Wahisani:Bajeti tuliyopewa ni tofauti na ile iliyosomwa Bungeni

Babu Lao

JF-Expert Member
Nov 2, 2010
2,044
179
KUNDI la wahisani wanaochangia bajeti kuu ya Tanzania (GBS) limeibua kashfa baada ya kueleza kuwa serikali iliwapelekea bajeti tofauti na ile iliyopitishwa na Bunge Julai mwaka huu.Taarifa za kashfa hiyo ziliwekwa hadharani jana asubuhi na mwenyekiti wa wahisani hao, Svein Baera wa Sweden katika mkutano wa kitaifa wa mwaka wa majadiliano ya kisera na bajeti uliofanyika jijini Dar es salaam.
Source: Mwananchi - Tuesday, 07 December 2010

Waungwana hii imekaaje????
 
Hii ndio tanzania original hawa wanapaswa kuelewa kuwa hawa wa tz ni mwisho wa matatizo ya ukweli na uwazi duniani.
 
Duu hii awamu ya nne ina mambo ya ajabu, yani mnawapiga fix mpaka wahisani, dawa yao hao ni wahisani kufuta misaada tu kwani sisi watu wa chini hatufaidika na chochote zaidi ya hao vigogo kuneemeka na misaada hiyohiyo, CLARKE na wenzako fanyeni kweli!!
 
Huwezi kuamini kuwa jamaa kila sehemu wanachakachua. mweeee!!!!!!!!!!!!!!!

Mwandishi Wetu (Exuper Kachenje)
KUNDI la wahisani wanaochangia bajeti kuu ya Tanzania (GBS) limeibua kashfa baada ya kueleza kuwa serikali iliwapelekea bajeti tofauti na ile iliyopitishwa na Bunge Julai mwaka huu.Taarifa za kashfa hiyo ziliwekwa hadharani jana asubuhi na mwenyekiti wa wahisani hao, Svein Baera wa Sweden katika mkutano wa kitaifa wa mwaka wa majadiliano ya kisera na bajeti uliofanyika jijini Dar es salaam.Sweden ndiyo inayoshikilia uenyekiti wa kundi hilo linalojumuisha taasisi za kimataifa na nchi mbalimbali zilizoendelea.

Kuibuliwa kwa kashfa hiyo kunakuja wakati wahisani hao wakiwa wamezuia theluthi moja ya zaidi ya dola 800 milioni za Kimarekani ambazo zinatakiwa zichangie kwenye bajeti kuu ya 2010/11, wakiishinikiza serikali iharakishe utekelezaji wa programu ya mageuzi, yakiwemo ya mfumo wa usimamizi wa fedha za seikali.
Akitoa hotuba yake ya ufunguzi wa mkutano huo wa siku tatu, Baera aliainisha maeneo sita kuwa ndiyo mhimili wa mjadala wao na serikali.
"Napenda kuainisha maeneo sita ya ujumbe wetu ili kuweka sawa jukwaa la majadiliano yetu haya ya mwaka. Kuna tofauti kati ya bajeti iliyowasilishwa kwa bodi ya (Shirika la Kimataifa la Fedha) IMF na ile iliyopitishwa na Bunge Julai 2010," alisema Baera.

Alisema bajeti ambayo serikali iliwasilisha kwa wahisani hao ilibeba "matumaini makubwa ya kuzaa matokeo mazuri na kufanywa kama sababu ya kupitisha matumizi makubwa ya fedha zitokanazo na mapato ya ndani".
Baera alisema kuwa kukosekana kwa uwazi katika matumizi, vipaumbele, mapato na mfumo mzima wa fedha kunapunguza kuaminika kwa bajeti hiyo mbele ya wafadhili.

Kwa mujibu wa wahisani hao, kumekuwepo na mtiririko wa athari katika bajeti katika miaka ya karibuni huku ikionyesha ongezeko kubwa la matumizi ya kawaida kuliko yale ya maendeleo.
Kwa mujibu wa bajeti ya mwaka 2010/11 ambayo ni ya Sh11.1 trilioni, matumizi ya kawaida ya serikali ni Sh7.8 trilioni wakati fedha zilizotengwa kwa ajili ya shughuli za maendeleo ni Sh3.2 trilioni.
Bajeti hiyo inaonyesha kuwa kati ya Sh11.1 trilioni, serikali ilitarajia kupata Sh6 trilioni kutoka katika vyanzo vya ndani, wakati inatarajia Sh2.8 trilioni kutoka kwa wahisani na mikopo. Fedha nyingine zinatarajiwa kutoka mikopo ya ndani, masharti ya kibiashara na ubinafsishaji.

"Matumaini makubwa kupindukia katika bajeti hii na kutokuwepo kwa mikakati inayoeleweka ya kipaumbele katika matumizi katika hali inayoweza kutokea ya mapato madogo na ukosefu wa fedha, yanaweza kuondoa kuaminika kwa bajeti kama chombo cha ufanisi wa sera na mipango," alisema Baera.
Zaidi ya hapo, ukweli kwamba bajeti hii tofauti ilipitishwa bila ya kuwepo mawasiliano ya awali na wabia wa maendeleo inaweka maswali kwenye ubora wa mazungumzo yetu ya sera na ubia. Tunatarajia kujadili suala hili kwenye sehemu muhimu ya bajeti.
"Zaidi ya hapo, bajeti iliyotumiwa kuanzia mwaka jana iliendeleza mwenendo wa miaka ya karibuni ambako matumizi ya kawaida yanaendelea kupanda kwa kasi kuliko matumizi kwenye maendeleo."
Kutokana na hali hiyo GBS imeitaka serikali kujipanga upya na kuweka mkazo katika kupunguza misamaha ya kodi ili kuweka uwiano na ufanisi sawa na nchi za kundi lake katika uchumi, hatua ambayo Baera alisema itapunguza pengo la bajeti linaloikabili Tanzania kila mwaka.

Tayari GBS imebainisha kuwa bajeti ijayo inaweza kuwa na nakisi ya hadi Sh1 bilioni.
Hata hivyo, Waziri wa Fedha na Uchumi, Mustafa Mkulo ambaye alishiriki mkutano huo, alipatwa na kigugumizi kujibu madai hayo ya GBS, akimkaribisha mwenyekiti huyo wa kundi la nchi wahisani aende ofisini kwake ili wazungumzie masuala hayo.
"Kuna mengine yanazungumzika; Baera ninakukaribisha ofisini kwangu; mengine yanazungumzika ofisini," alisema Mkulo.
Naibu kiongozi wa kambi ya upinzani bungeni, Zitto Kabwe alizungumzia kasoro hiyo jana akieleza kuwa imemshtua na kwamba ataifuatilia.

Zitto, ambaye pia ni mbunge wa Kigoma Kaskazini na ambaye alihudhuria mkutano huo jana, alisema kambi ya upinzani itaunda kamati kulifuatilia suala hilo.
Alisema pia watahoji suala hilo bungeni na kuitaka serikali iweke wazi kwa Watanzania ni bajeti ipi inayotumika kati ya iliyopitishwa na Bunge na ile iliyopelekwa IMF.

"Huu ni mshtuko kwangu; hili limenishtua. Tutaunda timu ya kulifuatilia; tutalifikisha bungeni na kuihoji serikali ieleze ni bajeti ipi inayotumika. Ni ile iliyopitishwa na Bunge au iliyopelekwa IMF," alisema Zitto.
Kundi hilo la nchi wahisni limesema kuwa linaunga mkono mkakati wa serikali wa Kilimo Kwanza na wa Jumuia ya Afrika Mashariki (EAC) kuhusu maendeleo ya kilimo, hifadhi ya chakula na kupunguza umasikini.

MyTake: Ndiyo maana wananunua Mashangingi ya bei mbaya kama hawana akili nzuri vile. Wapo zaidi kujifikiria wao na si Taifa. Yaani matanuzi ni makubwa kuliko pesa ya maendeleo.
Ukisoma juu utaona kuwa wanatengeneza bajeti mbili. Moja kwa ajili ya kuwapa Wazungu na nyingine kwa Wadanganyika. Nafikiri sasa hivi watakuwa wanahaha kuziba pengo la pesa waliyochota kwa ajili ya Uchaguzi. Ndiyo maana wanakuja na bajeti mbili ila wanasahau kuwa mchezo huu, Wazungu wameanza kuufanya miaka mingi sana. Wamedakwa kama watoto. Mkulo, aibu hiyoooo.........
 
Wahisani wanatushangaza pale wanapogundua dubious za serikali halafu utasikia wamewapa muda wa kurekebisha mimi sielewi wahisani wanakuwa na lengo gani haswa.Ni bora wakaondoa fungu lao tubaki na kidogo chetu ili tupate muda wa kukatana mapanga na hawa kina RA
 
Hivi hii ilifanyika kwa makusudi au kwa bahati mbaya au kwa Uzembe? Kama ni kwa uzembe, kwanini Mkullo asiujuzulu? Kama ni kwa makusudi, haibu kubwa kwa serikali ya Kikwete!!! Ninaanza kuamini kwamba mambo yanaendeshwa kisanii sanii !!!!

Tiba
 
Wanawapa mda wa kujirekebisha maana hapo na wao wamepata opportunity ya kutukaba zaidi,hivyo katika kipindi hiki cha kujirekebisha wanawaletea wataalamu wa kutengeneza bajeti nzuri au wataalamu wa kufuatilia kama kuna uwiano.Hawa jamaa ni wajanja na watatumia mwanya huo vizuri kuikandamiza serikali.Ni kama umemfumania mtu,siku ukitaka na wewe unamwingilia kwa gia kuwa usiponipa nitakusemea,naye kwa unyonge hata kama hataki atakubali ili yaishe.
 
Mpaka kieleweke ndo maana jamaa anaomba wakutane ofisini kwake faragha. Manake nini!!??
 
Mpaka kieleweke ndo maana jamaa anaomba wakutane ofisini kwake faragha. Manake nini!!??

Wamezoea kufanya dubious kwa kila sehemu muhimu, hawana uoga ndiyo maana hata kura walizichakachua bila woga wamezoea hawa.Dawa yao ni kwa wahisani kuweka tight controls ambazo hazitawapa mwanya wa kuchakachua data.
 
...........................Alisema bajeti ambayo serikali iliwasilisha kwa wahisani hao ilibeba "matumaini makubwa ya kuzaa matokeo mazuri na kufanywa kama sababu ya kupitisha matumizi makubwa ya fedha zitokanazo na mapato ya ndani".
Baera alisema kuwa kukosekana kwa uwazi katika matumizi, vipaumbele, mapato na mfumo mzima wa fedha kunapunguza kuaminika kwa bajeti hiyo mbele ya wafadhili............................

Ndio maana Mh Mkullo amemwambia huyo Baera kuwa hilo linazungumzika ofisini..............ili aende akamchakachue......Baera watch out!
 
Wahisani nao hovyo wana biashara zao kubwa tena za faida kwa Nchi zao sasa ujinga na fedheha kama hii ikifanywa na serikali hakika nao unakuwa umewapa mafasi kubwa kukuchezea.Ni aibu mno Membe kusimama au JK na kumwaga sifa za uongozi za CCM hii inapelekea hata sisi watu wenye heshima zetu kuzidi kudharaulika mbele ya wazungu.Kama serikali inachakachua unategemea nini toka kwa raia wake?Lakini pia sishangai sana maana baraza la mawaziri wako wenye vyeti vilee na JK wala hashangai ili mradi ni mwanamtandao na mwana CCM basi kazini tu
 
Wahisani wanatushangaza pale wanapogundua dubious za serikali halafu utasikia wamewapa muda wa kurekebisha mimi sielewi wahisani wanakuwa na lengo gani haswa.Ni bora wakaondoa fungu lao tubaki na kidogo chetu ili tupate muda wa kukatana mapanga na hawa kina RA

Wakiondoa fungu lao tutaweza kulipa Dowans? Au unataka nchi ipigwe mnada, usishangae mikoa ya Arusha, Mara na Kilimanjaro zikaangukia Kenya kama nchi itafilisiwa.
 
KUNDI la wahisani wanaochangia bajeti kuu ya Tanzania (GBS) limeibua kashfa baada ya kueleza kuwa serikali iliwapelekea bajeti tofauti na ile iliyopitishwa na Bunge Julai mwaka huu.Taarifa za kashfa hiyo ziliwekwa hadharani jana asubuhi na mwenyekiti wa wahisani hao, Svein Baera wa Sweden katika mkutano wa kitaifa wa mwaka wa majadiliano ya kisera na bajeti uliofanyika jijini Dar es salaam.
Source: Mwananchi - Tuesday, 07 December 2010

Waungwana hii imekaaje????

Na hata inayopitishwa bungeni si sawa na matumizi na mapato halisi.
 
Wanawapa mda wa kujirekebisha maana hapo na wao wamepata opportunity ya kutukaba zaidi,hivyo katika kipindi hiki cha kujirekebisha wanawaletea wataalamu wa kutengeneza bajeti nzuri au wataalamu wa kufuatilia kama kuna uwiano.Hawa jamaa ni wajanja na watatumia mwanya huo vizuri kuikandamiza serikali.Ni kama umemfumania mtu,siku ukitaka na wewe unamwingilia kwa gia kuwa usiponipa nitakusemea,naye kwa unyonge hata kama hataki atakubali ili yaishe.
Ahaaaaa kumbe.... Ten percent here, there...magumashi kila kona.
 
Mkuu sidhani kama anaweza kumchakachua huyo Mswidi..huo usanii wanauweza na wamefanikiwa sana dhidi yetu wadanganyika tuu!!
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom