayoingia na inayotoka na kazi zingine kulingana na kiwanda husika.

(ii) Fursa kwenye standi za mabasi ya abiria
Pia kwenye standi za mabasi kuna baadhi ya fursa zisizohitaji mitaji au zinazohitaji mitaji midogo, mfano kubeba mizigo ya abiria kuwa wakala wa kukata tiketi na kuunza bidhaa ndogo ndogo kama karanga maji, juisi na matunda.

(iii) Kununua chupa za plastiki na kwenda kuziuza
Hapa kuna hii fursa ya kununua au hata kuokota chupa za plastiki na kwenda kuuza mfano kilo moja unanunua kuanzia 300 hadi mia 400 na kuuza iliyosagwa ni kuanzia 800 hadi 1200 isiyo sagwa ni 800 bei ya kuuza. Hii ni fursa japo inadharauliwa.
View attachment 1865584
Chanzo cha picha Mwananchi

(iv) Kuwa dalali wa mazao shambani au magari ya kusafirisha mizigo au dalali wa nyumba viwanja nk
Hii nayo haihitaji mtaji kwenye kuanza uaminifu wako na kujua chimbo za unachofanya ndio mtaji wako.

(v) Kuanzisha twisheni (tuition) mtaani kwenu
Hii pia saa zingine haihitaji mtaji itajitaji tu utayari wako na uwepo wa wanafunzi wanaosoma na kuitangaza. Japo maeneo mengine hii haina nafasi maana muitiko unakua mdogo.

(vi) Kubeba mizigo kwenye masoko kupakua na kupakia mazao na bidhaa mbalimbali
Tunaweza kuidharau lakini ni fursa ukibeba mizigo 25 yenye kulipwa 1000 kila mzigo kwa siku una shilingi 25000. Inafaa japo haitaki mtu mwenye aibu na usharobaro.

(v). Kipaji kiwe cha uandishi, uimbaji, ususi, uchoraji, na michezo
Kipaji pia ni fursa kubwa tena isiyo hitaji mtaji ila itataka utayari wako kujituma na ubunifu zaidi na uvumilivu uliomithilika.

Hizo ni baadhi ya fursa zisizo hitaji mitaji mikubwa au zinazohitaji mtaji mdogo.

2. Fursa zinazohitaji mitaji mikubwa au ya kiasi. Nitataja baadhi na ambazo ni rahisi kujichanganya kama ifuatavyo:-

(i). Kununua mazao mashambani na kuleta mjini kwenye masoko
Hapa kuna mazao mfano mboga mboga kama nyanya, mchicha, na mboga mboga zoote zinazolimwa nchini na mazao ya nafaka kama mahindi, mchele, viazi, ndizi mbivu na za kupika, machungwa na matunda mengine hizi zinataka mitaji yaweza kuwa laki kadhaa mpaka milioni kadhaa kutegemea na biashara unayotaka mana mfano huwezi linganisha anaepeleka mchicha sokoni na anaepeleka viazi mviringo mitaji itatofautiana na zaidi kutambua misimu mizuri ya hiyo biashara unayotaka kuanzisha.

(ii). Umachinga wa kuuza vitu mtaani kando ya barabara au kutembeza au kutengeneza banda lako sehemu inayoonekana kwa wateja
Hii inahitaji mtaji nayo inategemea na biashara husika. Mfano kuuza matunda, bisi, juisi na kadhalika

(iii). Kilimo, uvuvi na ufugaji
Hizi nazo ni fursa lakini zinahitaji mtaji maana kilimo lazima uwe na shamba, mbegu, pembejeo za kilimo kama mbolea na dawa za kupulizia kuua vijidudu hatarishi kwa mazao nacho kilimo kitategemea na aina ya mazao unayolima. Uvuvi pia utahitaji mtaji kununua nyavu nk ufugaji pia kama ni kuku lazima uwe na mtaji wa kununua kuku, pumba, uduvi na mifupa. Hii ni baadhi ya mifano.

(iv). Udereva boda boda au bajaji
Huu nao utahitaji uwe na mtaji kama utahitaji boda boda yako mwenyewe lakini kama utapata boda boda ya mtu itakubidi ujifunze kuendesha pikipiki au bajaji. Mfano boda boda anayendesha ya kwake mwenyewe kwa siku anauhakika wa kupata 30000 haipungui itategemea na eneo alilopo.

(v). Kuanzisha saloon zote za kunyoa nywele na kusuka nywele
Hapa kwa wanaume na kwa wanawake kuna kunyoa na kusuka hivyo sehemu uliyopo kama panauhitaji hii ni fursa.

(vi). Zipo zingine kama kutuma pesa yani (m pesa, airtel money, tigo pesa na halopesa) ndio makato mmmhh yameongezwa lakini ni fursa.

(vii). Kuanzisha mgahawa, mama ntilie au ukaangaji wa chipsi na kuchoma mishkaki.
Hii nayo ni fursa nzuri tena inalipa saana. Mfano banda la chipsi kwenye kiloba cha viazi cha ndoo 4 kama utaweza au utapata sehemu ambayo unauza kiloba chote kwa siku unauwezo wakupata faida sio chini ya 50,000 kwa maana kila ndoo unayomenya itakupa sahani 35 hadi 37 inategemea na upimaji wako. Kwenye ndoo 4 au 3 na nusu itakupa hesabu nzuri.

Zipo fursa nyingi na nyingi hizo ni baaadhi nikizitaja na kuelezea zote andiko halitatosha.

Hitimisho
Nimetoa baadhi ya fursa na nilianza kwa kutoa changamoto zinazowakabili wahitimu ni baadhi sio zote. Ila ushauri wangu kwa vijana wasaka tonge wahanga wa ajira na vijana woote kwa ujumla napenda kutoa ushauri kama ufuatao:-

(i). Uvumilivu kwenye hizo fursa tunazoenda kuanzisha maana nako pia tutakutana na changamoto za kudondoka kukwama nakadhalika ila tusivunjike moyo na tusikate tamaa mapambano yaendelee.

(ii). Tuzijue hizo fursa na kutambua majira ya hizo fursa itasaidia kutambua muda gani muafaka wa kuanza tusikurupuke kuna kuanguka pia.

(iii). Kama unamtaji usianze na pesa yote ya mtaji maana hauna uhakika 100% kuwa itaenda sawa hivyo kujipanga kwa hilo ni muhimu.

(iv). Kupata ushauri kwa waliofanikiwa ni muhimu itakuongezea maarifa kwa yale usiyo yakua.

(v). Usimwamini kila mtu katika kufanya utafutaji wako wengine watakukwamisha. Mfano wanao kopa hawa ni sumu kwako unaeanza utafutaji.

(vi). Tambua hitaji la jamii ikizungukayo. Kama jamii inataka mahindi wapelekee mahindi na sio mchele. (Hitaji la wateja).

(vii). Ishi vizuri na watu na waheshimu watu kwa imani zao makabila yao na rangi zao.

(viii). Kuwa msafi au zingatia usafi kwenye ofisi yako kuwa na mpangilio mzuri na boresha mazingira ya ofisi yako. Kwa zile fursa zinazohitaji usafi kama mamantilie kibanda cha chipsi duka na nyingine hata machinga kuwa msafi katika bidhaa zao na wewe mwenyewe.


Hapa nimefikia mwisho wa andiko langu. Natumaini kidogo kitaeleweka kwa wengi haijaelezea kila.kitu ila nimeelezea kwa uchache kwa yale niliyojionea na kujifunza mtaani


View attachment 1861642View attachment 1861643
Picha chanzo mtanzanonk

Umeandika vizuri sana, tatizo la ajira linasumbua na wahitimu wetu wamejaa mitaani hawana cha kufanya
Niseme tu tusiwaachie serikali peke yake...ukipata nafasi soma kitabu kilichoandikwa na Baltazay Luhanga "succeed before your graduation" hii inasaidia sana kuwanoa Wana chuo na kuwapa mwangaza mkubwa sana
 
H



Niseme tu tusiwaachie serikali peke yake...ukipata nafasi soma kitabu kilichoandikwa na Baltazay Luhanga "succeed before your graduation" hii inasaidia sana kuwanoa Wana chuo na kuwapa mwangaza mkubwa sana
Asante kwa mchango wako. Ndugu vyote hivyo ni katika hali ya kupeana ufahamu kuhusu changamoto hiyo ya ajira na sio suala la kuiachia tu serikali hapana kila mtu au hata taasisi binafsi pia wahitimu wenyewe lazima kupata ufahamu wa yote tunayoona yanaweza kuwasaidia kuondokana na changamoto ya ukosefu wa ajira

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Asante kwa mchango wako. Ndugu vyote hivyo ni katika hali ya kupeana ufahamu kuhusu changamoto hiyo ya ajira na sio suala la kuiachia tu serikali hapana kila mtu au hata taasisi binafsi pia wahitimu wenyewe lazima kupata ufahamu wa yote tunayoona yanaweza kuwasaidia kuondokana na changamoto ya ukosefu wa ajira

Sent using Jamii Forums mobile app
Umenena sawa kabsa mkuu
 
Elimu Yetu tuliyorithi toka kwa wakoloni ndio tatizo , kipindi hicho watu walisoma ili wakasaidie kazi za ofisini kwa sababu wanataaluma walikua wachache sana, sasa tatizo ni kwamba watu tumeongezeka ajira hakuna inasikitisha kijana wa kitanzania anamaliza chuo akiwa na 27 yrs na hajui akirudi mtaani atafanya nini!
 
Elimu yetu inamfanya kijana awe muoga na asijiamini leo hii kiukweli tunahitaji kuwekeza kwenye ujuzi zaidi kuliko kwenye hizo theory wanazofundishwa huko mashuleni,
Talent based education tuitilie mkazo na zaidi elimu iendane na mazingira hali ni mbaya na inasikitisha, kijana alieishia darasa la saba akaenda gereji au aliishia formfour akaenda gereji na akajifunza umeme wa magari tu kamwe wewe na degree yako unakuja kurudi tayari keshajenga na anamiradi kadhaa inaingiza kipato cha uhakika na hakupoteza muda wake vyuoni na asilimia kubwa mambo unayosoma vyuoni kiukweli ni machache sana utayatumia kwenye maisha halisi
 
Leo hii mtu akikuuliza hivi hesabu za logarithm au aligebra unazitumia wapi huwezi kutoa jibu, kumbe ilitakiwa ujue kusoma na kuandika na labda kujumlisha, kutoa, kuzidisha na kugawana ambazo ndio hesabu unazotumia kila siku kwenye maisha na sio zaidi, ndio maana walioendelea kitu specialization wanakijali sana mtoto anausoma ubongo toka mdogo yeye hadi anakua daktari wa ubongo anaelewa kila kitu hao ndio tunawaita madaktari bingwa na tunawafuata kwao na kupeleka pesa huko
 
Angalia kwanza unapochanganyikiwa wewe toka darasa la kwanza masomo kumi, ndio ukiingia darasa la pili yale masomo darasa la kwanza ushasahau, haya chuo masomo kibao yaani ukimaliza semister unaanza semister mpya yale ya nyuma ushasahau kwakua kichwa unakilisha mambo mengi halafu useless, lazima haya mambo yaangaliwe na ndio sababu nchi inazidi kua maskini kwakua mindset zetu hazijiamini pamoja na kua na fursa kibao
 
Back
Top Bottom