Wahisani wagoma kueleza lini watatoa fedha kwa Tanzania | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wahisani wagoma kueleza lini watatoa fedha kwa Tanzania

Discussion in 'Biashara, Uchumi na Ujasiriamali' started by BAK, Sep 7, 2008.

 1. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #1
  Sep 7, 2008
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,701
  Likes Received: 82,626
  Trophy Points: 280
  Date::9/6/2008
  Wahisani wagoma kueleza lini watatoa fedha kwa Tanzania
  Na Boniface Meena
  Mwananchi

  NCHI wahisani zinazochangia bajeti ya serikali katika miradi ya maendeleo zimesema kuwa, hazijui lini mazungumzo kati yake na serikali yanayoendelea yatakwisha ili wakabidhi mchango huo.

  Hivi karibuni, wahisani hao walieleza kuwa wangependa kuendelea kuwa na mazungumzo ya uso kwa uso na serikali mpaka watakapofikia maamuzi ya kutoa fedha hizo baada ya hotuba ya Rais Kikwete bungeni Dodoma Agosti 21 mwaka huu

  Akizungumza na Mwananchi Jumapili kwa njia ya simu, mmoja wa maofisa wa ubalozi wa Denmark nchini ambao ndiye mwenyekiti wa wahisani hao alisema pamoja na kuamua kukutana na serikali mara kwa mara ili kuzungumzia suala hilo hawajui ni lini mazungumzo hayo yatafikia ukomo.

  "Kwa kweli sijui ni lini mazungumzo yataisha na kufikia uamuzi ila tutaendelea kukutana na serikali hadi hapo tutakapofikia uamuzi wa kutoa fedha hizo," alisema ofisa huyo.

  "Kutokana na taarifa ya Rais Kikwete bungeni Dodoma, nchi wahisani zinaona ni vema kuendelea na mazungumzo ya uso kwa uso na serikali na yatakapofikia ukomo, tutatoa taarifa," alisema ofisa huyo.

  Kutokana na msimamo wa wahisani hao, ufadhili wa miradi ya maendeleo katika bajeti ya serikali utazidi kuchelewa baada ya nchi wahisani zinazochangia bajeti hiyo kupata kigugumizi cha kusema lini zitaanza kutoa fedha walizoahidi kuchangia katika mwaka wa fedha 2008/09.

  Wahisani hao wamekuwa wakikutana na viongozi wa serikali kutoka Wizara ya Fedha na Uchumi kujadili mambo ya kutekelezwa ili waweze kuto fedha hizo, lakini ufisadi wa EPA umekuwa kikwazo kufikia mwafaka.

  Walipokutana kwa mara ya mwisho, Julai 19 mwaka huu, hawakutamka ni lini hasa watatoa fedha.

  Taarifa ya maandishi kwa gazeti hili Julai 19, kutoka kwa Mwenyekiti wa kundi la wafadhili hao 11, ambaye pia ni Balozi wa Denmark nchini, Bjarne Sorensen, ilisema: "Nathibitisha kwamba, kundi la nchi wafadhili lilifanya mkutano na Mheshimiwa Mkulo, Waziri wa Fedha na Uchumi.

  "Mkutano huo ni sehemu ya mikutano ya kawaida na mijadala tunayofanya na mheshimiwa waziri wa fedha, ambako hujadili na kuangalia maendeleo muhimu yatakayotupa fursa ya kuamua ni lini tutaanza kutoa fedha kwa Bajeti ya mwaka 2008/09."

  Kutokana na kauli ya wahisani hao, ilionekana bado wanaendelea kuiminya serikali hadi itakapochukua hatua zilizopendekezwa dhidi ya watuhumiwa wa fedha za Akaunti ya Madeni ya Nje (EPA); ufisadi ndani ya Benki Kuu ya Tanzania na taarifa ya Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Serikali (CAG).

  Msimamo huu unakwenda sambamba na kauli waliyotoa wakati wakiridhia kusaidia katika bajeti ya mwaka huu, wakisema: "Kabla ya kutoa fedha kusaidia bajeti hiyo tunatazamia kupokea taarifa zaidi za utekelezaji wa namna serikali inavyopambana na tuhuma za rushwa, kuboresha utawala, na utekelezaji wa mapendekezo ya CAG yaliyohusu ukaguzi wa hesabu za Benki Kuu ya Tanzania kwa mwaka wa fedha wa 2005/06."

  Wafadhili hao wameahidi kuchangia asilimia 34 kwenye bajeti ya mwaka huu ya Sh 7.2 trilioni, hali ambayo inaiweka serikali kwenye wakati mgumu kama hazitatolewa kwa wakati kwani ndizo zinategemewa kuendesha miradi ya maendeleo.

  Mara ya mwisho wafadhili kuibana serikali katika bajeti yake ni wakati wa utawala wa Rais wa awamu ya pili ya Ali Hassan Mwinyi, walipokataa kufadhili Tanzania kutokana na serikali kushindwa kukusanya kodi kiasi cha Sh bilioni 70 wakati huo.

  Makusanyo ya kodi serikalini wakati huo, yaani mwaka 1995, ilikuwa ni Sh 28 bilioni kwa mwezi. Kiasi kikubwa cha kodi ambazo hazikukusanywa ilikuwa ni misamaha ya kodi pamoja na wafanyabiashara wakubwa kukwepa kodi. Hali hiyo ilidhibitiwa baada ya Rais Benjamin Mkapa kuingia madarakani.
   
 2. M

  MiratKad JF-Expert Member

  #2
  Sep 7, 2008
  Joined: May 2, 2008
  Messages: 294
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Wakuu, Bubu

  Kuna mtu anafahamu details (emails, post, phone) za hawa wahisani ili tuendelee kuwapa shinikizo la kutochangia bajeti mpaka serikali ihakikishe kuwa haki zinapatikana. E.g., jamaa wa EPA nk nk wafikishwe kwenye mikono ya sheria. Asante
   
 3. M

  MiratKad JF-Expert Member

  #3
  Sep 7, 2008
  Joined: May 2, 2008
  Messages: 294
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Here we go! Details za Danish Ambassador ambaye anaweza kutusaidia.

  ...EPA scandal. Denmark withdrew 4.1bn/- in general support....

  Bjarne Henneberg Sørensen
  Royal Danish Embassy
  Ghana Avenue
  P.O. Box 9171
  Dar es Salaam Tel. +255 (22) 211 3887
  Fax +255 (22) 211 6433
  E-mail: daramb@um.dk
   
 4. Freetown

  Freetown JF-Expert Member

  #4
  Sep 7, 2008
  Joined: Apr 6, 2008
  Messages: 887
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 35

  Royal Danish Embassy
  Tel. +255 (22) 211 3887
  Fax +255 (22) 211 6433
  E-mail: daramb@um.dk


  Royal Danish Consulate
  Tel. +255 (27) 250 4865
  Fax +255 (27) 250 4865
  Mobile: +255 (0) 754 276 980
  E-mail: geertholm@yahoo.com
   
 5. Mshiiri

  Mshiiri JF-Expert Member

  #5
  Sep 7, 2008
  Joined: Jun 16, 2008
  Messages: 1,893
  Likes Received: 66
  Trophy Points: 145
  Tufanye hima kabisa wanaJF kushinikiza kisomi kwamaba hamna haja ya nchi hisani kutoa misaada ambayo ni kidogo ukilinganisha na fedha zinazoliwa kifisadi. Actually ni ujinga uliokithiri. Kutumia vibaya milioni moja ikiisha unaomba mia moja. Tunza na tumia vizuri milioni moja yako na kisha usiombe mia moja na hapo utatunza heshima yako katika world map. Au mnasemaje wanajamvi?
   
 6. M

  Mwikimbi JF-Expert Member

  #6
  Sep 7, 2008
  Joined: Mar 8, 2008
  Messages: 1,745
  Likes Received: 109
  Trophy Points: 160
  Wahisani wengine wanafiki, ebu fikiria yule mkurugenzi wa imf aliyemwambia kikwete kuwa hatua alizochukuwa kuhusu epa ni madhubuti na hazijawahi kuchukuliwa mahali popote duniani? Hivi bush angefanya alichofanya kikwete kuhusu epa white house kungetosha?
   
 7. M

  Mwikimbi JF-Expert Member

  #7
  Sep 7, 2008
  Joined: Mar 8, 2008
  Messages: 1,745
  Likes Received: 109
  Trophy Points: 160
  Anyway! Sikatishi tamaa, naomba kama kuna mwenye email ya yule mk..aliyemsifia kikwete kuhusu epa, kule amerca anipe nianzane naye kuhusu unafiki wake
   
 8. M

  Mwikimbi JF-Expert Member

  #8
  Sep 7, 2008
  Joined: Mar 8, 2008
  Messages: 1,745
  Likes Received: 109
  Trophy Points: 160
  Weka emails za balozi zote za ulaya na marekani zinazochangia bajeti, wachina achana nao
   
 9. T

  Tom JF-Expert Member

  #9
  Sep 8, 2008
  Joined: May 14, 2007
  Messages: 472
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Wahisani wataendelea kutoa misaada na wataendelea kuiendesha Tanzania wapendavyo kama omba omba asiyekua na akili. Toka enzi za raisi wa kwanza TZ ni omba omba, labda ndoto kuiondoa CCM ijikamishe yenyewe. Watz ilivyologwa na CCM, CCM haitaondoka karibuni.
   
 10. Bongolander

  Bongolander JF-Expert Member

  #10
  Sep 8, 2008
  Joined: Jul 10, 2007
  Messages: 4,882
  Likes Received: 47
  Trophy Points: 135
  Ndugu yangu usije ukadhani kama watanzania ni wajinga kiasi hicho, lakini ni kweli kwa sasa CCM inaonekana ina maana zaidi kuliko Tanzania, no body cares whether Tanzania itapata misaada au la, kama CCM inapata mambo mdundo tu. NI wazi kuwa CCM ikipasuka au kuondolewa madarakani, pamoja na matatizo yanayoweza kutokea, itakuwa baraka kutoka kwa mungu.
   
Loading...