Wahindi Wamtukana Yesu | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wahindi Wamtukana Yesu

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Bujibuji, Feb 20, 2010.

 1. Bujibuji

  Bujibuji JF-Expert Member

  #1
  Feb 20, 2010
  Joined: Feb 4, 2009
  Messages: 40,252
  Likes Received: 33,569
  Trophy Points: 280
  Kampuni moja ya kupiga chapa vitabu vya kutumika mashuleni imetoa picha ya Yesu akiwa anavuta sigara na kunywa bia ya kopo.
  [​IMG]

  sorce: BBC
   
 2. Sumbalawinyo

  Sumbalawinyo JF-Expert Member

  #2
  Feb 20, 2010
  Joined: Sep 22, 2009
  Messages: 1,286
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 0
  Da, kweli dunia imeisha.
   
 3. Kikojozi

  Kikojozi JF-Expert Member

  #3
  Feb 20, 2010
  Joined: Mar 24, 2009
  Messages: 331
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Ndo yaleyale ya picha za Mtume Muhammad. Uchokozi tu wa kijinga.
   
 4. Gamaha

  Gamaha JF-Expert Member

  #4
  Feb 20, 2010
  Joined: Jul 17, 2008
  Messages: 2,729
  Likes Received: 874
  Trophy Points: 280
  Kwani ni lini Bwana Yesu aliwahi kupigwa picha, huo ni mfano tu wa sura ya yesu wazungu waliutengeneza, halafu kama kinywaji yesu si alikuwa anakunywa lejea harusini kule kana , lejea maneno yake ya kuwa yeye wanamwita mlevi na mlafi kwa kuwa anajichanganya si kama yohana, lejea siku ya kuagana na wanafuzi wake alipowaambia kunyweni hii kama dam yangu ina yeye si alipiga pafu ya divai, labda sigara tu lkn hata hiyo si kwa yesu ni kwa picha ya mfano wa Yesu so sioni haja ya kugombana hapo
   
 5. Sumbalawinyo

  Sumbalawinyo JF-Expert Member

  #5
  Feb 20, 2010
  Joined: Sep 22, 2009
  Messages: 1,286
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 0
  Tutayasikia mengi leo.
   
 6. RayB

  RayB JF-Expert Member

  #6
  Feb 20, 2010
  Joined: Nov 27, 2009
  Messages: 2,755
  Likes Received: 89
  Trophy Points: 145
  Habari ni ya lini hii ni ya leo? Yaani hizo zote zinatokea leo? Au mtu anaenda kwenye google na kusearch "insults on Jesus" ili maradi uzilete hapa? Please lets bring things which are more productive lads!
   
 7. Kiranja Mkuu

  Kiranja Mkuu JF-Expert Member

  #7
  Feb 20, 2010
  Joined: Feb 18, 2010
  Messages: 2,100
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 0
  Tunahaki ya kupata habari,
  hii mi niliona kule nifahamishe, nikaipuuzia
  sikuisoma na wala sikuona umuhimu wa kuileta hapa.
  Nilipoiona kwa mara nyingine hapa ndio imenibidi nisome mtiriko mzima.
  Kweli hizi ni siku za mwisho.
  Watu hawana hofu ya Mungu hata kidogo.
   
 8. Chimunguru

  Chimunguru JF-Expert Member

  #8
  Feb 20, 2010
  Joined: May 3, 2009
  Messages: 9,893
  Likes Received: 322
  Trophy Points: 180
  Mfalme wa amani mpeni heshima, bethlehemu mjini anaingia.bwana yesu njoo kwetu, njoo kwetu karibu ukae nasi
   
 9. B

  Bull JF-Expert Member

  #9
  Feb 20, 2010
  Joined: Nov 4, 2008
  Messages: 984
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Una hakika gani kama hii ndio picha ya YESU?
   
 10. Kiranga

  Kiranga JF-Expert Member

  #10
  Feb 20, 2010
  Joined: Jan 29, 2009
  Messages: 36,095
  Likes Received: 7,673
  Trophy Points: 280
  Hata kama picha ni ya Yesu, kuhusu kunywa Yesu mwenyewe imeandikwa kwamba ndiye aliyebadili maji kuwa mvinyo. Kwa hiyo Yesu mwenyewe alifagilia kunywa.

  Kuhusu kuvuta wakati unaodaiwa kuwa wake hata sigara kulikuwa hakuna, na wala hakuwahi kukataza kuvuta sigara. Isitoshe katika culture zetu nyingine kuvuta ni alama ya hekima na wazee na ma priest walikuwa hawakutani bila kuvuta.

  Kwa hiyo tatizo liko wapi?

  Kwanza Yesu mwenyewe alikuwa more gangster than that, angekuwa anaishi leo watu wa PETA wangemuandama kichizi for his unethical treatment of animals, nyie mnashangaa kuvuta?

  Acheni kuwa brainwashed na wazungu.
   
 11. Regia Mtema

  Regia Mtema R I P

  #11
  Feb 20, 2010
  Joined: Nov 21, 2009
  Messages: 2,974
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 0
  Wanafikiri YESU anatukanika?huwezi kumtukana MUNGU hata siku moja,wanajidanganya bure..Poor them!
   
 12. Mpaka Kieleweke

  Mpaka Kieleweke JF-Expert Member

  #12
  Feb 20, 2010
  Joined: Feb 27, 2007
  Messages: 4,136
  Likes Received: 71
  Trophy Points: 145
  Nani kasema waliotengeneza hiyo picha ni wahindi?
   
 13. Waberoya

  Waberoya Platinum Member

  #13
  Feb 20, 2010
  Joined: Aug 3, 2008
  Messages: 12,001
  Likes Received: 4,409
  Trophy Points: 280
  Lakini jamani, nani kasema hiyo picha ni YESU??
  Halafu sio wanawa mock wakristo wengi walio walevi na wavuta sigara??

  siwezi kabisa kukasirika kuina hii picha, nifasihi naona anawasema wakristo wanaoyafanya hayo ili hali wakijiita wafuasi wa Yesu!!!!

  Yesu hana double standard, mlianza na masanamu yanaaanza kuwarudia , mkicheza na neno moja la Mungu unaharibu kila kitu
   
 14. Bujibuji

  Bujibuji JF-Expert Member

  #14
  Feb 22, 2010
  Joined: Feb 4, 2009
  Messages: 40,252
  Likes Received: 33,569
  Trophy Points: 280

  Kwanza matusi aliyotukanwa alipokuwa akisulubiwa ni m akubwa kuliko hayo ya wahindi wasio na nidhamu na hofu ya Mungu.
  Wataabudu ng'ombe mpaka wakome.
   
 15. Utingo

  Utingo JF-Expert Member

  #15
  Feb 22, 2010
  Joined: Dec 15, 2009
  Messages: 7,179
  Likes Received: 248
  Trophy Points: 160
  Wamewabeza wakatolic, ndiyo wanaoendekeza mapicha na masanamu. Nani aliwahi kumpiga picha Yesu?
   
 16. G

  Gianna Member

  #16
  Feb 22, 2010
  Joined: Feb 17, 2010
  Messages: 5
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Naomba ufafanue hiyo treatment alokuwa akiwafanyia wanyama, maana huyu ni nabii alietukuka ambae hata waislam wanamuamini na wanampa heshima zote kama nabii Issa, na kwanini tuwe brain washed na wazungu?? Yesu hakutokea US, UK au Vetican katokea MIDDLE EAST na tafadhali kila mtu anachagua own path, kwa hiyo chunga ulimi wako juu ya imani za watu wengine. by the way you know nothing.
   
 17. Lekanjobe Kubinika

  Lekanjobe Kubinika JF-Expert Member

  #17
  Feb 22, 2010
  Joined: Dec 6, 2006
  Messages: 3,067
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  Unajua eeh! Kilicho kikubwa hapo ni kuwapuuza. Lakini kama wamechapa vitabu vya mashuleni ni kuwapuza vizuri zaidi, kwa sababu wanataka wanafunzi wanaosoma mvitabu hivyo waone kwamba makampuni hayo hayastahili kuishi. Lakini mjinga ni mstaarabu sana - ukimwelimisha hugundua kosa lake na kubadilika kwa kuomba radhi kama mwenye makampuni ya Toyota aliyekosea break za magari yake akakubali gharama kuyarudisha magari yote kiwandani kwa pesa yake! Mpumbavu ni hopeless kuliko msukule, maana anajua kabisa kwamba yeye hamnazo, lakini atakomalia kuinywa hatari mpaka pumzi yake ya mwisho. Bora Msukule anaweza kuombewa Ubungo na akarudi tena kuanza maisha upya.

  Si muda mrefu makampuni hayo yatafilisika yasipojirudi, maana kipofu mbishi aendaye hatarini utamsaidiaje ila kumwambia kisha kumwacha aende zake afe ili wenzake wapate somo lililo bora zaidi? Ukibishana na mwehu bila shaka wehu wako unakaribiana na mwehu mwenzio. Hivi ukioga mtoni na mwehu akachukua nguo zako nchi kavu na kukimbia nazo, ukitibuka mtoni na kumkimbiza ukiwa uchi ukimdai mwehu nguo zako, watu watajua ni yupi aliye mwehu zaidi?

  Tuwaache wahindi hao maana ndicho kipindi cha wapinga Kristo kinavyoingia duniani. Mungu sio kama masanamu ya Budha yasiyopumua wala kukimbia wakati majengo yalimowekwa yakiungua moto, Yesu mwenyewe anajua kujitetea. Tusichukuwe mapanga, silaha kuu ni kuwapuza na kumuuliza Yesu mwenyewe awaonyeshe wabaya wake alivyo tofauti na wao, wataokoka kama Paulo alivyokutana na wokovu wa Mungu. Umewahi kusikia wezi wa Biblia jinsi wanavyopata taabu mpaka wanapookoka? Weacha tu, tumwache Mungu aitwe peke yake Mungu Jehova Yire Sharma!
   
 18. mayenga

  mayenga JF-Expert Member

  #18
  Feb 22, 2010
  Joined: Sep 6, 2009
  Messages: 3,822
  Likes Received: 614
  Trophy Points: 280
  Lumbe be tolerant,huwezi kujustify kuwa ur denomination is more accurate than others.Hata hivyo it suffices to say MUNGU AWASAMEHE HAO na AKUSAMEHE PIA NA WEWE!!!!!!!!!!!!
   
 19. kisasangwe

  kisasangwe JF-Expert Member

  #19
  Feb 22, 2010
  Joined: Feb 16, 2010
  Messages: 294
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 33
  hebu atokee mtu aigize picha ya mojawapo ya miungu ya wahindu iwe inakula nyama ya ngombe uone kama hawata tembea kwa mguu kuvuka bahari kumtafuta mbaya wao.

  kejeli kwa Yesu hazikuanza leo,hapa ni mwanzo tu wa harakati za mpinga kristo. ila kwa vile yalishatabiriwa haina haja ya kureact,na kuendeleza malumbano, kila mtu atatoa hesabu ya matendo yake.baba hatamsemea mwanae wala mwana hatamsemea mamae. kiongozi atajibu kivyake na sio kwa taifa lake. mwenye kuharibu na aendelee kuharibu,mwanye kutukana na aendelee,mzinzi azidi, ila yeye ajae aja upesi kumlipa kila mtu ujira wake,
   
 20. kisasangwe

  kisasangwe JF-Expert Member

  #20
  Feb 22, 2010
  Joined: Feb 16, 2010
  Messages: 294
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 33
  vita vyetu wakristo si juu ya nyama na damu bali mi vita vya kiroho.liko jeshi kubwa sana la ibilisi ambalo ukisema upigane nalo kwa bunduki,majambia nyuklia na vitu kama hivo huwezi, ila kwa roho mtakatifu yule tuliepewa kuwa msaidizi.

  shetani mwenyewe anajua kua hawezi kamwe kumshinda mungu na anachofanya ni kuwahimiza wanadamu kuamini kua yeye ni zaidi ya mungu ili pia apate wafuasi wengi kwenda nao jehanam. mojawapo ya njia atumiazo ndo hizi za kejeli na kutaka watu watende dhambi na kukwazana.
   
 1. This site uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
  By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.
  Dismiss Notice
Loading...