Wahisani waiumbua serikali

TUKUTUKU

JF-Expert Member
Sep 14, 2010
11,769
4,032
Kundi la wahisani wanaochangia bajeti kuu ya Tanzania (GBS) limeibua kashfa baada ya kueleza kuwa serikali iliwapelekea bajeti tofauti na ile iliyopitishwa na bunge julai mwaka huu.
Taarifa za kashfa hiyo ziliwekwa hadharani jana asubuhi na mwenyekiti wa wahisani hao,Svein Baera wa Sweden katika mkutano wa kitaifa wa mwaka wa majadiliano ya kisera na bajeti ulifanyika jijini Dar es salaam.
Sweden ndiyo inayoshikilia uenyekiti wa kundi hilo linalojumisha taasisi za kimataifa na nchi mbalimbali zinazoendelea.Kuibuka kwa kashfa hiyo kunakuja wakati wahisani hao wakiwa wamezuia theluthi moja ya zaidi ya dola 800 milioni za kimarekani ambazo zinatakiwa zichangie kwenye bajeti kuu ya 2010/2011,wakiishinikiza serikali iharakishe utekelezaji wa programu ya mageuzi ,yakiwemo ya mfumo wa usimamizi wa fedha za serikali. “Napenda kuainisha maeneo sita ya ujumbe wetu ili kuweka sawa jukwaa la majadiliano yetu haya ya mwaka.Kuna tofauti kati ya bajeti iliyowasilishwa kwa bodi ya (Shirika la kimataifa la fedha)IMF na ile iliyopitishwa na bunge julai 2010” alisema Baera.
Alisema bajeti ambayo serikali iliwasilisha kwa wahisani hao ilibeba “matumaini makubwa ya kuzaa matokeo mazuri na kufanywa kama sababu ya kupitisha matumizi makubwa ya fedha zitokanazo na mapato ya ndani”.
Baera alisema kuwa kukosekana kwa uwazi katika matumizi ,vipaumbele,mapato na mfumo mzima wa fedha kunapunguza kuaminika kwa bajeti hiyo mbele ya wafadhili.
Kwa mujibu wa wahisani hao,kumekuwepo na mtiririko wa athari katika bajeti katika miaka ya karibuni huku ikionyesha ongezeko kubwa la matumizi ya kawaida kuliko yale ya maendeleo.[Chanzo cha habari:Mwananchi 7 Desemba 2010.pp 1&4]

My take
Duh!jamani uchakachuaji mbaka kwenye bajeti zinazowasilishwa kwa wahisani!je hili ni kosa la kibinadamu au kulikuwa na nia maalumu!hii ni kujiabisha mbele ya wahisani kwamba sisi ni wasanii tuliyobobea na inawezekana wahisani wajawahi kukutana na kitu kama hiki tangu waanze programu ya kuzisaidia nchi masikini!
 

Mtu wa Mungu

JF-Expert Member
Nov 9, 2010
444
19
"Mficha ficha maradhi kilio kitamfichua" ndiyo tunayoambiwa hapa!!!!!!Chadema kaza buti!!!!, watang'ooka tu!!!!!!!!!! Hizi ni dalili njema za msingi tayari umeanza kukubali pressure ya CDM!!!!!! Wafadhili wanawaogopa walipa kodi kule kwao, ambao siyo kama hawa wa bongo!!!!!! Wambieni wafadhili JK, RA, AC, EL, + associates wana mpango wa kufidia gharama za uchaguzi, na kujiandaa kuchakachua uchaguzi wa 2015!!!!!!!!! Ndiyo maana kuna bajeti mbili!!!!!! Heri jamaa wamewatonya mapema wakashituka!!!!!!!!!!!!!!!!!!! Wambieni wafadhili pia habari za Tshs bilioni 184 kuwa ni sehemu ya mpango wao hawa mafisadi!!!!!!! Hawa mafisadi washukuru nchi ya bongo-ingekuwa Gatundu kingdom ya mzee haraaaaambeee, sasa hivi vichwa vingi vingekwisha katwa kudai haki!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

0 Reactions
Reply
Top Bottom