Wahindi waajiriwe serikalini na wapewe uwaziri | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wahindi waajiriwe serikalini na wapewe uwaziri

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by RICHEST, Jul 14, 2011.

 1. RICHEST

  RICHEST Member

  #1
  Jul 14, 2011
  Joined: Jun 23, 2011
  Messages: 25
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Nilikuwa naangalia documentary TBC siku moja wakionyesha harakati za uhuru wa Tanganyika wahindi na masingasinga walikuwa msitari wa mbele hata walikuwa wakijitokeza kwa wingi mikutano ya nyerere na kwenye sherehe za kitaifa kwenye viwanja. Na wengi waliajiriwa serikalini, majeshini na mashirika ya umma na wengine kupewa ubunge na kuwa mawaziri na wakuu mbalimbali. Kuna wasomi wahindi kama akina Professor Shivji na wengine wengi waliajiriwa vyuo vikuu na waliisaidia sana nchi katika nafasi zao.

  Hivi ni kwa nini wahindi hawaajiriwi serikalini wakati sifa wanazo tena kali kuliko za watanzania weusi wakati ni raia wa nchi hii. Hivi Tanzania ni nchi ya weusi tu au nchi ya raia wote wenye uraia halali wa kuzaliwa Tanzania wakiwemo wahindi,wazungu,waarabu na watu weusi. Wahindi wengi toka Afariki nyerere hawapewi nafasi tena serikalini za ajira wala kupewa madaraka yawe ya ukuu wa wilaya,mikoa wala uwaziri.

  Hata sherehe za Kitaifa huwaoni tena viwanjani.Zamani walikuwa wakiingia na kucheza hadi ngoma za kihindi sherehe za kitaifa. Sasa hivi hakuna sherehe za kitaifa zimesuswa na wahindi baada ya kususwa na serikali kwa kuwabagua kwenye ajira. Serikali ya Afrika kusini iliacha ubaguzi wa rangi na wamewaajiri kibao. Sisi ndio kwanza tunawaacha kuwaajiri. Hivi kuna ubaguzi wa rangi kwenye ajira serikalini?

  Naomba tunaposherehekea miaka hamsini ya uhuru tukumbuke wahindi nao katika ajira za serikali na vyeo vya kiserikali ikiwemo uwaziri.

  Naomba kutoa hoja.
   
 2. Nduka

  Nduka JF-Expert Member

  #2
  Jul 14, 2011
  Joined: Dec 3, 2008
  Messages: 8,479
  Likes Received: 761
  Trophy Points: 280
  Mkuu niletee CV za wahindi 14, kuna nafasi za waandika Hansard bungeni nizipeleke utumishi tuwaajiri kama ulivyoagiza.
   
 3. MVUMBUZI

  MVUMBUZI JF-Expert Member

  #3
  Jul 14, 2011
  Joined: Jan 8, 2011
  Messages: 4,970
  Likes Received: 666
  Trophy Points: 280

  Tatizo hapo kwenye RED umeonyesha wewe ni mbaguzi na ni kama TUSI kwamba wahindi ni more educated na deserving kuliko Wazawa. Neno WaTZ weusi limeniudhi sana kwani ni bora ungesema waTZ WAZAWA

  Tatizo wahindi hawatapokea mshahara wa shilingi 100,0000 kwani wao wanataka kuuza maduka. halafu wasichana wa kihindi siyo rahisi kukubalika kuajiriwa kwani mila na desturi za kihindi haziwaruhusu kuwa exposed. Tatizo la kuto ajiriwa wahindi siyo la kibaguzi bali mila na desturi zao haziwapi nafasi hiyo.
   
 4. DSN

  DSN JF-Expert Member

  #4
  Jul 14, 2011
  Joined: Feb 2, 2011
  Messages: 2,745
  Likes Received: 76
  Trophy Points: 145
  Waambie kwanza watoke uhindini, kariakoo na kitumbini,kisha wakubali mabinti zao waolewe na wabongo wazawa [kwa rangi ]
   
 5. kyemo

  kyemo Senior Member

  #5
  Jul 14, 2011
  Joined: Dec 10, 2010
  Messages: 196
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  we utakuwa sio mzima
   
 6. Bongolander

  Bongolander JF-Expert Member

  #6
  Jul 14, 2011
  Joined: Jul 10, 2007
  Messages: 4,882
  Likes Received: 47
  Trophy Points: 135

  Sifa ya kwanza ya kuwa mtanzania ni uzalendo kwa Tanzania. Lakini bahati mbaya haina kipimo. Angalia Rostam Aziz ni mtanzania wa kuzaliwa angalia aliyotufanya, wahindi ni even worse (sio wote). Angalia waliyofanya mpaka sasa. Angalia wazungu wamekaa kwa miaka mingapi Tanzania na walichofanya, angalia wahindi. NI wezi na wabaguzi wa kutupa, angalia wamekaa Tanzania kwa miaka mingapi na wameshindwa ku-integrate na ku-adapt wanata sisi tu-adapt kwao. Ni heri tuibiwe na mmakua mwenzetu ambaye atawekeza hapa Tanzania kuliko kuibiwa na mtu anayepeleka hela Uingereza, Canada au India.
   
 7. CAMARADERIE

  CAMARADERIE JF-Expert Member

  #7
  Jul 14, 2011
  Joined: Mar 3, 2011
  Messages: 4,427
  Likes Received: 158
  Trophy Points: 160
  Muhindi hawezi kukubali kuwa na bosi Mswahili
   
 8. Anko Sam

  Anko Sam JF-Expert Member

  #8
  Jul 14, 2011
  Joined: Jun 30, 2010
  Messages: 3,216
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  Kama huwajui ama huji desturi za kihindi bora usiandike upupu humu. Wahindi mila zao haziwakatazi kujichanganya na wabongo kwani shule za zamani tulikuwa tunasoma nao kwenye shule hizihizi za serikali. Na wabongo walikuwa wanawachukua mademu wa kihindi na hakuna aliyeshangaa. Hawakulazimishwa kujifunika mahijarb kama waislamu.

  Wahindi utamaduni wa kutubagua umeanza hivi miaka ya '90 tu baada ya kuona viongozi wa serikali na chama tawala havina muelekeo wa maendeleo bali kuendekeza wizi, rushwa na ufisadi.
   
 9. T

  Tata JF-Expert Member

  #9
  Jul 14, 2011
  Joined: Dec 3, 2009
  Messages: 4,731
  Likes Received: 647
  Trophy Points: 280
  Sidhani kama Serikali yetu ina sera ya kuajiri watu kwa misingi ya rangi, kabila au dini. Lakini pia huwezi kuajiri "wahindi" serikalini kwani wana nchi yao huko India na kama sijakosea sheria imeweka mipaka ya idadi ya wageni wanaoruhusiwa kufanya kazi Tanzania. Labda kama kwa kusema wahindi unamaanisha watanzania wenye asili ya asia. Kama ni hivyo naomba urekebishe kichwa cha habari kwani utakuwa unaendeleza ubaguzi kwa misingi ya mtu alipotoka.

  Suala la mtu atafanya wapi kazi ni suala binafsi na kama watanzania wenye asili ya asia wanapenda zaidi kufanya biashara huwezi kuwalazimisha. Mimi mfano sishangai kutowaona hawa wenzetu wakifanya kazi JWTZ, Magereza au Polisi kwani hawana interest za kufanya kazi huko.
   
 10. K

  Kamundu JF-Expert Member

  #10
  Jul 14, 2011
  Joined: Nov 22, 2006
  Messages: 2,109
  Likes Received: 455
  Trophy Points: 180
  Kama watajiingiza kwenye siasa hili sio swala la Mhindi au Mwarabu bali ni swala la kujihusisha na wafanyabiashara wengi hawapendi siasa.
   
 11. Ndachuwa

  Ndachuwa JF-Expert Member

  #11
  Jul 14, 2011
  Joined: Mar 8, 2006
  Messages: 4,530
  Likes Received: 725
  Trophy Points: 280
  Wahindi hawako interested kwenye kazi za mishahara midogo kama Serikalini.
   
 12. Lunyungu

  Lunyungu JF-Expert Member

  #12
  Jul 14, 2011
  Joined: Aug 7, 2006
  Messages: 8,836
  Likes Received: 75
  Trophy Points: 145
  Unaongelea wahindi ? Utata huu am out kwa kweli.
   
 13. TODO

  TODO JF-Expert Member

  #13
  Jul 14, 2011
  Joined: Jul 14, 2011
  Messages: 219
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  nimeipenda hii, wakubali kwanza kujumuika na wazawa ndo wapate nafasi ya kuajiliwa vinginevo wakiajiliwa na serikali watakuwa wanajihudumia wenyewe tu (wenye asili ya kihindi)
   
 14. r

  rakeyescarl JF-Expert Member

  #14
  Jul 14, 2011
  Joined: Dec 9, 2007
  Messages: 408
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 35
  Nakushauri uende India siku moja au kuangalia documentary yoyote ya India utapata majibu.
  Kubwa kuliko lote waingie serikali ili?Kwani hawa wanaotutesa na hawajapata direct line wametufikisha hapa, bado hujatosheka tu?Wewe kama ni Mhindi Mtz jivue gamba kwanza. Hivi una habari wahindi wote wakija TZ jambo la kwanza huwa ni kununua Pasi ya Tanzania ili waweze kuwa mguu 1 ndani mmoja nje?Na ukitaka kuyajua zaidi nenda DSM ujue kuwa mpaka leo kuna un official/official Indian streets,mosque,restaurants,hotels,offices, schools kutoka kindergaten mpaka High schools.
  Wewe kama sio mhindi Mtz basi una pepo-simaanishi kwa ubaya!Tuko wote ndg yangu wacha tupambane na hawa kwanza wanoyumbisha mpaka uchumi wetu.
  Na wewe nenda India ukatoe hoja kama hii ndio utajua uhusiano wetu na wao ukoje.
   
 15. MANAMBA

  MANAMBA Senior Member

  #15
  Jul 14, 2011
  Joined: Jan 16, 2011
  Messages: 169
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Kuna Mswahili yeyote au hata mzungu aliyeajiriwa katika serikali ya india? Manufaa wanayopata ya kufanya biashara kwa uhuru na kukwepa kodi hayatoshi? Kwa taarifa yako kule india mswahili hawezi kupata hata kibarua cha kuosha maiti na ikitokea hivyo wahindi wataandamana kupinga.
   
 16. A

  Anold JF-Expert Member

  #16
  Jul 15, 2011
  Joined: Jul 15, 2010
  Messages: 1,380
  Likes Received: 300
  Trophy Points: 180
  Kwa siasa hizi uchwara afadhali hao wahindi waendelee kuanzisha viwanda vyao ili watuajiri sisi watu weusi tuliojaa unafiki na hila: Ni hakika kuwa kama tungekuwa na mchanganyiko tungeshapiga hatua ila kwa ubaguzi wetu na unafiki wetu hakuna sababu kwa hawa jamaa kujitakia matatizo
   
 17. Barubaru

  Barubaru JF-Expert Member

  #17
  Jul 15, 2011
  Joined: Apr 6, 2009
  Messages: 7,162
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 0
  Alafu mnasema Serikali ya Tanzania sio wabaguzi.

  Haya sie yetu macho.
   
 18. 3D.

  3D. JF-Expert Member

  #18
  Jul 15, 2011
  Joined: Sep 7, 2010
  Messages: 1,022
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Naunga mkono hoja.
   
Loading...