Waheshimiwa wabunge ambao ni wagonjwa kwa muda mrefu sana wajiuzulu!

Mimi naona tufike mahali Serikali itueleze kama mtumishi anaumwa muda mrefu na hawezi kutekeleza kazi zake sababu ya Ugonjwa alio nao,ni lazma aachie ngazi wachaguliwe wengine.

Angalizo kuokoa pesa na muda unaotumika kufanya uchaguzi upya.Napendekeza mshidi wa pili apitshwe kuongoza kipindi kilicho bakia.Hii itapunguza gharama zisizo za lazma.
 
Muda mrefu sana ni miaka/miezi/wiki ngapi?
Policy ya bunge kuhusu kusimamishwa kazi kutokana na ugonjwa inasemaje?

Bwana/Dada Kongosho, mi ninavyo jua Wabunge ni waajiriwa wa wananchi, sheria za kazi kwa nchi yetu zipo wazi kabisa, ukiumwa kwa muda wa siku 63 bila kuwepo kazini (labda una E. D, au umelazwa) mwezi unaofuata unatakiwa kulipwa nusu mshahara, then utapewa miezi 6, ukipita hiyo then termination under medical grounds though hapa wenye VVU na ukimwi, sheria hii haiwahusu.

Sina hakika kama serikali huwa inafanya hivyo kwa mawaziri but wafanyakazi wa idara zingine kama walimu, nimeona baadhi wakipewa nusu mshahara kwa sheria hiyo. Kingine, kama watunga sheria, yaani hawa wabunge, wanatakiwa kuwa mfano kwa yale walioyatunga wenyewe, kama vipi wa resign tu.
 
Mzee wasira sio ugonjwa amechoka na Mchakamchaka hawezi,Mheshimiwa Rais Wazee kama hawa watafutiwe kazi mbadala lasvyo lawama kwa chama hazitaisha na wewe ndiyo unayetarajiwa kunusuru chama kwa Sasa.
 
Na kweli magamba wanamchanyato wa kila aina ndani ya bunge. watuhumiwa wa ufisadi, wauza sura, wachungaji feki, waganga wa kienyeji, poyoyo na zuzu(recall uchaguzi wa arumeru), wanaorithi nyadhifa za ndugu/wazazi wao, mawazo mgando, etc
 
Back
Top Bottom