Wahindi wanasoma na kuiba nyota ya watu

SWALI : Mtaalamu, kwa heshima na taadhima ninaomba unisaidie suala langu. Mimi ni mwanamke mkaazi wa manispaa ya Nyamagana, jijini Mwanza, umri wangu ni miaka 37, mume wangu ana miaka 45 sasa. Tangu tumefunga ndoa, huu ni mwaka wa kumi na tano. Mimi nina jishughulisha na biashara ya ufundi cherehani. Mume wangu amesoma hadi Chuo Kikuu, amesomea mambo ya kompyuta.



Tangu mwaka 2000 mume wangu amekuwa akifanya kazi kwenye Internet Café ya Muhindi . Hela anayo lipwa kidogo sana, na kutokana na uchapaji kazi wake, kampuni nyingi zimekuwa zikimfuata zikitaka kumuajiri tena kwa kulipa hela nyingi zaidi ya zile anazo lipwa kwa huyo tajiri muhindi.

Unyayo


Lakini cha kushangaza mume wangu amekuwa akiwakatalia. Maisha tunayo ishi hayaridhishi hata kidogo, tunazidiwa mpaka na vijana wadogo walio anza maisha juzi tu. Nikimwambia mume wangu, atafute sehemu yenye maslahi, anakataa. Nikiwambia tutunze hela, afungue nay eye internet café yake, anakataa pia, yeye amekazana na kumtumikia huyo muhindi.


Siku moja nikiwa naongea na shoga yangu mmoja, akaniambia inawezekana mume wangu atakuwa amefanywa msukule wa ofisini na huyo bosi wake muhindi. Eti mtaalamu, hivi ni kweli, jambo hilo linawezekana kwamba kweli mume wangu amefanywa msukule wa kazi na bosi wake ? kama ni kweli ninamtoaje kwenye huo utumwa ?


JIBU.

Pole sana dada angu kwa madhila yaliyo mkuta mume wako. Ni kweli kabisa, wapo misukule wa ofisini. Uchawi huu, hufanywa na wamiliki wa kampuni na biashara mbalimbali. Walengwa wakuu wa uchawi huu ni kwanza wafanyakazi wachapakazi walio na weledi wa kazi husika, na pili wafanyakazi ambao nyota zao zinaendana na biashara husika.


Wapo misukule wa aina mbili. Misukule wanao onekana kwa macho ya nyama, na misukule wasio onekana.



Misukule wasio onekana ni watu wanao dhaniwa kufa, lakini kiukweli wanakuwa hawajafa, isipokuwa wanakuwa wamechukuliwa kichawi.



Ilihali misukule wanao onekana, ni watu wanaoishi kama watu wengine, lakini nyota zao zinakuwa zimechukuliwa na wachawi kwa matumizi yao binafsi (wachawi ) na pia nafsi.




Misukule wa maofisini wapo katika kundi la misukule wanao onekana . Watu hawa hupumbazwa kufungwa kichawi na kufanywa watumishi wa walio wapumbaza, kwa kadri walivyo nuiziwa. Wapo walio nuiziwa kuwatumikia mabosi wao kwa miaka kumi, wengine ishirini, wengine thelathini na w engine katika maisha yao yote.



Msukule huyu anaweza kuwa bar maid, meneja wa bar, House Girl, House Boy, Mkata majani, mkurugenzi wa kampuni kubwa, Mwalimu, daktari,mwanasheria, fundi wa magari, Mtayarishaji wa muziki, muuza mayai, au Ice Cream nakadhalika.


JINSI MISUKULE WA MAOFISINI WANAVYO TENGENEZWA.

Ili kumtengeneza mtu na kumfanya awe msukule wa ofisi mambo yafuatayo hufanyika.



Kwanza zinachukuliwa nyayo zake, kisha zinafungwa kwenye kitambaa cheusi pamoja mchanganyiko wa miti ya kichawi ya aina arobaini na dua maalumu ya kumfunga muhusika.


Pili linachimbwa shimo lenye urefu wa futi saba, ndani ya shimo hilo inafanyika kafara ya PUNDA MWENYE ALAMA YA MSALABA MGONGONI na kondoo mwenye rangi nyeusi bila doa lolote, halafu nyayo za mtu huyo zilizo fungwa kwenye kitambaa cheusi zikiwa pamoja na miti arobaini ya kichawi na dua yake, vinatupiwa kwenye shimo hilo huku maneno Fulani ya kichawi yakitamkwa.


Baada ya hapo litachukuliwa jiwe lenye uzito unao endana na idadi ya miaka ambayo mchawi anataka kumtumikisha muhusika.


Kama anamtaka kwa mwaka mmoja, basi jiwe huwa na uzito wa kilo moja, kama ni miaka kumi basi jiwe huwa na uzito wa kilo kumi, kama ni miaka thelathini, basi mawe yawe na uzito wa kilo thelathini, na kama anataka kumtumikisha maisha basi ataweka mawe yenye uzito wa kilo hamsini hadi miaka. Mawe hayo hukandamiza hicho kitambaa.


Baada ya hapo shimo hilo litafukiwa kwa udongo wa makaburini. Mambo haya yakisha fanyika, utachukuliwa mchanga wa kwenye kivuli cha muhusika, utachanganywa na dawa nyingine za kichawi ambazo idadi yake ni tisa, vitu vitafungwa kwenye kitambaa cheusi, na kuhifadhiwa kwenye kibuyu au chungu cheusi chenye dawa za kichawi kwa siku saba, baada ya hapo atachukuliwa kuku mweusi ambaye ataunguzwa kwenye chungu cheusi akiwa mzima hadi awe majivu.


Majivu hayo, yatagawanywa mara mbili, kisha fungu la kwanza atalishwa PUNDA MWENYE ALAMA YA MSALABA MGONGONI na kisha atazikwa akiwa mzima mzima, na fungu la pili atalishwa kondoo mweusi na kuzikwa akiwa mzima mzima.


Baada ya hapo litafanyika tambiko jingine la kafara ya PUNDA MWENYE ALAMA YA MSALABA MGONGONI na kondoo mweusi.


Kabla ya kuchinjwa kondoo pamoja na punda hao watalishwa dawa fulani za kichawi, na baada ya kuchinjwa nyama ya punda na kondoo watakao tolewa kafara, itatumika kumlisha mtu au watu walio kusudiwa. Mara nyingi huwa kwenye sherehe, hafla, au anaweza kukuita nyumbani kwake, kisha nyama husika ikawa kitoweo chako.



MTU AKIFANYIWA ULOZI HUU, HUWA MTUMISHI MTIIFU KATIKA MAISHA YAKE YOTE. AINA HII YA ULOZI HUTUMIKA PIA KATIKA MAPENZI.


Jinsi Ya Kujikinga Na Ulozi Huu:

Ili kujikinga na ulozi huu, mhusika afanyiwe tambiko maalumu la kumkinga dhidi ya uchawi na ulozi wa aina yote ile. Na kama tayari mtu ameshafanyiwa ulozi huu, basi lifanyike tambiko maalumu la kurudisha nyota yake na kumfungua kutoka kwenye kifungo hicho.



Katika tambiko hilo, ni lazima sehemu iliyo tumika kuzika unyayo wa muhusika, igunduliwe na kisha tambiko maalumu likafanyike katika eneo hilo.
itabidi ulipie tangazo lako la biashara.mtu kamaliza chuo kang'ang'ania kazi ya internet cafe?halrogwa huyo ana ugonjwa wa akili
 
Hii inawahusu sana wanaoamini katika nyota, kwani ni zile nyota za angani au zipi hzi
 
Hizi habari zipo sana na uhalisia wake ni zaidi ya asilimia 70. Ninafahamu mengi na madam kwakuwa umeligusia ninaweza kuleta full version.... wengi wa watumishi wa muda mrefu kwa wahindi hawana vivuli hata u search kwa darubini kali ya Afande Sele

mshana jr lidadavue hili swala maana kuna ndugu yangu limemsibu
 
Hizi habari zipo sana na uhalisia wake ni zaidi ya asilimia 70. Ninafahamu mengi na madam kwakuwa umeligusia ninaweza kuleta full version.... wengi wa watumishi wa muda mrefu kwa wahindi hawana vivuli hata u search kwa darubini kali ya Afande Sele

Mchana hapo kwenye kivuli umeniacha, kinaenda wapi?
 
Haya mambo ya kurogana na nyota yapo sana. Na ukishawishika kuyaweka akilini yanatesa sana
 
Da Kwa Iman hizi za kiafrika tutazid kuwasindikiza wenzetu na maendeleo kuyasikia bombani Kwa nadharia hizo za kusadikika
 
Haya mambo kiukweli yapo kabisa.... Ila sikuhizi waganga wa kuagua mambo mazito ya kinyota kama haya ni wachache sana na kuwapata ni ngumu. Hata hivyo walio wengi ni waongo na matapeli.
 
Muongeacho ,nikweli ila kwa anayebisha abishe tu sababu yeye ajui ya rohoni anajua tu ya mwilini na hamtaweza kuelewa,but wewe unasema kivuli wapo waliovalishwa miili yao vijakazi vya majini na nafsi zao zinapiga kazi usiku na mchana na mshahara ni mdogoo na mtuu ukimwangalia hata ile kutamani kuacha kazi hawazi ,but inatubidi sasa tufanye opertion chomoa mtu ndani ya mtu"
 
Hizi habari zipo sana na uhalisia wake ni zaidi ya asilimia 70. Ninafahamu mengi na madam kwakuwa umeligusia ninaweza kuleta full version.... wengi wa watumishi wa muda mrefu kwa wahindi hawana vivuli hata u search kwa darubini kali ya Afande Sele
Nasubiria kwa hamu mshana jr
 
Hii ndo hali halisi,na sio wahindi tu,kuna wasomali ht wabongo .....
Kko ndo balaa watu wana maduka wanauza kwa kutumia nyota za watu....

Njoo kwenye maofisi humu mbapo tuna omba kazi,unatuma cv ,watu wakiisoma tu wanajua wanafanya yao,unashangaa hupati kazi kabisa,au ukipata za kipato ambacho kwakweli sio hadhi yako!

Nina mifano kibao!

Yaani in short usipokua kiroho ndo basi
Wao wapo kiroho kwa upande wa giza!
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom