Elections 2010 Waheshimiwa Waliomfukuza Zitto Kabwe- Big up wapiga kura

SG8

JF-Expert Member
Dec 12, 2009
3,955
2,125
Kama record zangu ziki sawasawa waheshimiwa waliomtoa Bungeni Mh. Zitto Kabwe karibu wote wameshindwa kutetea nafasi zao. Mfano John Malecela, Nazir karamagi, Batilda Burian, Ruth Msafiri na "Joka la Mdimu" Mudhihir wa Mudhihir. Kumbe watanzania wanajua kutoa adhabu! Big up wapiga kura wa majimbo husika.
 
duuhhh, ndio maaana napapenda hapa JF maana watu wa hapa wanafikiri sana na kwa umakini.
kumbukumbu zangu zinaonyesha upo sahihi kabisa mkuu.
Hili la kupigwa chini hawa jamaa linadhihirisha mambo mawili makubwa
1. hawa jamaa hawana uwezo wa kujenga hoja zaidi ya kufuata mkumbo wa ushabiki wa kisiasa (U ccm dhidi ya Upinzani)
2. wananchi wa tanzania kwa sasa wameamka kwani wanafuatilia kwa karibu sana jinsi mambo yanavyoendeshwa na pia wanauwelewa mkubwa wa mambo yanayoendelea hapa nchini kwao,hivyo basi kutokana na kuona kazi nzuri iliyofanywa na Mhe Zito na ukimbele mbele wa hawa jamaa, wananchi wakaona itakuwa sahihi kama watawapiga chini.

HII NDIO MSINGI MZURI WA KULETA MAPINDUZI YA KWELI KATIKA TANZANIA YETU
MUNGU IBARIKI TANZANIA, MUNGU IBARIKI AFRIKA, AMEEEEEN
 
Of all the people Mudhihir naona alikuwa na hati miliki na bunge as aliongea with full authority
 
Mudhihil alipata malipo mengi kwa ajili ya ufedhuli wake. Sina haja ya kutaja lakini mwajua. Mungu si mchezo hata achezewe na wana siasa dhidi ya watu wake.
 
Bado na wale waliomsababishia Dr. WP Slaa kukosa ushindi watapigwa moja baada ya mwingine hadi wajute kuzaliwa. Mungu lazima atawapa mapigo saba matakatifu tukianzia na mh. Mie Kuchakachua Janja yangu na wapambe wake km kina Mh. Chungulia Anguko na wengineo wengi sitaki kuwataja wanajijua.
 
dah,you are a great thinker for sure!
sikuwahi fikiria hilo kabisa
 
Kama record zangu ziki sawasawa waheshimiwa waliomtoa Bungeni Mh. Zitto Kabwe karibu wote wameshindwa kutetea nafasi zao. Mfano John Malecela, Nazir karamagi, Batilda Burian, Ruth Msafiri na "Joka la Mdimu" Mudhihir wa Mudhihir. Kumbe watanzania wanajua kutoa adhabu! Big up wapiga kura wa majimbo husika.

Mkuu hiyo redi si nilisikia imeenda mahakamani kupinga matokeo? na vp kuhusu hali yake kihafiya:rip::rip:
 
Kama record zangu ziki sawasawa waheshimiwa waliomtoa Bungeni Mh. Zitto Kabwe karibu wote wameshindwa kutetea nafasi zao. Mfano John Malecela, Nazir karamagi, Batilda Burian, Ruth Msafiri na "Joka la Mdimu" Mudhihir wa Mudhihir. Kumbe watanzania wanajua kutoa adhabu! Big up wapiga kura wa majimbo husika.
Hivi Hawa Ghasia hakuwa mmoja wao?maana kama na yeye pia alichangia kama kumbukumbu zangu zipo sawa. Au kama nitakuwa nimesahau basi itakuwa ni issue ingine.
Ila amerejea bungeni this time.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom