Wahindi tena! Polisi na raia wetu nao waige? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wahindi tena! Polisi na raia wetu nao waige?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Zhule, Mar 15, 2010.

Thread Status:
Not open for further replies.
 1. Z

  Zhule JF-Expert Member

  #1
  Mar 15, 2010
  Joined: May 22, 2008
  Messages: 354
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  [FONT=&#23435][/FONT]
  [FONT=&#23435]T[/FONT][FONT=&#23435]ANZANIA[/FONT][FONT=&#23435] STUDENTS ASSOCIATION BANGALORE
  (TASABA)

  WANAFUNZI WA KITANZANIA NUSURA [/FONT]
  [FONT=&#23435][/FONT]​
  [FONT=&#23435]KUUWAWA KWA MOTO BANGALORE - INDIA

  Tarehe 11/03/2010 majira ya saa 11:30 wanafunzi wawili ,Hamis Mbelwa Fintan mwenye na Olais Alexendra Siarra waliokuwa wanakaa No.1093/1.11th Cross,Swarnanagar,Robertsonpet,KGF-563 122. Walinusurika kuuwawa kwa moto baada ya fujo iliyofanywa na wahindi wakidai kuwachukia waAfrika. [/FONT]
  [FONT=&#23435][/FONT]​
  [FONT=&#23435]Wahindi hao waliamua kuchukua mafuta ya petrol na kumwaga dirishani na mlangoni, walifanikiwa kuwasha moto kupitia malangoni na moto kuanza kuingia ndani wakati vijana hao wakiwa ndani. Kwa bahati nzuri walifanikiwa kuuzima moto uliokuwa unaingia ndani na ule wa nje wasamalia wema waliuzima, bahati nzuri petrol ilikuwa chache hivyo hakuna madhara makubwa yaliyotokea.

  Nilipopata taarifa hii nilitoka na kufika kituo cha Police cha Hennur Cross, nilitoa taarifa hiyo wakatoka maafisa wa police na kufika sehemu ya tukio wakati huo mimi nikiwa nimebaki kituoni. Baada ya dakika 30 police walirudi bila watuhumiwa, nilipouliza walinijibu nirudi nyumbani wameshawatuliza na hawatarudia tena nilibishana sana na police juu ya hilo maana walipofika waliwakuta watuhumiwa na kuwaachia waende huru. [/FONT]
  [FONT=&#23435][/FONT]​
  [FONT=&#23435]Nilizidi kupigania haki lakini walinijibu “This is India not Tanzania and we have to cop with them like it or not” niliwauliza kama huo ndio utamaduni wao wa kumwagia watu petrol na kuchoma moto kutaka kuwaua? Wakasema kama naona hawajanisaidia niende kutafuta msaada mahali pengine. [/FONT][FONT=&#23435][/FONT]​
  [FONT=&#23435]Nilisikitika sana kwa kauli za police hasa ukizingatia kuwa toka kifo cha mwenzetu Imran Mtui ni mwezi tu na siku 7 mpaka sasa na hatujapata taarifa ya kuridhisha kutoka kwa police halafu linatokea jaribio lingine la kuua kwa kutumia petrol.[/FONT][FONT=&#23435][/FONT]​
  [FONT=&#23435]Hali hii inatisha hasa nikiwa kama mwenyekiti wa jumuiya ya wanafunzi kuona raia wenzangu wanatishiwa kutolewa maisha yao kwa moto na bila hatia huku police wakiona jambo hilo ni la kawaida kwao na kuwaachia watuhumiwa waende huru. Watu hawa wanaishi nchini kwetu kwa amani na kufaidi matunda ya uhuru na uchumi wa nchi yetu bila bugudha.


  Baada ya kuona hakuna masaada kutoka police niliwashauri Hamis Mbelwa Fintan na Olais Alexendra Siarra wahame mahali pale kwani hapana usalama tena. Tunaomba sana msaada toka nyumabani na ofisi zetu za ubalozi zilizopo New-Delhi India kutafuta jinsi ya kufanya waTanzania waishio Bangalore –India na kwingine kote kuishi kwa amani, imezoeleka kuwa mara zote wanafunzi ni wakorofi lakini kwa tukio hili nakataa kabisa kama chanzo ni wahanga hawa bali ni chuki binafsi iliyoko dhidi ya wa Afrika ambayo inatufanya tuishi kwa uoga na wasiwasi mkubwa sana. Leo hii petrol ilikuwa chache siku nyingine itakuaje? Je wangefanikiwa kutoa roho za vijana hawa majibu kutoka vyombo vya dola vya India ingekuwa ni nini? Au wangesema wamejiua tena vijana hawa kwa moto? Haya ni maswali machache ya kujiuliza.


  “Mungu ibariki Tanzania, Mungu tubariki wanafunzi wa kiTanzania tuishio Bangalore India ”


  Fidelis Msomekela


  Mwenyekiti – TASABA

  +919742176980 [/FONT]
  [FONT=&#23435][/FONT]​
   
 2. M

  Mdondoaji JF-Expert Member

  #2
  Mar 15, 2010
  Joined: Mar 17, 2009
  Messages: 5,106
  Likes Received: 45
  Trophy Points: 145
  Habari hii inasikitisha na kuhuzunisha hasa ukichukulia hapa tanzania jamii za kihindi zinaishi kwa amani na utulivu but sie tunanyanyaswa nchini mwao. Hofu yangu watanzania wakianza nao kujibu mapigo tanzania hali haitakuwa nzuri nadhani ubalozi wa india uwasiliane na wenzao india kurekebisha hii hali ama sivyo itakuwa hali si nzuri
   
 3. Ndibalema

  Ndibalema JF-Expert Member

  #3
  Mar 15, 2010
  Joined: Apr 26, 2008
  Messages: 10,916
  Likes Received: 131
  Trophy Points: 160
  Hali ya ubaguzi wa wazi wazi ya wahindi kwa wa'Afrika ilianza zamani sana.
  Kinachoniuma mimi hata wahindi waliopo hapa nchini kwetu wanatubagua wazi wazi ingawa tupo kwetu.
  Labda na sisi tuwafanyie unyama pengine watajirekebisha.
  Wanatuona kama sisi sio binadamu.
  I hate them.
   
 4. T

  Tom JF-Expert Member

  #4
  Mar 15, 2010
  Joined: May 14, 2007
  Messages: 472
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Kujibu mapigo! - toka lini mkawa na ubavu wa kuwafanyizia wahindi? Diplomacy ya TANZANIA inasema hivi, "Mtz ukipigwa shavu moja na mhindi ama mchina, basi mgeuzie na la pili".
   
 5. Z

  Zhule JF-Expert Member

  #5
  Mar 15, 2010
  Joined: May 22, 2008
  Messages: 354
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Duh!
   
 6. Juma Contena

  Juma Contena JF-Expert Member

  #6
  Mar 15, 2010
  Joined: May 21, 2009
  Messages: 1,195
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  Duuh poleni i cant imagine maisha yenu ya kila siku yana endeleaje. Lakini si hata vyombo vyetu vya habari vinaweza weka pressure hapa nyumbani kwa ubalozi wa India au ndio Miafrika tena ndivyo ilivyo. habari kama hizi si deal na wala azina umuhimu, mpaka ufisadi hata wa pipi ndio habari za kuongelea.

  Hila hongera kwa jitihada Kaka na kujaribu kufuatilia usalama wa nduguzo huko mungu aendelee kuwalinda na kuwaongezea ulinzi kwa namna zake.
   
 7. Ben Saanane

  Ben Saanane Verified User

  #7
  Mar 15, 2010
  Joined: Jan 18, 2007
  Messages: 14,603
  Likes Received: 3,692
  Trophy Points: 280
  -Nadhani hili suala liko juu ya uwezo wa ubalozi wetu India,sasa nadhani wizara iingilie kati moja kwa moja.Lile tukio la kuuwa yule kijana Imran bado halikupewa uzito wa kutosha na serikali yetu,bado tunarudi kule kule kwamba ukimkabidhi mtu dhamana ya kuongoza misheni na kusimamia maslahi ya watanzania nje ya nchi basi hakikisha kiwango cha uzalendo cha mtu huyo si cha kutilia mashaka

  -Grudges si nzuri sana.Hisia ambazo zinajengeka miongoni mwa wananchi si nzuri sana
   
 8. B

  Boramaisha JF-Expert Member

  #8
  Mar 15, 2010
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 820
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Waziri Membe anasemaje/Wizara yake inachukua hatua gani?
   
 9. Lunyungu

  Lunyungu JF-Expert Member

  #9
  Mar 15, 2010
  Joined: Aug 7, 2006
  Messages: 8,836
  Likes Received: 75
  Trophy Points: 145
  Dawa ni kuacha kwenda kusoma India na sisi hapa TZ tuamke na kujibu mapigo kwa uwezo ule ule .
   
 10. Ben Saanane

  Ben Saanane Verified User

  #10
  Mar 15, 2010
  Joined: Jan 18, 2007
  Messages: 14,603
  Likes Received: 3,692
  Trophy Points: 280

  -Mimi najua huyo balozi wa India Tanzania ana kiburi sana,hata majibu yake baada ya yule kijana Imran kuuawa hayakua majibu mazuri sana katika hali ya kawaida ya kidiplomasia

  -Waandishi wa habari nao wanahitajika sana katika kutia pressure.Wanatakiwa kuitia pressure serikali yetu,pia wapinzani nao sasa nawatilia mashaka.Kurugenzi zao za mambo ya nje hazijatoa ushirikiano wa kutosha katika hili,wamekua kama serikali tu kwa kukaa kimya.

  Mauaji au mateso wanayofanyiwa wahindi huko Australia yanaitia pressure sana serikali ya India ,na hii ni kutokana na active media ya India.Vyombo vya habari vya india kweli vinadhihirisha kwamba vinastahili nafasi yake kama mhimili wa nne wa dola.Maslahi ya nchi na wananchi wake wanayashupalia sana hasa pale ambapo wanapoona wanakandamizwa na nguvu au elements zilizoko nje ya mipaka ya Nchi yao.Media ijaribu kuisukuma serikali coz najua kwa jinsi kiwango cha uzalendo wa viongozi wetu kilivyo chini hawatatoa tamko bila kusukumwa ingawa hata matamko yao ni ya kinafiki coz hayaendani na vitendo
   
 11. Ben Saanane

  Ben Saanane Verified User

  #11
  Mar 15, 2010
  Joined: Jan 18, 2007
  Messages: 14,603
  Likes Received: 3,692
  Trophy Points: 280
  -Lunyungu,hebu tuanze kujiuliza kwanza.Kwa nini vijana/wadogo zetu wanaenda kusoma India?Ni kitu gani wamekosa nchini mwao hadi kwenda kusoma huko?Ni fursa gani wameona huko?Ni hali gani imewafanya kwenda kusoma huko? Sasa nadhani hapo tutaanza kuufikiria huu wito

  Owise tuko pamoja mkuu!
   
 12. K

  Kishazi JF-Expert Member

  #12
  Mar 15, 2010
  Joined: Nov 14, 2007
  Messages: 485
  Likes Received: 77
  Trophy Points: 45
  The government ya URT should wake up and save this mess in India, as inakoelekea ni pabaya kwani wa-Tz hawakawii kuzidi kuwachukia wahindi hasa ukiangalia dharau zinazoendelea nchini mwetu. Na dharau hizi zinaashiria message from wahindi to Tanzanians kuwa "nyie wajinga wa kutupwa, tunawatawala nchini mwenu, and vijana wenu wanalia njaa kule kwetu and tunawanyanyasa as we wish and hamuwezi kutufanya lolote".
   
 13. nzalendo

  nzalendo JF-Expert Member

  #13
  Mar 15, 2010
  Joined: May 26, 2009
  Messages: 7,875
  Likes Received: 2,680
  Trophy Points: 280
  time will tell''watanzania sio mazuzu kama unavyofikiri''---ila yakianza tu sie malawiiiiiii
   
 14. Prodigal Son

  Prodigal Son JF-Expert Member

  #14
  Mar 15, 2010
  Joined: Dec 9, 2009
  Messages: 963
  Likes Received: 60
  Trophy Points: 45
  Huu ni wakati mzuri kwa wazazi kufikiria kabla hawajapeleka watoto huko kwa hao wabaguzi, ni vizuri wakaangalia nchi kama FINLAND elimu ni bure kabisa mwanafunzi anajigaramia accomodation na chakula chake, ni kwli India wamebobea kwenye masomo ya biashara lakini Serekali ikimaarisha vyuo vyake kama Mzumbe, IFM inaweza kabisa kukidhi haja na kuokoa pesa nyingi zinazotumiwa na wazazi kuwapeleka watoto India na kwingineko

  Ni vema kwa ujumla wetu Tususie bidhaa za hawa wahindi kwani itakuwa ni njia mojawapo ya kuwaadhibu
   
 15. Ben Saanane

  Ben Saanane Verified User

  #15
  Mar 15, 2010
  Joined: Jan 18, 2007
  Messages: 14,603
  Likes Received: 3,692
  Trophy Points: 280
  -Kususia bidhaa za wahindi ni tactic nzuri

  -Lakini kuna madhara makubwa kiuchumi,ni sawa na kupiga mkuki ngumi
   
 16. Juma Contena

  Juma Contena JF-Expert Member

  #16
  Mar 15, 2010
  Joined: May 21, 2009
  Messages: 1,195
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  Thats the idea 'Kaka' kwa maneno yako lakini hawa jamaa (waandishi wetu) hata sielewi wana skills gani au elimu gani zaidi ya uandishi hili kuweza weka kiji pressure.

  Things dont change on their own hili huyo muhindi mjeuri inabidi aelewe kwamba we are no longer willing to tolerate these sort of behaviours and intimidations facing our fellow citizens in their land.

  Hiki bidi walipe compensation for the loss of lives if it ever happens again. Lakini kukaa kimya tu ni kusema 'hewala bwana' a belief i do not agree with.
   
 17. Ngambo Ngali

  Ngambo Ngali JF-Expert Member

  #17
  Mar 15, 2010
  Joined: Apr 17, 2009
  Messages: 3,194
  Likes Received: 134
  Trophy Points: 160
  Understatement, wanaishi kwa raha na juu ya sheria. Hawatendi makosa ya jinai labda kuua tena wahindi wenzao, hawana kesi za traffic pamoja na kuendesha magari na kusababisha ajali. Kesi za madai walizonazo ni za mahakama ya ardhi tu na si nyinginezo is it by design or default???????
   
Thread Status:
Not open for further replies.
Loading...