Waheshimiwa wana JF - Hongereni!

Status
Not open for further replies.

Mzee Mwanakijiji

Platinum Member
Mar 10, 2006
33,475
39,988
THE AUDACITY OF FREEDOM AND THE TENACITY OF DEMOCRACY
Utangulizi:

Waheshimiwa,

Nimetumia muda kusoma kila post na kutoa shukrani kwa michango yenu yote na pia kupata muda wa kuachilia yote yaliyosemwa yazame moyoni na kuyafurahia. Yazame moyoni kwa sababu yanatoka kwa watu ambao wanathamini kile ninachokifanya na ambao licha ya tofauti zao nami za kila namna lakini tunajikuta tumefungamanishwa na historia na hivyo kujikuta tuko karibu.

Lakini pia kufurahia kama vile mkulima afurahivyo mazao yanapokuwa tayari kuvunwa na kama mvuvi anaponyanyua nyavu na kuona jinsi zilivyojaa samaki na hivyo furaha yake japo ni ya kutegemea mauzo lakini anajua ana pa kuanzia.

Shukrani

Hivyo basi naomba nitumie fursa hii baada ya kumshukuru kila mmoja wenu aliyechangia nitoe shukrani za dhati kabisa kwa kila mmoja wenu na kwa jumla ya wale wote ambao wanafurahia kile ambacho nakifanya. Nasema asante sana na Mungu awabariki ninyi nyote na kuwazidishia mara nyingi zaidi yale yote mnayonitakia mimi.

Hata hivyo, niseme pia kuwa nawashukuru wale ambao ni wakosoaji wangu wa kudumu; wale ambao ukosoaji wao ni kwa ajili ya kuniweka sawa na kunijenga na wale ambao ukosoaji wao ni kwa ajili ya kunikwaza, kunikatisha tamaa na kuniangusha.

Kwa wakosoaji

Kwa wale mnaoteka kunijenga na kunisaidia kuwa bora zaidi, makini zaidi na mwangalifu zaidi naomba msikome kufanya hivyo na msisite kufanya hivyo wakati wowote. Mimi nashaurika na ninapenda kusikia mashauri ya watu. Haijalishi kama wewe ni mgeni au mwenyeji lakini kama unakitu tafadhali usisite kuniambia iwe chemba au hadharani.

Nakubali hilo kwa sababu kuna msemo usemao "chuma hunoa chuma, ndivyo mtu aunoavyo uso wa rafiki yake". Ni bora rafiki yangu aniambie ukweli kuliko adui anisifie ili aniangamize.

Kwa wale ambao ni maadui na ambao wanafanya na wamefanya kila jitihada ya kunitega nianguke basi niwape ujumbe mmoja tu; liwalo na liwe niko tayari kwa lolote na hakuna kitu ambacho mnaweza kufanya ambacho kinaweza kuzima fikra zenye nguvu. Hakuna. So, jifunzeni kuishi nami na watu wengine ambao mawazo yao kwenu yamekuwa mwiba. Hatuendi kokote na hatupigi magoti kuwaomba radhi! Kwani tumegoma kupiga panda mbele ya altare ya kafara za mafisadi!

Jambo Forum ndiyo imenijenga
Lakini ndugu zangu niseme kuwa, yote niliyoyafanya hadi hivi sasa na ambayo nakusudia kufanya huko mbeleni yamefungamana kwa namna ya pekee na forum hii kiasi kwamba najua kuwa nawiwa deni kubwa na forum hii na hususan wanachama wake wengi ambao wamekuwa ni chanzo cha faraja, vyanzo vya hoja, na kwa hakika mwali uwashao moto wa fikara.

Mambo mengi ambayo nayafikiria na kuyajengea hoja mara nyingi yanatokana hapa au yanapata kuinuliwa zaidi hapa. Hivyo, nitakuwa mwongo na mkosefu wa fadhila kama sitakiri kuwa Jambo Forums imekuwa ni kisima cha mawazo ambapo kila kukicha nadamka kuwahi kuchota maji ya masafi yakatayo kiu na yenye kupoza wakati wa hari.

Nitakuwa si muungwana nikiamini kuwa jina hili la Mwanakijiji limejengwa nje ya Jambo Forums. Ni kweli kabla ya hapa nilishaanza kuandika na kufanya mambo mengi, lakini nina uhakika watu wengi zaidi wamefahamu uwepo wa "Mwanakijiji" kupitia Jamboforums. Kwa hili sina cha kulipa isipokuwa kusema "ninashukuru".

Tujipongeze wenyewe
Marafiki, tuliyoyafanya pamoja si kidogo, tulikotoka si mbali na tunakoenda bado hatujajua umbali wake; lakini kwa vyovyote vile hatuna budi kujipa mkono wa pongezi kwani tumeweza kufanya mambo kadhaa pamoja ambayo kwa hakika hayana budi kusimuliwa kama hadithi huko mbeleni.

Kwanza, tumesukuma uhuru wa maoni kuliko chombo kingine chochote kile. Ninaamini kabisa kuwa kabla ya JF kulikuwa na fora nyingine kama Nyenzi, bcstimes, youngafrican, africaonline, n.k ambazo zote zimechangia kwa kiasi kikubwa kutufikisha hapa. Wale tulioanza na Africaonline au Nyenzi na hadi leo karibu miaka 10 baadaye tunajua ni jinsi tumetoka mbali.

Mabadiliko makubwa hata hivyo yalitokea baada ya kupata nafasi ya kuweza kupenyeza mawazo yetu kwenye vyombo vya habari na pia baada ya watu walioko kwenye madaraka kupata nafasi ya kutusikiliza. Kwa hili, ni lazima tujivunie safari yetu iliyotufikisha hapa.

Pili, tumesababisha JF kuwa kama godoro ambalo watu huangukia na kupata mapumziko yao. Kabla ya sisi kuanza kulazimisha hoja, kupangua majibu ya viongozi, kuwanyoshea vidole viongozi na watawala wetu mambo mengi yalikuwa yanasemwa pembeni na sirini au kwenye vikao maalum.

Naamini JF ilifikia kipindi cha mabadiliko tulipofikia kuzungumza suala la Amina na Zitto (na hatimaye msiba wa Amina), suala la vijana Ukraine, na kwa namna ya pekee naamini pale ambapo tuligongana kimawazo na Waziri Mkuu Lowassa na "ndege yake iliyopaa huku abiria wameachwa wameduwaa". Kama kuna kitu ambacho naamini Lowassa anakijutia ni kosa la waandishi wake kujaribu kujibu kizembe jinsi walivyofanya. Lile lilikuwa ni kosa la mtu aliyelewa madaraka na ninaamini kwa wananchi wengi jina la "Mwanakijiji" lilianza kusikika kwa namna ya pekee.

Lakini kuna jambo jingine ambalo Jambo Forums ilijikuta inajipatia heshima kwa namna ya pekee. Kabla ya Mkataba wa Richmond kupatikana na kuwekwa hapa, wana JF waliotawanyika mahali mbalimbali duniani walianza kuhoji na kuuchunguza mkataba huu na kutoa maswali juu ya maswali. Mwanzoni watu walipuuza lakini kwa hakika nafasi ya JF katika suala hili ni kubwa kuliko wengi mnavyoweza kufahamu.

Kwa wale wasio na majina
Natumaini siku moja historia itaandikwa sawasawa na ripoti zitakapoandikwa jina la forum hii litapaswa kuandikwa na kuwekewa nyota (*) pembeni kuelezea ni jinsi gani tulisaidia katika kuchambua na kutafuta ukweli wa mkataba huu. Kuna watu ambao majina yao yatabakia sirini ambao walitoa msaada mkubwa kwa Kamati Teule na ambao bila ya wao sidhani kama ripoti ya Mwakyembe ingekuwa ilivyokuwa. Kwa hawa (walioko nyumbani na nje) wanastahili makofi na heshima ya pekee kwani walifanya kitu zaidi na juu kabisa ya wajibu wao.

Changamoto bado zipo
Pamoja na hayo yote, bado tunakabiliwa na changamoto; changamoto ya kuamua ni nini tunataka kufanya na wapi tunataka kwenda. Haitoshi kuzungumza na kujadiliana bila kukomesha mijadala, na haitoshi kukosoa bila kutoa mapendekezo ya masuluhisho; haitoshi kunyosha kidole cha kuonya bila kuonesha njia mbadala. Kama kweli tunataka tuwe kisima cha mawazo hatuna budi pia kuumiza vichwa vyetu kuja na mapendekezo ya utatuzi wa matatizo tunayoyalalamikia.

Bado masuala ya Rada, Madini, ufisadi n.k yanaendelea kujitokeza hivyo tusibweteke!

Kukua ni kubadilika
Baada ya sakata ya kina Manumba na JF, tumeona ipo haja ya kuhakikisha kuwa JF inakuwa organized kwa namna fulani. Baadhi ya wanachama waandamizi na wachangiaji tumekutana na tumekuwa tukizungumza juu ya nini tufanye. Natumaini baada ya ya kama wiki hivi tutakuwa tumepata mahali pa kuanzia na jumuiya hii itajulishwa.

Hivyo, jambo moja ninaloomba na kuwasihi tena kwa kuwapigia magoti! Tusiiache Jambo Forums kugeuka kuwa kijiwe cha wapiga porojo na kamwe tusiiache iwe mahali pa watu kulipiziana visasi visivyo na msingi. Pawe ni mahali huru pa hoja lakini pasiwe mahali pa hoja ambazo hakuna furaha kukaa. JF siyo chuo kikuu hivyo ni mahali ambapo watu wanazungumza, na wanacheka huku wakiburudika. Lakini tuwe wepesi kuwekana sawa ili tusije kupoteza mwelekeo.

Wiki kama mbili zilizopita nilipokuwa nimekimbia kwa bibi (japo nilikuwa nachungulia chungulia) zilikuwa ni wiki za ajabu na nina uhakika kama kuna mtu aliingia hapa kwa mara ya kwanza alijikuta kuwa yuko turned off. Tulikuwa kwa namna fulani kama vichaa wanaoshinda kuona nani kichaa zaidi! Na nikitumia mfano mbaya tulikuwa kama machangudo ambao wanashindana nani ameweza kutoa huduma kwa watu wengi zaidi!! Kwa kweli tulijidhalilisha na ninatumaini ngwe ile imepita.

Na sitashangaa kuwa mojawapo ya mabadiliko ambayo yanaweza kuja ni jinsi gani ya kuhakikisha kuwa jambo forums haigeuki na kuwa danguro la mafisadi wa vihoja.

Tusonge mbele!
Twende na tuwe wasimamizi wamulikao ufisadi wa kila aina! Twende mbele tuwe waangalizi na walinzi wa nchi yetu! Twende na tuwe walinzi wa ndugu zetu! Twende na tuwe walinzi wa uhuru wa maoni na mawazo! na Twende na tuwe watu wabebao mwengwe umulikao matumaini katika mioyo ya watanzania. Tuoneshe kuwa ujasiri wa uhuru ni kiini cha kuweza kuleta mabadiliko ya kweli ya kijamii katika Tanzania.

Ni ujasiri huu ndio ambao umeifikisha Jambo Forums ilipo sasa. if we protect and cherish this audacity of freedom and tenacity of democracy we are infact setting the new standard in African body politics and by doing so fostering the emergence of a new generation of African problem solvers and thinkers; those who would not take "no" for an answer.

Watawala msiogope
Kwenu watawala wetu, msiogope! Jambo Forums si adui yenu na wala haina lengo la kuwaangusha, isipokuwa endapo mkiangushwa ni kwa sababu Jambo Forums imeonesha nini kitawaangusha. Hivyo nawasihi msisite kuja kusoma, na kutoa mawazo ili muweze kupata mawazo ya watu wasio na maslahi ya hisani, fedha, au vyeo na watu ambao watawaambia ukweli bila kujikomba!

Na kama ninapendekezo ni kuwa anzeni kusafisha nyumba zenu kwani tunakoenda ni moto zaidi. Huko tunakokwenda Jambo Forums itaanza kugusa kwa ukaribu zaidi, mnayoyafanya sirini yaacheni, na yale ambayo mnadhani ni ya kawaida yakwepeni kwani muda si mrefu siri zenu chafu zitafichuka. Kumbukeni yanaanzia JF yanaisha kwenye vyombo vyetu vya habari kama itakavyokuwa kesho kwenye moja ya magazeti! Wajumbe Butiama kaeni chonjo...

Kwa wanachama wote
Kwenu ninyi nyote, wanachama mpatao 4631 (568 zaidi waliojiunga baadaya ndani ya mwezi mmoja uliopita) na ninyi mtakaojiunga; nawaomba tuwe pamoja katika kuhakikisha kuwa Jambo Forums inadumu, na inadumu kama mahali ambapo mawazo huru na fikra zinazokinzana zaweza kuwekwa pasipo hofu yoyote ile. Kabla hatujaweza kuleta mabadiliko katika nchi, ni lazima tubadilishe fikra na Jambo Forums ni mahali ambapo fikra zinachongwa na kupigwa msasa na kutoka hapo hutengenezwa na kuwa vitu vya thamani.

Kwenu nyote ambao mmenifikisha hapa nilipo ni nyinyi kwa hakika ndio "mwanakijiji"; ni nyinyi ambao mawazo na fikra zenu zimechangia kwa kiwango kikubwa katika mabadiliko yaliyopo. Hata hivyo changamoto bado ni nyingi na huu si wakati wa kubweteka; huu ni wakati wa kusimama na kusonga mbele hadi tujue nini kinaendelea.

Kwa kila mmoja nisema

"havache, usengwile, ndaga fijo (na pikipiki), thank you, asante, danke, merci, grazie, Arigato, muchas gracias, ngiyabonga, wabeja, wabale, ... "
 
Wiki kama mbili zilizopita nilipokuwa nimekimbia kwa bibi (japo nilikuwa nachungulia chungulia) zilikuwa ni wiki za ajabu na nina uhakika kama kuna mtu aliingia hapa kwa mara ya kwanza alijikuta kuwa yuko turned off.

Tulikuwa kwa namna fulani kama vichaa wanaoshinda kuona nani kichaa zaidi! Na nikitumia mfano mbaya tulikuwa kama machangudo ambao wanashindana nani ameweza kutoa huduma kwa watu wengi zaidi!! Kwa kweli tulijidhalilisha na ninatumaini ngwe ile imepita.

Na sitashangaa kuwa mojawapo ya mabadiliko ambayo yanaweza kuja ni jinsi gani ya kuhakikisha kuwa jambo forums haigeuki na kuwa danguro la mafisadi wa vihoja. ! Twende na tuwe walinzi wa uhuru wa maoni na mawazo! na Twende na tuwe watu wabebao mwengwe umulikao matumaini katika mioyo ya watanzania. Tuoneshe kuwa ujasiri wa uhuru ni kiini cha kuweza kuleta mabadiliko ya kweli ya kijamii katika Tanzania.

Ni ujasiri huu ndio ambao umeifikisha Jambo Forums ilipo sasa. if we protect and cherish this audacity of freedom and tenacity of democracy we are infact setting the new standard in African body politics and by doing so fostering the emergence of a new generation of African problem solvers and thinkers; those who would not take "no" for an answer.

Asiyekubali au kuielewa hii dozi ya Mkulu Mwanakijiji, kwa niaba ya sisi wote tunaotaka mabadiliko ya kisheria na kisiasa, kwa kutumia hoja nzito, basi huenda hapa sio mahali pake, anahitaji kujiondoa hapa mapema na haraka sana,

Maana hiii ndio imetoka hiyo, sisi tunasonga mbele, hakuna muda wa viroja hapa tena, hiii ni changamoto nzito tena ni sindano ya moto kama ile ya kutoka kwa Mangelepaaa ya Kai Kai, mwongozo siku zote huwekwa na great leaders tu, sisi wengine yaaani great wananchi ni kufuata tu na kumkoma nyani bila ya kumuangalia usoni.

The main point hapa, ni enough of the virojas.

Ahsante Mkuu Mwanakijiji kwa changamoto nzito sasa tuendelee kumkoma fisadi, tena bila huruma mchana kweupeee, maana tukimkoma usiku tutageuka fisadi!
 
Unaona sasa...tatizo humu kuna mijitu inajiona yenyewe ndiyo yenyewe...eti ina akili sana kushinda wengine....na mawazo yao kila siku ndio bora!! Kila siku inashindana hapa kuonyesha imesomea nini hata kama haijasomea hivyo vitu. Hii tabia ni mbaya sana na inapofikia jitu kujiona lenyewe ndio lina akili kushinda wengine basi ujue ni tupu na ili kujilazimisha kuamini kwamba lina akili inabidi liwa-put down wengine.

This is not directed at any one in particular but if the shoe fits then you know what time it is....
 
Thanks MKJJ,Pia kwa yeyote aliye na tatizo la haya yalioandikwa tunamwomba naye aandike yake nayo tuyasome ndio tutabaini yapi sisi tuyakubali.
 
Idumu JF na members wake
Inaaminika kuwa wanyama huwa wanatambua baadhi ya rangi na so wote wanaona rangi sawa lakini hiyo haiwatoi ktk credibility ya kuwa wanyama....
 
Thanks MKJJ,Pia kwa yeyote aliye na tatizo la haya yalioandikwa tunamwomba naye aandike yake nayo tuyasome ndio tutabaini yapi sisi tuyakubali.

hata hivyo, binadamu wote sio sawa. sir pilato aliwahi kubainisha hilo,

kuna wengine wameumbwa kwa dhahabu ili wawe viongozi, na wengine kwa silver ili kuwa waandamanaji na walinzi wa kusafisha njia. wakati wengine wameumbwa kwa iron and steel ili wawe wakulima na wafanyabiashara.

sasa kama sisi wenyewe tunamwamini kumtumia mwanakijiji kufuatilia mambo ili kupata habari, kama kumpigia simu Manumba na Mwema katika sakata tofauti, na kujibu vihoja pale palipo na haja, kufanya maojiane n.k kwa nini asijibu shukrani kwa wale wanaomtumia yaani wanaJF; he is right to show his appreciation

kwa kifupi, inabidi atoe shukrani kwa nini hatumwi Mushobozi na mwingine kufatilia badala yake ni mwanakijiji?

MY PHILOSOPHY "The man meant that all the efforts so far made by JF are futile to reach the goal, though some elements of achievents have started to enshrine"

Hata akija Lunyungu kutoa shukrani tutazipokea kwa namna tunavyomtumia Bungeni Dodoma na Musoma wakati wa NEC, au Pundit na Icadon kule Comoro vitani n.k. kila mtu ana upande wake anapouweza.

challenges kwa wale tuliosalia akiwemo mimi, contribution yetu ni nini? tunatumikaje na JF, au tuko hapa kupinga kila hoja inayojengwa na wengine. swali hilo hata mimi ninalitafakari, ila yawezekana wengine majukumu hanatubana, na mwanakijiji ni zaidi ya hapo

jesus anasema, huwezi kuwatumikia mabwana wawili, yaani kazi na JF, shule na JF, Chama na JF, Familia itakula nini na JF inataka nini, ila mwanakujiji yuko zaidi ya hiyo philosophy kuwa anaweza kuwatumikia wawili.

sijikombi, ila kazi yake hapa Tz inakubalika, mpaka watu wanauliza mwanakijiji ni nani na anakaa wapi. kama unavyomsikia Osama bin laden anvyofikirika marekani, ndivyo mwanakijiji alivyo tanzania.
 
thanks MMwanakijiji. Bwana akubariki milele na milele, amen

Naomba tu nikupongeze kwa hayo uliyoyaandika hapo juu na kutilia mkazo baadhi ya uliyoyasema.

You are right kwamba changamoto inayotukabili si tu kuibua dosari na kukemea matatizo mbali mbali yanayotokea katika nchi yetu, nadhani inabidi tuende mbele zaidi katika kutoa mawazo ya nini kifanyike. Tukiwa katika msimamo huo tutaweza kuijenga JF na kuwa ni source ya information muhimu ambazo zinaweza kuwasaidi wale wenye nia njema na nchi katika kutekeleza majuku yao ya kulitumikia taifa

Jambo la pili nafikiri kuhusu JF kuwa kijiwe. Pamoja na kwamba mimi ni mgeni hapa JF lakini nimekuwa msomaji mzuri wa taarifa za JF hapo kabla, na kuna tafauti kubwa ya JF ya zamani na sasa na tusipokuwa makini hali itabadilika na muda si mrefu JF itakuwa kijiwe kweli sio utani. Ingawa baadhi ya wadau wanasema sio lazima usome kila kitu lakini nadhani ipo haja ya kuwa na quality control mechanism

Once again ngiyabonga mkulu
 
"Mkjj hebu timiza usemi wako huu"
Kumbukeni yanaanzia JF yanaisha kwenye vyombo vyetu vya habari kama itakavyokuwa kesho kwenye moja ya magazeti! Wajumbe Butiama kaeni chonjo...
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom