Waheshimiwa Zitto, Kitila na Mnyika eti hii ni kweli? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Waheshimiwa Zitto, Kitila na Mnyika eti hii ni kweli?

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by kifrogi, Jun 24, 2011.

 1. kifrogi

  kifrogi Member

  #1
  Jun 24, 2011
  Joined: Jun 8, 2011
  Messages: 42
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Habari zenu wapiganaji wetu.

  Leo nimeona kwenye gazeti silikumbuki jina kuwa Chadema chama tunachokipenda kimeungana na chama cha kikristo cha ujerumani kinachoitwa CDU Christian Democratic Union na kitasaidia Chadema kwa hali na mali ikiwa ni pamoja na semina ili kuimarisha uhusiano wa vyama hivi.

  Kumekuwa na maneno ya chini kuhusu chama chetu tegemeo letu kuwa cha kidini kwa hili ikiwa ni kweli basi wale ambao tulikuwa tukiwatuliza watatuona tumewahadaa. Pengine si dhambi kushirikiana na chama hicho lakini tuangalie mazingira ya nchi yetu imefika mpaka jamaa ameniuliza hivi wewe ingekuwa CUF imeungana na Muslim Brotherhood ya Misri vyombo vya habari vingeisakamaje? huoni chama chenu kimeanza kushirikiana na Christian Democratic Union vyombo vya habari kimya?

  Nawasihi mtupe maelezo je hizi habari ni za kweli? au ni uzushi na propaganda? na ikiwa ni kweli nini faida yake? je hakutakuwa na hasara zozote?

  Nawakilisha.

   
 2. kifrogi

  kifrogi Member

  #2
  Jun 24, 2011
  Joined: Jun 8, 2011
  Messages: 42
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Jamani chadema wenzangu mbona mnaikimbia hii hari kwanini tusiijadili maana nimeanza kushikwa na hofu ya kukimbiwa na wanachama wasiokuwa Christians.
   
 3. m

  mzee wa njaa JF-Expert Member

  #3
  Jun 24, 2011
  Joined: Jun 16, 2011
  Messages: 1,368
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  hakuna tatizo kusaidiwa na chama cha kikristo..............mbona ccm ilishasaidiwa na waarabu wa saudia arabia tuseme wao waislamu na serikali yake au? porojo hizo msiogope.
   
 4. Lokissa

  Lokissa JF-Expert Member

  #4
  Jun 24, 2011
  Joined: Nov 20, 2010
  Messages: 7,079
  Likes Received: 155
  Trophy Points: 160
  lengo kuu ni kuendeleza mpambano ili haki kamili ipatikane. wanaokusudiwa kwenda ujerumani sii wakristo pekee na pia chama hicho hakina wakristo pekee huko Ujerumani. mpaka kieleweke.
   
 5. Matola

  Matola JF-Expert Member

  #5
  Jun 24, 2011
  Joined: Oct 18, 2010
  Messages: 36,045
  Likes Received: 13,279
  Trophy Points: 280
  Humu JF imevamiwa na members wenye hoja za kuokoteza, kama wewe ni mtu makini na unafuatilia siasa za nchi hii ni kwamba CDU ilikuwa inawasupport CUF, lakini baada ya CHADEMA kupanda chati sasa hivi wanaisupport CHADEMA, hapa cha msingi kwamba siasa zao ni za mlengo gani?
  Hakuna mambo ya Yesu kwenye hicho chama cha CDU. na kama unashangaa hilo jina basi kuna chama kingine kinaitwa chama cha kijani upo hapo mkuu?
  Mimi eneo ninloishi tunategemea dispensary ya kanisa kutibiwa na wanaokwenda pale wengi wao ni waislamu, na by the way kwa nini usiulize haivi Kikwete alivyosoma kwenye shule za kanisa alibadilishwa dini?
  Hii ni hoja mufilisi kutoka kwa mtu mwenye akili Half empty glass.
   
 6. Matola

  Matola JF-Expert Member

  #6
  Jun 24, 2011
  Joined: Oct 18, 2010
  Messages: 36,045
  Likes Received: 13,279
  Trophy Points: 280
  Akili yako haina tofauti na chura kukimbia mvuwa, halafu unkwenda kwenye maji!
   
 7. Ng'wanza Madaso

  Ng'wanza Madaso JF-Expert Member

  #7
  Jun 24, 2011
  Joined: Oct 21, 2008
  Messages: 2,278
  Likes Received: 60
  Trophy Points: 145
  Kumbuka hiki ni Chama Tawala kinachowaongoza watu Milioni 81,802,000 kwa hiyo si vibaya kushirikiana na Chama tawala na ambacho kinaidhinisha misaada yote kutoka Germany kuja huku kwetu
  The leader of the party, Angela Merkel, is the current Chancellor of Germany. The CDU is a member of the European People's Party (EPP), and sits in the EPP Group in the European Parliament. Internationally, the CDU is a member of the Centrist Democrat International and the International Democrat Union. The CDU is the largest political party in Germany, followed by the Social Democratic Party of Germany.
   
 8. N

  NCHABIRONDA JF-Expert Member

  #8
  Jun 24, 2011
  Joined: Jun 6, 2011
  Messages: 238
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  Sasa wewe uliyeanzisha mada hii, wewe umeona kuna ubaya gani kama cdm ikuwa na urafiki na hicho chama? Kwani hicho chama huko kwao Ujurumani kinakashifa gani kwa wananchi wa ujurumani kiasi kwamba umeona cdm itakuwa imefanya makosa kuwa na urafiki na hicho chama? Ninawasiwasi na umri wako labda huenda ni utoto unakusumbua, au kama sivo huenda utakuwa umetumwa na hao shemeji zako Magamba.
   
 9. j

  jnuswe JF-Expert Member

  #9
  Jun 24, 2011
  Joined: Nov 2, 2010
  Messages: 1,271
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  Mimi ninachoweza kukusaidia ndugu yangu ni kimoja , yaani hapa ni kama tunataka kuweka mipaka kati ya uislam na ukristo sioni taabu hapo maadam kile ni chuo na sio dini , naamini chuo yoyote anaweza akasoma chuo chochote, mkristo anaweza akasoma chuo cha uislam kama tu pana kozi ambazo ni nje na dini ya kislam, vivyo hivyo muislam, kwani vyuo kama Tumain University, RUCCO, MAKUMIRA vyote hivyo ni vya kikristo lakini pale utakuta waislam wapo wanasoma masomo mengine kama kawaida, mimi sioni kama kuna tatizo
   
 10. Nanren

  Nanren JF-Expert Member

  #10
  Jun 24, 2011
  Joined: May 11, 2009
  Messages: 1,739
  Likes Received: 184
  Trophy Points: 160
  Umeonesha tofauti.
  Watu wanaleta hoja ambazo zipo kama za vijiweni.
  Kwa mtu makini hakutakiwa hata kuleta hoja kama hii.

  Thanks, man!
   
 11. samirnasri

  samirnasri JF-Expert Member

  #11
  Jun 25, 2011
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 1,377
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  hakuna tatizo lolote hapo kwani umeambiwa chadema wamepewa hiyo support kwa ajili ya kueneza injili ?????????????????????
   
 12. Sokomoko

  Sokomoko JF-Expert Member

  #12
  Jun 25, 2011
  Joined: Mar 29, 2008
  Messages: 1,918
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  Si jambo la tetesi tena kwamba sera na mrengo wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) ni ule wa Kikristo. Hii ni kutokana na hatua yake ya kuweka wazi urafiki wake wa karibu na Chama cha Kikristo cha Ujerumani, Christian Democratic Union (CDU). Kutokana na urafiki huo, CDU kimesema kuwa kitawapa nafasi za mafunzo nchini Ujerumani vijana na viongozi wa Chadema, kusomea maadili na uongozi.

  Maadili na uongozi ambao kwa mujibu wa mtizamo na sera za CDU ni yale ya Kikristo kama yalivyobuniwa na mwasisi wa chama hicho Konrad Harman Joseph Adenauer. Taarifa zilizotolewa hivi karibuni na mwenyekiti wa Chadema Mhe Freeman Mbowe zinasema kuwa fursa hiyo imetolewa kwa chama chake baada ya kufanya mazungumzo ya faragha na ujumbe wa CDU uliokuwa ukiongozwa na Rais wa zamani wa Ujerumani Profesa Dk. Horst Kohler. Mazungumzo hayo yalimshirikisha katibu mkuu wa chama hicho Dk Wilbrod Slaa na viongozi wengine wa juu.

  Mbowe meviambia vyombo vya habari kuwa katika mazungumzo yao Kohler alisema dhamira ya kuwapa nafasi za masomo vijana viongozi wa Chadema inalenga kuwafanya wawe viongozi wenye maadili mazuri kwa taifa lao. "Tumekubaliana ambapo tutapata nafasi za masomo kwa vijana ambao ni viongozi wa Chadema kwenda kusomea uongozi na maadili chini Ujerumani" alisema. Kwa hapa nchini imeelezwa kuwa Chadema itafanya kazi kwa karibu na kwa kushirikiana na taasisi ya Conrad Adenauer Foundation ambayo ni ya taasisi ya Kikristo iliyo chini ya Chama cha CDU.

  CDU kikiwa kimeanzishwa mwaka 194, ni chama cha Kikristo kilichowaunganisha Wakatoliki na Protestant kikilenga kujenga Ujerumani yenye maadili ya Kikristo katika siasa, kijamii, maadili na kila kipengele cha maisha.Mwanzilishi wake Konrad Hermann Joseph Adenauer anatajwa kuwa mfuata Ukatoliki aliyekuwa tayari kuufia Ukatoliki wake na ambaye amefanya kazi kubwa kutaka kuona maadili ya Kikristo yakitawala na kuongoza siasa za Ujerumani na Kimataifa. Anatajwa kutoa mchango mkubwa katika kujenga Ulaya mpya ya Kikristo na umoja chini ya NATO baada ya vita Kuu ya pili ya dunia.

  Kwa upande mwingine rekodi zinaonyesha kuwa Konrad alichangia kwa kiasi kikubwa kuanzishwa kwa taifa la Israel, jambo lililoenda na kuporwa ardhi ya wapalestina na kudhalilishwa hadi hii leo.

  Ujerumani ikitajwa kama nchi ya Kikristo hii leo, mchango mkubwa unatokana na Konrad Hermann Joseph Adenauer na chama chake cha CDU pamoja na ile taasisi yake Konrad Adenauer Foundation ( Konrad - Adenauer - Stiftung ) (KAS). Hii ni taasisi iliyo chini ya chama rafiki wa Chadema, yaani CDU ambayo iliundwa mwaka 1956 ikiwa taasisi ya Kikristo ya kutoa elimu ya siasa na kiraia kwa mtizamo wa Kikristo. Awali ilipoanzishwa mwaka 1956 ilijulikana kwa jina la "Society for Christian Democratic Education Work" ndio mwaka 1964 kikapewa jina la Konrad Adenauer kwa heshima ya mwanzilishi wake.

  Ni taasisi ambayo ina miradi 200 katika nchi mbalimbali duniani ikiwemo hii ya kutoa elimu ya siasa, maadili, uongozi na hata uchumi kwa vyama vya siasa ambavyo vinakubaliana na sera zake za Kikristo. Kwa upande wa chama cha CDU ambacho ni rafiki wa Chadema inaelezwa wazi kuwa "is Christian- based applying the principles of Christian democracym and emphasizes the Christian understanding of humans and their responsibility toward God" Kwa japo wale ambao sio wakristo wanaruhusiwa kujiunga na chama hicho lakini wajue misingi yake ni kinafuata maadili na kanuni za Kikristo katika siasa zake na namna ya kumwelewa binadamu na wajibu wake kwa "Mungu"

  Kutokana na msimamo wake huo wa kikristo chama tawala cha Ujerumani CDU kimekuwa mstari wa mbele madhubuti kupinga Uturuki isikubaliwe kuwa mwanachama wa Umoja wa Ulaya. Uturuki inaonekana kama nchi ya Kiislamu kwa vile wananchi wake karibu wote ni Waislamu. Wakristo wa ndani ya Uturuki ni wale wahamiaji. Hata hivyo, pamoja na jitihada za CDU na Konrad yake kufanya juhudi za kujenga jamii ya Kikristo Ujerumani, Ulaya na Ulimwenguni dalili zinaonyesha kuwa Ujerumani inazidi kusilimu kila uchao. Hali hiyo imepelekea kiongozi wa nchi hiyo Chancellor Angela Merkel kutoa kauli akiwazindua Wajerumani wenzake kwamba nchi yao hivi sasa inakimbilia kuwa ya Kiislamu. Akinukuliwa na vyombo vya habari mwaka jana Kansela Angela amesema kuwa Wajerumani (Wakristo) wameshindwa kugundua jinsi Waislam walivyojipenyeza na kupenyeza dini yao Ulaya jambo ambalo limebadili hali ya mambo. Akasema kutokana na hali hiyo sasa itabidi Wajerumani wajifunze kuona Misikiti mingi zaidi ya Makanisa waliyo kuwa wamezoea kuyaona huko nyuma. Kwa mujibu wa gazeti la Frankfurter Allgemeine Zeitung, si muda mrefu misikiti Ujerumani itakuwa mingi kuliko makanisa.

  My take

  Wasio kuwa vijana viongozi wa wakristo jiandaeni kufundishwa maadili ya kikristo nawatakieni kila la heri.
   
 13. N

  NCHABIRONDA JF-Expert Member

  #13
  Jun 25, 2011
  Joined: Jun 6, 2011
  Messages: 238
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  Mh kazi kwelikweli.
   
 14. Mr. Mwalu

  Mr. Mwalu JF-Expert Member

  #14
  Jun 25, 2011
  Joined: Feb 4, 2010
  Messages: 812
  Likes Received: 175
  Trophy Points: 60
  mkipambana na kutuondolea umasikini ujinga na maradhi, mkatupa nafuu ya maisha! hapo tutakuwa na choices, kwa sasa chadema wanaonekana kutupigania regardless ya imani yao! kupigika hamna dini BRO!
   
Loading...